Tiba mbadala ya chumvi: Sehemu ya kwanza

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
140,946
2,000
Habarini za usiku huu
Ningependa kushare nanyi hii tiba mbadala ya chumvi kwa wale waamini na wenye uhitaji, hii si uchawi ushirikina wala ulozi na wala huhitaji kwenda kwa 'mtaalam' kupoteza pesa na muda wako huku ukiwa kwenye hatari ya kutapeliwa nk

Chumvi yenye matokeo bora ni chumvi ya mabonge, au ile chumvi ya kuchimba kwa vifaa vya kawaida (epuka chumvi ya viwandani ni mfu) japo inaweza kusaidia kwa kasi chake

Chumvi ni kinga bora kwa nguvu hasi zote ushirikina na nguvu nyingine za giza! Hata wale wanaohisi kuibiwa ama kuchafuliwa nyota zao, stimulus bora ni chumvi... Hata zile hatari nyingine katika ulimwengu wa roho, zote zinazokunyelemea kinga kuu pamoja na sala na imani yako kwa Mungu ni chumvi

MATUMIZI
Chukua kiasi kidogo cha chumvi nyunyizia kuzunguka kitanda, chumba au hata nyumba yako, fanya hivyo huku ukinia ama kunuizia yale utakayo... Fanya ukiamini na kumaanisha.

Hapo hiyo ni kinga ya kujikinga na nguvu hasi lakini ukitaka kusafisha nyota yako(mtima/aura) kila uogapo weka chumvi kidogo kwenye maji kisha ogea..... Masharti ya kuoga ni siku 7 14 au 21 ama la mara 7 14 au 21
Nb: hii haipingani na imani yako kwakuwa hata kwenye maandiko tunaona chumvi ilivyotumika kutakasa
a7a04db0b1254ba994fe9e7e3de1522c--magical-herbs-witchcraft-wiccan-herbs.jpg


Mubashara:
Pamoja na kwamba mada yetu ni ya chumvi lakini nakupa nyongeza ya hii ya kipande cha mkaa kwa wale wenzangu wa Uswazi kwenye chumaulete zongo na kulogana kusikoisha
1799584c214ef3a2268d4feb911aabe0.jpg


Alamsiki.......!!!!!!


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Bajuda

JF-Expert Member
Nov 29, 2018
206
250
Safi sana hao hawakuwa siafu wale wa kawaida tunaowajua sisi

Sent using Jamii Forums mobile app
Habar mkuu mshana .
Sasa mkuu kutokana na kilichomfika huyo Dada wa siafu chumbani kwake.
Je ipi ni njia bora na yenye nguvu zaidi?
Katika kukinga ama kulinda ama kuepusha nyumba isiingiwe na wadudu wa hatari kama nyoka, siafu na wengineo wabaya zaidi walio hatari???
Chumvi ya mawe itatumikaje hapo kuchoma ama?????

Naomba majibu mkuu
Shukrani.
 

Blac kid

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
4,982
2,000
Mie nimeoga miezi mitatu mfululizo cheche mambo hayasongi kabisa, sijui na huyu mhutu pale magogoni ndo tatizo.
 

DREAMBOY

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
1,861
2,000
Mi sitaki hizo dawa za kuoga wala kupaka, mi nataka dawa ya kuwa kuwapumbaza mabosi ,nikienda na andiko langu wanalikubal
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
140,946
2,000
Habar mkuu mshana .
Sasa mkuu kutokana na kilichomfika huyo Dada wa siafu chumbani kwake.
Je ipi ni njia bora na yenye nguvu zaidi?
Katika kukinga ama kulinda ama kuepusha nyumba isiingiwe na wadudu wa hatari kama nyoka, siafu na wengineo wabaya zaidi walio hatari???
Chumvi ya mawe itatumikaje hapo kuchoma ama?????

Naomba majibu mkuu
Shukrani.
Usichome chumvi.. Ni kitu kibaya sana... Tunachoma chumvi pale tunapotaka kufanya manuizi mabaya
Imwage tu kuzunguka nyumba inatosha kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Masasaa

JF-Expert Member
Oct 23, 2015
452
500
Sasa ndio nimeelewa kwa nininmaji ya baraka kabla padri hajayaombea na kuyabariki huwa tunaweka chumvi

Stay home, stay safe
Corona kills
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom