Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,481
- 40,000
Siku chache zilizopita Rais Mstaafu Ndg. Benjamin Mkapa alipokea tuzo ya Uongozi Duniani kutoka Taasisi ya mhifadhi wa sokwe-mtu Dr. Jane Goodall katika maadhimishisho ya miaka 30 the taasisi hiyo. Rais Mkapa aliipokea tuzo hiyo "kwa niaba ya Watanzania" kwa maneno yake mwenyewe.
Sasa, sipendi tena sitaki Rais Mkapa aendelee kuzungumza kwa niaba yangu huko nje ya nchi na kupokea tuzo kwa niaba ya Watanzania wakati ameamua kuwadharau na kuwaona hawana mpango. Kitendo cha yeye kuendelea kukaa kimya dhidi ya tuhuma mbalimbali zinazomkabili ni kitendo cha dharau, kiburi, na kisicho cha kiungwana dhidi ya watu waliompatia nafasi hiyo aliyonayo leo!!
Wakati umefika Rais Mkapa azungumzie tuhuma zote zinazomkabili zinazohusiana na utendaji kazi wake akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
a. Kutumia vibaya ofisi yake kwa kufanya biashara akiwa Ikulu
b. Kutumia madaraka yake vibaya kujipatia mali kwa kutumia cheo chake na kujiingizia biashara kutoka fedha za serikali
c. Kujichumia mali za haraka haraka kwa kutumia cheo chake kama Rais
Na aseme sasa, au anyamaze milele!

Yaani, anachoonesha ni kilele cha kiburi.. hizi sisi watanzania wote tuna wivu au wajinga kiasi cha kwamba tunashindwa kumhoji. Nadhani Rais Kikwete aulizwe kama anaona ipo haja ya Rais Mkapa kujibu tuhuma zilizoinuliwa juu yake..
Jamani kikwete was very clear aliposema yeye hafikirii kuchunguza wala kuwashtaki marais waliopita, that means hana huo mpango kabisa. By the way Mkapa yuko busy kweenye seminar na wafanyakazi wake wa Mkapa AIDS Foundation alhamis na ijumaa kunduchi beach hotel, muda wa kujibu tuhuma hana i think.
JF ni venue ya wadadavuzi kweli? Kuna shari gani kupokea tuzo ya wanayamapori kwa niaba yetu? Pengine ingalikuwa madini ningethubutu kujiuliza rohoni.
Hana la kujibu,huyu jamaa alishasema when a'm done with Tz na CCM sintajihusisha na siasa za ndani na hiyo ndio tafsiri ya ukimya wake.
Heri yenu mnaokomalia kumshinikiza bubu wa siasa za Bongo toka 2006 alipoacha u-chairman wa chichiem aongee. Sahauni hilo halitatokea,maandamo dhidi ya mtu asiye dola wala mamlaka ni matumizi mabaya ya nguvu ya umma.