Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,546
- 41,050
Sisi wengine ambao hatubebwi na mihemko ya kivyama bali ukweli wa nafasi, tunaona dhahiri kuwa Rais Samia kuna mambo amekosea lakini pia kuna mambo amefanya na anafanya vizuri.
Lakini pia kwa kuitambua CCM ilivyojaza watu waovu, hata hayo machache mazuri ambayo Rais Samia kayafanya, anastahili pongezi kubwa.
Nchi yetu kwa miongo kadhaa imekuwa ikipita katika giza nene la utawala wa mabavu, utawala usiozingatia katiba wala sheria. Utawala uliojaa ulaghai. Na yote yakisababishwa na watu waovu ndani ya CCM. CCM imekuwa kama kinara wa uovu.
Mema/mazuri aliyoyafanya vizuri Rais Samia, tena katikati ya uovu wa CCM:
1) Kumtoa Mbowe toka gerezani baada ya kuridhika kuwa Siro na wenzake akina walikuwa waongo kwenye tuhuma walizombambikia Mbowe. Na kwa uungwana, alimwalika Mbowe ikulu na kumwomba msamaha.
2) Kuanzisha vikao vya maridhiano ambayo wale waovu wa CCM baadaye walimzidi nguvu kiasi cha yeye kushindwa kuelewa afanye nini.
3) Kuwatoa gerezani wapenzi na viongozi wa CHADEMA waliobambikiwa kesi na kuwekwa kwenye mahabusu mbalimbali.
4) Falsafa yake ya 4Rs ambayo kiutekelezaji inakutana na upinzani mkubwa kutoka kwa wale waovu wa CCM ambao kwao uovu ndiyo imani yao.
5) Kuamua kwenda kinyume na waovu wa CCM ambao walitaka sana haki ya kikatiba ya maandamano na mikutano kwa vyama vya upinzani iendelee kukanywagwa.
6) Kuzuia uovu wa watendaji wa serikali kupora pesa za matajiri kwa nguvu, ref. Sabaya na Makonda, maduka ya kubadilisha fedha za kigeni, na wale waliobambikiwa kesi za uhujumu uchumi.
7) Kuzuia ushetani wa kuteka, kutesa na kuua watu wanaokosoa Serikali.
Mambo Aliyoyafanya Vibaya:
1) kutoa haki kupindukia kwa wageni kuhusiana na rasilimali za nchi. Ref. bandari, misitu na mbuga za wanyama.
2) kukubali baadhi ya ushauri bila ya kuupima kwa umakini, kama ule wa Siro wa kumkamata na kumtesa Mbowe gerezani.
3) Kufumbia macho baadhi ya maovu ya wazi, ref. ufisadi ulioibuliwa na CAG, kutochukua hatua dhidi ya waovu wakubwa wanaohusishwa na mauaji na mashambulio ya kukusudia kuua, ref. shambulio dhidi ya Lisu na kupotezwa kwa Ben Sanane na Azory Gwanda. Badala ya kumchukulia hatua mtuhumiwa, amemzawadia cheo ndani ya chama, na kuzidi kuthibitisha kuwa ouvu kwa CCM ndiyo falsafa ya chama.
4) Kutofanya uchunguzi binafsi, na hivyo kuhadaiwa kiurahisi na waovu. Kama angekuwa makini na mtafutaji ukweli juu ya ushauri anaopewa, kwa mfano asingemteua Naibu Waziri, kwa uchafu mwingi ambao huyu bwana amekuwa akiufanya na kila mara kuwahonga anaoamini wana uwezo wa kumfikia Rais kila kunapokuwa na minong'ono ya kubadilisha baraza la mawaziri.
5) Kumteua mtu anayetajwa alikuwa kiongozi wa wasiojulikana ambao walikuwa wakiteka, kutesa na kuua watu wanaookosoa serikali, kuwa mwenezi.
Lakini pamoja na yote hayo, kwa kuzingatia mfumo mbaya wa nchi ulivyo, na muundo wa CCM ulivyojengeka kiovu, Rais Samia kwa hayo machache mazuri aliyoyafanya, anastahili pongezi, maana si rahisi sana mtu mmoja ambaye yupo katikati ya mazingira ovu, kufanya mabadiliko makubwa ya ghafla.
Rais Samia, kwa ushauri wangu, ni vema akasimama imara akijua kuwa maadui wake wakubwa wapo ndani ya CCM, na hawa wanataka CCM, Serikali na mifumo yote ya kiutawala iendelee kukaa kiuovu maana ni kwa namna hiyo ndiyo uhakika wao wa kuendelea kuiba na kufisadi. Fanya yale ambayo ni mazuri uliyokuwa umedhamiria kuyafanya toka mwanzo ili siku moja uje ujisifu namna ulivyosimama imara kwenye mambo yenye maslahi kwa Taifa katikati ya upinzani mwingi ndani ya cha chako; wala usiwe mtu wa kujuta kama Hayati Mkapa aliyesema kuwa anajutia kwa vile alishiriki kwenye kuiba pesa ya Serikali kuipatia CCM.