TRA someni hapa: EFD zenu WIZI MTUPU

TRA someni hapa: EFD zenu WIZI MTUPU

mkuu
mbali ya hiyo mashine leseni sasa ni.kuanzia tsh 200,000 hadi 800,000 wanaangalia uwezo wa duka kila mwaka.
_fire kila mwaka 100,000.
~taka sh 24,000kila mwezi.
na hizi zote wamemlenga mwenye duka.
sasa tumechoka kuwa chuma ulete,kesho mgomo unaendelea

Nyie wezi tu! Kodi ni lazima tumechoka na misaada!
 
Acheni visingizio, tulipe kodi. Tumeshavuna sana kwenye biashara pasipo kulipa kodi halali ya serikali. Tuache visingizio na vijihesabu vya uongo.
 
Yule mfanyakazi anayelipa PAYE wakati anapokea Sh. 180,000/- mapato yake kwa siku ni Sh.6000; yaani umemzidi zaidi ya mara sita! Huyu nae anakatwa kabla hajalipa pango, mfanyakazi, maji, umeme n.k! Wakati wewe ukilipa hivyo vitu unabaki na angalau sh.1000 kwa siku, mwenzako anabaki na Negative Income na ndio maana, mshahara wanalipwa tarehe 25, lakini inapofika tarehe 26 or 27 of the same month, anabaki hana kitu.

naona wewe pia hesabu zinakuchenga mbaya. Rudi post yangu ya kwanza utaona mapato halisi ya mfanyabiashara mdogo wa mauzo ya sh 38,000 kwa siku. Tofautisha mauzo ghafi na faida. Kwenye mauzo ghafi bado ndani yake kuna mtaji na gharama za biashara. Na nimeeleza awali kuwa kwa faida ya asilimia 10%, mtu huyu faida yake ghafi haizidi sh 4,000 ambayo ni ndogo kuliko hiyo 6,000 ya mfanyakazi mwajiriwa. Na kumbuka, sisemi asitumie EFD, nasema asiuziwe, apewe kama kifaa cha kazi ya TRA, akitumie kukusanya kitakachopatikana hata kama ni sh 300 apeleke huko TRA. Na narudia kusema, kumlazimisha mtu wa hali hii kununua EFD ya laki sita ni WIZI MTUPU.
 
Kuna mtu mmoja hapa naongea nae analalamika, anasema yeye duka kafungua na efd anayo na anaitumia lakini leo anashindwa kufanya biashara kwa kuwa umeme hamna na atauzaje bila kuwapa watu risiti za efd?

TRA mpo? Hebu tumpe majibu huyu mtu afunge biashara na gharama awaletee nyinyi muwape TANESCO wamlipe au awapelekee gharama TANESCO moja kwa moja? Au auze bila risiti za EFD?

Kizungumkuti.
 
Waswahili wabishi sana nyie. Hiyo machine ikinunuliwa inakaa mwaka mmoja na unanunua ingine?! Lipeni kodi kwa maendeleo ya nchi na si kubisha bisha upuuzi. Kodi lazima ilipwe, piga ua, hata aje kutawala.
 
Mkuu, hii ni Tanzania. Una uhakika gani kuwa TRA wamewaeleza hawa wasiohusika namna ambavyo inatakiwa iwe? Inawezekana kabisa watendaji wadogo wa TRA wakawa wanawasumbua wasiohusika kwa ukosefu wia mashine ili wapewe rushwa. Siamini kama wafanyabiashara hawa wadogo ni wajinga wafunge biashara zao kama hiyo mashine haiwahusu. Kuna kikubwa zaidi ya hiki.

Kumbuka, OP Tokomeza ilikuwa na umuhimu mkubwa kwa nchi na pia nia na dhumuni lake ilikuwa nzuri tu. Ila kwa Tanzania, ikawa mradi wa watu - kamata ng'ombe lipisha faini, weka mfukoni. Ujangili ukachukua nafasi ya pili baada ya wafugaji. Nina wasiwasi hili zoezi linahujumiwa na wafanyakazi wa TRA wenyewe. Kumbuka kuwa hizi mashine zinakata mrija wa wafanyakazi wa TRA kukisia kodi hivyo chanzo chao kikubwa cha rushwa kitakatika.

Fikiria tena

Mkuu mbona iko wazi hii kila siku kwenye vipindi vya radio tv.kama kipima joto, malumbano ya hoja na kupitia tbc 1.wafanyakazi wa mamlaka ya mapato tz (TRA)wanatoa elimu hiyo ya kama hujapata barua toka Tra inayokutaka ununue mashine hizo wewe huusiki.Kinachofanyika ni wale waliopata barua hizo wanawaingiza mkenge hata ambao hawahusiki madamu hawajapata elimu hiyo.ili wapate huruma wakati si kweli,
 
Yule mfanyakazi anayelipa PAYE wakati anapokea Sh. 180,000/- mapato yake kwa siku ni Sh.6000; yaani umemzidi zaidi ya mara sita! Huyu nae anakatwa kabla hajalipa pango, mfanyakazi, maji, umeme n.k! Wakati wewe ukilipa hivyo vitu unabaki na angalau sh.1000 kwa siku, mwenzako anabaki na Negative Income na ndio maana, mshahara wanalipwa tarehe 25, lakini inapofika tarehe 26 or 27 of the same month, anabaki hana kitu.
naona wewe pia hesabu zinakuchenga mbaya. Rudi post yangu ya kwanza utaona mapato halisi ya mfanyabiashara mdogo wa mauzo ya sh 38,000 kwa siku. Tofautisha mauzo ghafi na faida. Kwenye mauzo ghafi bado ndani yake kuna mtaji na gharama za biashara. Na nimeeleza awali kuwa kwa faida ya asilimia 10%, mtu huyu faida yake ghafi haizidi sh 4,000 ambayo ni ndogo kuliko hiyo 6,000 ya mfanyakazi mwajiriwa. Na kumbuka, sisemi asitumie EFD, nasema asiuziwe, apewe kama kifaa cha kazi ya TRA, akitumie kukusanya kitakachopatikana hata kama ni sh 300 apeleke huko TRA. Na narudia kusema, kumlazimisha mtu wa hali hii kununua EFD ya laki sita ni WIZI MTUPU.
Labda uzungumze lingine lakini sio kupigwa chenga na hesabu....Nimesoma Maths kuanzia O-Level hadi Versity, and very interesting, nimesoma Economics na kufanya kazi kwenye commercial banks so nafahamu vizuri what's the difference btn net and gross income!

Wewe reference yako ni kwa mfanyabiashara anayepata mapata mapato ghafi ya sh. 38,000/- kwa cku; ndipo nami nikakuambia kwamba, mfanyakazi anayelipwa Sh.180,000/- kwa mwezi, mapato yake ghafi kwa siku ni sh.6000/-; ambapo ni pungufu kwa zaidi ya mara sita as compared na hayo ya 38,000/- kwa siku! Sasa ni nani hapo anayetia shaka shaka kuhusu uelewa wake wa hesabu?

Aidha, wewe ukasema kwamba kwa mfanyabiashara kama huyo kwa siku anaweza kubakiwa na sh. 1000/- kwa siku baada ya kutoa gharama zote, nami nikakuambia huyo wa gross income ya sh.6000/- hawezi kubaki hata na hiyo sh.1000/- kwa siku...

Tukija suala la kununua EFD, hata kama ni kweli wafanyabiashara wanalipia hiyo 600K, lakini pesa yao wanarudishiwa na TRA wanapowasilisha tax returns.
 
Kuna mtu mmoja hapa naongea nae analalamika, anasema yeye duka kafungua na efd anayo na anaitumia lakini leo anashindwa kufanya biashara kwa kuwa umeme hamna na atauzaje bila kuwapa watu risiti za efd?

TRA mpo? Henu tumpmjibu huyu mtu afunge biashara na gharama awaletee nyinyi muwape TANESCO wamlipe au awapelekee gharama TANESCO moja kwa moja? Au auze bila risiti za EFD?

Kizungumkuti.
FaizaFoxy nishakushtukia...isije na wewe una kaduka pale mitaa ya Kariakoo lakini kutokana na mahaba uliyonayo kwa serikali yako tukufu ndo unataka kusingizia kwamba kuna "rafiki yako hapo unaongea nae!!" Acheni ujanja ujanja...tumieni EFDs tupate kodi yetu! Huo umeme umekatika lini; jana? EFDs si kama Desk Top PC, kwamba ukikatika umeme ndo basi tena...ina maana hiyo ya shoga'ako haitunzi chaji??!! Wengine ukienda dukani huwa hawatoi risiti kwa kusingizia network wakati suala la kutoa risiti wala halina uhusiano na network!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hapa sijakusoma hizo hesabu zako kabisa.Umepiga hesabu za darasa la saba.
Kwanza unaposema faida ni 1000 kwa siku mwenye mauzo ya mwaka 14m sijaelewa kbs labda mimi mgeni?
Pili kwa hiyo watu wasilipe kodi kwa utaratibu ambao serekali itatambua makato yote.Serekali namaanisha TRA.
Tatu hiyo mashine sio kila mwaka utainunua kama wewe unavyotaka kuonesha katika huo mlolongo wako wa breakdown ya sijui friji,pango,umeme.Hii ni mfumo tuu wa kulipa kodi kisasa.

Note.Sifanyi kazi TRA usije ni hukumu hivyo wala mimi sio mwana siasa yaani mwan CCM sababu ushaonekana huku ukizungumzia EFD basi kosa.

Walewale wa division five. Hesabu zero. Nakushauri uendelee tu na ajira yako hapo kwa mhindi.
 
Naona Mku wangu unakazana kujikita na revenue floor iliyotolewa na TRA kama ndio bas yako! Kimahesabu upo sawa lakini practically hao wanaouza sh. 38,000/- wala bado hawajaguswa! Wanaofanya biashara ya mapato ghafi ya sh. 38,000/= kwa siku wengi wao kama sio wote ni wale wenye viduka vidogovidogo huku uswahilini tena mitaa ya ndani! Hao wa sh.38,000/ kwa siku ni wale wanaouza mafuta ya taa na ya kula kwa vipimo vya shilingi mia mia....hawa ni wale wanaouza majani ya chai ya shilingi 50/-, hawa ni wale wanaouza sukari au bidhaa zingine hata kwa robo kilo...hawa ni wale mtu unafika dukani, unalazimika kutoa mia mfukoni kugonga nondo ili mwenyewe aliyekaa sebuleni akusikie na kuja kukupa huduma!! In short, ni wale ambao viduka vyake ni vile ambavyo mteja anasimama dirishani na ni MARUFUKU kuingia ndani!!!! Hawa ndio hao wanaofanya mauzo ya sh.38,000/-na wala sio wale wanaogoma! And in fact, hata hawa nao wanauza zaidi ya hiyo....waht does it take? Maharage 10kg@2000+Unga 15kg@1000+Mchele 10kg@1500=50,000/- per day....hatujataja sigara, viberiti, mafuta ya taa, mafuta ya kula ya mia mia, majani ya chai ya hamsini hamsini and so much more!

Mimi nilikuwa na biashara ya aina hiyo na nimeletewa barua ya kunua EFD. Nimeifunga, of course kwa sababu tofauti, lakini hata nisingeifunga, nisingeweza kuendelea nayo kama msisitizo huu utaendelea. Ndio maana nasema ni WIZI MTUPU maana hata wafanyabiashara wa ngazi hiyo wamefikiwa, barua zimesambazwa na mara kwa mara wakala anapiga simu kukumbushia.

Nina uhakika kuwa wanaoandamana kupinga ni wenye hali kama niliyokuwa nayo na kabiashara kangu. TRA wanaona shida gani kugawa bure hizo EFD kwa hao wadogo? Imagine mtu amekopa milioni moja kwenye SACCOS afanye kabiashara duni hako, halafu wanamtaka anunue EFD laki sita na ushee. Ni nini hii kama sio wizi mtupu?

Hicho ulichokiita wewe "revenue floor" ndicho ninachosema wameweka cha chini mno. Wangeanzia na milioni 100 hizi fujo za wamachinga na wenye viduka vya vibanda-umiza usingezisikia.
 
Waswahili wabishi sana nyie. Hiyo machine ikinunuliwa inakaa mwaka mmoja na unanunua ingine?! Lipeni kodi kwa maendeleo ya nchi na si kubisha bisha upuuzi. Kodi lazima ilipwe, piga ua, hata aje kutawala.

Kwa hiyo inakaa miaka mingapi hiyo mashine mheshimiwa TRA? Na unajua huyo mwenye mtaji wa laki tano ilimchukua miaka mingapi kupata mtaji huo? Walioshiba za ufisadi utawajua tu!
 
Mkuu mbona iko wazi hii kila siku kwenye vipindi vya radio tv.kama kipima joto, malumbano ya hoja na kupitia tbc 1.wafanyakazi wa mamlaka ya mapato tz (TRA)wanatoa elimu hiyo ya kama hujapata barua toka Tra inayokutaka ununue mashine hizo wewe huusiki.Kinachofanyika ni wale waliopata barua hizo wanawaingiza mkenge hata ambao hawahusiki madamu hawajapata elimu hiyo.ili wapate huruma wakati si kweli,

Kigezo cha kuchagua wa kusambazia barua hizo pia kinalalamikiwa. Ukiona mwenzio anayeuza kreti mbili za soda kwa siku kaletewa barua hiyo, wewe unayeuza mbili na nusu utakaa tu ukidhani haikuhusu? Ni wizi wanaufanya, kwa zamu.
 
mi ni mfanyakazi lakini nawasapoti wafanyabiashara.hata wakinunua hizo mashine bado mzigo ni kwetu sisi walaji.kama ujuavyo biashara za bongo ni maelewano.hatujafika hatua ya kuwa na fixed price.nguo ya elf 40 utainunua kwa 15000.just imagine wauza mitumba wa karume au mchikichini wawe na efds unategemea walalahoi tutavaa?.suruali ya ekf 10 utainunua kwa elf 25.ile ya dukani ya elf30 utainunua kwa 50.mshahara wenyewe laki 4 utaweza kuishi?usiwe na myopic minded.kabla ya kuropoka uwe unafikiria matokei ya kitu kwa mapana yake.sio tu ushabikie wafanyabiashara kulipa kodi bila kujua position yako itakuwaje kama mlaji katika mzunguko wa kibiashara.
kwa wafanyabiashara kulipa kodi ni sawa kabisa kakini kuwepo na utaratibu ambao hautaleta madhara kwaa end user.bei ya umeme imepanda maji nayo yamepanda kutoka50 kwa ndoo moja hadi 100 tsh.kwa uelewa wako mdogo hapo muathirika ni nani?unadhani ni tanesco au serikali?acha ushabiki usiokuwa na tija kijana

Upo sawa ndugu , unajua wanachi hawajui hii kitu kama ita kula mpaka kwao..
 
setuba noel ulichosema ni sawa kuwa mwenye mauzo ya kuanzia milioni 14kwa mwaka anatakiwa kuwa na mashine.ila kwa taarifa yako kwa awamu hii ya pili hicho c kigezo pekee kinachotumika wao tra walisambaza barua kwa wafanyabiashara 200,000 tz nzima ambao wanatakiwa kutumia mashine hizi awamu ya pili na ni wafanyabiashara wakubwa tu.

Sio kweli kama unavyodai kuwa kwa awamu hii hata mwenye mauzo ya 38,000 kwa siku anatakiwa kuwa na mashine,na wengi wanafuata mkumbo tu bila kujua.na wafanya biashara wa kariakoo wengi wanafanya biashara ki magumashi ndio maana hawataki kusikiaa habari za efd.kwani mwanzoni walianza kuwa tatizo ni bei sasa wanadai hata wakipewa bure hawataki!

Which is which?

Ila nashukuru serikali inapokuja na msimamo ambaye hawezi arudishe leseni na tin. Akafanye shughuri nyingine,uone kama hawatafyata mkia.kuna ubaya gani serikali kujua mauzo yako?

Kama hakuna kitu unachoficha kwani ktk kodi mauzo ghafi ndio yataonyesha kiwango cha kodi unachotakiwa kulipa.

mkuu niliyokaambiwa kwenye semina pale tra mbona tofauti na huu uongo wako unaouweka hapa?
 
Last edited by a moderator:
Setuba Noel Mbona mnamiliki simu za laki 8?

Kumiliki simu ya elfu moja adi mamilion ni juu ya mtumiaji mwenyewe na uwezo wake na matumizi ya simu yake binafsi, kama ilikuwani kwamatumizi ya TRA na sababu ni wao waliopendekeza na wakaona ni muhimu kwao wangenunua mashine ata kama ni milioni kumi wawape wafanya biashara sababu wao ndo wako concern kama waliona kutumia njia ya analogia wanibiwa.
 
Last edited by a moderator:
Vile vile hizi efd ni kwa wafanyabiashara wenye leseni tuu ama mpaka hawa machinga...!??coz machinga wanauza vitu kwa bei poa kama tunavyojua huyu aliyepangisha pango ataweza kufanya biashara ukitizam kuna machinga anauza homogenious pembeni yako....!??almost tunajua kama huyu wa pamgo hatoweza coz ua hizi expenses zengne ni haki yao kuandamana kila kitu kipo juu mpaka huo umeme wa kuendeshea hiyo cjui EFD ni bei juuu aiseee hii nchiiiiii uzalendo utatushinda tukane titafte uraia kwngne
 
Labda uzungumze lingine lakini sio kupigwa chenga na hesabu....Nimesoma Maths kuanzia O-Level hadi Versity, and very interesting, nimesoma Economics na kufanya kazi kwenye commercial banks so nafahamu vizuri what's the difference btn net and gross income!

Wewe reference yako ni kwa mfanyabiashara anayepata mapata mapato ghafi ya sh. 38,000/- kwa cku; ndipo nami nikakuambia kwamba, mfanyakazi anayelipwa Sh.180,000/- kwa mwezi, mapato yake ghafi kwa siku ni sh.6000/-; ambapo ni pungufu kwa zaidi ya mara sita as compared na hayo ya 38,000/- kwa siku! Sasa ni nani hapo anayetia shaka shaka kuhusu uelewa wake wa hesabu?

Aidha, wewe ukasema kwamba kwa mfanyabiashara kama huyo kwa siku anaweza kubakiwa na sh. 1000/- kwa siku baada ya kutoa gharama zote, nami nikakuambia huyo wa gross income ya sh.6000/- hawezi kubaki hata na hiyo sh.1000/- kwa siku...

Tukija suala la kununua EFD, hata kama ni kweli wafanyabiashara wanalipia hiyo 600K, lakini pesa yao wanarudishiwa na TRA wanapowasilisha tax returns.

Versity ya wapi umesoma wewe? Hivi siku hizi huko wanapokea hadi division five kumbe? Wewe kwa mawazo yako nikinunua bidhaa kwa 34,000 nikaziuza kwa 38,000 kumbe nimepata 38,000 mapato ghafi? Na mtaji uko wapi?
Kama ni kweli wewe umesoma hizo economics unazosema basi kumbe ndio maan nchi hii haiendelei!

Sasa nikufundishe na economics zako za feki. Mapato ghafi ni kile kinachobakia ukishatoa bei ya kununulia bidhaa uliyouza. Mapato halisi yanakuja utakapotoa gharama nyingine za biashara.

Huyo anayelipwa mshahara wa sh 6,000 kwa siku hiyo ndiyo mapato ghafi, akitoa gharama za kuihudumia hiyo ajira (usafiri, mlo wa mchana nk) anabaki na mapato halisi. Aliyeuza mali ya 38,000 kutoka manunuzi ya 34,000 mapato yake ghafi ni sh 4,000, nako pia akitoa gharama za kuhudumia biashara yake (nauli, pango, ulinzi, usafi, umeme nk) anabaki na mapato halisi. Yupi mwenye mapato halisi kubwa hapa boss mchumi? Hapa pia unahitaji hesabu za "versity"?

Kwahiyo mheshimiwa wa hesabu za "versity", mapato ghafi ya sh 4,000 kwa siku na yale ya sh 6,000 kwa siku yapi makubwa boss mchumi? Hesabu zako na economics za "versity" zikasema sh 4,000 ndiyo kubwa (umeichanganya kwenye mtaji ikawa 38,000! kwahiyo unataka huyu ndugu ale mtaji wake kwa kujidanganya ana mapato makubwa kuliko huyo wa 6,000, na kesho atazungusha mtaji upi?)

Hili janga la division five sikujua kama limeenea hadi "versity"!
 
Wamezoea kutuibia hawa(serikali)

Kama mnakumbuka serikali iliwahi kuleta gadget za ku-track mwendo kasi ili ku-replace tochi iloyoonekana na mapungufu mengi, lakini mwisho wa siku gadget ile ilikataliwa na wamiliki wa mabasi kama zinavyokataliwa mashine hizi-na hadi leo ni kimya, hatusikii ten a wamiliki wa mabasi wakilazimishwa.

Hivyo, ni wazi huu ni mradi wa wajanja wachache wakitaka kuwakandamiza wafanyabiashara ili kujinufaisha wao.

Binafsi naona ni kamchezo ka-kitoto, serikali imekosea tena...yes wajipange!
 
Haya mambo ya TRA na EFD zao ni WIZI MTUPU. Wanataka mtu mwenye mauzo ghafi ya kuanzia TSh 14,000,000 kwa mwaka anunue hiyo kifaa ambayo bei yake ni kuanzia laki sita na ushee. Twende kimahesabu. Mauzo ya sh 14mil kwa mwaka ni kama wastani wa kuuza sh 38,000 kwa siku. Kwa profit margin ya 10-15% mfanyabiashara kama huyu ana faida ghafi ya kama Tsh 4,000 hivi kwa siku. Akitoa gharama za pango, ulinzi, umeme, usafi, na tukichukulia hana mfanyakazi, huyu mtu faida yake net haizidi 1,000 kwa siku. Watu ambao mmewahi kufanya biashara mnaelewa, mtu mwenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku ni mfanyabiashara MDOGO SANA, wa chini kabisa, ni mtu wa kima cha chini huyu. Mtaji wa kuuza 38,000 kwa siku ni mdogo kuliko hiyo laki sita ya kununulia EFD.

TRA wametumia akili gani kudhani kuwa mtu huyu wa kima cha chini anayechuma chini ya sh 1,000 kwa siku anaweza kununua hiyo EFD ya sh 600,000? Mtu anunue kadude hako kwa bei kubwa kuliko mtaji alionao? Halafu wanashangaa kuona watu wanaandamana! Nyie TRA mnashangaa nini kuhusu maandamano? Hamuwajui wanaoandamana? Ni wafanyabiashara ndogondogo wenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku, eleweni hivyo. Na hawa wako wengi sana, hawahitaji kutumwa na mtu.

Jamani hivi huko TRA mbona mnataka tudhani kuwa wote mlifeli hesabu? Sh laki sita atazipata wapi mtu anayechuma elfu moja kwa siku? Hata akifanya kazi mwaka mzima bila kula, jumla ya kipato chake itakuwa sh 365,000 bado haitoshi kununua EFD. Mtumie akili jamani. Hicho kiwango hakiwezekani kwa wafanyabiashara mnaowalenga.

Cha kufanya. Rejeeni hicho kiwango mrekebishe, muanzie labda kwenye mauzo ghafi ya sh 100,000,000 kwa mwaka (ambayo ni sawa na wastani wa sh 270,000 hivi kwa siku) hawa angalao wangeweza, na nadhani hawalalamiki maana tunaona zikitumika kwenye maduka. Na hawataandamana.

Haya ni tisa kumi ni kwamba kiasi kikubwa cha kodi inayotozwa na TRA inaingia mifukoni mwao haiendi serikalini; sasa serikali inalazimika kurekebishia pengo kwenye biashara za wanyonge ili TRA waendelee kutesa na ukwasi wa kufuru
 
Back
Top Bottom