JINSI YA KUTUMIA CHUMVI,MAJI,UDONGO KIROHO

JINSI YA KUTUMIA CHUMVI,MAJI,UDONGO KIROHO

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
3,799
Reaction score
4,356
Kwa wale wanaopenda sana kutumia vitu VYA upakao vya mitume na manabii WA UONGO(maajenti WA kuzimu,wanyemikataba na kuzimu,wanaochukua nguvu zao kuzimu/wanaotumia mafuta na VITU VYA upako kutoka kuzimu ambavyo vimebeba Roho za mauti na kaburi,vimenuiziwa LAANA,na vifungo vya mauti na kuzimu.


Nitakufundisha hapa kutengeneza vitu vya upako WEWE mwenyewe ambavyo vimeruhusiwa ki BIBLIA AMBAVYO vitakuwa salama KWAKO na vitafanyika baraka na uponyaji.

ANGALIZO nguvu inayotumika siyo ya vitu vyenyewe peke yake ila ni NENO la MUNGU ambalo ni YESU ndilo hilo NENO unaliunganisha na VITU hivi,na kamwe usivitegemee Wala usivitumaie vitu hivi nitakavyokufundisha,nguvu ni ya YESU inayofanya KAZI tunatumia TU vitendo vya IMANI..sio tunavutegemea vitu,BILA YESU/NENO ukivitumainia vitu peke yake inakuwa haifai.

VITU HIVYO NI
1.chumvi ya mawe/chumvi ya ASILI ya nyumbani mwako usiazime ya MTU ,usipewe na mtu , chukua ya kwako mwenyewe nyumbani mwako uliyonunua sokoni.

Chumvi hutumika kuweka agano mkataba kwamba kile unachokitamka kuomba kwa Mungu kupitia chumvi kitokee na Mungu anakitimiza kwa kuliangalia agano la chumvi,unaweza kuomba uponyaji,kusafishwa,kuondoka Roho za uharibifu katika maisha Yako,mwili WAKO,nyumba Yako n.k

Matumizi chukua chumvi Yako iombee kwa Mungu vile unataka halafu tupia kwenye ardhi ya nyumba Yako kama unataka kujiponya,ama weka kwenye maji OGA au muoshe mtoto..mfano ,kuna mtoto mdogo alipozaliwa wakawa wanakuja watu kumtazama yule mtoto,ndugu Mmoja alikuja kumuona mtoto akiwa na miezi 3 akaleta zawadi ya nyama,yule mgeni alikuwa ana aminika na asifika kwa uchawi alipo ondoka TU yule mtoto mchanga akaanza KULIA BILA kunyamaza mpaka anazimia...bahati nzuri kulikuwa na jirani pale akamshauri huyo mgeni aliyekuja kumuona mtoto siyo MTU MZURI,amempiga JICHO ,KIJICHO mana katoto kalikuwa kabonge kazuri,akamshauri alete chumvi ya mawe ya ASILI jikoni akaiombea chumvi AKASEMA navunja nguvu ya uchawi ya KIJICHO itoke akachanganya kwenye maji ya KUOGEA kwa beseni akamuogeshea mtoto,na mtoto akanyamaza kulia muda huo huo.

Ukiiombea chumvi yako ya nyumbani INAKUWA ya chumvi ya baraka,unaweza kumwaga hata kwenye kona ya nyumba Yako,nyingine ukaweka kwenye maji ya KUOGEA.,Kwenye eneo la biashara Yako.Chumvi imetumika kama kielelezo Cha AGANO na Mungu MKATABA mpya WA baraka na Mungu kuponya na kubariki eneo ambalo utaliombea kwa NENO/YESU kutumia kitendo Cha Imani Cha chumvi

Mistari ya biblia
Katika Biblia, chumvi ilitumika kama alama ya agano thabiti, utakatifu, kuhifadhi vitu, na kuongeza ladha au uponyaji.

Matumizi na Maana Kuu ya Chumvi

• Agano la Chumvi: Ilikuwa ishara ya agano lisiloharibika na lenye kudumu milele kati ya Mungu na watu wake, kama vile agano la ufalme kwa Daudi (2 Nyakati 13:5, Hesabu 18:19).

• Sadaka na Ibada: Chini ya Sheria ya Musa, kila sadaka ya unga au nafaka iliamriwa kutiwa chumvi kuonyesha usafi na kutokuwa na ufisadi
(Mambo ya Walawi 2:13).


• Uponyaji na Kutakasa: Nabii Elisha alitumia chumvi kuponya maji yaliyokuwa yanasababisha shida na vifo huko Yeriko (2 Wafalme 2:21).

• Mfano wa Tabia ya Waamini: Yesu aliwaita wafuasi wake "chumvi ya dunia" (Mathayo 5:13), akimaanisha kuwa na ushawishi mzuri, kuzuia uovu, na kuleta amani au ladha ya kiroho katika jamii.

2.MAJI MASAFI YA NYUMBANI MWAKO.
Maji yanaweza kubeba NENO,umbo,MICHORO ,alama ,namba ,hata nguvu ya kiroho ya watu WALIOPO karibu na maji kama hasira au HUZUNI na hata nguvu ya kiroho iliyopo eneo karibu na maji yalipo.
Ndio MAANA Huwa NASHAURI kama unapika chakula usipike chakula umenuna ,ama una HUZUNI mana unatumia maji kupika Ile Roho ya HUZUNI au chuki ,Hasira ,ugomvi..inaingia kwenye maji YALIYOPO kwenye glass MEZANI,sufuria ya maji ya chakula,kwa hiyo MTU akila bila kuomba anaibeba,ndio mana kwenye baadhi ya maeneo watu wengi wanapika pika usiowajua wanapokuwa wanapika vyakula kama msibani wanakuwa wanavinenea maneno ya LAANA Ile LAANA inaingia kwenye maji ya kupikia hicho chakula.

Maji yanabeba NENO lolote au hisia YOYOTE iliyopo karibu na maji yalipo,
Ndio unaona tunabatiza KWA maji mana yanakuwa maji yaliyobeba ungana na NENO sio MAJI MATUPU TU(UBATIZO),maji yanasafisha ,nguo,uchafu,maji Yana UHAI..
(USIENDE KUCHUKUA MAJI YA UPAKO kwa manabii Huwa wanachanganya na maji ya kuoshea maiti,au wanayatoa kuzimu,au wanayanenea laana..hivyo unabeba maroho ya mauti na LAANA.)

Ndio mana ukienda kwa waganga WA kienyeji wanaandika kwenye karatasi nyeupe maandishi kwa kalamu nyekundu halafu wanaiyeyusha kwenye maji yale maandishi yanaingia kwenye maji (KOMBE )halafu wanakwambia ikaogee au ukanywe..na hata usipoloweka karatasi kwenye maji ukiguaisha TU karatasi hata kwenye chupa iliyobeba maji ,mfano hizi LEBO za chupa,KOPO za vinywaji..yake maandishi yaliyopo kwenye LEBO za vinywaji kama SODA,AU POMBE yanaingia kwenye maji Ile nguvu ya ROHO CHAFU na alama za kishetani zilizopo na mbaya zaidi haya masoda na ma eneji drink na pombe zile LEBO zake Zina namba za kishetani,na maandishi ya kishetani code namba 666 the beast,na Huwa wanavinenea LAANA inakaa kwenye vinywaji vimimika hivyo ukinywa unabeba LAANA.

Ndioa MAANA akina MESHACK SHEDRACK ABEDINEGO waliepuka kujitia UNAJISI kwa kunywa na kula VINYWAJI VYA MFALME ,au vya matambiko,ili wasibebe Ile Roho ya LAANA,wakaamua kula mtama na maji,ndio mana unaona Nabii KIJANA aliambiwa asile chakula Cha mfalme Wala kinywaji,VINGINE ni vya matambiko vimenuiziwa.

maji yana maana kubwa sana ya kiroho na kimwili, yakitumiwa kama ishara ya uzima, utakaso, wokovu, na roho.
Hapa kuna makundi makuu ya matumizi na maana ya maji katika Biblia:

Utakaso na Ubatizo

• Utakaso wa Kimwili na Kiroho: Chini ya Sheria ya Musa, maji yalitumika kuosha makuhani na vitu vya ibada ili kuwa safi mbele za Mungu (Kutoka 30:18-20).

• Ubatizo: Katika Agano la Jipya, maji yanatumika kwa ajili ya ubatizo kama ishara ya toba, kufa kwa utu wa kale, na kufufuka katika maisha mapya (Mathayo 3:11, Warumi 6:3-4).

Uzima na Uwepo wa Mungu

• Maji ya Uzima: Yesu alijitambulisha kama chanzo cha "maji yaliyo hai," ambayo mtu akiyanywa hatatafuta kiu tena milele, akimaanisha uzima wa milele (Yohana 4:14).
• Neno la Mungu: Biblia inafananisha Neno la Mungu na maji yanayoliosha na kulitakasa kanisa (Waefeso 5:26).

WENGINE wanachanganya MAJI+CHUMVI vyote anaviombea mwenyewe anavitumia kama maji ya baraka,kunyunyiza maeneo yake,kuweka kidogo kwenye maji ya KUOGEA, biashara zake n.k.

3.UDONGO/mchanga,ardhi Yako ,USICHUKUE udonge kutoka kwenye ardhi ambayo siyo Yako,eneo lisilo la biashara Yako,chukua kwenye eneo lako hata kama umepanga fremu ya biashara,chukua kwenye mlango WA kuingilia duka lako TU,USICHUKUE kwa mwenzako.
Udongo WA nyumbani kwako ,ardhi inasikia ,ardhi Ina Nena,ardhi Ina mlango,ISEMESHE ARDHI YA NYUMBANI Kwako ,kwenye eneo la biashara Yako inenee MANENO ya biblia sala ,FUTA mikataba na maagano ya mauti/kuzimu YALIYOPO katika hiyo ardhi,sema popote nitakapo kanyaga BWANA amenipa hiyo ardhi ,iteke ardhi Yako kwa jina la YESU.
CHUKUA udongo,mchanga kidogo WA ardhi Yako ,uombee mwenyewe halafu ukishauombea uridishie mwaga katika eneo ulipoutoa.

USICHUKUE MAUDONGO YA MITUME NA MANABII..UTAPEWA UDONGO ULIOCHANGANYWA NA UDONGO WA KABURI,ULIONENEWA LAANA NA MAUTI,HALAFU UNAKUJA KUUMWAGA NYUMBANI KWAKO..UNAPANDIKIZA MAUTI/LAANA nyumbani kwako.


. Udongo: Asili ya Mwanadamu na Familia

• Asili ya Uhai: Biblia inasema Mungu alimuumba mwanadamu kutoka kwa mavumbi au udongo wa ardhi (Mwanzo 2:7). Udongo wa nyumbani kwako unakukumbusha udhaifu wa kibinadamu, unyenyekevu, na tegemeo kamili kwa Mungu aliyetupa uhai.

• Hali ya Moyo wa Familia: Katika Mfano wa Mpanzi (Luka 8:4-15), Yesu alifananisha udongo na hali ya moyo wa mtu. Udongo wa nyumbani kwako unawakilisha "ardhi ya kiroho" ya familia yako. Je, ni udongo mzuri unaozaa matunda ya upendo na amani, au una magugu na miiba ya migogoro?

2. Ardhi: Urithi na Baraka za Mungu

• Eneo la Umiliki na Mipaka: Katika Agano la Kale, Mungu aligawa ardhi kwa kila kabila na familia kama urithi usiopaswa kupotea (Hesabu 36:7). Ardhi ya nyumbani kwako kibiblia ni eneo la kisheria ambalo Mungu amekukabidhi ulitunze, ulilime (kuzalisha), na ulilinde kiroho na kimwili.

• Madhabahu na Utakaso: Maandiko yanaonyesha kuwa ardhi inaweza kuchafuliwa na dhambi au kumwaga damu (Hesabu 35:33). Hivyo, ardhi ya nyumbani kwako inahitaji kutakaswa kwa maombi ili iwe mahali pa baraka, usalama, na uwepo wa Mungu badala ya laana.

3. Mchanga: Ulinzi, Msingi, na Uzao

• Msingi Imara wa Nyumba: Yesu alitoa mfano wa mtu mwenye akili aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba, na mpumbavu aliyejenga juu ya mchanga (Mathayo 7:24-27). Mchanga wa nyumbani kwako unakukumbusha usijenge familia yako juu ya misingi isiyo imara ya kidunia (mchanga unaohama), bali uijenge juu ya Kristo (Mwamba).

• Ahadi ya Uzao na Ufanisi: Mungu alimwahidi Abrahamu kwamba uzao wake ungekuwa mwingi kama mchanga wa pwani (Mwanzo 22:17). Mchanga unawakilisha baraka zisizohesabika na ongezeko ndani ya nyumba yako.

• Ulinzi na Mipaka: Mungu ameweka mchanga kuwa mpaka wa bahari usiopitika (Yeremia 5:22). Hii inamaanisha Mungu anaweza kuweka ulinzi wa kimungu kwenye mipaka ya nyumba yako ili adui asivuke.

ANGALIZO,SIPENDINKUFUNDISHA juu ya vitu hivi kwa sababu wengine HUANZA KUVITUMAINIA NANKUVITEGEMEA badala ya KUWEKA IMANI YAKE KWA MUNGU..
Yani MTU maji ya upako yakiisha anakosa Imani , UNAFIKIRI sasa YESU AMEISHA ,TUNATAKIWA TUSITEGEMEE NENO LA MUNGU YESU mwenyewe na KUSOMA BIBLIA.
sio KUVITUMAINIA vitu VYA upakao,hiyo inakuwa sasa kama ibada ya SANAMU,YESU ANATOSHA.

ila sasa kama unashindwa kabisa ni Bora sasa utumie vitu VYA upako vya KWAKO mwenyewe kuliko kwenda KUPEWA NA MITUME NA MANABII..utalogwa italeta vitu VYA kutoka kuzimu WEWE,utafikiri ni upako.

HASARA kubwa ya Kutegemea vitu VYA upako,utapunguza NGUVU ya maombi,na Imani Yako kwa Mungu,itahamia kwenye vitu,utashindwa kuomba mwenyewe muda MREFU,KUSOMA BIBLIA,utabaki unategemea vitu VYA upako inakuwa kama HIRIZI YAKO(ibada ya SANAMU)

Kama unaweza MUAMINI YESU PEKEE na NENO lake ,YESU ANATOSHA..huitaji vitu VYA upako.
 
Mtumishi a sinner saved by Christ ni sahihi kutumia mitishamba na kujivukiza kama dawa?

Ni sahihi kutumia chumvi
Ya mawe, kwa mda fulani may be siku 30 kama dawa ya panadol 2x3 bila kuhitaji maombi... Na ukapona.
 
Mtumishi a sinner saved by Christ ni sahihi kutumia mitishamba na kujivukiza kama dawa?

Ni sahihi kutumia chumvi
Ya mawe, kwa mda fulani may be siku 30 kama dawa ya panadol 2x3 bila kuhitaji maombi... Na ukapona.

Mitishamba ndiyo iliyoruhisiwa kutumika kama dawa majani ya miti iliyopo mtoni,matunda yenye MBEGU
Hizi big pharma dawa za viwandani nyingine nyingi zinaenda kinyume na MFUMO WA mwili WAKO nature ,zinaitwa ANTI something,Zina side effects nyingi,dawa nyingine side effects zake ndio inatumika kama ufanyaji kazi wake,na Zina madhara MENGI ,na nyingine zinasababisha madhara makubwa sana.

Sio Mpango WA Mungu TUTUMIE big pharma ama MBOLEA ama dawa za viwandani za kuua wadudu,MBOLEA za VIWANDANI,GMO genetically modified MBEGU na foods ,ni biashara za watu na MFUMO WA KUMTAWALA mwanadamu,na kumfnaya tegemezi,na kumbadilisha DNA yake vinasaasaba.

• (Ezekieli 47:12): Nabii Ezekieli anaelezea miti inayokando ya mto mtakatifu ambayo matunda yake ni chakula na majani yake ni dawa (andiko hili linafananishwa na Ufunuo 22:2 kuhusu mti wa uzima unaotoa majani ya kuponya mataifa).
• Magonjwa na Tiba Asili (Isaya 38:21): Nabii Isaya alimwambia mfalme Hezekia atengeneze na kupaka mgandamizo wa tini (fig cake) kwenye jipu lake ili apone.
• Mimea ya Kawaida ya Tiba au Viungo (Mathayo 23:23): Bibilia inataja mimea midogo na viungo kama vile mnanaa (mint), bizari (anise/dill), na cumin.

MSOME DOKTA SEBI...DR SEBI DR SEBI DR SEBI.
Magonjwa yote yametengenezwa ni biashara,na dawa zote ni biashara,na magonjwa yote yanatibika kwa tiba za mitishamba KIASILI..mwimbaji Mmoja aliomba THERE IS NO TRUTH IN THIS WORLD

vitu vingi sana karibu vyote tumedanganywa ,Leo kututawala AFYA YETU ni fursa ya biashara kwao UNAFIKIRI watu wote wasipoumwa biashara ya big pharma dawa si itakufa.
Ardhi yetu KILIMO chetu ni fursa kwao..biashara ya MBEGU,MBOLEA,viwatilifu..n.k

Matumizi ya CHUMVI,UDONGO NA MAJI kwa Mimi binafsi si vipendelei nitatumia mara chache sana pale AMBAPO nitasikia sauti ndani yangu inaniambia Fanya hivi tumia kitendo Cha Imani,mara chache chache sana.Na nitatumia maji yangu,chumvi yangu, udongo wangu mwenyewe nitaombea mwenyewe kwa uongozo muongozo WA Mungu aliyeko ndani yangu.
 
Back
Top Bottom