BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,357
8,073
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza kuwasajili wafanyabiashara wadogo ‘wamachinga’ waliopo katika Soko Kuu la Biashara Kariakoo

Akizungumza na wanahabari leo Jumatatu Desemba 12, 2022 Meneja wa Mkoa wa Kikodi, Alex Katundu amesema tayari machinga 5273 wameshasajiliwa ili kuingizwa kwenye mfumo wa malipo ya kodi wa makadirio.

“Usajili huu unafanyika kwa kila machinga aliyepo Kariakoo kwa sababu tulibaini baadhi ya wafanyabiashara wengine sio waaminifu, haonekani akifanya biashara ila mizigo yake anaisambaza kwa machinga ili akwepe kodi.

“Lakini tunawasajili baada ya kujiridhisha kwamba wote wanaingiza mapato zaidi ya Sh4milioni kwa mwaka, kuna mapato mengi yanapotea hivyo wataanza kulipa kodi” amesema Katundu.

Usajili huo ulioanza Februari mwaka huu, unafanyika ikiwa ni utekelezaji wa tangazo la Kamishna wa TRA la Julai mosi mwaka huu, linaloagiza kila machinga kusajiliwa eneo hilo.

Katundu amesema baada ya kusajiliwa wote watakabidhiwa mashine za EFDs kwa ajili ya kushiriki kwenye ulipaji wa kodi ya makadirio.

Kwa sasa machinga wote wataingizwa kwenye makadirio ya kiwango sifuri kabla ya Januari mwakani kuanza kuingizwa wote kwenye mfumo wa makadirio ya mapato yao halisi ya mwaka.

Pamoja na uamuzi huo, Katundu pia amezindua mkakati mwingine wa uhamasishaji wa matumizi ya EFDs katika mabango kumi wakati huu wa Sikukuu za mwisho wa mwaka.

Kikanuni, usipotoa risiti utatozwa faini kati ya Sh3milioni hadi 3.5milioni na usipodai risiti utatozwa faini kati ya Sh30,000 hadi Sh1.5milioni.

Ikumbukwe mwaka 2017 - 2018 Hayati Rais Magufuli aliagiza Machinga wote nchini kulipa kodi kwa kununua Vitambulisho maalumu ambavyo vinatolewa kwa Tsh. 20,000 ikiwa ni malipo ya mwaka mmoja.

MWANANCHI
 
Kwa staili hiyo machinga watapungua sana kkoo watabaki wale wakutembea tu wale wavimeza watajiondoa wenyewe ni mgumu kusurvive na makadirio ya TRA huwa hayashuki hata ulie machozi ya damu kila mwaka lazima yapande hata kama biashara sio nzuri
 
kwa staili hiyo machinga watapungua sana kkoo watabaki wale wakutembea tu wale wavimeza watajiondoa wenyewe ni mgumu kusurvive na makadirio ya TRA huwa hayashuki hata ulie machozi ya damu kila mwaka lazima yapande hata kama biashara sio nzuri
Huoni ndo vizuri kila mtu akilipa kodi?
 
Kodi ni muhimu na binafsi Sina tatizo kabisa kuhusu umuhimu wa kulipa kodi, ila ninatofautiana sana na TRA wanapokimbizana na vikodi hivi vidogo, kodi hizi zilitakiwa ziwe mapato ya municipalities, hii ni pamoja na kodi za leseni za udereva, faini zinazotokana na makosa ya barabarani, usajili wa magari (mikoa iruhusiwe kusajili magari)my TRA ijikite zaidi na wafanya biashara wakubwa, viwanda mama, etc etc, ni wazo langu maana TRA tunaifanya like linyama likubwa mno
 
Hongereni sana TRA, sana
Mungu awajalie maarifa katika majukumu yenu muhimu kwa Taifa letu

Machinga wazidi kurasimishwa na kusajiliwa
 
Kodi ni muhimu na binafsi Sina tatizo kabisa kuhusu umuhimu wa kulipa kodi, ila ninatofautiana sana na TRA wanapokimbizana na vikodi hivi vidogo, kodi hizi zilitakiwa ziwe mapato ya municipalities, hii ni pamoja na kodi za leseni za udereva, faini zinazotokana na makosa ya barabarani, usajili wa magari (mikoa iruhusiwe kusajili magari)my TRA ijikite zaidi na wafanya biashara wakubwa, viwanda mama, etc etc, ni wazo langu maana TRA tunaifanya like linyama likubwa mno
Tatizo unadhani mauzo ya machinga Kariakoo ni madogo
 
Serikali corrupt na ovyo ovyo ndio zinakusanya kodi kwa watu maskini kama machinga, Mwalimu Nyerere aliwahi kuonya hili na kuna clip yake youtube, hawana ubunifu na wanaotakiwa kulipa kodi hawalipishwi, Tanzania anayelipa kodi sawasawa ni mfanyakazi wa umma tuu, wamebaki kukamua matozo yasiyo halali na maskini tuu
 
Back
Top Bottom