Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu malalamiko ya Bw. Emmanuel Gadi kuwa, TRA imetengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini nje ya mfumo halali wa Serikali kinyume na Sheria ya Forodha.
Tunapenda kuufahamisha umma na jamii kwa ujumla kuwa, Mamlaka haina mfumo wowote mwingine inaouendesha wa kuingiza mizigo nchini nje ya mfumo wa Forodha wa TANCIS ambao unatumika kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACCMA).
Bw. Emmanuel Gadi alifikisha malalamiko yake kwa njia ya barua tarehe 27 Februari, 2023 akidai kupewa uthibitisho na TRA wa kuingiza mzigo wa vifurushi 471 vya “Toner Cartridges’’ kupitia kampuni ya Tosh Logistics Ltd. TRA ilifanya uchunguzi wa kutosha na kuthibitisha kwamba, hapakuwa na mzigo wowote ulioingizwa nchini kwa jina la Wintech Tanzania Ltd wa vifurushi 471 vya “Toner Cartridges” kupitia kadhia yenye namba TZDL-22-1382193 ya tarehe 18 Agosti 2022 kama anavyodai.
Hivyo, TRA ilimjibu mhusika kupitia barua yenye kumbukumbu namba CF 8/92/01 ya tarehe 25 Julai 2023 ikimjulisha kuwa, kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa “House Bill of Lading” na kutoonekana kwa mzigo huo kwenye kadhia iliyowasilishwa na kampuni ya Tosh Logistics Ltd, TRA isingeweza kuthibitisha kuingizwa kwa mzigo huo nchini.
Kupitia taarifa yake aliyoitoa kwenye vyombo vya habari tumebaini kuwepo viashiria vya ukwepaji kodi kwani ni dhahiri kuwa mzigo huu uliingizwa kwa njia za magendo. TRA inamtaka mlalamikaji kuwasilisha nyaraka na uthibitisho wa kampuni yake kuingiza mzigo huo nchini mara moja ili hatua stahiki zichukuliwe.
===========
Video ya Mfanyabiashara akiituhumu TRA