Desemba 11, 2022 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Pindi Chana amepokea tuzo kwa niaba ya Rais Samia jijini Dodoma

Mocumentary

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
769
1,959
Wakati Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akitajwa kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye ushawishi duniani, ametunukiwa tuzo ya muongoza watalii bora nchini kutoka Taasisi ya Kimataifa ya International Iconic Awards ya nchini India.

Juzi, Rais Samia alitajwa kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye ushawishi mkubwa walioorodheshwa katika Jarida la Forbes la wanawake wenye uwezo mkubwa duniani 2022, ikiwa ni mara ya pili mfululizo.

Leo Desemba 11, 2022 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Pindi Chana amepokea tuzo kwa niaba ya Rais Samia jijini Dodoma ambayo imemtambua Mkuu huyo wa nchi kama muongoza wataliii bora kupitia filamu ya 'The Royal Tour' ambayo imetajwa kuleta ushawishi wa kitalii nchini.

Kwa mujibu wa Dk. Chana sekta ya utalii imeendelea kukuwa nchini, kwani mwaka 2021 Tanzania ilipokea watalii 992,692 lakini mwaka 2022 imepokea watalii zaidi ya milioni 1 huku wengine wakiendelea kuingia.

Mwananchi updates.
 
Back
Top Bottom