Tabora yalenga kukusanya Shilingi Bilioni 4 za kodi ya Ardhi

Tabora yalenga kukusanya Shilingi Bilioni 4 za kodi ya Ardhi

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
238
Reaction score
148
IMG-20260425-WA0034.jpg
Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Tabora, Tumaini Gwakisa amesema Wizara ya Ardhi kupitia Mkoa wa Tabora imejiwekea lengo la kukusanya shilingi bilioni nne kwa mwaka kupitia kodi ya ardhi inayokusanywa katika halmashauri zote za mkoa.

Akizungumza Aprili 25, 2026 katika kipindi cha Kontena kupitia redio ya UFR, Gwakisa amesema ni wajibu wa kila mwananchi mwenye umiliki wa ardhi kulipa kodi hiyo kwa mujibu wa sheria huku akibainisha kuwa, malipo hufanyika bila adhabu yoyote kuanzia Julai 1 hadi Desemba 31 kila mwaka.
Screenshot 2026-04-27 103746.jpg
Ameeleza kuwa, kutolipa kodi ya ardhi kunaweza kusababisha hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya mmiliki, ikiwemo kufikishwa mahakamani au kufutiwa umiliki wa ardhi husika.

Aidha, Gwakisa amesema kuanzia mwezi Januari hadi sasa, ofisi yake imefanikiwa kuwatumia ilani wamiliki wa ardhi 1,200 katika halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Tabora, huku wakipewa nyongeza ya siku 14 kuanzia leo aprili 25 hadi Mei 8, 2026, kukamilisha malipo kabla ya sheria kuchukua mkondo wake kwa watakaoshindwa kutekeleza wajibu huo.
 
Back
Top Bottom