TRA someni hapa: EFD zenu WIZI MTUPU

TRA someni hapa: EFD zenu WIZI MTUPU

Mfanyakazi hana gharama???au mnazo nyinyi tu??acheni kulialia mlipe kodi

Umeielewa post lakini? Hata katika wafanyakazi kuna kima cha mshahara ambacho hakitozwi kodi. Nimekuambia kuwa mfanyabiashara mwenye mauzo ghafi ya sh 14,000,000 kwa mwaka ni mfanyabiashara mdogo sana kwa sababu mauzo yake kwa siku ni 38,000 (yenye faida ghafi isiyozidi sh 4,000 kabla ya gharama), na mtaji wa kama laki tano hivi. Huyu ni wa kununua EFD ya sh laki sita?
 
Hii nchi bwana, yani anapojitaftia mtu wa hali ya chini serikali nayo ndo inataka ichume hapo. Ss hv tunaumia na shule na umeme, ngoja ifike mda hata panadol hainunuliki sababu ya bei kubwa labda ndo tutaamka kupinga huu unyonyaji. Kama Shida ni ela na serikali ipo kumlinda mwananchi basi wangeanza kwa kupunguza izo posho za laki 2 hadi laki 7 kwa siku bungeni zingepunguza bajeti ya serikali sana tu
 
Ulichosema ni sawa kuwa mwenye mauzo ya kuanzia milioni 14kwa mwaka anatakiwa kuwa na mashine.Ila kwa taarifa yako kwa awamu hii ya pili hicho c kigezo pekee kinachotumika wao TRA walisambaza barua kwa wafanyabiashara 200,000 tz nzima ambao wanatakiwa kutumia mashine hizi awamu ya pili na ni wafanyabiashara wakubwa tu.Sio kweli kama unavyodai kuwa kwa awamu hii hata mwenye mauzo ya 38,000 kwa siku anatakiwa kuwa na mashine,na wengi wanafuata mkumbo tu bila kujua.Na wafanya biashara wa kariakoo wengi wanafanya biashara ki magumashi ndio maana hawataki kusikiaa habari za EFD.Kwani mwanzoni walianza kuwa tatizo ni bei sasa wanadai hata wakipewa bure hawataki!!!!which is which?ila Nashukuru serikali inapokuja na msimamo ambaye hawezi arudishe leseni na TIN.Akafanye shughuri nyingine,uone kama hawatafyata mkia.Kuna ubaya gani serikali kujua mauzo yako?kama hakuna kitu unachoficha kwani ktk kodi mauzo ghafi ndio yataonyesha kiwango cha kodi unachotakiwa kulipa.

Mkuu, hii ni Tanzania. Una uhakika gani kuwa TRA wamewaeleza hawa wasiohusika namna ambavyo inatakiwa iwe? Inawezekana kabisa watendaji wadogo wa TRA wakawa wanawasumbua wasiohusika kwa ukosefu wa mashine ili wapewe rushwa. Siamini kama wafanyabiashara hawa wadogo ni wajinga wafunge biashara zao kama hiyo mashine haiwahusu. Kuna kikubwa zaidi ya hiki.

Kumbuka, OP Tokomeza ilikuwa na umuhimu mkubwa kwa nchi na pia nia na dhumuni lake ilikuwa nzuri tu. Ila kwa Tanzania, ikawa mradi wa watu - kamata ng'ombe lipisha faini, weka mfukoni. Ujangili ukachukua nafasi ya pili baada ya wafugaji. Nina wasiwasi hili zoezi linahujumiwa na wafanyakazi wa TRA wenyewe. Kumbuka kuwa hizi mashine zinakata mrija wa wafanyakazi wa TRA kukisia kodi hivyo chanzo chao kikubwa cha rushwa kitakatika.

Fikiria tena
 
Kinachotakiwa ni elimu kwa mlipa kodi itolewe, mtu aone umuhimu wa kurequest TRA receipt kila anapofanya manunuzi, kwa sababu anaelipa kodi si mfanya biashara anaelipa kodi ni mwananchi ( end user) mfanyabiashara anachofanya ni kukusanya kodi kwa niaba ya TRA kwa kila kitu anachouza, napendekaza pia TRA waje na kodi ya kuwakata wafanyabiashara (Pay e) apa namaanisha baada ya kupeleka kodi walizokusanya kwa niaba ya TRA faida wanayopata wakatwe pay e, mfano mzuri ni kwa mfanyakazi analipa pay e na akinunua kitu kwa mfanya biashara analipa tena VAT, tufike mahali tuone umuhimu wa kulipa kodi tuache siasa.
 
Wafanya biashara acheni usanii bana!
enough is enough. lipeni kodi inayostahili acheni visingizio.
Tembeleeni nchi zilizoendelea mkajifunze.
Tatizo lililopoo ni matumizi mabaya ya kodi zetu lakini kwa hili la mashine kwakweli wafanyabiashara hamna hoja.
 
Ulichosema ni sawa kuwa mwenye mauzo ya kuanzia milioni 14kwa mwaka anatakiwa kuwa na mashine.Ila kwa taarifa yako kwa awamu hii ya pili hicho c kigezo pekee kinachotumika wao TRA walisambaza barua kwa wafanyabiashara 200,000 tz nzima ambao wanatakiwa kutumia mashine hizi awamu ya pili na ni wafanyabiashara wakubwa tu.Sio kweli kama unavyodai kuwa kwa awamu hii hata mwenye mauzo ya 38,000 kwa siku anatakiwa kuwa na mashine,na wengi wanafuata mkumbo tu bila kujua.Na wafanya biashara wa kariakoo wengi wanafanya biashara ki magumashi ndio maana hawataki kusikiaa habari za EFD.Kwani mwanzoni walianza kuwa tatizo ni bei sasa wanadai hata wakipewa bure hawataki!!!!which is which?ila Nashukuru serikali inapokuja na msimamo ambaye hawezi arudishe leseni na TIN.Akafanye shughuri nyingine,uone kama hawatafyata mkia.Kuna ubaya gani serikali kujua mauzo yako?kama hakuna kitu unachoficha kwani ktk kodi mauzo ghafi ndio yataonyesha kiwango cha kodi unachotakiwa kulipa.

Si kweli. Mimi niko Arusha nimeajiriwa lakini nilikuwa na kiosk fulani cha kuongezea japo mboga. Tukienda kazini asubuhi housegirl anabaki anashinda pale anauza mishumaa, mikate, sabuni za kuogea nk kwa majirani. Mauzo kwa siku ni kati ya 10,000 na 60,000, haijawahi kuzidi hapo. Cha kushangaza TRA waliniletea notice ya hicho EFD na matisho kibao. Mtaji wangu pale ndani ni laki saba na pango nalipa laki moja, jumla laki nane, eti ninunue kifaa cha laki sita, inawezekanaje?

TRA wametumia akili gani kujumuisha mtaji wangu wa laki nane kuwa miongoni mwa hao "wafanyabiashara" 200,000 nchi nzima wakati mimi naganga njaa tu pale? Yaani katika watu laki mbili wenye biashara za maana nchi hii, hata wa mtaji wa laki nane yumo? Huu ni wizi.

Anyway, nimefunga kile kiosk. Lakini bado kuna wakala wao huwa ananipigia simu kunikumbusha kuhusu hicho kidubwasha. Majuzi alinichefua almanusura nimtukane.

Natahadharisha tu kuwa hii kitu itaturudisha kwenye ule utamaduni wa magendo ambao ulikuwa unaelekea kwisha. Vitu vitauzwa kwa "mlango wa uani" na kazi ya TRA itakuwa ngumu zaidi. Kama kweli nia ni serikali kujua mauzo, igawe hivyo vidubwasha bure kwa wale wafanyabiashara wa kima cha chini. Hao wenye mauzo makubwa wanunue, kwanza nadhani wangependa kuwa navyo vya quality kubwa kama biashara zao. Lakini hii ya kumtaka mfanyabiashara mdogo anayeganga njaa anunue kitu ya laki sita, bei kubwa kuliko mtaji wake, ni WIZI MTUPU.
 
Utayari wa mwananchi kulipa kodi unategemea na hiyo kodi inamnufaishaje huyo mwananchi, nchi za wenzetu hasa Scandinavian countries watu wanapenda kulipa kodi tena hajisikii vizuri kutokulipa kodi.....! Lkn sisi hata hiyo kodi inayokusanywa ni magumashi tupu..! Mfanyabiashara hata kama awe anapata pesa kubwa kiasi gani inauma sana yeye ka-fight kuitafuta wengine wanaigawana tu kiurahic rahic tena kwa manufaa yao binafic...! washikaji wanag'aa tu kwenye suti kali na mashangingi, mfanyabiashara yeye suti hata ya mtumba hana..! Washikaji tunawafadhili kwenda mijengoni i.e bungeni kupeana mipasho kama waimba taarab..! wengine kusinzia wanapata millions of shs..!n.k. Chamsingi viongozi wanatakiwa wajue kuwa wanchi wameamka haliwi mtu apa. Aidha, nawasapoti wafanyabiashara coz mm nimefanya kazi TRA najua uchafu wote uliko hasa ktk hizi EFDs. EFD-phase I ilihusisha wafanyabiashara wenye mauzo kuanzia 40mil. ambao hawa ndo ma-VAT agents na sio VAT-payers, EFD-phase II inawahusisha wafanyabishara hadi wale wenye mauzo kuanzia 14mil. ila hawa hawahusiki na VAT-agency, point apa ni kurahisisha kujua annual turnover/ mauzo yao kwa mwaka ili walipe Income tax stahili..! coz ukitumia EFD machines mauzo yako yanakuwa recorded kwenye system moja kwa moja ambayo ni EFDMS. Chanzo cha uozo ni pale walivozileta hizi EFD wahusika(yaani wauzaji wa EFDs) wakishirikiana na watu wa TRA walikuwa na mpango wa kuhujumu uchumi kwa kuwauzia wafanyabiashara izi machine kwa bei kuuuuubwa ili na wao wa take advantage on it....!! mbaya zaidi serikali sio kwamba haijui huu utumbo ulikuwa ukifanyika, inajua lkn No-comment! Tz ni chukua chako mapema usepe. Ndo maana izi machine for the first time zilivokuwa zikija zilikuwa na bei kuuubwa kama millions 2+, uone kuwa huu ni wizi hizi za EFD-phase II nazo zilikuwa zinauzwa kwenye Million 1+ baada ya makerere ya wafanyabiashara ndo wameshusha mpaka kwenye hiyo laki 6....! Wizi mtupu@Development activist
 
Haya mambo ya TRA na EFD zao ni WIZI MTUPU. Wanataka mtu mwenye mauzo ghafi ya kuanzia TSh 14,000,000 kwa mwaka anunue hiyo kifaa ambayo bei yake ni kuanzia laki sita na ushee. Twende kimahesabu. Mauzo ya sh 14mil kwa mwaka ni kama wastani wa kuuza sh 38,000 kwa siku. Kwa profit margin ya 10-15% mfanyabiashara kama huyu ana faida ghafi ya kama Tsh 4,000 hivi kwa siku. Akitoa gharama za pango, ulinzi, umeme, usafi, na tukichukulia hana mfanyakazi, huyu mtu faida yake net haizidi 1,000 kwa siku. Watu ambao mmewahi kufanya biashara mnaelewa, mtu mwenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku ni mfanyabiashara MDOGO SANA, wa chini kabisa, ni mtu wa kima cha chini huyu. Mtaji wa kuuza 38,000 kwa siku ni mdogo kuliko hiyo laki sita ya kununulia EFD.

TRA wametumia akili gani kudhani kuwa mtu huyu wa kima cha chini anayechuma chini ya sh 1,000 kwa siku anaweza kununua hiyo EFD ya sh 600,000? Mtu anunue kadude hako kwa bei kubwa kuliko mtaji alionao? Halafu wanashangaa kuona watu wanaandamana! Nyie TRA mnashangaa nini kuhusu maandamano? Hamuwajui wanaoandamana? Ni wafanyabiashara ndogondogo wenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku, eleweni hivyo. Na hawa wako wengi sana, hawahitaji kutumwa na mtu.

Jamani hivi huko TRA mbona mnataka tudhani kuwa wote mlifeli hesabu? Sh laki sita atazipata wapi mtu anayechuma elfu moja kwa siku? Hata akifanya kazi mwaka mzima bila kula, jumla ya kipato chake itakuwa sh 365,000 bado haitoshi kununua EFD. Mtumie akili jamani. Hicho kiwango hakiwezekani kwa wafanyabiashara mnaowalenga.

Cha kufanya. Rejeeni hicho kiwango mrekebishe, muanzie labda kwenye mauzo ghafi ya sh 100,000,000 kwa mwaka (ambayo ni sawa na wastani wa sh 270,000 hivi kwa siku) hawa angalao wangeweza, na nadhani hawalalamiki maana tunaona zikitumika kwenye maduka. Na hawataandamana.

Kama hakuna faida si muache kufanya, mnang'ang'ania biashara ya nini. Mbona min supermarket nyngi tu wanatumia machine hizi na hawajalalamika?
 
Utayari wa mwananchi kulipa kodi unategemea na hiyo kodi inamnufaishaje huyo mwananchi, nchi za wenzetu hasa Scandinavian countries watu wanapenda kulipa kodi tena hajisikii vizuri kutokulipa kodi.....! Lkn sisi hata hiyo kodi inayokusanywa ni magumashi tupu..! Mfanyabiashara hata kama awe anapata pesa kubwa kiasi gani inauma sana yeye ka-fight kuitafuta wengine wanaigawana tu kiurahic rahic tena kwa manufaa yao binafic...! washikaji wanag'aa tu kwenye suti kali na mashangingi, mfanyabiashara yeye suti hata ya mtumba hana..! Washikaji tunawafadhili kwenda mijengoni i.e bungeni kupeana mipasho kama waimba taarab..! wengine kusinzia wanapata millions of shs..!n.k. Chamsingi viongozi wanatakiwa wajue kuwa wanchi wameamka haliwi mtu apa. Aidha, nawasapoti wafanyabiashara coz mm nimefanya kazi TRA najua uchafu wote uliko hasa ktk hizi EFDs. EFD-phase I ilihusisha wafanyabiashara wenye mauzo kuanzia 40mil. ambao hawa ndo ma-VAT agents na sio VAT-payers, EFD-phase II inawahusisha wafanyabishara hadi wale wenye mauzo kuanzia 14mil. ila hawa hawahusiki na VAT-agency, point apa ni kurahisisha kujua annual turnover/ mauzo yao kwa mwaka ili walipe Income tax stahili..! coz ukitumia EFD machines mauzo yako yanakuwa recorded kwenye system moja kwa moja ambayo ni EFDMS. Chanzo cha uozo ni pale walivozileta hizi EFD wahusika(yaani wauzaji wa EFDs) wakishirikiana na watu wa TRA walikuwa na mpango wa kuhujumu uchumi kwa kuwauzia wafanyabiashara izi machine kwa bei kuuuuubwa ili na wao wa take advantage on it....!! mbaya zaidi serikali sio kwamba haijui huu utumbo ulikuwa ukifanyika, inajua lkn No-comment! Tz ni chukua chako mapema usepe. Ndo maana izi machine for the first time zilivokuwa zikija zilikuwa na bei kuuubwa kama millions 2+, uone kuwa huu ni wizi hizi za EFD-phase II nazo zilikuwa zinauzwa kwenye Million 1+ baada ya makerere ya wafanyabiashara ndo wameshusha mpaka kwenye hiyo laki 6....! Wizi mtupu@Development activist.
 
Wahuni nyie, na wezi wakubwa na sisi wafanyakazi

Wewe ni mfanyakazi wa wapi? Basi unalipwa mshahara mkubwa sana mwenzetu, vinginevyo nawe pia mwizi tu. Mimi ni mfanyakazi pia, mshahara hautoshi kwahiyo najitahidi kuongezea na biashara ndogo, kwahiyo tatizo nalielewa.

Wewe mwenzetu mwenye mshahara mkubwa kaa pembeni wadogo tuongee shida zetu. Maana wewe utakuwa miongoni mwa mafisadi tu wanyonyaji wakubwa.
 
Mbona mnamiliki simu za laki 8?

Wewe ndio unamiliki simu ya laki nane. Nazungumzia wafanyabiashara wadogo hapa sizungumzii wamiliki wa simu. Hata hivyo simu ni starehe ya mtu, siyo mtaji. Wewe mbona unalewa pombe na kuhonga mademu nani anakuuliza?
 
Usiwe mvivu wa kufikiria kiasi icho bwana mdogo...! ongea point sio kuibuka kama samaki kwenye maji.....! Ukubwa wa mshahara sio kigezo after all hujui unachokipigia kelele, so jikite kwenye point najua izo ndo zenu wa-TZ mlioshindwa ku-base kwenye complaining without getting stuck in seeking the vital solution of the problem.....! Kama mshahara wako ni mdogo basi fight hard one day utaupata mkubwa unaoutazamia.......! Cha msingi itabidi mfike mahali mkubali kuwa ss ivi tuko kwenye transitional era, haliwi mtu apa@Development activist...!
 
Kama hakuna faida si muache kufanya, mnang'ang'ania biashara ya nini. Mbona min supermarket nyngi tu wanatumia machine hizi na hawajalalamika?

Post hujaielewa. Mauzo ghafi kwenye minisupermarket ni sh ngapi kwa siku? Unadhani ni sh 38,000?
 
Kuwabebesha wafanya biashara kodi kubwa ni kama kuchezesha bahati nasibu bila kuahidi jackpot. Mwisho wa siku hakuna atakayecheza bahati nasibu na serikali itakosa mapato kabisa.

Mkuu Dingswayo, Mimi kimsingi sioni tatizo katika kulipa kodi iwapo Kodi hii ingekuwa inatumika na kuleta tija ya kweli na mabadiliko katika Maisha ya watu. Siyo wafanya biashara tu wanaolipa Kodi. Walipa kodi wakubwa katika nchi hii ni wafanyakazi na waajiriwa katika sekta za umma na binafsi licha ya kwamba TRA hata kwenye mikutano ya walipa Kodi wakubwa nachelea kusema kuwa hawaalikwi wala kutambuliwa.

Hoja ya msingi ni kwamba watu walipe kodi na kodi itumike kufanya kazi za maendeleo kwasasa kinachokera ni pale unapokuta unaongozwa na Rais asiyelipa Kodi kutoka katika mapato yake, Waziri Mkuu anayelipwa mamilioni asiyelipa Kodi,Wabunge wanaowashauri wafanyabiashara kuwa wazalendo na kulipa Kodi wakati wao wanapokea malaki ya maposho lakini bado hawalipi Kodi.

Makampuni makubwa ya wawekezaji kutoka nje hayalipi Kodi lakini ajabu TRA kujitutumua kuwakamua wananchi wanao jaribu kuinuka ambao hutozwa lundo la kodi na gharama kwa malaki za leseni kwa kila Mwaka .Cha ajabu fedha hizi zinatumika kwa kutapanywa na watawala kwa safari ,posho na semina zisizo na vichwa wala Miguu .Tusiwalazimishe watu kulipa Kodi kwa kutumia vitisho tuwaaibishe kwa kuwaonesha huduma bora za msingi kwa binadamu kama Elimu,Afya,Maji,Miundombinu,wanazopata na kuzifaidi kama uthibitisho wa uadilifu wa watawala katika matumizi ya Kodi na kuwakumbusha kwamba wasipolipa kodi huduma hizo zitazorota.

Kutokana na kundi hili linalopata mamilioni ya fedha kwa mwezi kutokulipa Kodi mzigo mkubwa wa kulipa kodi unabebwa na waajiriwa ambao ni rahisi kuwakandamiza kupitia PAYEE na wafanya biashara kupitia viongozi wa mkoa na wilaya. Hapa ndipo kulazimishana matumizi lakini kimsingi tunachotakiwa ni kujenga tabia ya kupenda kulipa Kodi na hili lianze na Ikulu kwanza Mheshimiwa Rais atangaze kwamba kuanzia sasa atalipa kodi,Waziri Mkuu afuate na wengine wafuate nadhani migomo hii itaisha.

VINGINEVYO ITAKUWA YALEYALE YAFUATA NINAYOSEMA USIFUATE NINAYO TENDA HAPANA WAKUU LAZIMA WOTE TUWAJIBIKE.
 
Kama hakuna faida si muache kufanya, mnang'ang'ania biashara ya nini. Mbona min supermarket nyngi tu wanatumia machine hizi na hawajalalamika?

Okay, mimi nimeacha. Umefurahi sasa? Na TRA imepata nini?
 
kila mwaka watakuwa wanafanya ukaguzi wa mtungi na kukupa certificate.
kumbuka mtungi unanunua na auhusiani na laki moja.
na wanasema hiyo sheria imepitishwa na halmashauri ya jiji la mwanza ambayo na wenje yumo
Hapa Arusha ninalipa kila mwaka LAKI MBILI kwa ajili ya kupata FIRE SAFETY CERTIFICATE na kila miezi sita kuna kampuni/wakala wa Fire anakuja kukagua fire extinguishers na nawalipa zaid ya LAKI MOJA.Kumbuka hiyo fire safety certificate inategemea na bishara yako,kuna watu wanalipa mpaka millioni kwa mwaka. Hii nchi kila kitu ni kodi pesa,huu mfumo wa kodi inatakiwa uwe wazi ili kuvutia wafanya biashara wengi kulipa kodi na wajue mwisho wa siku kodi zao zinafanya nini..?? Siyo kusikia deni la taifa linapanda wakati kadi zinalipwa mwanzo mwisho...!!!!
 
wafanya biashara acheni kuiibia serikali mapato, mkiiba nyie poa, mkibanwa mnaanza kulialia, imefikia wakati muacha kuwa waibaji wa huduma za wananchi na kujifunza utamaduni wa kulipa kodi...mataifa makubwa yameendelea kwa kuwa na utaratibu mzuri wa makusanyo ya kodi katika shughuli za ndani na nje, mkikosa huduma bora mnaaza kutoa ulalamishi wa serikali, hatuwezi endelea kwa utaratibu huu wa kukwepa majukumu yetu kama raia kulipa kodi, hakuna serikali inayoendeshwa bila kodi...hata wakija hao machadema hawatafanya muujiza wowote ule bil amakisanyo ya kodi..sio lazima upata faida kubwa sana kwa mara moja, tuwe wazalendo tulipe kodi
 
Subirini mfumuko wa bei utakapo anza mwisho wa siku anaumia mwananchi wa mwisho mlaji
Kwa sisi tulivyo tutanunua tu, kila siku bei zinapanda umesikia hata mara moja tukiandamana kwamba hatuwezi,. hii ndio bongo bro, acha walipe kodi kama tunavyolipa sisi wengine
 
Back
Top Bottom