TRA someni hapa: EFD zenu WIZI MTUPU

TRA someni hapa: EFD zenu WIZI MTUPU

Biashara inawalipa ndo mana wanalipa kwa miaka 2-3-4-5 tena mwingine ananunua nyumba nzima anajernga mwenyewe wanakatana juu kwa juu ingekuwa hailipi wangefanya hivi ? sema wanalalamika hela ya mlalahoi inatafunwa na wajinga wa taifa hili. nenda kariakoo kama utapata frem Arusha mjini kama utapata frem Mwanza mjini kama utapata frem Dodoma mjini kama utapata frem wote walioshikilia ni wazamani
 
Umejaa matusi na kejeli lakini nimegundua jambo moja kuhusu wewe! Unajifanya kujua kumbe ni boya tu hujui lolote!!
rudi shule ukajifunze....sijui unapata wapi mambo ya ajabu kama haya!! Kama kweli unafanya biashara utakuwa unafanya biashara ya sidiria wewe!! Yaani kama mtu amenunua mchele gunia 10 kwa sh. 100,000/- kisha akauza kwa sh. 150,000/-, hapo sh. 50,000/- ndo gross income!!! omg! this's might be one of the monthly joke.
Kama gharama zipi?
Ndo maana nikasema we kilaza? Kwani mie nimesemaje? Au hufahamu kwamba mapato ghafi na Gross Income ni kitu kile kile?Pamoja na kwamba umejaa matusi na kashifa lakini kila unachoandika kinadhihirisha tu usakala na ukilaza wako! Nimekuambia mfanyakazi ana gross income ya sh.6000 kwa siku (180,000 kwa mwezi)...gross income ni mapato ghafi...hapo hajakatwa PAYE, hajalipa nauli, n.k...na zile cost zinazokuwa associated na kazi yake. Na ndio maana nikakuambia, ukishatoa gharama zote hizo; unakuta anabaki na negative balance na ndio maana wengi wao kama sio wote mshahara unakuwa umeisha tarehe 27 ya mwezi ule ule aliopokea; implying kwamba tayari ana-operate under negative balance...kwahiyo kwa akili yako unadhani huyo anayebaki na negative balance anabaki na pesa nyingi sio?
Wewe hufahamu nini maana ya mapato ghafi....rudi darasani ukajifunze!
Ndo tatizo la vilaza...hawafahamu kwamba ni vilaza! Jielimishe mambo yafuatayo...gross income, net income, gross profit, net profit! Hapa unachanganya mambo

Wewe rudi primary kabisa maana naona economics zako za "versity" zishakuvuruga. Hiyo sentensi yako ya mwisho inakuhusu wewe mwenyewe kwa 100% maana hakika wewe ni kilaza usiyejijua. Huoni hata haya kujidhihirisha kuwa hujui gharama za biashara, bila aibu unauliza "kama zipi". Ilimradi tu umefika "versity" (hivi ndio wapi huko maana hata kwenye kamusi hakuna neno hili) unajiona mjuaji kumbe bora hata boya kabisa. Hayo maneno machache ya kiingereza hapo sijui gross income, net income...etc ulivyoyakariri basi wajisikiaaaa!

Sasa sikia we kilaza mwandamizi, rudi kajifunze tofauti kati ya "income" na "revenue" halafu uje tuzungumze kulinganisha kati ya biashara na ajira, labda hapo tutaelewana. Maana hizo economics zako za kukariri terminology za kwenye "madesa" zimekuyumbisha sana.
 
muonamambo,
kwanza nakubaliana na hoja yako kwa kiasi fulani kwa kuangalia jambo moja; nalo ni bei ya mashine. Hili la bei hata mimi nimepata kulizungumzia hapa siku za nyuma. Tatizo ni kwamba, hadi leo hii ni ngumu kufahamu wanachogomea wafanyabiashara ni nini hasa...am very certain hata leo hii serikali ikitangaza kwamba inatoa hizi mashine bure; bado kuna watu watapinga tu coz' wengine wengine ambao ni wengi tu, msingi wao wa madai yao wala si bei ya mashine bali hawataki tu hizi mashine; hususani wafanyabiashara wa Kariakoo! Pale Kariakoo, bei ya fremu kwa uchache kabisa ni sh.500,000/- kwa mwezi....huku uswahilini ni kama laki 2! So, it doesn't make any sense mtu awe na uwezo wa kulipa laki 5 kwa mwezi kukodi fremu lakini ashindwe kununua mashine ya laki 8 ambayo utaitumia for years.

Tukija suala la maintenance kwamba ni hadi laki 2, ulitakiwa kufafanua....hadi laki 2 kwa muda gani na ktk mazingira gani coz' hizi mashine zinatolewa kwa 3 years guarantee!

Sasa tuje kwenye hiyo hoja ya kwamba wanaotakiwa kutumia EFDs ni wale wenye annual sales of at least 14m ambazo calculation zako zimekupa daily sales ya sh.44,000/-! Let's be honest here mkuu...hata usipotaka kukiri hapa hadharani basi angalau nafsini mwako! Wanaofanya daily sales ya sh.44,000/- ni wafanyabiashara wadogo sana; tena sana na wala sio wale wanaogoma! Hao wanaofanya daily sales za 44,000/- ni hawa wenye viduka vidogo vidogo vilivyopo mitaani tena mitaa ya ndani ambao biashara zao kubwa ni for daily domestic consumption! Hawa wa daily sales za 44,000/- ni wale wanaotupimia mafuta ya taa ya mia mia, mafuta ya kula ya mia mia; majani ya chai ya hamsini hamsini...and the like...tuwe wakweli hawa ndio wenye daily turnover ya tsh. 44,000/- ambao kwa maelezo yako ni kweli kabisa kwamba hawawezi kununua mashine kwa laki 6. Hata hivyo, wengi wao hawa wala hawajaguswa hata kama sheria inasema wenye annual sales ya 14m ndio wanatakiwa kutumia EFDs. UKichukua mfano wa post yangu uliyo-quote, nimeonesha jinsi sh.50,000 inavypopatikana kwa siku kwa kuuza maharage 10kg, unga 15 kg, mchele 10kg!Narudia, waliogoma sio hao wa sh.50,000/- kwa siku ambao unawaombea public sympathy...

Sasa hebu sample wenye maduka ya namna hii uliyoeleza hapa uwaulize kama wameletewa barua ya kununua EFD. Mimi ni mmojawapo, nina kiosk changu mtaani kina-fit kabisa kwenye description hii na nilileletewa barua tangu mwaka jana, na kuna mtu amekuwa akinikumbushia kwa simu mara kwa mara. Ndio maana nasema na nitasema tena na tena, HUU NI WIZI MTUPU.
 
Kulipa kodi si tatizo na sio tu kwamba ni suala la uzalendo but hiyo kodi inamfaidisha nani ndio shida inaanzia hapo, na kwa nn wanakomaa na wafanya biashara wa buku kadhaa tu kwa nn anayetakiwa kulipa miliomi 60 analipa just 5m? Je hii mashine inagharimu kiasi chote hicho? 600K kweli? TZ ishavurugwa....
 
Haya mambo ya TRA na EFD zao ni WIZI MTUPU. Wanataka mtu mwenye mauzo ghafi ya kuanzia TSh 14,000,000 kwa mwaka anunue hiyo kifaa ambayo bei yake ni kuanzia laki sita na ushee. Twende kimahesabu. Mauzo ya sh 14mil kwa mwaka ni kama wastani wa kuuza sh 38,000 kwa siku. Kwa profit margin ya 10-15% mfanyabiashara kama huyu ana faida ghafi ya kama Tsh 4,000 hivi kwa siku. Akitoa gharama za pango, ulinzi, umeme, usafi, na tukichukulia hana mfanyakazi, huyu mtu faida yake net haizidi 1,000 kwa siku. Watu ambao mmewahi kufanya biashara mnaelewa, mtu mwenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku ni mfanyabiashara MDOGO SANA, wa chini kabisa, ni mtu wa kima cha chini huyu. Mtaji wa kuuza 38,000 kwa siku ni mdogo kuliko hiyo laki sita ya kununulia EFD.

TRA wametumia akili gani kudhani kuwa mtu huyu wa kima cha chini anayechuma chini ya sh 1,000 kwa siku anaweza kununua hiyo EFD ya sh 600,000? Mtu anunue kadude hako kwa bei kubwa kuliko mtaji alionao? Halafu wanashangaa kuona watu wanaandamana! Nyie TRA mnashangaa nini kuhusu maandamano? Hamuwajui wanaoandamana? Ni wafanyabiashara ndogondogo wenye mauzo ya sh 38,000 kwa siku, eleweni hivyo. Na hawa wako wengi sana, hawahitaji kutumwa na mtu.

Jamani hivi huko TRA mbona mnataka tudhani kuwa wote mlifeli hesabu? Sh laki sita atazipata wapi mtu anayechuma elfu moja kwa siku? Hata akifanya kazi mwaka mzima bila kula, jumla ya kipato chake itakuwa sh 365,000 bado haitoshi kununua EFD. Mtumie akili jamani. Hicho kiwango hakiwezekani kwa wafanyabiashara mnaowalenga.

Cha kufanya. Rejeeni hicho kiwango mrekebishe, muanzie labda kwenye mauzo ghafi ya sh 100,000,000 kwa mwaka (ambayo ni sawa na wastani wa sh 270,000 hivi kwa siku) hawa angalao wangeweza, na nadhani hawalalamiki maana tunaona zikitumika kwenye maduka. Na hawataandamana.
Wanachowaza ni tumbo tu rushwa imewapofusha na kudumaza akili zao. Uroho ni mkubwa kupindukia hawajali hata mkisema nini.
 
kila mwaka watakuwa wanafanya ukaguzi wa mtungi na kukupa certificate.
kumbuka mtungi unanunua na auhusiani na laki moja.
na wanasema hiyo sheria imepitishwa na halmashauri ya jiji la mwanza ambayo na wenje yumo

Sio wala sheria ya halmashauri ya Mwanza nchi nzima wanadai sheria hii ilitungwa na bunge. Kila mahali wanadai kukagua mitungi ya gesi ya kuzima moto kila miezi sita.
 
cdm mza bure kabisa wametia lami barabara ya kwenda malaika hotel na kuacha barabara ya buswelu na kiseke inayotumiwa na wapiga kura wao.

Tumia akili kidogo tu barabara ya malaika imelazimishwa na mkulu si ndo mwenye hoteli!
 
Setuba Noel Mfanyakazi hana gharama? Au mnazo nyinyi tu?
Acheni kulialia mlipe kodi

Mzee wa Ndogo, mfanyakazi analazimishwa kununua na kutumia EFD machine? Tumia akili usije jamvini ukitoka kupata kiroba. Wafanyabiashara kodi wanalipa siku zote, wanachokataa ni mpango wa kufaidisha wateule wa kusambaza mashine za tshs 150,000/= kwa tshs 600,000/= hadi 800,000/=!
 
tatizo wafanyabiashara wengi hawana mazoea ya kulipa kodi na wamezoea kuwaibia wateja kwa ajili ya kutengezeza milima ya faida...jamani lipeni kwani mnategemeaje Tz kuwa kwenye nchi zilizoendelea bila ya kumpa kaisari cha kwake

Wewe silly, endelea na usingizi wako kama avatar yako inavyokutambulisha, kazi utafukuzwa na utakuja kujaribu kwenye uwanja wa biashara ndio hapo utakapojua kinacholalamikiwa baada ya wewe na familia yako kukosa kwenda chooni kwa siku kadhaa!
 
Setuba Noel Ulichosema ni sawa kuwa mwenye mauzo ya kuanzia milioni 14kwa mwaka anatakiwa kuwa na mashine.Ila kwa taarifa yako kwa awamu hii ya pili hicho c kigezo pekee kinachotumika wao TRA walisambaza barua kwa wafanyabiashara 200,000 tz nzima ambao wanatakiwa kutumia mashine hizi awamu ya pili na ni wafanyabiashara wakubwa tu.

Sio kweli kama unavyodai kuwa kwa awamu hii hata mwenye mauzo ya 38,000 kwa siku anatakiwa kuwa na mashine,na wengi wanafuata mkumbo tu bila kujua.Na wafanya biashara wa kariakoo wengi wanafanya biashara ki magumashi ndio maana hawataki kusikiaa habari za EFD.Kwani mwanzoni walianza kuwa tatizo ni bei sasa wanadai hata wakipewa bure hawataki!

Which is which?

Ila Nashukuru serikali inapokuja na msimamo ambaye hawezi arudishe leseni na TIN. Akafanye shughuri nyingine,uone kama hawatafyata mkia.Kuna ubaya gani serikali kujua mauzo yako?

kama hakuna kitu unachoficha kwani ktk kodi mauzo ghafi ndio yataonyesha kiwango cha kodi unachotakiwa kulipa.


white wizard. hakuna mfanyabiashara aliyesema hata akipewa mashine bure hataki tena, ACHA UONGO, kwa nini mnakwepa kuzungumzia bei ya mashine? mashine bei yake sokoni ni tshs 150,000/= kama wenzetu kenya wanavyonunua, sasa kwa nini iuzwe tshs 600,000/= mpaka 800,000/= au wewe ndio wale wateule wanaobebwa na wakubwa kuuza mashine? Wafanyabiashara ndio walipaji kodi inayondesha nchi hii, wakiendelea kufunga milango hasara kwa serikali zaidi yao. WASIKILIZWE. ACHENI UBABE WA MATAMKO KWENYE MAKARATASI, MTAUMIA!
 
Labda uzungumze lingine lakini sio kupigwa chenga na hesabu....Nimesoma Maths kuanzia O-Level hadi Versity, and very interesting, nimesoma Economics na kufanya kazi kwenye commercial banks so nafahamu vizuri what's the difference btn net and gross income!

Wewe reference yako ni kwa mfanyabiashara anayepata mapata mapato ghafi ya sh. 38,000/- kwa cku; ndipo nami nikakuambia kwamba, mfanyakazi anayelipwa Sh.180,000/- kwa mwezi, mapato yake ghafi kwa siku ni sh.6000/-; ambapo ni pungufu kwa zaidi ya mara sita as compared na hayo ya 38,000/- kwa siku! Sasa ni nani hapo anayetia shaka shaka kuhusu uelewa wake wa hesabu?

Aidha, wewe ukasema kwamba kwa mfanyabiashara kama huyo kwa siku anaweza kubakiwa na sh. 1000/- kwa siku baada ya kutoa gharama zote, nami nikakuambia huyo wa gross income ya sh.6000/- hawezi kubaki hata na hiyo sh.1000/- kwa siku...

Tukija suala la kununua EFD, hata kama ni kweli wafanyabiashara wanalipia hiyo 600K, lakini pesa yao wanarudishiwa na TRA wanapowasilisha tax returns.

kwa biashara ya kawaida mauzo ya 38,000 sio mapato. These are sales not gross revenues. Mtu aliyeuza 38,000 amenunua hiyo bidhaa ili aiuze. kwa mahesabu ya kuinunua kwa kuiuza kwa faida ya asilimia 10, basi huyu bwana amenunua mzigo kwa dealer/distributor/wholesaler kwa 34,000 yeye anauza 38,000. mapato ya huyu bwana kwa siku ni 4,000 tu!!
kama kweli hii ndio cutoff ya TRA waache hawa jamaa walalamike, mfanaybiashara mwenye mapato ya 4,000/= kwa siku bado ni mtu wa kipato cha chini sana. Kwa nini? hii 4,000 inaitwa gross revenue. kwa maana kuwa baadae ataondoa gharama za umeme/kodi za pango la eneo la biashara etc/ Net revenue ya huyu bwana haiwezi kuzidi 2,000 kwa siku.

Hii anarudi nayo nyumbani, huko sasa anakutana na matumizi ya kila siku ambayo hata mfanyakazi anakuwa nayo. na yeye anatakiwa anunue umeme nyumbani, anunue maji, anunue chakula, watoto waende shule.huyu mtu kama hajaiba basi atafilisika baada ya kipindi kifupi, kwani atakuwa anakula kamtaji kadogo alikonako bila yeye kujua.


Tukirudi kwa wafanyakazi wanaolalamia PAYE, naomba niseme kuwa hii wanayokatwa wao mwisho wasiku wanapewa NET PAY. hii wanarudi nayo nyumbani.wakiwa makazini kwao, hawalipi kodi ya ofisini, hawalipii umeme ofisini, hawalipii hata hela ya mlinzi. Mapato ya mfanyakazi anayepata net pay ya 180,000 kwa mwezi ni zaidi ya mapato ya mfanya biashar aanayeuza 14M kwa mwaka. Hili liko wazi kwa yeyote ambaye hesabu hazimpigi chenga.kwani Mfanyabiashara kabla hajaenda nyumbani ana net income ya 2,000. mfanyakazi ana net income ya 6,000. ni zaidi ya mara tatu.
na wanaosema laki 600,000 kwa mwaka ni pesa kidogo, kun amtu yoyote anayelipwa 180,000 anayetumia laki 6 kununua kitu asichokihitaji na kisichomuongezea kipato chake kwa namna yoyote?

Serikali iongeze cuttoff point ya hayo mapato ya mwaka. Serikali ibuni njia mpya za kukusanya mapato. tumewasema wanategemea sigara na pombe basi wameona wahamie kwenye kukusanya kodi za watu ambao kodi zenyewe hazikusanyiki.tunarudi kulekule kwenye mambo ya kodi ya kichwa. wagawe hizo machine bure, wawaelimishe wafanyabiashara, kama zinafaida kwao, nina uhakika watazichukua.

TRA wanaona wafanyabiashara ni wezi kwa kuwa wao ni majambazi nambari wani, hivyo si ajabu.bahati mbaya hii mbinu yao haitaongeza mapato.waiobereshe.
 
Upande wa pili, kwenu wafanyakazi msiwe wapuuzi, hizi 18% ambazo wafanayabiashara wanagomea kuzitoa ndio zilikuwa ahueni yenu pale mlipokuwa mnang'ang'ania kupunguziwa bei. Wangapi humu mnanunua nguo/bidhaa Mlimani CITY? wangapi mnauwezo wa kuingia kwenye maduka ya POSTA? hivi mnafikiri KKOO wana viwanda vyao tofauti na vya POSTA? kilichokuwa kinatokea ni kuwa Mfanyabiashara wa KKOO hakuwa na 18% kwenye bei yake. hivyo kitu cha 40000 alikuwa na uwezo wa kukiuza 32,000. sasa ukifika dukani ukiomba kupunguziwa bei ndio atashuka kutoka 40000 hadi 33000-35000. unatoka pale unakenua meno nje ukijiita wa mjini. umepata bidhaa kkoo kama ya MCITY kwa bei pungufu. kwa akili yako fupi unafikiria huyu mfanyabiashara hili punguzo ametoa kwenye faida yake?

kitakachotokea kitakuwa na madhara makubwa zaidi kwa wanunuzi, kwani bei zitapanda kwa at least 18%. na Punguzo la bei litakuwa marufuku. sasa wewe mwenye kipato cha 180,000 anza kujifunza kununua vitu mlimani city unakopewa risiti bila shuruti. au utaanza kununua KKOO kwa bei ya MCITY.

kwa wenye kipato cha juu haitawaathiri sana kwani wao wameshazoea kulipa bei za juu. sanasana sasa wataanza kushea matatizo haya na mahohehahe. AU mnaamini hizo risiti mtakazopewa mtazi-claim maofisini?good luck with that.

kwa nchi huu utakuwa mfumo mzuri, kw awafanyakazi muda wa kutafuta kadi zenu za TUCTA na kuandamana muongezwe mishahara ndio huu, kwani kila kitu kiko mbioni kupanda bei.
 
Tatizo nilionalo ni bei ya EFD na hiyo ya kuchukua 18% ya mauzo. Kama wangesema wanachukua 18% ya faida sawa lkn ya mauzo wamekula hadi mtaji wangu.

Mfano kg 1 ya mchele kwa sasa ni 1,000 kwa bei ya jumla. Ukienda kuuza dukani bei ni 1,200. Halafu anakuja mtu wa EFD anachukua 18% ya mauzo ya 1200 sawa na 216/- ukifanya hesabu ya kutoa 1200-216#984. Hapo hujalipa kodi ya chumba, hujala, hujalipa umeme na maji.

Pamoja na kwamba kodi hizo hazichukuliwi, ukifanya utafiti utabaini kuwa kila baada ya mwaka mmoja mfanyabiashara anaachia chumba sawa na kufilisika kwani anashindwa kulipa pango la chumba. Kinachosababisha watu wasione haya, ni kile kitendo cha anatoka mmoja, anaingia mwingine. Na huyu aliyeingia hajisumbui kuuliza kwa nn mwenzake katoka, kwa kuwa anamtaji tayar na pesa ya kulipa pango anayo mkononi, analipa na kuanza biashara. Mkataba ukiisha anajijuta hajakusanya pesa ya kulipa kodi ya chumba hivyo anaamua kuhama. Kila mwaka kuhama hadi mtaji wote kwisha.

Kwahiyo ili hizo EFD zifanye kazi yafuatayo yafanyiwe kazi:-
1. Wapange kuchukua 18% ya faida na si mauzo ya siku.
2. Mashine bei ipungue kwani baada ya muda ni kukusanya faida tu.
3. Kodi za vyumba vya biashara zizibitiwe. Lisiachwe mikononi mwa mwenye nyumba tu, serikali ipange kiwango cha kodi hizo na wasimamie.

La sivyo tutarajie kuona kila siku kuibuka kwa wajasiria mali halafu baada ya mwaka wanapotea wanakuja wengine.
 
Upande wa pili, kwenu wafanyakazi msiwe wapuuzi, hizi 18% ambazo wafanayabiashara wanagomea kuzitoa ndio zilikuwa ahueni yenu pale mlipokuwa mnang'ang'ania kupunguziwa bei. Wangapi humu mnanunua nguo/bidhaa Mlimani CITY? wangapi mnauwezo wa kuingia kwenye maduka ya POSTA? hivi mnafikiri KKOO wana viwanda vyao tofauti na vya POSTA? kilichokuwa kinatokea ni kuwa Mfanyabiashara wa KKOO hakuwa na 18% kwenye bei yake. hivyo kitu cha 40000 alikuwa na uwezo wa kukiuza 32,000. sasa ukifika dukani ukiomba kupunguziwa bei ndio atashuka kutoka 40000 hadi 33000-35000. unatoka pale unakenua meno nje ukijiita wa mjini. umepata bidhaa kkoo kama ya MCITY kwa bei pungufu. kwa akili yako fupi unafikiria huyu mfanyabiashara hili punguzo ametoa kwenye faida yake?

kitakachotokea kitakuwa na madhara makubwa zaidi kwa wanunuzi, kwani bei zitapanda kwa at least 18%. na Punguzo la bei litakuwa marufuku. sasa wewe mwenye kipato cha 180,000 anza kujifunza kununua vitu mlimani city unakopewa risiti bila shuruti. au utaanza kununua KKOO kwa bei ya MCITY.

kwa wenye kipato cha juu haitawaathiri sana kwani wao wameshazoea kulipa bei za juu. sanasana sasa wataanza kushea matatizo haya na mahohehahe. AU mnaamini hizo risiti mtakazopewa mtazi-claim maofisini?good luck with that.

kwa nchi huu utakuwa mfumo mzuri, kw awafanyakazi muda wa kutafuta kadi zenu za TUCTA na kuandamana muongezwe mishahara ndio huu, kwani kila kitu kiko mbioni kupanda bei.

Kimweri, kuna bidhaa za aina nyingi. Zilizo ba bei kubwa mlimani city ni non consumable goods. Lkn vitu kama maji, sukari, sabuni, majani ya chai nk bei zao ni nafuu kuliko mtaani. Unajua kwa nini?

Wale mlimani city, wanachukua hidhaa toka kiwandani hadi dukani na sometime wanaletewa dukani kwa gharama za kiwanda. Hapo anapopanga bei, hata akijumlisha hyo 18% huwa hana hasara kwa kuwa kachukua kwa bei ya kiwanda.

Kazi inakuwa pevu kwa wauzaji wasiochukulia wasiochukulia kiwandani. Hadi bidhaa ifike kwake imepitia kwa wafanyabiashara wengine hivyo yeye kubaki na faida kiduchu. Na haiwezekan kila mtu kuchukulia kiwandani.

Kinachotokea kila mnunuzi analipa kodi hivyo bei lzm ziwe juu.
 
Wafanya biashara mlipe kodi.
Wafanyakazi wamekuwa wakibebeshwa zigo hili la kodi miaka yote. Sasa ni zamu yenu kuonja hii shubiri
 
Kimweri, kuna bidhaa za aina nyingi. Zilizo ba bei kubwa mlimani city ni non consumable goods. Lkn vitu kama maji, sukari, sabuni, majani ya chai nk bei zao ni nafuu kuliko mtaani. Unajua kwa nini?

Wale mlimani city, wanachukua hidhaa toka kiwandani hadi dukani na sometime wanaletewa dukani kwa gharama za kiwanda. Hapo anapopanga bei, hata akijumlisha hyo 18% huwa hana hasara kwa kuwa kachukua kwa bei ya kiwanda.

Kazi inakuwa pevu kwa wauzaji wasiochukulia wasiochukulia kiwandani. Hadi bidhaa ifike kwake imepitia kwa wafanyabiashara wengine hivyo yeye kubaki na faida kiduchu. Na haiwezekan kila mtu kuchukulia kiwandani.

Kinachotokea kila mnunuzi analipa kodi hivyo bei lzm ziwe juu.

Nafahamu, sidhani kuwa wafanyabiashara wa kariakoo wengi wana-fall kwenye kundi hili. Watanzania wa kawaida maji,sukari, chumvi wananunua dukani kwa mpemba. wengi pale ni wauzaji wa Consumer goods, hasahasa FMCG. Ingawa kuna wauzaji wa nafaka na vilaji, lakini naamini cocacola na Azam wameondoa haja y awatu kwenda KKOO kununua haya, wengi sasa wanasambaziwa maduka yalipo mtaani.

Shughuli ipo kwa sisi wazazi, tunaotegemea kununua nguo za sikukuu kariakoo, madaftari, vifaa vya shule pamoja na mahitaji mengine ya hapa na pale kama nguo na vifaa vya nyumbani. Hapa ndio ndugu zetu wamachinga wanapokuwa na msaada.

sie tuliozoea kutokutoa noti hadi bei ipungue we are in for a shock. kwani Advantage ya VAT iliyokuwepo KKOO ndio inatoweka. Si jambo baya kwa wengi, ila nilitoa tahadhari kwa wale wanaochekelea. ILE net yao ya 180,000 ni sawasawa na kuwa itagawanywa kwa mbili, maana wafanya biashara watanzania, hawana mazoea ya kupandisha bei wa asilimia kadhaa, wao hu-dabo tu.
 
on the other hand nawahurumia wafanyabiashara, kwani wanawatetea watu wasiohitaji utetezi. wanachotakiwa kufanya ni kuongeza bei kwa asilimia 18 kwa kila bidhaa wanayouza,ili hao mabwana kodi waendelee kuchukua 18% bila kuathiri faida.

mahesabu yawe hivi.

mchele umenunua 1000

uza 1200

faida yako 200

kabla mama havintishi hajalipa unamwambia apunguze kasi, muda wa kulipa kodi kujenga nchi.

unajumlisha 18% ya kodi ya jamaa zako wa TRA.

mama havintishi inabidi akung'ute 1416 kwani kuna kashilingi 216 ka TRA hapa kati.

sasa shida ipo hapa, watanzania wangapi wako tayari kulipia hiyo 216 ya ziada ili wapate mchele wao wa 1200?

watanzania wangapi wako tayari kusamehe risiti walipe 1200 wajikate zao?

hizi EFD zitafanikiwa kiutendaji kutokana na mtazamo huo?

jibu la hili swali ndio kazi ya Kamishna wa TRA. kama hana jibuhadi leo, hatakiwi kuwepo kazini.


kuna kitu TRA wanajisahau, kwa makampuni na taasisi, RISITI ni kitu cha muhimu kwa ajili ya kuweka kumbukumbu. Muuza vitumbua wa Kitanzania hahitaji risiti ya kikaangio chake alichouziwa 12000 na muuza vikaangio pale karume. hiyo 2160 ya ziada, ili apewe risiti ingemtosha kufanya nauli, na chenji inayobaki mtoto aendee shule kesho.NDIO maisha ya watanzania wengi.

Kufanikiwa kwa EFD kwenye makampuni yenye mauzo makubwa ni kwa sababu wateja wao si hawa wauza maandazi, si watanzania wa chini, wateja wa haya makampuni ni wale wanaogawana 7% GDP increase ya Tanzania kwa miaka 15 iliyopita. Ingawa hata hawa wanazidoji hizi risiti saa nyengine, lakini hawa hawana jinsi.

Kama kamishna wa TRA halioni hili, sioni sababu ya yeye kuwepo pale.hana ufahamu wa idara anayoiongoza.kugombana na mabosi wake (wafanyabiashara/wananchi) sio njia salama kwake.
 
Kweli mkuu. Lkn ndio maana wafanyakazi wengi wabategemea wizi na posho ofsin wamud life.
 
Back
Top Bottom