The US Presidential Elections-2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The US Presidential Elections-2012

Discussion in 'International Forum' started by jmushi1, Sep 1, 2012.

 1. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Nakumbuka 2008 kulikuwepo na thread ya uchaguzi wa marekani ambayo kama sikosei ilikuwa ya GT.This year,miaka minne imepita na sasa uchaguzi ni November.Tunaweza kuitumia thread hii kutoa maoni yetu na pia kupashana habari za kuhusiana na kampeni na uchaguzi wenyewe.

  Binafsi ninaamini mchuano utakuwa mkali,na sasa kampeni zimepamba moto,tumeshuhudia vituko na mambo ya kushangaza,mfano ni ile hotuba ya Clint Eastwood kuweka kiti na kuongea nacho kama vile anaongea na Obama.Lakini kwa dharau kubwa na matusi!

  Mpinzani wa Obama,yani Romney,yeye anajinasibisha na ufanya biashara,kwamba ana uzoefu na biashara na ameendesha biashara zake kwa faida na hivyo ujuzi wake huo anaweza kuutumia kulikwamua taifa kwenye matatizo ya kiuchumi inayokabiliana nayo.

  Obama wote tunajuwa,yeye anasema anapigania haki za middle class pamoja na wananchi wenye vipato vya chini.

  Anasema kwamba maendeleo ya nchi yanatokana na kipaumbele kupewa middle class,amekuwa akitumia maneno kama vile "we will build the economy from "the middle out" and "from the bottom to top"

  Anasema wanaostahili msamaha wa kodi ni wananchi ambao hizo pesa watazitumia na hivyo uchumi kukuwa,na si kuwapa misamaha zaidi matajiri wakubwa ambao hawazihitaji, kwani hilo ndilo Bush alilolifanya lakini matokeo yake ni economic crisis,kwahiyo anasema hatuwezi kurudia hayo tena kwani doing the same thing over and over again expecting different results ni dalili za ukichaa!

  Issue wanazopingana ni nyingi,tutaendelea kukumbushana,kuna women rights na mambo mengine kama vile health care na National security vikiwemo vita.

  Lakini kubwa kuliko yote ni uchumi,na wakipimwa kwenye hilo,inaonekana kama vile Romney ana upper hand kwani polls zinaonyesha kuwa watu wana imani naye kwenye issue za kiuchumi kuliko Obama.

  Jambo ambalo wengine tusingependelea,ni kama watu wa Obama wataanzisha vita kwasababu wanajuwa kuwa ikija kwenye security,basi Obama yuko juu especially mara baada ya seal 6 team kumwua Bin Laden kwa amri yake...Tuombe Mungu hilo lisiwe the case kwasababu vita always si nzuri,lakini tumeshashuhudia mambo kama hayo yakitokea.

  Nitaendelea kuleta habari na maoni kuhusiana na uchaguzi huu,pia mnakaribishwa kuchangia lolote kuhusiana na uchaguzi na wagombea pamoja na kampeni zao.

  Kama kuna thread kama hii imeshaazishwa,basi mods mniwie radhi na muiunganishe na hiyo nyingine kama ipo.
   
 2. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kuna report nimesoma inasema Iran's nuclear plants are at the highest level of activities, hii inanipa sababu za kuamini kuwa October Surprise itatokea kwa Obama kulipua vinu vya nuclear vya Iran, kama polls zitaonesha mambo magumu upande wake. Tusubiri tu ila nina wasiwasi na hilo. two weeks before election Iran itapata kichapo cha ghafla.
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Tuko pamoja kwenye hilo,kama ikionekana issue ya economy inaweza kumlet down,wanaweza wakafanya hivyo watu wake.
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Republicans wana spin machinery yenye nguvu sana, wakati Obama na Democrats wako passive sana na ndiyo maana walinyang'anywa Congress mwaka 2010.
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Don't underestimate the Chicago political machine.
   
 6. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Nasubiri kwa hamu watakapokutana kwenye debate...
   
 7. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Republicans this time wamepania aisee!nadhani hizi kampeni zita turn realy dirty as days goes on.Ile issue ya kiti ya Eastwood inatafsirika kwa namna nyingi sana.Kwanza miaka ya nyuma ndo ilikuwa racial stunt ya an "invisible blackman",ila sidhani kama watu wa Obama wata capitalize on that.

  Btw si unajuwa kuna wanajeshi watatu wana face death penalty kwa kupanga kumu assasinate Obama?halafu wakawauwa wenzao wawili ambao walisema watalikisha habari.Kuna mambo mengi sana ambayo hatujui yanaendelea.However miye nachosubiri ni hiyo debate.
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Hilo la dirty campaign nakubaliana nalo.Lakini hao msnbc hata kama ni kweli wanaona issue zina racial undertones,kuna ukweli pia kwenye hayo kwasababu Romney campaign ni lazima waifurahishe base(kama unavyojuwa alistruggle for one reason yeye ni a mormon).Na pia kuwa please wale ma "far right nuts" na tea partiers.Kama wanataka kura za wale wanaoamini Obama si mmarekani nk.

  Ni kweli enthusiasm si kama ile ya 2008,maybe wataenergize base baada ya convention ya on Monday.Kwasababu hata Romney convention imemsaidia sana na kum "humanize"
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Sep 1, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Ila ukweli GOP wako negative sana na wanasema uwongo sana, na hawataki kumpa Obama credit yoyote anayostahili.

  Alipoamua kutuma majeshi kwenda Pakistani kumwua Bin Laden katika mazingira yaliyokuwa yamejaa uncertainty; wao wanadai "any president could have done it", aliposaidia viwanda vya magari kiasi kuwa leo Ohio na Michigan zanaanza kunafanya vizuri kiuchumi, wao wanadai kuwa hayo ni matokeo ya ya Republican Governors. leo hii Marekani inachimba mafuta na gesi kuliko wakati wa utawala wowote uliopita, wao wanadai Obama anazuia marekani ishichimbe mafuta na gesi. Aliposema kuwa tutasimamia Medicare ili kuzuia matumizi mabovu ya dola bilioni 716 ambazo huwa zinaliwa na makampuni ya insurance, halafu pesa hizo zifanye jambo jingine, waoa wanadaia Obama amchukua dola bilioni 716 kutoka Medicare.

  Ila kwa vile wamarekani wengi hupiga kura kwa kufuata upepo, inategemea sana upepo utavumia wapi. Huwa hawachambui facts. Tusubiri tarehe 15 October ndipoi tutajua upepo unavumia wapi, ingawa kweli nina wasi wasi sana kuwa Obama atazimiwa Oksijeni, kwa vile spin machinery ya GOP ikisaidiwa na Fox News iko well equipped kwa zaidi ya dola trilioni tatu za kumvuruga Obama tu. Superpacs zao zina fedha nyingi na zinaendelea kuvuta fedha zaidi kutoka kwa mamilionea, Fundrising zao za sahani moja kwa dola elfu hamsini zinaleta fedha nyingi sana kutoka kwa mamilionea hao hao, na sidhani kuwa Obama anaweza kushinda uchaguzi Marekani akiwa underfunded!
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Mkuu toka walipomkwamisha kwenye kupitisha issues kibao kwenye "house",ambazo zingemake a huge difference,naamini that they're capable of doing anything kama wakipata nafasi hiyo,kwasababu wamemsabotage in every possible ways.Hata licha ya kwamba Bush taxes bado zilikuwa applicable na pia lawful,bado hawakutaka kuinvest.Yani wanamchukia jamaa haswa.

  Wallstreet walmsapoti vibaya sana elections za 08,wakidhani atawapendelea kwasababu hiyo,ni ile nguvu ya umma iliwatisha,lakini msimamo wake baada ya kuchukuwa madaraka ulikuwa pale pale kuhusu regulations.Sasa wametupa all their support kwa Romney.Inasemekana itakuwa the first time in history for the incumbent kuwa outspent.

  Wale matajiri waliomsapoti mara ya kwanza,ndo sasa wamemgeuka na wako radhi kutumia mbinu yoyote ile.Hata Romney mwenyewe mormon lakini hawajali hiyo.Tujitayarishe kuona mengi,maana wamepania haswa.

  Tuombe tu usalama maana desperation yao si mchezo,kuna wanao suggest kuwa akishinda atauwawa ama nchi itaingia kwenye civil war
   
 11. sabasita

  sabasita JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  nasubiri utakapoficha uso wako
   
 12. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Katika historia ya uchaguzi marekani,haijawahi kutokea mgombea wa Republican kushinda urais bila ya kushinda jimbo la Ohio.Na kwahiyo wamejipanga kuhakikisha wanalichukuwa jimbo hilo.Ni mojawapo ya majimbo ambayo wanayaitwa "battle ground states"

  Uchaguzi uliopita,Obama alishinda lakini it was close.Mojawapo ya sababu ambazo democrats wanadai ziliwasaidia kushinda,ni pamoja na kuruhusu upigaji kura wa mapema(early voting),na watu ambao walipiga kura hizo ni wale wa kambi ya Obama,watu hao ni 93,000,namba ambayo ni very enough kubadili matokeo given that it is very close kwasababu Ohio ni pretty much a conservative state.

  Kuna kesi ambayo watu(viongozi wa state)ambao ni pro republicans ya kupinga upigaji kura wa mapema ambayo walishinda,madai yao ni kwamba watu watakopiga kura za mapema wawe ni either wanajeshi ama wamarekani walioko nje ya nchi.

  Watu wa Obama wali appeal,na wakashinda,na hivyo jaji akatengua maamuzi na kuruhusu upigaji kura wa mapema.Madai ya watu wa Obama ni kwamba hatua hiyo ingekuwa imekiuka constitutional right ya kuvote.Na pia wakidai kwamba hilo lilikisaidia chama chao kushinda uchaguzi.Pro republicans wanasema na wao wata appeal siku ya jumanne.

  Kwahiyo republicans wako radhi kushinda hata kama ikiwa ni kukiuka haki za kimsingi za raia wa nchi yao...
   
 13. chash

  chash JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Jamaa labda aokolewe na kura za wanawake na wazee kwa kuwa wanawake hawaja ridhika na kauli ya republicans kuusu rape na abortion, wakati nao wazee wanafaidi sana obama care. Vingenevyo wazungu ambao ni wengi naona wameshaamua kutoa nyeuthi kwenye uongozi. Vijana wa shule wataenda sawa kwa sawa.Miafrika ya marekani ina tabia mbaya sana kila ishu lazima waonyeshe kuwa wanaonewa kwa kuwa ni weusi. Hii imechosha wazungu sana sasa hivi wanataka mtu ambaye hatasikiliza upumbavu huo. Nayo miafrika ya kutoka bongo na nchi za afrika hawana tabia ya kujichanganya na wazungu au race zingine huko marekani. wanataka wakae wao kwa wao tu, hii inawafanya wasiwe na babadiliko sana tofauti na walivyo kuwa nyumbani na nafasi nyingi za maendeleo yao binafsi na jamii zao nyumbani wanazikosa.
   
 14. chash

  chash JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kwa kuwa marekani watu wote ni immigrants, kila kabila linataka liweze kufaulisha targets zake za kiuchumi na kuboresha masilahi ya jamii na kupata faida ya wingi wa watu wake. Kujiunga kwenye hivi vikundi inakuwa na faida kwa races zenye nguvu kama wayahudi na hispanics. Mormons pia wanatabia ya kujitenga kama race na nadhani 99% watampigia romney.Marekani ishu ya race ipo sana kuliko nchi zingine tukiacha nchi za kiarabu.
   
 15. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Kichuguu,

  To be fair kufuata upepo sio suala la waMarekani tu. Kama watanzania wangepiga kwa issue, nadhani landscape of Tanzanian politics could have changed long time ago.


  Now concerning the election, Obama doesn't control the narrative. For, the republicans have managed very successfully to turn the election or the narrative into a referendum on the way the president has handled the economy. Indeed, there are some racial issues in this election but they are peripheral for majority of independent voters.

  People who believe that Obama is a bad president because he’s black, they, probably, didn’t vote for him in 2008 when the economy was so bad and they won’t vote for him in 2012. So there’s no need to complain about this group of voters.
   
 16. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,808
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Yes there's racial issues. But he won in 2008 decisively. So if the tribes of white people in America didn't like him, they would't voted for him in 2008.

  Additionally, Obama is biracial and people who elevated his profile to prominence are white. So I don't know why the work of few and very vocal racists should invalidate the good work of other white who have helped Obama throughout his life.
   
 17. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa hyo tusubiri kuona Iran wakisambaratishwa! Siasa za nje za Merikani zina utata sana. Generally, kampeni za mwaka huu naona kama hazina moto kama za 2008 au ilikuwa ni mshawasha na tashwishi za kuona Rais mweusi na kwa sasa hiyo siyo issue tena?
  Naomba mnisaidie wakuu, blacks na spanish community sasa hivi wanasimama wapi.or their expectations on employment, health were not met and so decided to go against Obama?
   
 18. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Bado hao minorities wako na Obama.Hao wahispanic hawataki mambo ya Romney mzee wa "self deportation"

  Republicans walimsusia nchi,wamepinga karibia kila kitu alicho propose.
   
 19. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  I hear you! The Chicago boys are not out yet!!!
   
 20. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Vipaumbele vya Obama ktk kampeni yake nini,mbali na hyo ya kuwawezesha middle class ulotaja hapo mbeleni.
  Pia nilisikia issue ya dini kwa upande wa Romney kuwa inaweza ikamnyima kura,kwa maana ya kwamba dini yake inaonekana km sio dini ni sect flani tu.
   
Loading...