REALITY
JF-Expert Member
- Jul 2, 2014
- 4,391
- 1,960
- Thread starter
- #1,801
Majibu yako yapo mengi sana kwenye thread pitia taratibu utayaona.Kitu kisicho make sense kwako hakimaanishi kuwa na kwa wengine kiko hivyo. Tena hususani kwa watu waliofanya tafiti zao kwa muda mrefu sana.
Ni sawa na mtu anayeamini kuwa chombo pekee kinachosafiri baharini ni meli. Siku ukija kumuambia kuhusu uwepo wa submarines atakukatalia kata kata na kukuambia kuwa hakina maana, "chombo hicho chawezaje kusafiri kikiwa kimezama?" Practically nonsense! Bila shaka tegemea majibu au maneno yanayoshabihiana na hayo kutoka kwake.
"Uongo mtakatifu ulio generated from Babylon"??? Nini mantiki ya uwepo wa maneno haya katika hoja yako, unaweza kuthibitisha, kwa sababu gani na ili iweje???
Unasema kuwa "Flat Eathers wako sahihi asilimia zote", ya kwamba wanayaelezea mambo katika uhalisia wake.
Sawa, tuanzie katika maswali machache tu yafuatayo;
Je, unawezaje kuuzungumzia mzunguko wa jua katika hiyo flat earth kwa mujibu wa Flat Earthers? Ni kitu gani hulifanya jua liweze kuzunguka pembeni mwa dunia bila kugongana na uso wa dunia? Nipatie maelezo yaliyo na huo "uhalisia".
Swali jingine, nini hutokea pale ambapo kitu chochote kitakapofika na kujaribu kuvuka pembezoni mwa hiyo dunia ya tambarare?
Nikukumbushe tena kuwa, usisahau kunipatia maelezo yenye huo "uhalisia" kwa mujibu wa Flat Earthers.
Asante!
Sent using Jamii Forums mobile app
