Third terminal at Dar es Salaam airport

Third terminal at Dar es Salaam airport

kwa Tz hata tulizopata uhuru sawa hatulingani kiuchumi..Ingawa tumebarikiwa Rasilimali za kutosha..

Tumekuwa tukikaribiana kiuchumi na nchi kama Malaysia miaka ya 2000 mwanzoni..Lakini hivi sasa wametuacha mbali mnooo..Huku wakitegemea zao la....Mpira na Mafuta kidogo..

Tunahitaji kubadilisha mfumo..

Tatizo ni Leadership na sio Muda. FaizaFoxy
Mmepata jibu sina haja ya kuongezea faiza and liz
Nimekupa mfano mdogo wa Songwe airport Mbeya...iliimbw kuwa inajengwa international airport..juzi domestic freight tu..fastjet imekuwa shida mpaka waka adjust ratiba ya kuanza safari..hapo ndo siasa zilipotufikisha...ukubali au ukatae ndo tatizo la Tanzania!
 
Last edited by a moderator:
30 year ni mingi sana, usishangae 2016 wanaanza tena kubomoa kwa ajili ya kupanua, hii nchi wana plan za mwaka tu, Huwa najiuliza ilikuwaje Wakajenga Stend ya Mabasi Ubungo and then leo hii wanaibomo sijui kuipeleka wapi. na huko zinako pelekwa baada ya miaka mitano utasikia zinahamishwa tena

Kwa serikali hii, usishangae wakaihamishia bagamoyo au msata
 
Usilinganganishe Jomo Kenyatta airport na Mwl Nyerere airport , Jomo Kenyata kila baada ya dakika 20 ndege inaruka ,Mwl Nyerere airport ni kama airstrip tu
Wapi nimelinganisha kabla ya kujibu post jaribu kusoma uelewe mada.
 
Ritz...
Airport ya mkoloni ni pale Leaders Club....
Jengo la bar ndio lilikuwa terminal..

Tukirudi kwenye mada.
Eneo liliopo kwa upande wa barabara ya Nyerere (Pugu road) labda bado ipo nafasi ya terminals na support structures.
Tatizo kubwa ni katika kufanya runway length extension au kujenga parallel runway. Dar airport runway haizidi futi 10,000 ambazo ni chache mno kisheria kwa ndege kubwa kuweza kuruka na uzito wa juu.... (High Take Off Gross Weight). Kama maendeleo yatakwenda vilivyo, ikifikia kuingiza abiria 3mill na kutoa 3mill, inamaanisha runway utilisation itakuwa overstretched.
Kama wataalam wangekuwa wabunifu wazuri, pale ni pa kuhama, wawaachie jeshi/domestic na VIPs kutumia.
Mkuu,

Nikuulize swali la msingi hivi Tanzania tunaweza kuwa tuna wasafiri 15,000 kila siku.
 
Marekebisho Tanzania Airport Authority ndio wamempa mkataba BAM na wala sio Tanzania Civil Aviation Authority kwan izo ni Authority mbili tofauti kabisa
 
Huu uwanja wa Jomo Kenyatta ndiyo wakuutolea mifano wakati mweingine tuwe makini wanaukumbi hebu angalieni huu uwanja hapa chini amabao Mwita Maranya anautolea mifano kila kikicha.

eeh-eeh-eeh guys need to be serious hii ni airport ama ni old military base? sioni chochote cha maana JKIA mpaka wajenge hiyo airport yap mpya lets the truth be told
 
Mwita Maranya.

Haujaona airport ndiyo maana unapenda kuitaja Jomo Kenyatta, haiwezi hata kuwemo kwenye airport kumi bora afrika, toa mfano
OR Tambo, Cape Town, Cairo.

Hujamsoma Mwita, nadhani ailichokuwa anajaribu kusema ni kwann Joma Kenyatta wanaroom kubwa ya expansion wakati sisi hatuna na airport yetu ni mpya kuliko yao? Kwanini tufikirie kugrow kutoka 1.2m to 6m pekee na si zaidi ya hapo? That means tutakuwa tunajenga hivi viwanja mpaka lini? Besides, nimepata bahati ya kwenda OR Tambo and hiyo Joma Kenyatta several times, sidhani kama zinatofautiana kihivyo kama unavyojaribu kupain hivyo hapa.
 
Mmepata jibu sina haja ya kuongezea faiza and liz
Nimekupa mfano mdogo wa Songwe airport Mbeya...iliimbw kuwa inajengwa international airport..juzi domestic freight tu..fastjet imekuwa shida mpaka waka adjust ratiba ya kuanza safari..hapo ndo siasa zilipotufikisha...ukubali au ukatae ndo tatizo la Tanzania!

Mkuu Rugas hivi kigezo cha uwanja kuitwa wa kimataifa ni kipi? make Bongo viwanja vyote ni vya kimataifa hadi cha Kigoma, ingawa kwa siku zinatua ndege mbili au moja tu. Make uwanja kama wa KIA huwa wa kimataifa Jioni pale zinapo tua KLM baada ya hapo ni hakuna kitu
 
Last edited by a moderator:
Ukiangalia ukubwa wa Jomo Kenyatta International Airport lakini bado sasahivi serikali ya Kenya inafanya uwekezaji wa kutosha katika kuupanua na kukarabati majengo ya zamani na kuyafanya ya kisasa zaidi, pamoja na kuongeza ''run ways" ndipo utagundua kuwa serikali ya ccm imo shimoni inasubiri kumwagiwa udongo tu.

Yaani watu hawawezi kufukiria kujenga uwanja utakaohimili matumizi kwa miaka 30-50 ijayo wao wanafikiria umbali wa pua zao eti watu milioni 3!!!

Bobby

Msome tena Mwita halafu soma tena majibu yangu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ritz unapenda siasa!!! hata hii umeitupia huku!!

Mimi naamini hata wewe huridhiki na huo mchoro ..Ila ndio hakuna la kufanya..

Tanzania nchi ya maajabu sana...

Raia anaweza kumiliki Ndege lakini serikali haiwezi..

Pengine unge-binafsishwa tungepata bora kuliko huo tunao utarajia...
Mkuu prs

Siasa ndiyo zinatawala taifa letu na ndiyo zinafanya maamuzi kwenye jambo lolote linalohusu taifa.
 
Last edited by a moderator:
Go Tanzania Go,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Love you Tanzania.Kitu kama Heathrow Airport
Maajabu ya Waafrika utashangaa kwamba kuna wengine ambao ni Watanzania kwa 100% lakini huwa wananyongeka sana wanapoona taarifa kama hizi! Yaani watokacho wao ni kuona Tanzania inadidimia ili wapate cha kisema kwenye majukwaa ya siasa za nje na hapa JF! Mungu awalaani wote hawa!
 
Ndugu embu tupige hesabu ndogo tu.
Watu 6Mil kwa Mwaka ni sawa na watu 15,500 kwa Siku Je ni kweli tunaweza Kufikisha Idadi hiyo ya ABIRIA kwa siku ndani ya hata kipindi cha Miaka 10 ijayo?

Ndugu yangu, tunapaswa kuwaza na kutenda mambo makubwa. Enzi za Awamu ya Kwanza, walipochukua eneo la Chuo Kikuu (Mlimani), wapo walioishangaa Serikali ya wakati huo. Walihoji, eneo lote la nini? Leo mnajionea. Badala ya kuongeza vyumba vya mihadhara, maabara na maktaba, ninyi mnaongeza malls!! Awamu hiyo hiyo ya kwanza ilipojenga Port Access (Mandela Road) wakati huo, wapo walioshangaa na kubeza. Walihoji iweje barabara ya lami ipite porini (Tabata) na kuacha sehemu kama Magomeni zenye binadamu? Lakini wenye akili waliendelea na mradi na matokeo yake Tabata umekuwa mji mkubwa leo, na kwa kweli hata hiyo barabara inaonekana ni ya mtaa, na si ya Taifa! Ninachokusudia kukisema hapa ni kwamba tunapaswa kuwaza na kutenda mambo kwa kuona mbali zaidi. Hata nyumbani kwako, ukiwa na busara huwezi kununua kiti au meza ya 'mchina'. Ukiwa na busara utanunua mninga, na hapo utakuwa umeondokana na kununua kiti au meza kila mwaka! Ukiwa Marekani au Ulaya, utayaona majengo yaliyojengwa miaka 200 au 300 iliyopita. Unaona kabisa bado yataweza kuishi hata karne kadhaa zijazo. Hapa kwetu tunajenga kile kilichosemwa na Mateo Qares kule Mbeya kuwa ni nyumba ambazo teke la kuku linatosha kuzibomoa! Nasisitiza, tubuni na kutenda mambo makubwa yatakayodumu kwa miaka mingi ijayo.
 
Mimi nazani kinacho wasumbua viongozi hakijaanza tu from no where hii Inaonyesha jinsi gani watanzania hatuna utamaduni wa kutumia wataalamu katika shughuli zetu za kila siku hawa ndo viongozi walioenda kwenye kikombe cha babu wa samunge wakasahau madaktari wao. Ni mara ngapi tumejenga nyumba zetu kwa kutumia wataalamu kama sio mafundi wa mitaani. Mara ngapi tunakunywa dawa hata kabla ya kujua tunaumwa nini. Mara ngapi tumetumia wataalamu katika biashara zetu. Sasa haka ka tendency kanaamia hadi kwa viongozi na utaratibu wa kawaida sehemu ya kutumia wataalamu watu wana tumia busara zao na uzoefu kumbe wanaharibu
 
Haya mapicha nayaona zaidi ya miaka mitanoi sasa hapa JF

Hata pale airport yalibandikwa wakasema uwanja utakuwa tayari 2014. Ni yake yale ya Kigamboni City. Wameshajuawatanzania wanapenda sanaa za maonyesho
 
Ukiangalia ukubwa wa Jomo Kenyatta International Airport lakini bado sasahivi serikali ya Kenya inafanya uwekezaji wa kutosha katika kuupanua na kukarabati majengo ya zamani na kuyafanya ya kisasa zaidi, pamoja na kuongeza ''run ways" ndipo utagundua kuwa serikali ya ccm imo shimoni inasubiri kumwagiwa udongo tu.

Yaani watu hawawezi kufukiria kujenga uwanja utakaohimili matumizi kwa miaka 30-50 ijayo wao wanafikiria umbali wa pua zao eti watu milioni 3!!!
Mkuu Mwita Maranya,
Kwa upande mmoja nakubaliana na wewe umuhimu wa mambo in the Long Run! Hata hivyo, kwa upande unatakiwa kujiuliza je, umefanya projection na kufahamu hiyo idadi ya 6 million passengers itafikiwa lini? Hilo ni muhmu kuangalia coz' wanaposema wanajenga uwanja utakaoweza ku-cater 6 million passengers annually haina maana kwamba up on completion, hiyo idadi itafikiwa mara moja! Kwa mfano, ukiangalia takwimu za Tanzania Airport Authority, kipindi kuanzia 2001 hadi 2011 abiria waliongezeka ni takribani 1.2 million over the entire time; wastani wa abiria 120,000 kwa mwaka! Tukichukua kuanzia 2009-2011 (nimechukua hiyo interval coz' 2008 walifikia peak lakini 2009 wakashuka; probably kutokana na world's economic crisis), wastani wa abiria ambao waliongezeka kwa mwaka ni takribani laki 1.3 kwa mwaka, ingawaje namba ili-shoot between 2010-2011 (probably SA world cup ilisaidia kufanya watu kupitia JNIA na vile vile kipindi hicho Uwanja wa taifa ulikuwa busy sana na international matches). So, kwa kuangalia hayo, inawezekana kabisa hawaja-forecast far enough lakini vilevile sidhani kama forecast iliyofanyika ni ya kijinga zaidi! But on top of that, kinachojengwa ni terminal three; terminal two ipo pale pale hata kama itabadilishwa na kuwa for domestic flight; so any time inaweza ku-resume ku-cater international flights when necessary!
 
Last edited by a moderator:
Hapa wengine hatuwezi kuchangia maana Pasport zetu zimeishia kupigwa mihuri ya Malawi baaaaaasi!
 
..GUNDU la 10% nalihofia lisije penyeza mradi utakapoanza
 
Mkuu,

Nikuulize swali la msingi hivi Tanzania tunaweza kuwa tuna wasafiri 15,000 kila siku.

Kwa sasa hatuwafikii hara robo ya hao.
Lakini kumbuka hesabu hizo ni kwa arrivals na departures. Inamaanisha ndege kama ya Emirates Boeing 777 ni flights kama 25 tu kwa siku!
Linganisha na kiwanja cha Nairobi, ambacho ninahisi hawapungui flight zaidi ya 30 hadi 50 kwa siku.
Heathrow ndege kubwa inatuwa na kuondoka kila baada ya dakika tatu kwa wastani!!!

Hatuwezi kujilinganisha na Heathrow, lakini tunaweza kabisa kuchukua mfano wa explosion of South East Asian countries economies.

Why not plan ahead as Malaysians have done with monimal resources? Is our critical thinking so restricted to depend solely on what others tell us.
Iko obvious kama uchumi wa nchi ukipanda at the rate ya sasa, hio terminal ya 6million, ni miaka michache tu itazidiwa nguvu. Nafasi ya kupanua, hasa runways, pale kiwanjani hakuna tena.
Zaidi ya yote ni hatari saaana kwa makazi ya watu kuwa karibu na airports. Ikija tokea ajali ndege kuanguka on final approach pale kipawa, itakuwa ni janga kuu hilo.
 
Maajabu ya Waafrika utashangaa kwamba kuna wengine ambao ni Watanzania kwa 100% lakini huwa wananyongeka sana wanapoona taarifa kama hizi! Yaani watokacho wao ni kuona Tanzania inadidimia ili wapate cha kisema kwenye majukwaa ya siasa za nje na hapa JF! Mungu awalaani wote hawa!

Unachotaka ni kipi?
Maendeleo bora??? Au
Bora maendeleo???

Kuna ufinyu wa dira kuona mbali kwa wataalam
wetu. Wamevuruga mengi mno.
Kwa mfano hadi sasa barabara zinatengenezwa za lanes mbili tu kila upande.
Tatizo la traffic jam baada ya miaka michache tu toka sasa litarudi pale pale!!!
Mambo duniani siku hizi ni mabarabara ya lanes 3 au 4 na zaidi.
Ni gharama za kijinga kurudia kufanya kitu hicho hicho kila baada ya miaka michache, iwe ni ujenzi wa airports au barabara au vinginevyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom