Ni kitu gani kinafanya makabila mengi Tanzania kutokuwa na utamaduni wa kurudi kwao?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
Nazungumzia kurudi kama kabila ka ilivyo kwa lile kabila ambalo sina hata haja ya kuliweka hapa, Nadhani mnalijua nyomi lao hao wanaorudi ikifika December.

Huko wanakofikia ndio kwao, ndio chimbuko lao, ndiko vizazi hadi vizazi vimezaliana mpaka kuja kwa hapa duniani, Kwenu ni sehemu ambayo inabidi utembelee kujuana na ndugu zako, kujua chimbuko lako, kufanya mila mfano matambiko, n.k. ilimradi kutunza na kuendeleza asili.

Kuna watu kama wa Mwanza, Kagera, Njombe, Mbeya n.k yani unakuta wamefanikiwa vizuri huku mjini lakini kuhusu kurudi makwao hio sahau kabisa aisee, labda utokee msiba.

Kwa tathmini nliyofanya nmeona hizi ndio sababu.

1. Vipapai (kurogana) - Kuna makabila kwa ushirikina tu hawajambo aisee! Ukirudi huko kwenu hata na gari basi ni wivu na chuki, mtu umepeleka watoto vijijini huko matokeo yake wanazibwa macho, masikio, midomo, kuwa vichaa, n.k.

2. Kutokujenga vijijini- mtu anaweka heshima bar lakni kijijin hajajengea hata wazazi ama ndugu zake, nyumba ni ya makuti ipo vile vile tangu aondoke, ukijenga kijijini kwenu lazima upa miss, ila kama hujajenga kwenu ni vigumu kirudi kulala kwenye nyumba za nyasi.

3. Ushirikiano hafifu na chuki, mtu yupo radhi asaidie mtu wa kabila lengine ila chonde chonde hataki hata kusikia habari ya ndugu yake kufanikiwa.
 
Kurudi kufanyeje. Ama wakirudi lazima iwe matangazo.utaratibu wako sio lazima namie niu cope mkuu. Love your life.

Halafu kumbuka ajali ni nyingi Sana road so why ujazane na familia kisa kwenda kuuza sura.

Huwezi muelimisha mtu Cha kufanya yeye mwenyewe anayo priority yake ya maisha.
Waambie na watumwa waliopelekwa jamaika warudi kwao afrika.

Tangiapo wengi wapo kwenye mikoa Yao na Ina fursa na raslimali tele. Mfano mtu wa mwanza aende wapi yupo kwao kila kitu kipo,ardhi Ipo, mazingira mazuri ya biashara hakuna ubaguzi wa kikabila kuwa huwezi fanyapo biashara Kama wewe sio mzawa wa mwanza.

Wengine kwao Wana shida hawana ardhi ,hakuna biashara ya maana wanabaka kuhangaika kwa wengine.

Imagine kila mtu akae kwao afanyae biashara kwao utaweza ama utakufa.
 
Nazungumzia kurudi kama kabila ka ilivyo kwa lile kabila ambalo sina hata haja ya kuliweka hapa, Sio kwenda makwao kama ukoo bali kama kabila, Nadhani mnalijua nyomi lao hao wanaorudi ikifika december.
Sababu ulizozitaja nadhani ndizo kuu, kwa kuongezea

4. Uchumi umekuwa mgumu, nakumbuka wakati nipo kijijini baba zangu walikuwa wakija kila mwaka, siku hizi hata sikumbuki ni lini wamekuja
 
Kurudi kufanyeje. Ama wakirudi lazima iwe matangazo.utaratibu wako sio lazima namie niu cope mkuu.
Mkataa kwao ni mtumwa

Hii ndio sababu hilo kabila limepiga hatua kubwa sana kwenye maendeleo, kurudi kwenu ni jambo zuri linalohamasisha umoja, upendo na mshikamano.

Kuna watu humu hawajui kabisa hata mila zao wala kujua asili zao
 
Makabila mengi ya hapa kwetu Tanzania yaliisha achana na Mila za kutambika kwa mizimu ya kale,nadhani dini zilizoingizwa na wakoloni hapa nchini zilisababisha kwa kiasi kikubwa kuua utamaduni huo wa kutambika, ila kwa hawa wenzetu wa kabila la kaskazini bado wanaishi kwenye Mila za kale, kurudi kwao mwezi wa December ni jambo la muhimu sana kwao,wasipotambika wanaaminimambi yao hayataenda.
 
Mkataa kwao ni mtumwa
Unachoongea tofauti na ulichoandika. Wamepiga hatua gani ama ndio Hali ukiwa na milioni kumi unaenda kwa mama mwenye beseni kichwani na kujinadi kuwa una hela. Ni kwa Nini usiende kwa wenye hela wenzako ujinadi,ujitape kuwa unazo.

Yaani una bachelor unaenda kuuza sura kwa fomu Foo kuwa umesoma.jitafakari kwanza.

Kuna mtu amekataa kwao. Si yupo Tanzania ama unadhani kuwa yupo Burundi. Usikariri maisha.

Umoja huo unaongelea unaleta uhasmaa baina ya makabila ndani ya nchi. Saivi Rwanda hakuna mtutsi Wala mhutu Bali Kuna mnyarwanda.

Angalia Ethiopia wenye umoja wa kikabila unachoongelea.

Ukabila unaleta chuki na kutengana.unamtenga mwenzako kisa sio kabila lako.

Na ndo Mana huko Kenya Kama wewe ni mwalimu mkikuyu huwezi fundisha kwa wakalenjini unaona hiyo ni sawa.

Hivi unajua Kuna watu wakiwa mkoani kwao wanabaguana Sana.

Yaani ukiwa na ukabila Sana unaoita umoja huwezi enda nunua duka la mtu asiye kabila lako.

Yaani ni mambo ya tribalism kwenda mbele. Ukipewa ofisi Fulani unajaza kabila lako afu unajiita umoja na huku uliacha wenye qualifications za kutosha.

Naona umejawa na ukabila unataka kuleta chama Cha kikabila.

Kuna watu ni watanzania Ila Wana asili ya nchi zinazoabudu sana ukabila.

Ukabila na udini ni mbaya Sana Mana unamuona asiye kabila lako sio binadamu.

Ukianza kunibagua mie ni mbara wewe ni mzenji mpaka huko zenji mtabaguana tu ,yaani mtabaguana mpaka family level kataa kubali.
 
sababu ulizozitaja nadhani ndizo kuu, kwa kuongezea
4.uchumi umekuwa mgumu, nakumbuka wakati nipo kijijini baba zangu walikuwa wakija kila mwaka, siku hizi hata sikumbuki ni lini wamekuja

Bado upo kijijini unasubiri waje, au sasa ni wewe unasubiriwa uende huko kwenu?
 
Wewe unawasema wabondei.

Hawa watu wanaogopa sana kurogwa ndio maana wakipata kazi mjini hawarudi bonde.

Na akirudi labda kwenye msiba halali Ni ku kwea Rahaleo Mara baada ya mazishi.

Hata kula hawataki.

Utamsikia akisema "papa kida mie" wakati papa ndio mboga yao kubwa.
 
Elimu ya Geography ilikupita kushoto

Pia elimu ya History ya Kidato cha tatu Kama sio cha nne ilikupita kushoto.

Watu kuhama kunakuwa sababu, sio kila anayehama kwao mi Kwa sababu hakuna Ardhi ya kutosha yenye rutuba, au hakuna hayo unachofikiria wewe.

Wengine wanahamia Maeneo yenye wajinga wengi ili watumie ujinga wao kujitajirisha.
 
Elimu ya Geography ilikupita kushoto,
Pia elimu ya History ya Kidato cha tatu Kama sio cha nne ilikupita kushoto.

Watu kuhama kunakuwa sababu, sio kila anayehama kwao mi Kwa sababu hakuna Ardhi ya kutosha yenye rutuba, au hakuna hayo unachofikiria wewe.

Wengine wanahama Maeneo yenye wajinga wengi ili watumie ujinga wao kujitajirisha.

Isomeke wanahamia.!
 
Back
Top Bottom