Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,036
Siku chache zilizopita Rais Mstaafu Ndg. Benjamin Mkapa alipokea tuzo ya Uongozi Duniani kutoka Taasisi ya mhifadhi wa sokwe-mtu Dr. Jane Goodall katika maadhimishisho ya miaka 30 the taasisi hiyo. Rais Mkapa aliipokea tuzo hiyo "kwa niaba ya Watanzania" kwa maneno yake mwenyewe.
Sasa, sipendi tena sitaki Rais Mkapa aendelee kuzungumza kwa niaba yangu huko nje ya nchi na kupokea tuzo kwa niaba ya Watanzania wakati ameamua kuwadharau na kuwaona hawana mpango. Kitendo cha yeye kuendelea kukaa kimya dhidi ya tuhuma mbalimbali zinazomkabili ni kitendo cha dharau, kiburi, na kisicho cha kiungwana dhidi ya watu waliompatia nafasi hiyo aliyonayo leo!!
Wakati umefika Rais Mkapa azungumzie tuhuma zote zinazomkabili zinazohusiana na utendaji kazi wake akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
a. Kutumia vibaya ofisi yake kwa kufanya biashara akiwa Ikulu
b. Kutumia madaraka yake vibaya kujipatia mali kwa kutumia cheo chake na kujiingizia biashara kutoka fedha za serikali
c. Kujichumia mali za haraka haraka kwa kutumia cheo chake kama Rais
Na aseme sasa, au anyamaze milele!