Kwa nini wauza simu hawana mashine za EFD?

Kwa nini wauza simu hawana mashine za EFD?

Candela

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2021
Posts
919
Reaction score
2,516
Nimefuatilia kwa muda mrefu na nimeona kuwa hawa watu hawatoi risiti kabisa. Sasa sijajua labda sheria iko hivyo, lakini ukiangalia mauzo yao, wanauza simu moja kwa Sh milioni 3 hadi 5, lakini hawakupi risiti.

Hata ukiomba, wanakuandikia ya mkono na hawana EFD kabisa.

Sasa TRA si walisema kama una mauzo ya Sh 35,000 kwa siku unafaa kuwa na EFD? Kuhusu hawa vipi? Au wao wanalipaje kodi zao?
 
Nimefatilia kwa mda mrefu hawa watu hawatoi risiti kabisa. Sasa sijajua labda ni sheria iko hivyo lakini ukiangalia mauzo yao wanauza simu moja tu milioni 3 mpaka 5 lakini hawakupi risitim na hata ukiomba wanakuandikia ya mkono hawana EFD kabisa.
Sasa TRA si walisema kama una mauzo ya 35000 kwa siku unafaa kuwa na EFD. kuhusu hawa vipi au wao wanalupaje kodi zao.
ni wahuni sana na wengi wanakwepa kutoa EFD receipt kukwepa kodi na pia uuza simu fake na uikosesha serikali mapato na hawajui au wanajua nini utokea wasipotoa EFD receipt ila wanajitoa akili hao na inachangiwa pia na watu kutodai izo risiti na wananchi elimu ya kodi wengi ni hawana hawajui asiyetoa na asiyedai wote wanamakosa.
 
na kutochukua EFD receipt kwa mnunuaji wa bidhaa au huduma ni hatari sana endapo ukiuziwa bidhaa au huduma mbovu unaweza kosa haki kisheria ,pia wabongo tunadai sana uwajibikaji kwa viongozi ila sisi pia hatutaki nchi kuongozwa kwa sheria fuatilia mtandaoni watu wameshawahi kuhukumiwa kwenda jela kisa izo -EFD na sheria zipo wazi google utaziona kuna EFD ACT,INCOME TAX ACT,TAX ADMINISTRATION ,VAT ACT NK
 
ulipe kodi then wale mafisadi? kama unaweza kwepa kulipa kodi KWEPA tu
 
Back
Top Bottom