Mkuu
Mwita Maranya,
Kwa upande mmoja nakubaliana na wewe kuhusu suala la kuwa na National Airline lakini kwa upande mwingine sioni ni issue sana especially under existing socio-economic activities in the country (nafahamu utanishangaa; but I mean it). Kwanza kabisa tukumbuke kwamba faida kubwa ya kuwa na National Airline ni kuongeza consumers(passengers) confidence especially domicile country(yenye ndege husika) inapokuwa haina socio-economic activities za kuweza ku-attract private airlines from different parts of the world. Hapa maana yangu ni kwamba, endapo nchi haina socio-economic activities za kutosha basi vilevile itakosa direct routes kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa sababu watu hawana sababu za kwenda huko; kwamba world population inakosa kikubwa cha kufuata kwenye nchi husika, so direct flight nazo zinakuwa haba coz hakuna demand kwenye given route! Chukulia UAE mathalani, kila mmoja duniani angependa kutembelea Dubai at least once in his/her life time. Kutokana na hilo, ndipo utakuta nchi mbalimbali zina direct routes/flights to Dubai coz tayari kuna wanaotaka kwenda huko for various socio-economic activities.
Hivyo basi, ikiwa nchi husika haina attractive socio-economic activities za kuweza kuvuta watu toka sehemu mbalimbali dunaini, hapo ndipo suala la kuwa na National Airline linapokuwa na umuhimu wa kipekee! Umuhimu huu unatokana na ukweli kwamba nchi husika haina opportunities za kutosha za kuweza kushawishi private companies ku-establish direct routes/flights kutoka sehemu mbalimbali duniani coz hakuna demand ya kutosha. Katika mazingira kama hayo, ndipo National Airline inatakiwa kuziba pengo ili hata wale wageni wachache wanaotaka kuja nchini kwako nao waweze kuja pasipo na usumbufu wa kubadilisha badilisha ndege na kuwa-disappoint kiasi cha kutotamani kuja tena ikiwa hana sababu za msingi za kuja! And in most cases, National Airlines za aina hii huwa zinajiendesha kwa hasara. So, hata leo hii ukawa na Air Tanzania, am afraid inaweza kujiendesha kwa hasara vilevile si tu kwa sababu hatuna uwezo wa kushindana na mashirika makubwa bali pia our socio-economic activities hazijawa attractive enough kuweza kuvuta watu toka sehemu mbalimbali duniani kiasi cha Air Tanzania nayo kuifanya kuwa na route nyingi zaidi na hivyo ku-enjoy economies of scale/size ( kwa lugha nyepesi, economies of scale ni ile hali inayofanya a unit production/operation cost kupungua with increase in sales).
Mungu ametujaalia gas, now its our turn ya ni namna gani tutayatumia/tuta-invest mapato ya gas (usiingize siasa hapa, CCM na CHADEMA wote sawa). We can then decide what kind of economy do we need to have? Weve wildlife na attractive beaches; but why do beach tourism isnt growing? Hivi wakati wa Ukoloni ingekuwa biashara ya utalii imekomaa kama hivi sasa, je kule Oysterbay Wakoloni wangefanya ni makazi ya watu au wangeanzisha tourism belt? Je, tubadilishe matumizi ya ardhi kuanzia Oysterbay hadi Msasani kwa eneo lote linalokaa within 500 meters or more from the offshore na kisha tukatengeneza tourism belt? Anyway, ikiwa ya kawaida yametushinda, tunaweza kuanzisha hata crazy stuffs! Tunaweza kukubaliana na kuanzisha Walking Naked Festival ambapo in one particular day; wote tunasaula kila kitu na kujimwaga mitaani huku tukisakata mdundiko huku madushelele yakininginia!! Watu/watalii lazima wafurike kuja kuangalia this crazy community!
Hivyo basi, kwa maoni yangu, issue kubwa kwa sasa si kuwa na National Airline ingawaje Watanzania wengi tunaamini kutokuwa na National Airline ni kosa kubwa sana kiuchumi! Jambo la msingi ni ku-diversify our socio-economic activities zitakazofanya watu kutoka sehemu mbalimbali duniani KULAZIMIKA kuja Tanzania! Kukiwa na various socio-economic activities, idadi ya wasafiri nayo itaongezeka, and automatically private airlines from different parts of the world zitaongezeka tu. Lakini kuongezeka kwa private airlines nako kunahitaji pamoja na mambo mengine uwanja wa kisasa unaoweza kuhudumia ndege za ukubwa wowote. So, kumbe hapo ndipo unapoonekana umuhimu wa kuwa na new terminal.Tukichanganya pia na suala zima la customer care, safety and security of our customers (airlines na abiria), basi number of passengers inaweza ku-skyrocket within few years hata kama hatuna national airline ingawaje am not abusing umuhimu wa kufufua shirika hilo.