Ijue mipaka ya kimamlaka kwenye video ya mzozo wa mwanajeshi na trafiki wa usalama barabarani inayosambaa mitandaoni

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,397
Kuna video inatembea mitandaoni!


Video ile inamuonesha mwanajeshi wa jeshi la wananchi akiwa na sare akiwa ni moja ya abiria kwenye bus (daladala) akizozana na askari wa usalama barabarani (trafiki)

Kipande hiko cha video kinaonesha kulikuwa na majibizano na lugha isiyofaa kabla!
Maneno machache yaliyosikika ni Mwanajeshi alijibu kwa kumwambia yule TRAFIKI kwamba! "Wewee huwezi kunionya Mimi wee paka tu"

Traffic alijibu kwa kuhoji "Mimi ni paka?

Mwanajeshi alijibu nae kwa kusema:
" Huwezi kunionya wewe Arooh nakucheki sana!

NANI ANA MAKOSA?
Hapo tukianza na mwanajeshi tunagundua either kwa kusahau au kwa kueleweka vibaya huenda baada ya gari alopanda (daladala) kukamatwa na kushikiliwa hakuona dalili njema za uadilifu kwa traffic ambazo zilionekana kuwachelewesha!

Hivyo kwa nia njema au mbaya huenda alimsihi yule TRAFIKI amalize kazi yake fasta wawahi!

Bahati mbaya huenda TRAFIKI aliitafsiri vibaya ile kauli ya manajeshi na kumuonya yule mwanajeshi! (Bad approach)

Kitendo cha TRAFIKI kumuonya yule mwanajeshi waziwazi kilikuwa na mlengo mbaya na mapokeo mabaya yanayoshusha hadhi ya JWTZ mbele ya RAIA (Na hapo ndipo unamuona mwanajeshi anapaniki kwamba unaweza kunionya wewe paka?)

Na baada ya TRAFIKI Polisi kugundua kwamba Kachemka, alitumia mwanya wa kuitwa PAKA kutafta kinga ya kisheria endapo mambo yataharibika!

Kimamlaka na sheria nani alikuwa sahihi?

Kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani (Road traffic act) zinampa mamlaka ya kisheria askari wa usalama barabarani kukamata na kuadhibu chombo chochote cha moto kinachohisiwa kukiuka sheria za usalama barabarani pasipo kujali kimebeba nani!

Mamlaka hayo yakisheria yanamlazimisha TRAFIKI Kuongea na dreva wa chombo husika peke yake (SIYO ABIRIA)
ABIRIA anaweza kutoa maoni au taarifa ya kutokutendewa haki na dreva au chombo lakini HARUHUSIWI KUMUAMRISHA TRAFIKI kutekeleza kazi yake!

ABIRIA akifanya hivyo anakuwa katenda KOSA LA KUMZUIA ASKARI Kufanya kazi yake!

Kwa matinki hiyo TRAFIKI Anaweza kukamata CHOMBO CHOCHOTE CHA KIRAIA (siyo majeshi) hata kama chombo hicho kitakuwa kimebeba kikundi cha wanajeshi kiasi cha kuhatarisha usalama barabarani!

Hivyo kimamlaka ya usalama barabarani TRAFIKI alikuwa sahihi LAKINI ALIKOSA BUSARA!

Mwanajeshi alikuwa sahihi lakini hakutumia BUSARA kufikisha ujumbe wake!

Hapa nachoweza kusema Shamba la bwana kheri, Mbuzi wa bwana kheri!
Maelekezo ya kinidhamu yanayotolewa kila siku HAYAKUZINGATIWA na wawili hawa!
KUKOSA Kwao BUSARA Kunaweza pelekea migogoro ya mihimili miwili ya kijeshi!
Hivyo wote wawili wanastahili ADHABU kutoka wakuu wao na endapo watakuwa na makosa mengine nyuma kama hayo inashauriwa hata KUFUKUZWA KAZI!
 
Kazi za jeshi ni ngumu zinahitaji morali sio kama polisi pushups kwenye Godoro sisi makamanda pushups kwenye kokoto... haiwezekani kamanda maji kupanda mlima

sasa kama me nikiwa depo naimba nyimbo za hivi... kwel polisi nitakuwa namwonaje.... hili bifu lipo tangu zamani hawapatani hawa
 
Kimedani imekaaje?

Mwanajeshi ana cheo cha Staff Sergeant. Huku polisi akionekana private (Constable).

Hata kama angekuwa na cheo sawa na mwenzake, polisi angelipaswa kumheshimu Mjeda kwa minajili ya kimedani.

Mjeda kakosea kumtolea mwenzake lugha inayokwaza akiwa katika uniform.

Ukweli ni kuwa hiyo ni mfano wa chuki iliyomo baina ya Polisi na JWTZ. Kuna mmoja anamwona mwenzake hamnazo alafu mwingine anamuona mwenzake wa kawaida.
 
Kimedani imekaaje?

Mwanajeshi ana cheo cha Staff Sergeant. Huku polisi akionekana private (Constable).

Hata kama angekuwa na cheo sawa na mwenzake, polisi angelipaswa kumheshimu Mjeda kwa minajili ya kimedani.

Mjeda kakosea kumtolea mwenzake lugha inayokwaza akiwa katika uniform.

Ukweli ni kuwa hiyo ni mfano wa chuki iliyomo baina ya Polisi na JWTZ. Kuna mmoja anamwona mwenzake hamnazo alafu mwingine anamuona mwenzake wa kawaida.
Rudia kusoma mkuu hapo juu!
TRAFIKI ANAMAMLAKA YA KISHERIA
(Road traffic act)
Kasomeni sheria!

Bila kujali cheo cha TRAFIKI anamlaka ya kukamata magari yote yaliyopo barabarani ukiondoa ya wakuu wa nchi yaliyo kwenye msafara au safari maalum!
 
sasa huyo mzee kama aliona anachelewa si angeshuka apande gari lingine!!na magari ya jwtz yapo,ukipanda daladala au bus basi wewe ni abiria kama wengine,uwe mtulivu.

aibu nyingine mtu anazitafuta kwa nguvu,maana sasa hapo abiria wanashangaa kwanini constable anamuwakia ssgt wa jeshi tena!!!na sijui aliishije humo garini hata baada ya kuachiwa.
 
Back
Top Bottom