NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 10,001
- 21,297
"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"!
Walikula vya watu Bure Bure Sasa wakubali kutapishwa,na kuwekwa juu ya mawe🤔Tuliweka uzi humu kuhusu Polisi wa barabara kupunguzwa , huku wengi wao wakipangiwa kulinda Mabenki Usiku , lakini kwa bahati mbaya Moderator akaunga uzi ule kwa mafundo mengi utadhani HIRIZI WANAZOTAPIKA WAUMINI WA MWAMPOSA .
Lakini leo Gazeti la Raia Mwema limeripoti kwamba tayari panga limekwisha tembea , huku MCHEZO WA UPATU waliokuwa wanacheza Trafiki hao kila siku ukibaki njia panda , kwa vile wengi wamepangiwa kazi zingine ambazo haziingizi chochote zaidi ya Mshahara , TAARIFA ZINADOKEZA KWAMBA TRAFIKI WENGINE WALIKUWA NA MCHEZO WA UPATU WA KULIPA HADI SH LAKI MOJA KWA SIKU , ambapo inaelezwa kwamba chanzo cha hela hizo ilikuwa ni Rushwa za barabarani .
Kwa mujibu wa gazeti hilo , Trafiki wengi wanamlaumu Kinana kwa kuibua jambo hilo .
Endelea kubaki JF kwa taarifa zaidi .
Walikuwa wakisaidia Kwa kula rushwa?Tena huenda walichangia ajali kuzidi kwani hata kama gari bovu,wakivuta mlungula gari linasonga mwendo🤔kumbuka ajali zitaongezeka sana maana walikuwa kwa kiasi fulani wanasaidia kuwadhibiti madereva washenzi
Spidi gavana hata ikiwepo kwenye gari dereva akiuondoa waya mmoja haifanyi kazi !! Kwahiyo spidi gavana ya kweli ni matrafiki kuwa wengi na tochi zao !! Vinginevyo tusubiri tuone !! Kisha wengine wataandika tuliwaonya wakadharau !!Hivi siku hizi hakuna Spidi gavana ?
Kwann ana biashara za magari huyu,au ndugu zake wanamiliki malori hadi aone traffic keroKinana juu Mawinguni
Speed gavana ilikuwa ni dili la lowasa kutakatisha kodi zetuSpidi gavana hata ikiwepo kwenye gari dereva akiuondoa waya mmoja haifanyi kazi !! Kwahiyo spidi gavana ya kweli ni matrafiki kuwa wengi na tochi zao !! Vinginevyo tusubiri tuone !! Kisha wengine wataandika tuliwaonya wakadharau !!
Waweza kuwa mmoja wa uliyekuwa kikaangoni.🤔Spidi gavana hata ikiwepo kwenye gari dereva akiuondoa waya mmoja haifanyi kazi !! Kwahiyo spidi gavana ya kweli ni matrafiki kuwa wengi na tochi zao !! Vinginevyo tusubiri tuone !! Kisha wengine wataandika tuliwaonya wakadharau !!
Mbona askari hawa wa kike Wana sense of humour sana huyo imekuwaje?Mpangieni Yule mla rushwa kulinda nyumba ya DC wa kike awe anasikiliza miguno usiku.
Aliringa utafikiri daraja la Ruvu kalijenga babake.
Wa kike akiwa peke yake ndio ana hiyo sense unayoisema. Akiwa yupo na askari wa kiume, yeye ndio anakuwa kipele.Mbona askari hawa wa kike Wana sense of humour sana huyo imekuwaje?
Tusuburi ajali za barabarani ziongezeke
Sio kweli Mkuu !! Mimi ni raia mwema tu ! Najaribu kutoa tahadhari maana mimi nimesafiri sana barabarani nawajua vizuri sana madereva wetu wa sasa huko barabarani akili zao huwa zinahama sijui huwa zinaenda wapi ! Ndio maana utaona kila wakati wanaulizana kwa ishara kama Trafiki wapo mbele au hawapo? Ili tu akanyage mafuta kisawasawa na bila kuchukua tahadhari yeyote !!Waweza kuwa mmoja wa uliyekuwa kikaangoni.🤔
Umenena !!Askari wa barabarani wapo na wanaendelea na kazi zao kama kawaida.
Kilichopungua ni ule wingi na kero ambao ulikuwa unapunguza ufanisi na kusumbua raia kwa sababu binafsi zaidi.
Taasisi za udhibiti zisizo za kitaalamu, zinatakiwa kuwa na watendaji wchache wanaoendana na hali halisi, ili kupunguza rushwa na kero kwa wananchi.
Kwahiyo ww ulikuwa ukiona sawa trafick kukaa makundi makundi vile barabarani utadhani pundamilia tena highway??Wakati mwingine unazitafakari akili za raia wa Tanzania katikati ya tafakuri yako ndio inakujia picha kwanini CCM bado ipo madarakani........kwa lugha nyepesi watanzania tuna uwezo mdogo sana wa kutafakari kwa kina na kuchanganua mambo.......ni kama mtoto mdogo anayepokonywa noti ya elfu kumi na kupoozwa na pipi ya mia akifurahia.....
Huyo amekuwa mbishi sana karne nzima anawatetea sana hao wala rushwa,Wewe utakuwa ni traffic
Tuliweka uzi humu kuhusu Polisi wa barabara kupunguzwa , huku wengi wao wakipangiwa kulinda Mabenki Usiku , lakini kwa bahati mbaya Moderator akaunga uzi ule kwa mafundo mengi utadhani HIRIZI WANAZOTAPIKA WAUMINI WA MWAMPOSA .
Lakini leo Gazeti la Raia Mwema limeripoti kwamba tayari panga limekwisha tembea , huku MCHEZO WA UPATU waliokuwa wanacheza Trafiki hao kila siku ukibaki njia panda , kwa vile wengi wamepangiwa kazi zingine ambazo haziingizi chochote zaidi ya Mshahara , TAARIFA ZINADOKEZA KWAMBA TRAFIKI WENGINE WALIKUWA NA MCHEZO WA UPATU WA KULIPA HADI SH LAKI MOJA KWA SIKU , ambapo inaelezwa kwamba chanzo cha hela hizo ilikuwa ni Rushwa za barabarani .
Kwa mujibu wa gazeti hilo , Trafiki wengi wanamlaumu Kinana kwa kuibua jambo hilo .
Endelea kubaki JF kwa taarifa zaidi .
Na kuna mmoja pale Bunju anaitwa Kichuya....Hahahahahaha kuna mmoja anaitwa kinyota Askari flani hivi yupo hapo Mlandiz saa ingine pale pale Ruvu Darajani