TRA yaweka rekodi tena, yavuna Trilion 6.6 robo ya 3. Mapato ya Mwezi yapaa kutoka Trilion 1.5 mwaka 2021 hadi Trilioni 2.2 mwaka 2024

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
45,630
52,766
Wakati Rais Samia anasherekea miaka 3 Madarakani,Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imeendelea kuandika rekodi Juu ya rekodi Kila msimu Kwa kufanikiwa kukusanya Shilingi Trilioni 6.63 Kwa robo ya Tatu ya mwaka yaani January -March.

Kiwango hicho ni kikubwa zaidi ya kiwango kilichokusanywa mwaka wa Fedha uliopita Kwa robo ya Tatu.

Ikumbukwe wakati Rais Samia anaingia madarakani TRA ilikuwa inakusanya wastani wa Shilingi Trilioni 1.5 Kwa mwezi.mwaka wa Fedha 2020/2021 lakini ndani ya miaka 3 tuu Makusanyo yamepaa na kufikia zaidi ya wastani wa Trilioni 2.2 Kwa mwezi.Mpaka Sasa ndani ya miezi 9 ya mwaka wa Fedha 203/24 TRA wamefanikiwa kukusanya Trilioni 20.5 wakati malengo ni Trilioni 27.

Hili ni ongezeko kubwa la zaidi ya Bilioni 700 ndani ya miaka 3 tuu ikilinganishwa na ongezeni la Bilioni 700 lillilopatikana awamu ya 5 Kwa miaka 5.

global ss.jpg

My Take: Hakuna aliyeporwa pesa zake Wala matumizi ya mtutu na kubambikiwa Kodi.

Hongera sana Samia na hongera sana walipakodi wote.Nchi itajengwa na Wazalendo.

mwananchi ss.jpg

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya Sh6.63 trilioni katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2023/24, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.6 ya makusanyo ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka wa fedha uliopita.

Katika mwaka wa fedha uliopita mamlaka hiyo ilikusanya Sh5.94 trilioni.

Hayo yameelezwa leo Jumanne, Aprili 2, 2024 katika taarifa iliyotolewa na TRA na kusainiwa na Kamishna wa mamlaka hiyo, Alphayo Kidata.

Taarifa hiyo inaeleza kiasi hicho kilichokusanywa ni ufanisi wa asilimia 95.17 ya lengo la kukusanya Sh6.97.

Mchanganuo wa makusanyo hayo kwa kila mwezi unaonyesha Machi, mwaka huu mamlaka hiyo imekusanya Sh2.49 trilioni chini ya lengo la kukusanya Sh2.56 trilioni.

View: https://www.instagram.com/p/C5c6SkOgg-Y/?igsh=MWdpdmx3ODJldGJpNw==
 
Hizo zinazovunwa zinafanya nini kila mara tunaona taarifa hizio, baadae CAG na Takukuru wanatoa taarifa za ulaji wa fedha hizo na hatua zinazochukuliwa hamna, yaani tunaenda mbele hatua kumi tunarudi nyuma hatua mia moja SHAME.
 
Wangesema ni percentage ngapi ya GDP?otherwise fedha imeshuka thamani na watu thmeongezeka wakati huohuo madeni yanazidi kukua,inaaamnaa tunachokusanya bado nikidogo kuliko mahitaji
Huo utaratibu wa percentage Kwa GDP sio rasmi kwenye reporting labda kama unataka kutafuta cost of Living.

Hapa tunaangalia malengo ya Mapato na kiasi kilichopatikana Kwa mujibu wa Bajeti.
 
Labda ndio zile zinapigwa huko halafu tunaambiwa zimekusanywa, maana hakuna mwizi anaefungwa
 
Tra hata wakitamba kuwa wanakusanya mabilion kadhaa, kama serikali haidhibiti matumizi yake basi tutaendela tu kuwa maskini. Land cruiser 300 series zimetapakaa mitaani wakati zahanati hazina dawa
 
Haya madege mapya yanayonunuliwa kila uchwao huku Atcl napata hasara kila. Mwaka sio ufisadi?
Sio Ufisadi Bali Kuna mismanagement ya mambo ya biashara.Kwanza ndege sio za ATCL maana hao wenyewe wanakodi Kwa wakala.wa ndege wa Serikali
 
Ndege kutokuwa za Atcl haimaanishi kuwa hazinunuliwi kwa kodi zetu. Tunalia na kodi zetu kwanza, hizo Dana Dana za wakala wa ndege na Atcl ni michezo tu ya mjini.
 
Ndio maana nimekwambia Kodi zimetekeleza wajibu wake wa kununua ndege,kuleta ufanisi wa kibiashara haihusiani na Ufisadi
 
SIJUI NIANDIKE UKWELI KUHUSU HIZO FEDHAAA?
anyway ngoja niache tuuu. Soon wataandika nilichokuwa nawazo

Ngoja niendelee kunywa mdalasini na wali hapa
 
Wakati Rais Samia anasherekea miaka 3 Madarakani,Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imeendelea kuandika rekodi Juu ya rekodi Kila msimu Kwa kufanikiwa kukusanya Shilingi Trilioni 6.63 Kwa robo ya Tatu ya mwaka yaani January -March.

Kiwango hicho ni kikubwa zaidi ya kiwango kilichokusanywa mwaka wa Fedha uliopita Kwa robo ya Tatu.

Ikumbukwe wakati Rais Samia anaingia madarakani TRA ilikuwa inakusanya wastani wa Shilingi Trilioni 1.5 Kwa mwezi.mwaka wa Fedha 2020/2021 lakini ndani ya miaka 3 tuu Makusanyo yamepaa na kufikia zaidi ya wastani wa Trilioni 2.2 Kwa mwezi.Mpaka Sasa ndani ya miezi 9 ya mwaka wa Fedha 203/24 TRA wamefanikiwa kukusanya Trilioni 20.5 wakati malengo ni Trilioni 27.

Hili ni ongezeko kubwa la zaidi ya Bilioni 700 ndani ya miaka 3 tuu ikilinganishwa na ongezeni la Bilioni 700 lillilopatikana awamu ya 5 Kwa miaka 5.

View attachment 2952509

My Take: Hakuna aliyeporwa pesa zake Wala matumizi ya mtutu na kubambikiwa Kodi.

Hongera sana Samia na hongera sana walipakodi wote.Nchi itajengwa na Wazalendo.

View attachment 2952508
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya Sh6.63 trilioni katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2023/24, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.6 ya makusanyo ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka wa fedha uliopita.

Katika mwaka wa fedha uliopita mamlaka hiyo ilikusanya Sh5.94 trilioni.

Hayo yameelezwa leo Jumanne, Aprili 2, 2024 katika taarifa iliyotolewa na TRA na kusainiwa na Kamishna wa mamlaka hiyo, Alphayo Kidata.

Taarifa hiyo inaeleza kiasi hicho kilichokusanywa ni ufanisi wa asilimia 95.17 ya lengo la kukusanya Sh6.97.

Mchanganuo wa makusanyo hayo kwa kila mwezi unaonyesha Machi, mwaka huu mamlaka hiyo imekusanya Sh2.49 trilioni chini ya lengo la kukusanya Sh2.56 trilioni.
mbona deni la taifa limeongezeka hadi trilioni 90 kwanini wasilipe,wajanja wanaishia tu kugawana fedha za wavuja jasho kwa ubadhirifu kibao rejea ripoti ya CAG
 
Back
Top Bottom