TRA mnajisikiaje kukamua kodi kutoka kwa wafanyabiashara wanaopata hasara kwa kukosa umeme na maji?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
TRA Tanzania hii hoja naiweka mezani kwenu.

Mnakusanya kodi kwa niaba yetu ili tuweze kuwekeza kwenye maendeleo ya nchi.

Lakini sasa, serikali inashindwa kuprovide umeme wa uhakika na kupelekea gharama za uzalishaji kuwa juu kwa sababu ya kutumia vyanzo mbadala vya nishati ya umeme.

Anguko la wafanyabiashara hususani viwandani na wasindikaji ni kubwa sana. Najiuliza, TRA mnapata guts gani kufurahia kukusanya kodi kutoka kwa wawekezaji wanaoporomoka kiuchumi?

Tuelimishane hapa

Serikali na hao TRA wao, wote ni rubbish tu 🚮. Kuna watu tutalazimika kutoa hela za mifukoni sasa ili kulipa marejesho ya mikopo. Na hizo jela zenyewe sijui tutazitoa wapi!

Kama wanakata umeme kuanzia asabuhi mpaka jioni, wanategemea tutapata wapi kodi za kuwalipa na pia marejesho ya kila mwezi benki?
 
Kuna vijana ni wajasiriamali wa juice na kusambaza kwenye migahawa, wameyumba sana kwa hili tatizo la umeme.
Kuanzia utunzaji wa matunda, ukamuaji na uhifadhi wa juice bila umeme wa uhakika ni wanapata hasara kila iitwayo leo, na bado wana marejesho ya mikopo kila wiki.

Serikali kwa kweli inawafukarisha raia wake kwa kukosekana umeme wa uhakika.
 
TRA Tanzania hii hoja naiweka mezani kwenu.

Mnakusanya kodi kwa niaba yetu ili tuweze kuwekeza kwenye maendeleo ya nchi.

Lakini sasa, serikali inashindwa kuprovide umeme wa uhakika na kupelekea gharama za uzalishaji kuwa juu kwa sababu ya kutumia vyanzo mbadala vya nishati ya umeme.

Anguko la wafanyabiashara hususani viwandani na wasindikaji ni kubwa sana. Najiuliza, TRA mnapata guts gani kufurahia kukusanya kodi kutoka kwa wawekezaji wanaoporomoka kiuchumi?

Tuelimishane hapa
Ukiamka vizuri Huwa unakuwa na hoja ,usikilizwe
 
Kariakoo wanaofanya biashara ktk basement floors ndio hatari aisee bila ya umeme hakuna biashara na ukisema uwashe generator kwa siku unatumia pesa nyingi kununua petroli.

Halafu Rais hata kuzungumzia hii kadhia haizungumzii badala yake tunaona akiwapongeza kina ramadhani brothers huko X.

Suala la mgawo wa umeme ni janga la Taifa hakuna wawekezaji watakuja kuwekeza viwanda ktk taifa lisilo na uhakika wa Umeme na maji.
 
Back
Top Bottom