Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,398
- 38,319
Hizi ni taratibu nne muhimu kabla ya kuhamia katika nyumba mpya, iwe ya kupanga au ya kujenga mwenyewe!
Kufanya Dua au Sala
Kabla ya kuingia rasmi, ni muhimu kumuomba Mungu akubariki nyumba hiyo, akupe amani, afya, na ulinzi dhidi ya mabaya yote. Kabla yako vipo viumbe viliishi hapo, vilikuwa na mambo yao ikiwemo hekaheka, Mizozo na mengine ya hivo!
Kusafisha Nyumba Kimwili na Kiroho
Safisha nyumba vizuri kwa kufagia, kufuta vumbi, na kuondoa uchafu. Wengine pia hufanya usafi wa kiroho kwa kusoma dua, Qur’an, Biblia, au kuombea nyumba. Flash Chumvi ama piga deki kwa kutumia Chumvi!
Chumvi hutumika kwa ajili ya utakaso na kuzuia nishati hasi. Nyunyiza chumvi kwenye mlango mkuu na kuzunguka madirishani ili kuzuia Mambo Meusi yasohitajika kuingia ndani ya nyumba.
Kuwasha Nuru
Kabla hujaingiza Samani zako... Fungua madirisha ili hewa iingie na kuwasha taa..... Washa mshumaa, Kibatari ama Chemli katikati ya Nyumba.
Hii inaashiria kuleta mwanga, matumaini, na maisha mapya ndani ya nyumba.
Kuingiza Vitu Vyenye Baraka Kwanza
Kabla ya kuingiza samani zote, ni vyema kuingiza vitu kama Qur’an, Biblia, mshumaa, au chakula kama ishara ya baraka, shukrani, na mwanzo mwema.
Ingia kila Chumba, shika ukuta huku ukinena yale unayotamani yakutokee ktk maisha ya Makazi mapya! Mf: Amani na Upendo vitawale Mahali Hapa, Makazi haya, Nyumba, nipate Mke/Mume mwema nikiwa Hapa, nipate Mtoto/Watoto wema... hii, Kaya hii...Lengo ni kuwa na Makazi mapya ya utulivu na Amani.
Ni muhimu kuyajua haya MwanaJF