TRA someni hapa: EFD zenu WIZI MTUPU

TRA someni hapa: EFD zenu WIZI MTUPU

Nashangaa kuona wafanya biashara wanakua wavivu kulipa kodi,huku kodi kubwa ikilipwa na wafanyakazi.kwanza TRA wanasema kwa wale wenye faida kuanzia 14mn kwa mwaka na sio mauzo ya biashara ya mtu,pili haiwezi kuathiri mfumuko wa bei nchini kwasababu EFD haimgusi mzalishaji bali inamgusa msambazaji au mchuuzi(supplier)ambaye hana nguvu katika upangaji wa bei.



Ngoja waanze kulipa kama utakavyo halafu uone kama bei za nguo dukani zitashikika,Muda si mrefu mtajua madhara ya hizi machine.After all sijawahi kuwaamini serikali katika jambo lolote wanalolifanya kwasababu ni wezi na matapeli watupu wamejaa kule.Kwanza waanze kulipa wao viongozi wa serikali kodi ndipo waje kwetu kwa walala hoi,Mbona wao hawalipi?Mimi naona ni sawa tu kwa wafanyabiashara kuzigomea machine za EFD kwanza hata wakilipa hizo kodi hazitatumiwa kwa busara kamwe badala yake Kikwete na genge lake watazitumia pesa za kodi za walala hoi kwenda kuzurula nje ya nchi,Si afadhali wasilipe tu.
 
Usiwe mvivu wa kufikiria kiasi icho bwana mdogo...! ongea point sio kuibuka kama samaki kwenye maji.....! Ukubwa wa mshahara sio kigezo after all hujui unachokipigia kelele, so jikite kwenye point najua izo ndo zenu wa-TZ mlioshindwa ku-base kwenye complaining without getting stuck in seeking the vital solution of the problem.....! Kama mshahara wako ni mdogo basi fight hard one day utaupata mkubwa unaoutazamia.......! Cha msingi itabidi mfike mahali mkubali kuwa ss ivi tuko kwenye transitional era, haliwi mtu apa@Development activist...!

Ukiongeza fine kwa makosa ya traffic unakuwa unaiongezea serikali mapato au unawaongezea Traffic Police wasiokuwa waaminifu?

Nchi hii hakuna uwajibikaji na umakini, pia kuna rundo la kodi mpaka unachanganyikiwa, ukiachana na kodi za TRA bado kuna msururu wa ushuru wa majiji/manispaa/halmashauri
 
mkuu
mbali ya hiyo mashine leseni sasa ni.kuanzia tsh 200,000 hadi 800,000 wanaangalia uwezo wa duka kila mwaka.
_fire kila mwaka 100,000.
~taka sh 24,000kila mwezi.
na hizi zote wamemlenga mwenye duka.
sasa tumechoka kuwa chuma ulete,kesho mgomo unaendelea

Aisee acheni stori zenu, lipeni kodi.Labda hoja yenu iwe bei ya EFD na maintenance cost yote, lakini sio main purpose ya EFD(Na-support EFD Kwa nguvu zote).
 
na wafanyakazi na sisi tugome haiwezekani kila mwezi wanakata kutoka kamshahara kangu laki ngapi sijui afu wafanyabiashara wanazingua. ni chizi tu anaweza kukuamini eti unauza 38,000 TZS faida kwa siku na bado unalipia pango more than a million, ni upuuzi acheni kutudanganya!!!!!! serikali kama mlivyosema asiyetaka arudishe leseni na TIN akalime au kuchunga ng'ombe kijijini kwao!!!!!! au akawe shamba boy kwa kaka yangu mbowe.
 
Haya mambo ya TRA na EFD zao ni WIZI MTUPU. Wanataka mtu mwenye mauzo ghafi ya kuanzia TSh 14,000,000 kwa mwaka anunue hiyo kifaa ambayo bei yake ni kuanzia laki sita na ushee. Twende kimahesabu. Mauzo ya sh 14mil kwa mwaka ni kama wastani wa kuuza sh 38,000 kwa siku. Kwa profit margin ya 10-15% mfanyabiashara kama huyu ana faida ghafi ya kama Tsh 4,000 hivi kwa siku. Akitoa gharama za pango, ulinzi, umeme, usafi, na tukichukulia hana mfanyakazi, huyu mtu faida yake net haizidi 1,000 kwa siku. Watu ambao mmewahi kufanya biashara mnaelewa, mtu mwenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku ni mfanyabiashara MDOGO SANA, wa chini kabisa, ni mtu wa kima cha chini huyu. Mtaji wa kuuza 38,000 kwa siku ni mdogo kuliko hiyo laki sita ya kununulia EFD.

TRA wametumia akili gani kudhani kuwa mtu huyu wa kima cha chini anayechuma chini ya sh 1,000 kwa siku anaweza kununua hiyo EFD ya sh 600,000? Mtu anunue kadude hako kwa bei kubwa kuliko mtaji alionao? Halafu wanashangaa kuona watu wanaandamana! Nyie TRA mnashangaa nini kuhusu maandamano? Hamuwajui wanaoandamana? Ni wafanyabiashara ndogondogo wenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku, eleweni hivyo. Na hawa wako wengi sana, hawahitaji kutumwa na mtu.

Jamani hivi huko TRA mbona mnataka tudhani kuwa wote mlifeli hesabu? Sh laki sita atazipata wapi mtu anayechuma elfu moja kwa siku? Hata akifanya kazi mwaka mzima bila kula, jumla ya kipato chake itakuwa sh 365,000 bado haitoshi kununua EFD. Mtumie akili jamani. Hicho kiwango hakiwezekani kwa wafanyabiashara mnaowalenga.

Cha kufanya. Rejeeni hicho kiwango mrekebishe, muanzie labda kwenye mauzo ghafi ya sh 100,000,000 kwa mwaka (ambayo ni sawa na wastani wa sh 270,000 hivi kwa siku) hawa angalao wangeweza, na nadhani hawalalamiki maana tunaona zikitumika kwenye maduka. Na hawataandamana.

Tanzania watu tumezoea kuishi kwa njia za mkato mkato. Basi kama huwezi kununua hiyo mashine wewe huna sifa ya kuwa mfanyabiashara. tafuta kazi nyingine.
 
mkuu mimi bado sijakuelewa hii laki moja kwanini ilipwe kila mwaka? Inamaana kila mwaka wanakupa fire extinguisher mpya?
Huwa wanaweka madude yao yanayo expire baada ya mwaka mmoja hivyo hata kama haukutumia inatakiwa ununue/ulipie lingine.
 
... Sh laki sita atazipata wapi mtu anayechuma elfu moja kwa siku? Hata akifanya kazi mwaka mzima bila kula, jumla ya kipato chake itakuwa sh 365,000 bado haitoshi kununua EFD. ...
Kama kweli kuna mtu anafanya biashara na kuingiza faida ya sh. 365,000/= kwa mwaka, basi mimi nashauri aache hiyo biashara kwani hailipi, na sio lazima uwe mfanyabiashara, hata kilimo kinalipa! Sio unajiita mfanyabiashara halafu unasumbua mamlaka halali za serikali.

Kama wewe ni mfanyabiashara kweli, nunua EFD kwa kuikopesha TRA, utalipwa ktk kipindi cha mwaka wa kwanza wa fedha kupitia makato ya kodi yako
 
Hapa Arusha ninalipa kila mwaka LAKI MBILI kwa ajili ya kupata FIRE SAFETY CERTIFICATE na kila miezi sita kuna kampuni/wakala wa Fire anakuja kukagua fire extinguishers na nawalipa zaid ya LAKI MOJA.Kumbuka hiyo fire safety certificate inategemea na bishara yako,kuna watu wanalipa mpaka millioni kwa mwaka. Hii nchi kila kitu ni kodi pesa,huu mfumo wa kodi inatakiwa uwe wazi ili kuvutia wafanya biashara wengi kulipa kodi na wajue mwisho wa siku kodi zao zinafanya nini..?? Siyo kusikia deni la taifa linapanda wakati kadi zinalipwa mwanzo mwisho...!!!!

Mimi sioni tatizo, umeambiwa unapofanya manunuzi ya bidhaa zako, ingiza namba ya kumbukumbu ya risiti ulizonunulia kwenye machine unayotumia, ukilipia pango omba risiti na ingiza number ya kumbukumbu kwenye mashine, na gharama nyingine zote. Mwisho wa siku machine itaonyesha gharama ulizoingia, mauzo yako na faida. Tozo la kodi litakuwa katika faida ya mwisho baada ya kukokotoa gharama.

Machine hizi zinakulazimisha ununue bidhaa zako toka vyanzo rasmi na si uchochoroni. Vinginevyo kama umezoea kuuza vitu vya wizi inakuwa imekula kwako.
 
Tanzania watu tumezoea kuishi kwa njia za mkato mkato. Basi kama huwezi kununua hiyo mashine wewe huna sifa ya kuwa mfanyabiashara. tafuta kazi nyingine.

Kweli mkuu, nchi zingine hata ukinunua pipi ya sent hamsini unapata risiti. Mimi nashauri TRA watangaze kuwa, wanunuzi watarudishiwa asilimia hamsini ya VAT kwa manunuzi waliyofanya ili kupromote watu kuomba risit
 
Mkome kuichagua ccm nyie lipa tu kusudi vx ziendelee kuvinjali kwenye mabaa
 
Kinachonishangaza ni tra wanapoangalia ulicholipwa wanachukua aslimia thelathini kama faida halafu wanaichaji kodi ya 30%! Kazi yenyewe unaweza kuwa umepata hasara hata ukiwaonyesha mahesabu hawakubali.
 
Leseni 100.000
Bango 75.000
Taka 180.000
Fire. 200.000
Fire service ya mtungi 40.000
Kodi ya ardhi 88.000
Kodi ya jengo city 80.000
Kodi ya kupanga jengo 300.000
Umeme kwa bei ya sasa 1.200.000
Maji 120.000
Brela 100.000
Bank sarvings charges 140.000
Maji taka 80.000
Ulinzi 1.200.000
Hii ni biashara ya huduma garage .nasina faida ya laki kwa siku ni elfu 40 au 60 sasa hapo ongezea efd na gharama zake za uendeshaji umeme ,karatasi ,na ikikorofisha .hiyo ndio tz .tunaishi kwa mbinu tuu,ni aibu sana .tanzania kuwa na viongozi wasiojuwa wana ongoza watu waaina gani.viongozi wachumia tumbo .shame on them .
 
Mwisho wa siku gharama zote za EFD zitarudishwa kwa mwananchi, Hakuna mfanyabiashara atakaekubali kupata hasara.

Nyie wafanyakazi na vimishahara vyenu mtajikuta mnalia na serikali
 
Subirini mfumuko wa bei utakapo anza mwisho wa siku anaumia mwananchi wa mwisho mlaji

Kwani mkuu, hata hiyo VAT wanayogomea kwani wanalipa wafanyabiashara? Au analipa mlaji?? Elimu inahitajika hapa!
 
Kama kweli kuna mtu anafanya biashara na kuingiza faida ya sh. 365,000/= kwa mwaka, basi mimi nashauri aache hiyo biashara kwani hailipi, na sio lazima uwe mfanyabiashara, hata kilimo kinalipa! Sio unajiita mfanyabiashara halafu unasumbua mamlaka halali za serikali.

Kama wewe ni mfanyabiashara kweli, nunua EFD kwa kuikopesha TRA, utalipwa ktk kipindi cha mwaka wa kwanza wa fedha kupitia makato ya kodi yako

Awache aje kula kwako !? Ndio biashara ya tanzania hiyo .biashara nyingi zipo hivyo .ukiondoa gharama za uindeshaji .ndio faida inazo pata biashari hapa tz .almost all busineess in tz .run in loss kutokana na kipato kidogo kwa wananchi wake .unategemea nini kwa nchi ambayo kipato per gdp ni sh 750.000 kwa mwaka ? Nini nguvu yake l
Kununua mahitaji yake zaidi ya mahindi,maharage,na mchicha
 
Sielewi mkanganyiko uko wapi....

1) Retailers wanunua mizigo ikiwa na 18% tayari... kisha anauza ule mzigo ukiwa na 18% na faida yake, 18% ya faida yake ndio inayokatwa kodi, ile 18% ya mwanzo TRA wataidai kwa wholesaler
2)kama suala ni bei ya mashine hilo linajadilika

Madhara
Kama mie ningekuwa mafanyabiashara basi ninge mtoza mlaji hiyo 18% ya faida yangu, hivyo mlaji ndie atakaye umia

Naomba kusahihishwa kama nakosea
 
Kwani mkuu, hata hiyo VAT wanayogomea kwani wanalipa wafanyabiashara? Au analipa mlaji?? Elimu inahitajika hapa!

Huyo mlaji ni nani kama sio wewe !? Kwa ushabiki unajitoa fahamu .unajila nyama yako mwenyewe .mwenzangu mzimaa kweli wewe !?
 
Back
Top Bottom