Kijakazi,hii issue ni very complex,na kuilezea ni shida sana,ila nitajaribu,na kama utakuwa na maswali ya ziada,basi nitajaribu pia kuendelea kuyajibu kadri ya uwezo pamoja na ufahamu wangu kuhusiana na issue hii.
Kimsingi,hao electors huchaguliwa na chama pamoja na wagombea wao.Ila chama kinateuwa mtu ambaye kinauhakika kwamba hawawezi kwenda kupiga kura tofauti na matakwa ya chama na mgombea wao.
Wanavyopatikana hao electors,ni kwamba kama chama kina member wa house of representative,basi kinapata elector mmoja,na kama chama kina senator,basi kinapata kibali cha kuwa na electors wawili.Kwasasa kiukweli,maybe ndo maana mahesabu ya The Boss yanaonyesha Obama ana electors wengi,ni kutokana na ukweli kwamba republicans wana representatives wengi kwenye house,however democrats,wao wana senetors wengi ambapo mmoja tu anacount kama electors wawili.
Kwa kifupi,kila state inawakilishwa na electors kulingana na namba ya congressional delegations.Kuna jumla ya electors 538,lili msindi apatikane,ni lazima ashinde electors 270 ama zaidi.
Inavyotakiwa,mgombea anayeshinda kura za wananchi(popular votes),ndiye anayetakiwa apigiwe kura na hao electors,lakini hawalazimishiwi kufanya hivy
😵nly in some states ndo huwa wanalazimishwa kufanya hivyo.
Pia kama ikitokea kwamba kuna elector aliyepiga kura tofauti na matakwa ya chama chake,"faithfulness"basi kuna states zinaruhusu chama kiwafungulie mashtaka na kutangaza kwamba kura hiyo imeharibika ama ni batili.Yani ikatokea kuwa elector akampigia kura mgombea wa chama pinzani.
Sheria hizi pia ni tofauti kwenye states za Maine pamoja na ile ya Nebraska.Utofauti wake ni kwenye upatikanaji wa hao electors.
Kabla sijaenda mbali zaidi,nataka nisubiri kuona kama umepata mwanga kidogo na kama una maswali zaidi.Ninavyofahamu,kuna pro electoral college na ambao wako against.
Wanaosapoti ndo wale wanaosema kwamba states zenye minorities zinaweza zisipate uwakilishi mzuri,yani kama kura za majority ndo zitaamuwa moja kwa moja,basi kuna hatari ya minorities kuwa sidelined kwenye maamuzi ya taifa.Pia walitaka states ndogondogo nazo ziwe na sauti kwenye uchaguzi wa rais.Kwahiyo hata kama state ina population kubwa,bado inaweza isiwe na electors wengi kuliko state yenye population ndogo,yote ni kudumisha muungano wao na kuondoa possibility ya tyranny,kama yale ya ujerumani na Hitler etc.Wanadai kuwa hiyo ni process amabyo pia dhumuni lake ni ku compromise kati ya uchaguzi wa rais kutoka kwa wananchi vs kutoka kwenye congress.
Na wanaopinga pia wanasababu zao,kubwa moja ndo hiyo kwamba sauti ya wengi ipo hatarini kutokusikilizwa.
Sababu zao zipo nyingi tu,lakini kama nilivyosema hapo awali,nataka niishie hapa ili uabsorb hizo details hapo juu kwanza,na kabla hatujaendelea mbele,kuona kama kuna pahala hukuelewa ama kama sikujieleza vyema.