REAL PEOPLE
Member
- Sep 28, 2012
- 11
- 2
Kariakoo uwezo wao ni mkubwa tu wakuweza kununua EFD pango milioni mashine 600,000/= halafu wanasema hawewezi waache uongo,patola shs 38,000/= utawezeje kupanga chumba cha milioni?
Yule mfanyakazi anayelipa PAYE wakati anapokea Sh. 180,000/- mapato yake kwa siku ni Sh.6000; yaani umemzidi zaidi ya mara sita! Huyu nae anakatwa kabla hajalipa pango, mfanyakazi, maji, umeme n.k! Wakati wewe ukilipa hivyo vitu unabaki na angalau sh.1000 kwa siku, mwenzako anabaki na Negative Income na ndio maana, mshahara wanalipwa tarehe 25, lakini inapofika tarehe 26 or 27 of the same month, anabaki hana kitu.Haya mambo ya TRA na EFD zao ni WIZI MTUPU. Wanataka mtu mwenye mauzo ghafi ya kuanzia TSh 14,000,000 kwa mwaka anunue hiyo kifaa ambayo bei yake ni kuanzia laki sita na ushee. Twende kimahesabu. Mauzo ya sh 14mil kwa mwaka ni kama wastani wa kuuza sh 38,000 kwa siku. Kwa profit margin ya 10-15% mfanyabiashara kama huyu ana faida ghafi ya kama Tsh 4,000 hivi kwa siku. Akitoa gharama za pango, ulinzi, umeme, usafi, na tukichukulia hana mfanyakazi, huyu mtu faida yake net haizidi 1,000 kwa siku. Watu ambao mmewahi kufanya biashara mnaelewa, mtu mwenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku ni mfanyabiashara MDOGO SANA, wa chini kabisa, ni mtu wa kima cha chini huyu. Mtaji wa kuuza 38,000 kwa siku ni mdogo kuliko hiyo laki sita ya kununulia EFD.
TRA wametumia akili gani kudhani kuwa mtu huyu wa kima cha chini anayechuma chini ya sh 1,000 kwa siku anaweza kununua hiyo EFD ya sh 600,000? Mtu anunue kadude hako kwa bei kubwa kuliko mtaji alionao? Halafu wanashangaa kuona watu wanaandamana! Nyie TRA mnashangaa nini kuhusu maandamano? Hamuwajui wanaoandamana? Ni wafanyabiashara ndogondogo wenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku, eleweni hivyo. Na hawa wako wengi sana, hawahitaji kutumwa na mtu.
cdm mza bure kabisa wametia lami barabara ya kwenda malaika hotel na kuacha barabara ya buswelu na kiseke inayotumiwa na wapiga kura wao.
Wanafahamu sana hilo, sema tatizo ni kwamba bila EFD; tukiwapa kodi zetu wapeleke TRA, wanakula wenyewe, lakini with EFDs, wanafahamu ni lazima watazipeleka tu...in sort, hawa jamaa ni kwamba zamani waliazimwa suruali lakini kuirudisha kwa mwenyewe hawataki!Hizo kodi zote zinalipwa na mlaji,mfanyabiashara ni mkusanyaji tu,waache uongo lipeni kodi kwa manufaa ya taifa
Kama kweli kuna mtu anafanya biashara na kuingiza faida ya sh. 365,000/= kwa mwaka, basi mimi nashauri aache hiyo biashara kwani hailipi, na sio lazima uwe mfanyabiashara, hata kilimo kinalipa! Sio unajiita mfanyabiashara halafu unasumbua mamlaka halali za serikali.
Kama wewe ni mfanyabiashara kweli, nunua EFD kwa kuikopesha TRA, utalipwa ktk kipindi cha mwaka wa kwanza wa fedha kupitia makato ya kodi yako
Tanzania watu tumezoea kuishi kwa njia za mkato mkato. Basi kama huwezi kununua hiyo mashine wewe huna sifa ya kuwa mfanyabiashara. tafuta kazi nyingine.
Wanafahamu sana hilo, sema tatizo ni kwamba bila EFD; tukiwapa kodi zetu wapeleke TRA, wanakula wenyewe, lakini with EFDs, wanafahamu ni lazima watazipeleka tu...in sort, hawa jamaa ni kwamba zamani waliazimwa suruali lakini kuirudisha kwa mwenyewe hawataki!
Nashangaa kuona wafanya biashara wanakua wavivu kulipa kodi,huku kodi kubwa ikilipwa na wafanyakazi.kwanza TRA wanasema kwa wale wenye faida kuanzia 14mn kwa mwaka na sio mauzo ya biashara ya mtu,pili haiwezi kuathiri mfumuko wa bei nchini kwasababu EFD haimgusi mzalishaji bali inamgusa msambazaji au mchuuzi(supplier)ambaye hana nguvu katika upangaji wa bei.
Naona hesabu zinakupiga chenga mbaya, labda ndiyo maana hufanyi biashara! Unaelewa maana ya mauzo ghafi? Hiyo sh 38,000 kwa siku ni mauzo siyo faida. Hebu jaribu biashara japo kidogo ujifunze. Mtu anapouza vitu vya sh 38,000 anakuwa amevinunua kwa sh 34,000 hivi, kwa hiyo faida ghafi hapo ni 4,000 (zaidi kidogo ya 10%).Na mtu wa namn hii mtaji wake hauzidi laki tano, kumbuka hela inazungushwa, siyo kwamba hizo milioni 14 unazosikia eti wanazo, hii ni kujumlisha tu mauzo ya kila siku ikifika mwisho wa mwaka hesabu inasomeka mil 14 lakini hela iliyokuwa inazunguka ni laki tano tu. Mtu mwenye mapato ya 4,000 kwa siku naamini sote tunakubaliana haya ni mapato ya kima cha chini.na wafanyakazi na sisi tugome haiwezekani kila mwezi wanakata kutoka kamshahara kangu laki ngapi sijui afu wafanyabiashara wanazingua. ni chizi tu anaweza kukuamini eti unauza 38,000 TZS faida kwa siku na bado unalipia pango more than a million, ni upuuzi acheni kutudanganya!!!!!! serikali kama mlivyosema asiyetaka arudishe leseni na TIN akalime au kuchunga ng'ombe kijijini kwao!!!!!! au akawe shamba boy kwa kaka yangu mbowe.
The way ulivyoongea utafikiri kufanya biashara ni very exceptional stuff like kumfanyia mtu upasuaji!!! Unauliza kama nimewahi kumpandishia bei mteja; kwani mie nimesema suala la kupandisha bei hapa? Ina maana face price ni kumpandishia mteja bei? Issue ni kwamba, unakuta face price(say) TZS 700K lakini mfanyabiashara anakuwa tayari kukuuzia kwa less than 700K lakini bila kutoa risiti...kwa maana yupo tayari kuuza (say) TZS 650K ili mradi tu asilipe kodi!!! Pamoja na kwamba nishafanya sana biashara lakini hilo halihitaji mtu kuwa mfanyabiashara...linahitaji tu mtu kuwa mnunuzi kuliona; and in fact, even window shopper unless kama unataka kuhoji ikiwa nimepata kuwa angalau window shopper hata kama si kuwa mnunuzi!!!!!umeshawahi kufanya biashara umeshawai kumpandishia bei mteja hata shiling mia? umewai kusikia majibu yao? unajua bidhaa zinakaa dukani kwa muda gani? unajua kwenye elfu unapata shiling ngapi? unatakiwa ulipe kodi shilingi ngapi na mashine ununue shilingi ngapi?
Kama kweli kuna mtu anafanya biashara na kuingiza faida ya sh. 365,000/= kwa mwaka, basi mimi nashauri aache hiyo biashara kwani hailipi, na sio lazima uwe mfanyabiashara, hata kilimo kinalipa! Sio unajiita mfanyabiashara halafu unasumbua mamlaka halali za serikali.
Kama wewe ni mfanyabiashara kweli, nunua EFD kwa kuikopesha TRA, utalipwa ktk kipindi cha mwaka wa kwanza wa fedha kupitia makato ya kodi yako
tatizo wafanyabiashara wengi hawana mazoea ya kulipa kodi na wamezoea kuwaibia wateja kwa ajili ya kutengezeza milima ya faida...jamani lipeni kwani mnategemeaje Tz kuwa kwenye nchi zilizoendelea bila ya kumpa kaisari cha kwake
Mimi sioni tatizo, umeambiwa unapofanya manunuzi ya bidhaa zako, ingiza namba ya kumbukumbu ya risiti ulizonunulia kwenye machine unayotumia, ukilipia pango omba risiti na ingiza number ya kumbukumbu kwenye mashine, na gharama nyingine zote. Mwisho wa siku machine itaonyesha gharama ulizoingia, mauzo yako na faida. Tozo la kodi litakuwa katika faida ya mwisho baada ya kukokotoa gharama.
Machine hizi zinakulazimisha ununue bidhaa zako toka vyanzo rasmi na si uchochoroni. Vinginevyo kama umezoea kuuza vitu vya wizi inakuwa imekula kwako.
Mkuu hapa sijakusoma hizo hesabu zako kabisa.Umepiga hesabu za darasa la saba.Haya mambo ya TRA na EFD zao ni WIZI MTUPU. Wanataka mtu mwenye mauzo ghafi ya kuanzia TSh 14,000,000 kwa mwaka anunue hiyo kifaa ambayo bei yake ni kuanzia laki sita na ushee. Twende kimahesabu. Mauzo ya sh 14mil kwa mwaka ni kama wastani wa kuuza sh 38,000 kwa siku. Kwa profit margin ya 10-15% mfanyabiashara kama huyu ana faida ghafi ya kama Tsh 4,000 hivi kwa siku. Akitoa gharama za pango, ulinzi, umeme, usafi, na tukichukulia hana mfanyakazi, huyu mtu faida yake net haizidi 1,000 kwa siku. Watu ambao mmewahi kufanya biashara mnaelewa, mtu mwenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku ni mfanyabiashara MDOGO SANA, wa chini kabisa, ni mtu wa kima cha chini huyu. Mtaji wa kuuza 38,000 kwa siku ni mdogo kuliko hiyo laki sita ya kununulia EFD.
TRA wametumia akili gani kudhani kuwa mtu huyu wa kima cha chini anayechuma chini ya sh 1,000 kwa siku anaweza kununua hiyo EFD ya sh 600,000? Mtu anunue kadude hako kwa bei kubwa kuliko mtaji alionao? Halafu wanashangaa kuona watu wanaandamana! Nyie TRA mnashangaa nini kuhusu maandamano? Hamuwajui wanaoandamana? Ni wafanyabiashara ndogondogo wenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku, eleweni hivyo. Na hawa wako wengi sana, hawahitaji kutumwa na mtu.
Jamani hivi huko TRA mbona mnataka tudhani kuwa wote mlifeli hesabu? Sh laki sita atazipata wapi mtu anayechuma elfu moja kwa siku? Hata akifanya kazi mwaka mzima bila kula, jumla ya kipato chake itakuwa sh 365,000 bado haitoshi kununua EFD. Mtumie akili jamani. Hicho kiwango hakiwezekani kwa wafanyabiashara mnaowalenga.
Cha kufanya. Rejeeni hicho kiwango mrekebishe, muanzie labda kwenye mauzo ghafi ya sh 100,000,000 kwa mwaka (ambayo ni sawa na wastani wa sh 270,000 hivi kwa siku) hawa angalao wangeweza, na nadhani hawalalamiki maana tunaona zikitumika kwenye maduka. Na hawataandamana.
Sielewi mkanganyiko uko wapi....
1) Retailers wanunua mizigo ikiwa na 18% tayari... kisha anauza ule mzigo ukiwa na 18% na faida yake, 18% ya faida yake ndio inayokatwa kodi, ile 18% ya mwanzo TRA wataidai kwa wholesaler
2)kama suala ni bei ya mashine hilo linajadilika
Madhara
Kama mie ningekuwa mafanyabiashara basi ninge mtoza mlaji hiyo 18% ya faida yangu, hivyo mlaji ndie atakaye umia
Naomba kusahihishwa kama nakosea
Wewe kdg utampa mwanga sababu huyu jamaa ametoa breakdown hata mama yangu muuza mandazi hana hizo hesabu japokuwa EFD haimuhusu.Yule mfanyakazi anayelipa PAYE wakati anapokea Sh. 180,000/- mapato yake kwa siku ni Sh.6000; yaani umemzidi zaidi ya mara sita! Huyu nae anakatwa kabla hajalipa pango, mfanyakazi, maji, umeme n.k! Wakati wewe ukilipa hivyo vitu unabaki na angalau sh.1000 kwa siku, mwenzako anabaki na Negative Income na ndio maana, mshahara wanalipwa tarehe 25, lakini inapofika tarehe 26 or 27 of the same month, anabaki hana kitu.
Kariakoo uwezo wao ni mkubwa tu wakuweza kununua EFD pango milioni mashine 600,000/= halafu wanasema hawewezi waache uongo,patola shs 38,000/= utawezeje kupanga chumba cha milioni?
Naona Mku wangu unakazana kujikita na revenue floor iliyotolewa na TRA kama ndio bas yako! Kimahesabu upo sawa lakini practically hao wanaouza sh. 38,000/- wala bado hawajaguswa! Wanaofanya biashara ya mapato ghafi ya sh. 38,000/= kwa siku wengi wao kama sio wote ni wale wenye viduka vidogovidogo huku uswahilini tena mitaa ya ndani! Hao wa sh.38,000/ kwa siku ni wale wanaouza mafuta ya taa na ya kula kwa vipimo vya shilingi mia mia....hawa ni wale wanaouza majani ya chai ya shilingi 50/-, hawa ni wale wanaouza sukari au bidhaa zingine hata kwa robo kilo...hawa ni wale mtu unafika dukani, unalazimika kutoa mia mfukoni kugonga nondo ili mwenyewe aliyekaa sebuleni akusikie na kuja kukupa huduma!! In short, ni wale ambao viduka vyake ni vile ambavyo mteja anasimama dirishani na ni MARUFUKU kuingia ndani!!!! Hawa ndio hao wanaofanya mauzo ya sh.38,000/-na wala sio wale wanaogoma! And in fact, hata hawa nao wanauza zaidi ya hiyo....waht does it take? Maharage 10kg@2000+Unga 15kg@1000+Mchele 10kg@1500=50,000/- per day....hatujataja sigara, viberiti, mafuta ya taa, mafuta ya kula ya mia mia, majani ya chai ya hamsini hamsini and so much more!Ni ama hauko nchi hii au huna taarifa au huelewi. Maelekezo ya TRA yako wazi kuwa EFD inapaswa kutumiwa na mfanyabiashara yeyote mwenye MAUZO GHAFI ya thamani ya mil 14 Tsh kwa mwaka, siyo faida. Nimeeleza ya kutosha kuhusu uduni wa mfanyabiashara anayeuza sh mil 14 kwa mwaka.