Obama anasema kuwa jamaa anafyatua risasi kwanza halafu ndipo analenga kwenye target yake, wakati risasi imekwisha enda hewani!
Nadhani yote hiyo ni sababu ya desparation; yeye aligombea kwa ego ya pesa tu bila kujua kuwa national politics zinahitaji busara zaidi ya mabavu ya pesa. Wakati akina Rush Limbaugh anatukana mtoto mdogo matusi ya nguoni, jamaa alishindwa kumkemea; nadhani huenda ni kutokana na makosa ya ububu wa wakati huo ndiyo sasa ameamka na kuanza kuropoka kwa kila tukio bila kutumia busara.
Ni kutapa tapa kwasababu anaona anashindwa.Juzi kwa upuuzi wake,eti ameponda hadi stimulus mpya ya feds iliyotolewa na Ben Bernanke juzi na markert zikareact positively(dow,nasdaq).
Yani kama unakumbuka,jamaa alivyoingia madarakani tu,ikaanza ile movement ya birthers,ambapo azimio lao kuu waliweka wazi kuwa ni kuhakikisha Obama ana fail in everything kwasababu si mmarekani!
Sasa wana wasiwasi kuwa move ya feds itamfavor Obama zaidi,mkuu yani hawa ni watu ambao wako radhi kulifelisha taifa lao simply kwa chuki dhidi ya Obama!
Sasa kwasababu ni wazi kampeni ya Romney inaelekea shimoni,usishangae kusikia na kuona vitu vya ajabu ajabu na kauli za kipuuzi kuliko wakati wowote kwenye historia ya taifa la marekani.
Halafu hata wengi wa republicans hata hawajui plan ya Romney,wakiulizwa wanakiri hawajui,wale wanazi huwa wanarukaruka bila kujibu na kutoka nje ya point.Huntsman ambaye ni republican,amesema naye hajui plan ya Romney,wanazi wa Romney hawajibu kwa kuelezea hizo plan,badala yake,wana pin point kwamba Huntsman aliteuliwa na Obama kuwa balozi wa marekani huko China,sasa hapo sijui ndo kumemfanya kuwa liberal kama Obama?Ni vituko...
Halafu juzi,kwenye Fox news poll ambayo ndiyo yao republicans,Obama ameonekana kuongoza kwa 6 points from likely voters!Bill Oreilly akaongea ujinga,badala ya kutangaza matokeo tu kama channels nyingine wanavyofanya kwenye polls,akamleta mnazi mmoja mchangiaji wa Fox News ambaye eti anadai kuwa Romney atashinda uchaguzi,yani hivyo ndivyo Fox news walivyoamuwa kutangaza kuongoza kwa Obama kwenye polls za tv station ya republicans.
Romney hana lake I can bet whatever on this,ushabiki acha pembeni,kuna akili za wengine humu ni fyatu tu,sitegemei kuona mtu anaongea ukweli zaidi ya kumdegrade Obama na vijimatusi vya kijinga.Mwulize huyo mtu kama anatengeneza over $250,000,halafu utapata jibu how some of us ni wajinga kabisa na matope humu.Yani ushabiki tu.