Setuba Noel
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 426
- 210
- Thread starter
- #121
Usipanic mkuu haya mambo sio unakurupuka kama mfuasi wa kibwetere.Relax
Kumbe unajijua ni mfuasi wa kibwetere. Sasa unafanya nini hapa wenzio washajichoma moto huko.
Usipanic mkuu haya mambo sio unakurupuka kama mfuasi wa kibwetere.Relax
Subirini mfumuko wa bei utakapo anza mwisho wa siku anaumia mwananchi wa mwisho mlaji
mkuu
mbali ya hiyo mashine leseni sasa ni.kuanzia tsh 200,000 hadi 800,000 wanaangalia uwezo wa duka kila mwaka.
_fire kila mwaka 100,000.
~taka sh 24,000kila mwezi.
na hizi zote wamemlenga mwenye duka.
sasa tumechoka kuwa chuma ulete,kesho mgomo unaendelea
Setuba Noel Mfanyakazi hana gharama? Au mnazo nyinyi tu?
Acheni kulialia mlipe kodi
Acheni visingizio, tulipe kodi. Tumeshavuna sana kwenye biashara pasipo kulipa kodi halali ya serikali. Tuache visingizio na vijihesabu vya uongo.
Naona Mku wangu unakazana kujikita na revenue floor iliyotolewa na TRA kama ndio bas yako! Kimahesabu upo sawa lakini practically hao wanaouza sh. 38,000/- wala bado hawajaguswa! Wanaofanya biashara ya mapato ghafi ya sh. 38,000/= kwa siku wengi wao kama sio wote ni wale wenye viduka vidogovidogo huku uswahilini tena mitaa ya ndani! Hao wa sh.38,000/ kwa siku ni wale wanaouza mafuta ya taa na ya kula kwa vipimo vya shilingi mia mia....hawa ni wale wanaouza majani ya chai ya shilingi 50/-, hawa ni wale wanaouza sukari au bidhaa zingine hata kwa robo kilo...hawa ni wale mtu unafika dukani, unalazimika kutoa mia mfukoni kugonga nondo ili mwenyewe aliyekaa sebuleni akusikie na kuja kukupa huduma!! In short, ni wale ambao viduka vyake ni vile ambavyo mteja anasimama dirishani na ni MARUFUKU kuingia ndani!!!! Hawa ndio hao wanaofanya mauzo ya sh.38,000/-na wala sio wale wanaogoma! And in fact, hata hawa nao wanauza zaidi ya hiyo....waht does it take? Maharage 10kg@2000+Unga 15kg@1000+Mchele 10kg@1500=50,000/- per day....hatujataja sigara, viberiti, mafuta ya taa, mafuta ya kula ya mia mia, majani ya chai ya hamsini hamsini and so much more!
Tatizo kubwa na la msing hapa ni zaidi ya Machine za EFD ni mfumo mzima wa kodi... Wafanyabiashara wana madai zaidi ya machine za EFD ambazo kwa sababu za makusudi serikali chini ya TRA ndio inachokishililia.. IKUMBUKWE Wafanyabiashara hawa ni walipa kodi wazuri wa kodi zao walizokuwa wanakadiliwa.kodi kubwa ipi??kinachogomba hapa ni kuwa wafanyabiashara hawataki mauzo yao ghafi yajulikane,ili walipe kodi stahiki.kwani kuna wafanya biashara kama 16,000 hivi wanazitumia mashine hizi toka mwaka 2010!hii awamu ya pili inayo walazimisha wengine 200,000 watumie machine ndio inakuwa nongwa???hapa serikali lazima ishinde tu na ndio maana wamesema ambaye hataki arudishe leseni ya biadhara afanye shughuri nyingine.Hata wakati VAT inaanza ilikuwa hivi hivi.Na kwa taarifa yako wafanya biadhara wengi hususani kariakoo wanalipa kodi ya mapato kwa makadillio ya mauzo yao hawataki kusikia kitu kiitwacho VAT,wanacho fanya ni kipunguza kiasi cha mauzo kwa mwaka.ila kwa mashine ya EFD hawataweza tena kuficha kiasi cha mauzo na moja kwa moja watakuwa na sifa za kusajiliwa kwenye ongezeko la thamani (VAT) ndio mziki hapo.Haka kwa akili ndogo tu pale kariakoo mtu analipia kodi ya pango milioni moja kwa mwezi ila kodi ya mapato analipa laki 5 kwa mwaka!!!!
FaizaFoxy nishakushtukia...isije na wewe una kaduka pale mitaa ya Kariakoo lakini kutokana na mahaba uliyonayo kwa serikali yako tukufu ndo unataka kusingizia kwamba kuna "rafiki yako hapo unaongea nae!!" Acheni ujanja ujanja...tumieni EFDs tupate kodi yetu! Huo umeme umekatika lini; jana? EFDs si kama Desk Top PC, kwamba ukikatika umeme ndo basi tena...ina maana hiyo ya shoga'ako haitunzi chaji??!! Wengine ukienda dukani huwa hawatoi risiti kwa kusingizia network wakati suala la kutoa risiti wala halina uhusiano na network!
mi ni mfanyakazi lakini nawasapoti wafanyabiashara.hata wakinunua hizo mashine bado mzigo ni kwetu sisi walaji.kama ujuavyo biashara za bongo ni maelewano.hatujafika hatua ya kuwa na fixed price.nguo ya elf 40 utainunua kwa 15000.just imagine wauza mitumba wa karume au mchikichini wawe na efds unategemea walalahoi tutavaa?.suruali ya ekf 10 utainunua kwa elf 25.ile ya dukani ya elf30 utainunua kwa 50.mshahara wenyewe laki 4 utaweza kuishi?usiwe na myopic minded.kabla ya kuropoka uwe unafikiria matokei ya kitu kwa mapana yake.sio tu ushabikie wafanyabiashara kulipa kodi bila kujua position yako itakuwaje kama mlaji katika mzunguko wa kibiashara.
kwa wafanyabiashara kulipa kodi ni sawa kabisa kakini kuwepo na utaratibu ambao hautaleta madhara kwaa end user.bei ya umeme imepanda maji nayo yamepanda kutoka50 kwa ndoo moja hadi 100 tsh.kwa uelewa wako mdogo hapo muathirika ni nani?unadhani ni tanesco au serikali?acha ushabiki usiokuwa na tija kijana
[COLOR
- Kwanza ni BEI ya machine ulikinganisha na BEI ya soko ya machine husika kwa soko la sehemu nyingine duniani.. kenya tu mashine zinapatikana kwa chininya TZS 350,000. ukienda china na kwingineko ni chini ya $80.
A town
Hivi vimashine navichukia kwanza siyo imara network inasumbua ni majanga tu.
Ngoja nikuulize...yaani unaamini kweli nguo ya sh. 40,000/- huwa unanunua kwa sh. 15,000/-? Unadhani wafanyabiashara ni wapumbavu kiasi hicho? Hiyo nguo since then anafahamu bei yake ni sh. 10,000/- lakini kv mnapenda kuombea; ndo atakuambia 40,000/- na akikuuzia kwa elf 15 unajiona mjanja kumbe umeliwa elfu 5....so, elfu tano yako amekula na kodi halipi vilevile...mkilipwa mishahara midogo mnalalamika wakati mnatetea watu wasilipe kodi!mi ni mfanyakazi lakini nawasapoti wafanyabiashara.hata wakinunua hizo mashine bado mzigo ni kwetu sisi walaji.kama ujuavyo biashara za bongo ni maelewano.hatujafika hatua ya kuwa na fixed price.nguo ya elf 40 utainunua kwa 15000.just imagine wauza mitumba wa karume au mchikichini wawe na efds unategemea walalahoi tutavaa?.suruali ya ekf 10 utainunua kwa elf 25.ile ya dukani ya elf30 utainunua kwa 50.mshahara wenyewe laki 4 utaweza kuishi?usiwe na myopic minded.kabla ya kuropoka uwe unafikiria matokei ya kitu kwa mapana yake.sio tu ushabikie wafanyabiashara kulipa kodi bila kujua position yako itakuwaje kama mlaji katika mzunguko wa kibiashara.
kwa wafanyabiashara kulipa kodi ni sawa kabisa kakini kuwepo na utaratibu ambao hautaleta madhara kwaa end user.bei ya umeme imepanda maji nayo yamepanda kutoka50 kwa ndoo moja hadi 100 tsh.kwa uelewa wako mdogo hapo muathirika ni nani?unadhani ni tanesco au serikali?acha ushabiki usiokuwa na tija kijana
Aah Wapi! Ukijitolea wenzio wanajitwalia.Kulipa kodi nikitendo cha uzalendo
Umejaa matusi na kejeli lakini nimegundua jambo moja kuhusu wewe! Unajifanya kujua kumbe ni boya tu hujui lolote!!Versity ya wapi umesoma wewe? Hivi siku hizi huko wanapokea hadi division five kumbe? Wewe kwa mawazo yako nikinunua bidhaa kwa 34,000 nikaziuza kwa 38,000 kumbe nimepata 38,000 mapato ghafi? Na mtaji uko wapi? Kama ni kweli wewe umesoma hizo economics unazosema basi kumbe ndio maan nchi hii haiendelei!
rudi shule ukajifunze....sijui unapata wapi mambo ya ajabu kama haya!! Kama kweli unafanya biashara utakuwa unafanya biashara ya sidiria wewe!! Yaani kama mtu amenunua mchele gunia 10 kwa sh. 100,000/- kisha akauza kwa sh. 150,000/-, hapo sh. 50,000/- ndo gross income!!! omg! this's might be one of the monthly joke.Sasa nikufundishe na economics zako za feki. Mapato ghafi ni kile kinachobakia ukishatoa bei ya kununulia bidhaa uliyouza.
Kama gharama zipi?Mapato halisi yanakuja utakapotoa gharama nyingine za biashara.
Ndo maana nikasema we kilaza? Kwani mie nimesemaje? Au hufahamu kwamba mapato ghafi na Gross Income ni kitu kile kile?Huyo anayelipwa mshahara wa sh 6,000 kwa siku hiyo ndiyo mapato ghafi
Pamoja na kwamba umejaa matusi na kashifa lakini kila unachoandika kinadhihirisha tu usakala na ukilaza wako! Nimekuambia mfanyakazi ana gross income ya sh.6000 kwa siku (180,000 kwa mwezi)...gross income ni mapato ghafi...hapo hajakatwa PAYE, hajalipa nauli, n.k...na zile cost zinazokuwa associated na kazi yake. Na ndio maana nikakuambia, ukishatoa gharama zote hizo; unakuta anabaki na negative balance na ndio maana wengi wao kama sio wote mshahara unakuwa umeisha tarehe 27 ya mwezi ule ule aliopokea; implying kwamba tayari ana-operate under negative balance...kwahiyo kwa akili yako unadhani huyo anayebaki na negative balance anabaki na pesa nyingi sio?akitoa gharama za kuihudumia hiyo ajira (usafiri, mlo wa mchana nk) anabaki na mapato halisi. Aliyeuza mali ya 38,000 kutoka manunuzi ya 34,000 mapato yake ghafi ni sh 4,000, nako pia akitoa gharama za kuhudumia biashara yake (nauli, pango, ulinzi, usafi, umeme nk) anabaki na mapato halisi. Yupi mwenye mapato halisi kubwa hapa boss mchumi? Hapa pia unahitaji hesabu za "versity"?
Wewe hufahamu nini maana ya mapato ghafi....rudi darasani ukajifunze!Kwahiyo mheshimiwa wa hesabu za "versity", mapato ghafi ya sh 4,000 kwa siku na yale ya sh 6,000 kwa siku yapi makubwa boss mchumi? Hesabu zako na economics za "versity" zikasema sh 4,000 ndiyo kubwa (umeichanganya kwenye mtaji ikawa 38,000! kwahiyo unataka huyu ndugu ale mtaji wake kwa kujidanganya ana mapato makubwa kuliko huyo wa 6,000, na kesho atazungusha mtaji upi?)
Ndo tatizo la vilaza...hawafahamu kwamba ni vilaza! Jielimishe mambo yafuatayo...gross income, net income, gross profit, net profit! Hapa unachanganya mamboHili janga la division five sikujua kama limeenea hadi "versity"!