TRA someni hapa: EFD zenu WIZI MTUPU

TRA someni hapa: EFD zenu WIZI MTUPU

Niliwambia humu kuna watu wametumwa na TRA na Mafisadi wao kupima upepo. Nadhani mmeshawajua. ni wazandiki wezi wanafiki wanufaika wa mpango mkakati wa kukusanya fedha za uchaguzi. Niwaambie tu Tanzania ya sasa siyo ya miaka Ileee, kamwe hamtofanikiwa mna laana hasa wewe mwenye kiherehere unajifanya msomi kumbe huna lolote!
Umevurugwa wewe. EFD itakutokea puani. Unajijua sina haja ya kukutaja ikikuuma jinyonge mliberari mkubwa.
Sina tabia ya kutukana ila nimekereka na mijitu inajiita misomi alafu inashadadia wizi na unyonyaji.
Nikupe taarifa tu aibiwi mtu hapa kawambieni waliowatuma wameingia chaka. Mnakera sana.
 
Mheshimiwa matatizo makuu ni mawili nayo nimeyaweka kwenye post ya kwanza. Kwa kifupi ni:
  1. Kiwango cha mfanyabiashara waliyesema alazimike kununua EFD ni cha chini mno, mauzo ya sh 14mil kwa mwaka, ambayo kimahesabu ni sh 38,000 kwa siku. Nikasema mtu anayeuza kiwango hiki ni mfanyabiashara duni sana, kwani kipato chake halisi ni duni kuliko cha mfanyakazi wa kima cha chini. Mtaji wake hauzidi laki 5, so hawezi kununua EFD ya laki 6.
  2. Bei ya hicho EFD ni kubwa sana.
Nikapendekeza:
  1. Kiwango cha mauzo ambacho EFD ni mandatory kiongezwe, angalao mil 100 kwa mwaka
  2. Kama ni lazima kurekodi mauzo yote yakiwamo ya hawa wanaoganga njaa na mtaji wa laki 5, basi hawa wapewe hizi EFD bure maana kimsingi zinasaidia kazi ya TRA kuliko zinavyowasaidia wao.

Nasisitiza umuhimu wa kulipa kodi lakini haki izingatiwe, TRA isifanye kama inataka kuzuia watu fulani kuendesha maisha yao kwa shughuli halali. Hata kama mtu anaishi kwa biashara duni, kwa kuwa ni shughuli halali aachiwe fursa hiyo ya kujikimu kimaisha bila kukandamizwa, awekewe utaratibu mzuri wa kulipa kodi kwa kiasi kidogo anachopata bila kumuongezea mzigo wa ziada wa EFD, ambao kwa hao walengwa wanaouza sh 38,000 kwa siku kifaa hicho hakinunuliki.

Natumaini umenielewa mheshimiwa.

Nimekuelewa.
kwa upande wa bei za EFD, nami nasema bei hii haifai. Hii ni bei ya kupanga kwa malengo ya ufisadi. Kwa siku zote ukiwasikiliza TRA hawana sababu za msingi kuzifanya mashine hizi ziwe na bei kubwa kiasi hicho. EFD siyo kifaa cha mawasiliano kinachostahili kuwa na bei kubwa kama hiyo. Ni bei kubwa kuliko hata NOKIA 40!

tatizo liko kwenye maamuzi ya kuwa na suppliers wachache bila sababu yenye mashiko. Kama nilivyosema, TRA wangetoa specifications na kuomba kila mwenye uwezo alete kuuza au anunue mwenyewe anakojua. Sasa wao wanamfanya mfanyabiashara kuwa mtumwa wa hizo kampuni zao chache ambazo wote kwa tabia ya TRA tunajua wana rushwa zao huko.

hata hivyo usishangae. Serikali yetu ina makosa makubwa sana na hili tulishajadili, kwamba taasisi muhimu kama TRA na BOT ndo roho ya serikali, lakini ndiko tuna watu wengi wenye elimu za kubahatisha. Eti mtu alisomeshwa kodi tu. Kodi! Huyo ndo anapewa kuhangaishana na wenye ufahamu mpana. Sijui kama kuna anayefahamu kama kuna watu wenye elimu zilizonyooka.

Uhusiano wa kiwango cha mauzo na EFD mi naomba iwe kila aliye na biashara yenye anuani, awe na EFD. Nisichotaka kusikia ni kusema biashara hii ni ndogo kwa mdomo tu. Kutokana na kumbukumbu za EFD, kama biashara itaonekana ni ndogo basi huyo asamehewe kila mwaka lakini isiwe kwa kusema tu kwa mdomo. Pale Kariakoo kuna fremu ndogo sana utazikuta na matairi sita ya magari, lakini kumbe wana stoo za mabilioni nyuma yao. Ukitaka tairi 20, unaambiwa subiri dk 10 na kweli tairi unapata. Kasumba ya udanganyifu imekomaa. Angalia machinga wanavyouza bidhaa za wenye maduka bila risiti. Ukiwagusa unaambiwa eti hawana mitaji mikubwa kumbe ni wakala tu.

Bei za EFD zinaweza kufidiwa na serikali kwa kuziondolea kodi kama walivyofanya kwenye mchele. Au kwa wao TRA kuziagiza siyo kutumia hizo tenda zao. Kwa kuwa wanasema zitaongeza makusanyo ya kodi, basi hakika hawatakuwa na hasara kuziuza kwa bei ya chini. TRA SIYO WAFANYA BIASHARA.
 
Sasa tuko pamoja mheshimiwa, nakushukuru sana.
 
Back
Top Bottom