Mkuu wa Usalama Barabarani: Marufuku Trafiki na dereva kuzunguka nyuma ya gari

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
1,519
3,768
Kutokana na malalamiko ya rushwa dhidi ya askari Polisi Usalama Barabarani (Trafiki), Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Wilbrod Mutafungwa amepiga marufuku madereva kushuka na kuwafuata askari nyuma ya gari.

Mutafungwa alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Gazeti la Mwangaza kuhusu malalamiko ya rushwa dhidi ya askari wa Trafiki wanaosimamisha magari hasa daladala na madereva au makondakta kuwafuata na ‘kumalizana’ nao.

Mutafungwa alisema pamoja na madai ya rushwa kwa baadhi ya askari, lakini wapo waamifu wanaozingatia maadili na ndiyo maana licha ya kuwapo magari mengi nchini, lakini usalama barabarani upo kwa kiwango kikubwa.

"Lakini Jeshi ni taasisí kubwa, wapo wanajitokeza wachache wakajihusisha na vitendo vya rushwa, hivyo kwa hao wachache huwezi kusema Jeshi zima linahusika na rushwa," alisema Kamanda Mutafungwa.

Alisema Jeshi lina mifumo ya kuwachukulia hatua wala rushwa kama ilivyowekwa kwenye taasisi zote za Serikalı kuwa rushwa haitakiwi.

"Katika utekelezaji wa majukumu yetu, wanaokwenda kinyume wanachukuliwa hatua mbalimbali zikiwamo za kushitakiwa huku wengine wakifukuzwa kufikishwa mahakamani,” alisema Mutafungwa.

Akitoa mfano wa suala la rushwa na namna wanavyolishughulikia, Kamanda Mutafungwa alisema hivi karibuni alionekana askari kupitia mitandao ya kijamii, akijihusiha na vitendo rushwa Iringa, Polisi haikusita kumchukulia hatua kali za vya kinidhamu, ikiwamo kumfukuza kazi.

"Kwa vile umeongea suala la rushwa na mimi nitoe mwito, kwamba kupokea na kutoa rushwa yote ni makosa, kwa hiyo hata wanaojihusisha na vitendo vya rushwa wawe madereva au wamiliki wa magari, tunawataka waache kushawishi askari wetu, kwani kufanya hivyo pia ni kosa.

“Kwa hiyo, tunapoitazama rushwa tusitazame tu kwa wanaopokea, kutazama tunatakiwa pia wanaotoa, kwa kufanya hivyo tutaweza kukomesha vitendo vya rushwa,” alisema Kamanda Mutafungwa.

Hata hivyo, alisema katika usimamizi wa sheria kwa askari, wanawaelekeza wote kufanya kazi katika mazingira ya uwazi.

“Askari anapokamata mtu aliyevunja sheria za usalama barabarani kwa maana ya dereva, askari anatakiwa kumwajibisha katika hali ya uwazi, ili abiria kwenye gari hilo, waone hatua alizochukuliwa dereva wao.

"Daladala linakamatwa, kondakta anakimbia kwenda kwa askari, hii haitakiwi kabisa na tumeshalipiga marufuku. Kondakta amfuate trafiki kwani yeye ndiye anaendesha gari?

“Askari anayesimamisha gari, anatakiwa kulisogelea nabkumwajibisha dereva mbele ya abiria, wasikie kosa la dereva wao, si kwenda kuongelea kwenye uficho. Wanatakiwa kufanya kazi katika mazingira ya uwazi.”

Alisema katika kutanya hivyo, Dar es Salaam, vituo vya ukaguzi wadaladala vimepunguzwa baada ya kukaa na viongozi wa daladala na kukubaliana kuvipunguza.

“Mwito wangu ni kuwa askari anaposimamisha gari anatakiwa kulifuata lilipo na kufanya mahojiano kwa uwazı,” alisema.Source: Mwangaza
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
25,184
21,847
Hawa ndiyo makamanda waliopatikana kwa rushwa
  1. Anasubiri ahojiwe na gazeti ndipo atangaze marufuku, meaning bila gazeti kumuuliza asingezungumzia rushwa wanayopokea askari wake
  2. Hao baadhi wasio waaminifu amewachukulia hatua gani kukomesha tabia hiyo?
  3. Kwanini hataku kuweka vituo maalumu vya ukaguzi barabarani na viwe na camera kurekodi mienendo ya huo ukaguzi for transparence kama na yeye siyo mnufaika wa hiyo rushwa?
  4. Ni chombo gani anakitumia kujiridhisha kwamba hiyo marufuku yake inafanyiwa kazi?
 
Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
9,623
9,333
Pia waache kubambikiza makosa ya kutafutiza.

Sheria ya nchi inaruhusu kununua magari used sasa unategemea gari iwe nzima kwa kila kitu kwa asilimia 100 ?
 
Mkwe21

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,846
2,024
Nitajua kama Wabunge wetu wapo makini kama wakimbana Waziri WA mambo ya ndani, huwezi kutoka mwenge hadi Tegeta Kwa Dar, unapishana na Askari WA usalama barabarani zaidi ya 30, useme tuko sawa, kila mmoja anahitaji chochote Kwa nini wasibambike!?
 
Mkwe21

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,846
2,024
Kwa Dar Makonda alisema waongezwe Mara kumi zaidi ndio ilizaa hili tatizo " Madaraka ya kulevya"
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
69,824
82,221
Kuendesha gari sahvi imekuwa mateso

Asilimia kubwa ya wanaotumia magari wana wasi wasi wanapokuwa barabarani

Ova
 
Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
6,759
8,776
Hii marufuku itaanza kazi lini?

Leo nimeshuhudia traffic pale Mbezi njia panda ya kwenda Goba akimalizana na makonda kibao wa daladala nyuma ya bus.

Upigaji unaendelea kama Kawa 😂
 
Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
39,971
32,789
Traffic wanasaidia sana, kama sio wao, haya mabasi yanaovertaking za hatari sana,, sioni tatizo traffic kuoata hela za kubrash viatu
 
Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
72,220
145,437
Kutokana na malalamiko ya rushwa dhidi ya askari Polisi Usalama Barabarani (Trafiki), Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Wilbrod Mutafungwa amepiga marufuku madereva kushuka na kuwafuata askari nyuma ya gari.

Mutafungwa alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Gazeti la Mwangaza kuhusu malalamiko ya rushwa dhidi ya askari wa Trafiki wanaosimamisha magari hasa daladala na madereva au makondakta kuwafuata na ‘kumalizana’ nao.

Mutafungwa alisema pamoja na madai ya rushwa kwa baadhi ya askari, lakini wapo waamifu wanaozingatia maadili na ndiyo maana licha ya kuwapo magari mengi nchini, lakini usalama barabarani upo kwa kiwango kikubwa.

"Lakini Jeshi ni taasisí kubwa, wapo wanajitokeza wachache wakajihusisha na vitendo vya rushwa, hivyo kwa hao wachache huwezi kusema Jeshi zima linahusika na rushwa," alisema Kamanda Mutafungwa.

Alisema Jeshi lina mifumo ya kuwachukulia hatua wala rushwa kama ilivyowekwa kwenye taasisi zote za Serikalı kuwa rushwa haitakiwi.

"Katika utekelezaji wa majukumu yetu, wanaokwenda kinyume wanachukuliwa hatua mbalimbali zikiwamo za kushitakiwa huku wengine wakifukuzwa kufikishwa mahakamani,” alisema Mutafungwa.

Akitoa mfano wa suala la rushwa na namna wanavyolishughulikia, Kamanda Mutafungwa alisema hivi karibuni alionekana askari kupitia mitandao ya kijamii, akijihusiha na vitendo rushwa Iringa, Polisi haikusita kumchukulia hatua kali za vya kinidhamu, ikiwamo kumfukuza kazi.

"Kwa vile umeongea suala la rushwa na mimi nitoe mwito, kwamba kupokea na kutoa rushwa yote ni makosa, kwa hiyo hata wanaojihusisha na vitendo vya rushwa wawe madereva au wamiliki wa magari, tunawataka waache kushawishi askari wetu, kwani kufanya hivyo pia ni kosa.

“Kwa hiyo, tunapoitazama rushwa tusitazame tu kwa wanaopokea, kutazama tunatakiwa pia wanaotoa, kwa kufanya hivyo tutaweza kukomesha vitendo vya rushwa,” alisema Kamanda Mutafungwa.

Hata hivyo, alisema katika usimamizi wa sheria kwa askari, wanawaelekeza wote kufanya kazi katika mazingira ya uwazi.

“Askari anapokamata mtu aliyevunja sheria za usalama barabarani kwa maana ya dereva, askari anatakiwa kumwajibisha katika hali ya uwazi, ili abiria kwenye gari hilo, waone hatua alizochukuliwa dereva wao.

"Daladala linakamatwa, kondakta anakimbia kwenda kwa askari, hii haitakiwi kabisa na tumeshalipiga marufuku. Kondakta amfuate trafiki kwani yeye ndiye anaendesha gari?

“Askari anayesimamisha gari, anatakiwa kulisogelea nabkumwajibisha dereva mbele ya abiria, wasikie kosa la dereva wao, si kwenda kuongelea kwenye uficho. Wanatakiwa kufanya kazi katika mazingira ya uwazi.”

Alisema katika kutanya hivyo, Dar es Salaam, vituo vya ukaguzi wadaladala vimepunguzwa baada ya kukaa na viongozi wa daladala na kukubaliana kuvipunguza.

“Mwito wangu ni kuwa askari anaposimamisha gari anatakiwa kulifuata lilipo na kufanya mahojiano kwa uwazı,” alisema.Source: Mwangaza
Wakazungumze magendo au nyumba ya wageni? Achague moja
 
Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,424
1,973

Halafu viatu vya polish waache wavae raba!
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom