Trafiki wapukutishwa barabarani, Vilio vyatawala

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,600
218,001
1659765316210.png

Gazeti la Raia Mwema limeripoti kwamba tayari panga limekwisha tembea, huku MCHEZO WA UPATU waliokuwa wanacheza Trafiki hao kila siku ukibaki njia panda , kwa vile wengi wamepangiwa kazi zingine ambazo haziingizi chochote zaidi ya Mshahara , TAARIFA ZINADOKEZA KWAMBA TRAFIKI WENGINE WALIKUWA NA MCHEZO WA UPATU WA KULIPA HADI SH LAKI MOJA KWA SIKU , ambapo inaelezwa kwamba chanzo cha hela hizo ilikuwa ni Rushwa za barabarani .

Kwa mujibu wa gazeti hilo , Trafiki wengi wanamlaumu Kinana kwa kuibua jambo hilo .

Endelea kubaki JF kwa taarifa zaidi.

PIA SOMA: Kinana akerwa na Utitiri wa Traffic barabarani. Atoa maagizo mazito kwa Afande IGP Camilius Wambura
 
Tusuburi ajali za barabarani ziongezeke
Wahuni wale walikua hawapunguzi ajali Wala nini. Ajali ya gari la wanafunzi Mtwara isingetokea Kama Hawa Wala rushwa wangekua wanakagua magari.

Nimpongeze IGP kwa hatua hii nzuri hasa kumuondoa trafik mmoja wa kike pale Ruvu jirani kabisa na hoteli ya JKT.

Mpangieni Yule mla rushwa kulinda nyumba ya DC wa kike awe anasikiliza miguno usiku.

Aliringa utafikiri daraja la Ruvu kalijenga babake.
 
Tuliweka uzi humu kuhusu Polisi wa barabara kupunguzwa , huku wengi wao wakipangiwa kulinda Mabenki Usiku , lakini kwa bahati mbaya Moderator akaunga uzi ule kwa mafundo mengi utadhani HIRIZI WANAZOTAPIKA WAUMINI WA MWAMPOSA...
lakini kwa bahati mbaya Moderator akaunga uzi ule kwa mafundo mengi utadhani HIRIZI WANAZOTAPIKA WAUMINI WA MWAMPOSA
 
Wakati mwingine unazitafakari akili za raia wa Tanzania katikati ya tafakuri yako ndio inakujia picha kwanini CCM bado ipo madarakani.

Kwa lugha nyepesi watanzania tuna uwezo mdogo sana wa kutafakari kwa kina na kuchanganua mambo ni kama mtoto mdogo anayepokonywa noti ya elfu kumi na kupoozwa na pipi ya mia akifurahia.
 
Back
Top Bottom