The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
....CCM ni umaskini na kujirudisha nyuma tuu!

Watu hawataki kuliona hilo bali kuanzia sasa ni vitisho tu, imagine kama kesho hao wanaompinga Kikwete waitishe maandamano Dar, basi watamwaga manjagu kila kona ya jiji kuhakikisha hakuna maandamano yoyote!!! Tunaanza kufananafanana na Zimbabwe ya Mugabe.
 
Bubu ataka kusema,
Mkuu nadhani wewe ndiye usiyeliona maanake umekazania CCM...CCM, kama vile kuna lolote la maana.. CCM ni umaskini kama alivyosema Koba, sasa wewe unaandamana kitu gani ikiwa bado unataka umaskini utawale kwa kwenda nyuma!
 
Babu ataka kusema,
Mkuu kitu kimoja tu Kikwete hakufanya kulingana na wanaCCM nacho ni kumwacha Apson, Mahita, Lowassa, Karamagi, Meghji, na baraza zima la mawaziri . Kikwete katengua katiba ya chama kuwaondoa viongozi wote wanaotaka kufanya biashara wakiwa mawaziri. Utawala wa Kikwete umewafikisha Yona na Mpamba mahakamani..

Pungufu moja kubwa kwa wananchi ni mtu mmoja tu Lowassa..jambo ambalo hakuna kiongozi hata mmoja Tanzania ambaye angeweza hata kumsimamisha madaraka kwa sababu madhambi ya Chimwaga na uchaguzi mkuu waliyafanya wote ndani ya chama..
Na nakuhakikihsia Kitendo cha Kikwete kuwatema Lowassa na mtandao ni ushindi kwa wananchi na wana CCM kwa sababu hakuna mtu ndani ya chama hicho angeweza kufanya hivyo..na leo hii hakuna kiongozi yeyote anayeweza kufanya unayoyataka wewe.kwa sababu sifa unazotafuta hazipo ktk uongozi bora wa CCM isipokuwa nje ya chama.
Huo ndio UNAFIKI kupiga kelele nyuma ya pazia..na bado tu mkuu unakazania JK wakati sijakusikia ukitaja mtu anayefaa!.. sasa Unataka JK ongembee na UKUTA.. yaani turudishe zile picha za uchaguzi wa Nyerere na Ukuta mkuu wangu!
 
Wakuu kinachowauma nini haswa.. yaani hawa wazee hawana haki ya kumteua mtu wanayempenda?.. jamani semeni nanyi chaguo lenu kisha pinganeni na usemi huo wa wazee hao na kuzipanga sababu zenu lakini mnaposema Kikwete hafai aondolewe hali hamna mtu mwingne inachekesha...
Mada hii mefikia kurasa zaidi ya nne na hakuna hata mmoja wenu amediriki kumtaja mgombea dhidi ya Kikwewe kwa tiketi ya chama..
Na nimeliweka swali hilo makusudi kwa sababu naelewa fika kwamba CCM bila Kikwete haiwezi kwenda popote. hakuna na narudia kusema hakuna kiongozi CCM anayeweza kuwa mbora kuliko Kikwete ktk kiti cha Ikulu.. chama kizima Muflisi, kimeshikwa na mafisadi.. Sii Mwandosya, magufuli wala mjomba wake anayeweza kuinua hata kidole against kundi hilo..
Wanaojiweza kidogo ni Mwakyembe, Sitta, Mama Kilango, na Malecela.. hawa wote ni watu wa Kikwete na wanampendekeza Kikwete kwa sababu hawawezi kupita hata Ubunge 2010 kama sio nguvu ya Kikwete..haya tukiondoa hawa huko CCM kabakia nani?..nani anaweza kumkemea Rostam au Lowassa! nani anaweza kusimama na hawa jamaa na kuwatazama usoni akawaambia wanakwenda lupango!..hakuna...
Hakuna rais hata mmoja anayeweza kuendesha nchi peke yake bila nguvu ya chama nyuma yake -hakuna..Sii Tanzania wala Afrika nzima!

maneno mazito haya Bob... ni ukweli unaouma sana hasa kutokana na udhaifu/kutokukubalika kwa upinzani. Mungu ibariki Tanzania.
 
Kinachouma wengi hapa (pamoja na mimi) ni
1. kushindwa kwa kiongozi uliepo madarakani kuleta maendeleo yoyote ambayo aliahidi kwenye uchaguzi uliopita,
2. kushindwa kutekelezwa kwa ilani ya CCM (chama ambacho hata mimi ni mwanachama),
3. kushindwa kutekelezwa kwa sheria sawia kwa watu wote nchini (wezi wadogo kufungwa hata bila kuwepo ushahidi wa kutosha, na wezi wakubwa kutochukuliwa hatua zozote hata kama ushahidi upo),
4. kuanza kwa kampeni zenye nia ya kukemea wanaCCM kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais (kikatiba) ndani ya chama chao,
5. kuanza kwa kampeni kabla ya wakati (kumpigia chapuo kiongozi aliepo madarakani).

Siamini kuwa kuna mtu mwenye mamlaka ya kukataa mtu yeyote asiteue mtu ampendae. Kinachosumbua ni kuanza mapema uteuzi usio rasmi wenye nia ya kulazimisha (ku-influence) viongozi wengine wote kuunga mkono azimio lisilo la kikatiba, lenye nia ya kudhoofisha haki ya mtu kuchaguliwa. Viongozi wanaotakiwa kuwa na subira hadi wakati muafaka wa kuchagua/kuteua/kupendekeza wameanza mapema mno na hasa kwa kuwafanya wengine wasitumie haki yao kwa ukamilifu. Viongozi wengine wote wanalazimika sasa kuonyesha msimamo wao katika utetezi wa mgombea Urais (watake, wasitake). Madhara yake ni wao kushiriki kwenye kile wasichokiamini.

Kila mtu anaweza kuwa na chaguo lake la mTanzania anaemuona kuwa anafaa kuwa Rais wa nchi. Ila mapenzi yoyote kwa mtu huyo, hayana maana kama mtu huyo hana nia ya kuomba kuwa Rais kwa kufuata taratibu zilizopo (ambazo zimeanza kukiukwa makusudi). Mimi naweza kusema kuwa, ninaamini kuwa naweza kufanya vizuri zaidi ya yaliyofanywa na Rais wetu kwa miaka mitano (5 years). Ninaamini kuwa ninaweza:
1. kutetea na kuilinda sheria ya nchi kwa kuhakikisha kuwa inatumika ipasavyo kwa wote bila kujali tabaka la mhusika
2. Ninaamini kuwa ninaweza kulinda rasilimali za nchi hii zisitumike kufaidisha watu binafsi na kuliacha Taifa likiangamia katika umasikini
3. Ninaamini kuwa nchi ina watu wenye uwezo, nia, na matamanio ya kuwa na hali bora na wako tayari kushirikiana na serikali kufikia malengo yoyote yanayokubalika. Nina uwezo wa kuwashirikisha kufanya hivyo
4. Ninaamini kuwa ninaweza kudumisha/kuendeleza/kuhakikisha uhuru, amani na utulivu unakuwa wa kweli nchini
5. Ninaamini kuwa kila tatizo lina ufumbuzi wake, na ufumbuzi wake ni nia ya kulitatua tatizo hilo kwa vitendo bila subira.
6. Ninaamini kwa dhati kuwa KATIBA ya nchi hii inatakiwa iundwe upya ili kuweka usawa wa kweli kwa kila mtanzania, kuweka mipaka ya utendaji wa mihimili mikuu ya nchi, kuweka demokrasia zaidi, na kuhakikisha utawala bora.

Na nimeliweka swali hilo makusudi kwa sababu naelewa fika kwamba CCM bila Kikwete haiwezi kwenda popote. hakuna na narudia kusema hakuna kiongozi CCM anayeweza kuwa mbora kuliko Kikwete ktk kiti cha Ikulu.. chama kizima Muflisi, kimeshikwa na mafisadi.. Sii Mwandosya, magufuli wala mjomba wake anayeweza kuinua hata kidole against kundi hilo..
Wanaojiweza kidogo ni Mwakyembe, Sitta, Mama Kilango, na Malecela.. hawa wote ni watu wa Kikwete na wanampendekeza Kikwete kwa sababu hawawezi kupita hata Ubunge 2010 kama sio nguvu ya Kikwete..haya tukiondoa hawa huko CCM kabakia nani?..nani anaweza kumkemea Rostam au Lowassa! nani anaweza kusimama na hawa jamaa na kuwatazama usoni akawaambia wanakwenda lupango!..hakuna...
Hakuna rais hata mmoja anayeweza kuendesha nchi peke yake bila nguvu ya chama nyuma yake -hakuna..Sii Tanzania wala Afrika nzima!

Huu ni uongo mkubwa na aibu kwa Taifa hili. Haiwezekani kufikiria kuwa nchi hii ni masikini wa upeo/uwezo/ujuzi na akili kiasi cha kutokuwa na watu wenye uwezo wa kufanya mambo makubwa kwa Taifa hili zaidi ya JK. Ni kauli inayosikitisha sana.

Ninaamini kuwa ndani ya CCM kuna watu wengi sana ambao wana uwezo wa kufanya mambo mazuri zaidi ya wote uliowataja hapo juu. Watu hao ambao wamedidimizwa wasionekane au hawana nafasi ya kufanya mambo hayo (either kwa kujali amani, utulivu, na hekima) wanafanya hao unaowataja hapo juu waanze sasa kukemea nia ya yeyote kuomba kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania kupitia chama chake.
 
maneno mazito haya Bob... ni ukweli unaouma sana hasa kutokana na udhaifu/kutokukubalika kwa upinzani. Mungu ibariki Tanzania.

...huenda huo udhaifu/kutokukubalika kwa Upinzani pia kukaendelea kwa karne nyingi nyingine, wala sidhani 2010 hilo pengo litapungua kwa zaidi ya 15%...

14 December 2005 Matokeo ya Uchaguzi wa Rais Tanzania​
Kura​
Chama Cha Mapinduzi​
9,123,952 80.28​
Civic United Front​
1,327,125 11.68​
Chama cha Demokrasia na Maendeleo​
668,756 5.88​

...natanga yajayo, wagombea wataojitokeza 2015 kuja kutunusuru, Bora uhai!
 
Semilong,

Mkuu wangu weee hivi kweli umeshindwa kuliona kosa bali unavumbua kosa kwa mtindo wa Vasco Dagama..
Kosa ni kuwachagua Mwinyi na Mkapa kuwa marais...hakuna hata siku moja miaka ikawa sababu ya makosa ya uchaguzi bali ni uchaguzi wa mtu wenyewe ndio una makosa..
sasa unaposema makosa Kumchagua Kikwete ni vizuri sana ukafikiria kuchagua nje ya Kikwete na wagombea watakuwepo.. That's the ONLY solution uliyokuwa nayo. Usitake kulazimisha bus linalokwenda Mbeya lisimame kwa sababu Ulitegemea kwamba hao madereva hupokeza njiani..Umeshaambiwa utaratibu wao sio hivyo bado hutaki, kama hutaki safari ya CCM shuka wewe acha wengine waendelee na safari..

kumchagua tena kikwete itamaanisha kwamba watanzania tuko tayari kuchagua uzembe kwa mara nyingine na hao wazee unaowaona wote ni wa pambe na njaa zao.

ukiniuliza nani apewe nakuambia MAGUFULI. hata wizara ya minofu anafanya kazi na kama kawaida inaonekana kuna nguvu zinamsimamisha baada ya kuchukua hatua. hata alivyokuwa wizara za nyuma alikuwa anafanya kazi lakini bosi wake alikuwa anamsimamishwa, kama ilivyo bosi wa sasa hivi. kumpeleka magufuli minofu ni kumnyima media attention ili kuua nguvu yake kisiasa.

putin aliwekwa kwenye urais na oligarchs na alivyokuwa rais akawachukulia wote atua na kuhakikisha utajiri wa rusia unatumika kuinua uchumi wa russia na sio familia chache.

magufuli akichaguliwa atapambana na kina rostam kwa ajili yeye ndio mwenye nguvu zote.
kikwete sio kama hawezi kuwachukulia hatua bali hataki.

na magufuli nae asipofanya kazi miaka 5 tu mwisho.

mkandara unaabisha JF kuona kwamba ushakubali ya ishe, watu regular wa JF kama nyie mnakubali ya ishe inaonekana hamtaki CHANGE.

mabadiliko yanatakiwa kila miaka mitano mpaka viongozi waanze kufanya vizuri.
MKANDARA WEWE HUNA TOFAUTI NA HAO WAZEE SIJUI NA WEWE NI MZEE.
YOU ARE RESISTANCE TO CHANGE, IT IS TIME FOR YOU TO START SUPPORTING THE CHANGE MOVEMENT.
HII INAONYESHA WEWE NI MKAZI WA DAR NA SIO WA TARIME.
 
Last edited:
kumchagua tena kikwete itamaanisha kwamba watanzania tuko tayari kuchagua uzembe kwa mara nyingine na hao wazee unaowaona wote ni wa pambe na njaa zao.

ukiniuliza nani apewe nakuambia MAGUFULI.

na magufuli nae asipofanya kazi miaka 5 tu mwisho.

mkandara unaabisha JF kuona kwamba ushakubali ya ishe, watu regular wa JF kama nyie mnakubali ya ishe inaonekana hamtaki CHANGE.

...nilivyomuelewa Mkandara ni kwamba 'virusi' vya mtandao vimeenea kila pembe ya hicho chama kwa sasa, ugonjwa ushaenea na wala hautibiki kirahisi.

Kumbuka kwenye kura za maoni kupata wabunge na wawakilishi mpaka kiti cha Uraisi 2005, wangapi walitakiwa na wananchi lakini wakaishia kutupwa na kapu?

halafu kama hiyo haitoshi, jina lake (MAGUFULI) inabidi lipitie kwenye hili kapu linalojumuisha pia hawa;

Wajumbe wa Kamati Kuu, waliochaguliwa ni Dk Maua Daftari, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Bw. Muhammed Seif Khatibu, Bw. Omar Yusufu Mzee na Bi. Fatma Said Ali.

Wengine ni Bw. Yusuf Hamad Yusuf, Samia Suluhu Hassan, Bw. Rostam Aziz, Bw. Andrew Chenge, Bi. Pindi Chana, Dk. Abdallah Kigoda, Bw. Abdulrahman Kinana na Bi. Anna Makinda.
 
kumchagua tena kikwete itamaanisha kwamba watanzania tuko tayari kuchagua uzembe kwa mara nyingine na hao wazee unaowaona wote ni wa pambe na njaa zao.

ukiniuliza nani apewe nakuambia MAGUFULI. hata wizara ya minofu anafanya kazi na kama kawaida inaonekana kuna nguvu zinamsimamisha baada ya kuchukua hatua. hata alivyokuwa wizara za nyuma alikuwa anafanya kazi lakini bosi wake alikuwa anamsimamishwa, kama ilivyo bosi wa sasa hivi. kumpeleka magufuli minofu ni kumnyima media attention ili kuua nguvu yake kisiasa.

putin aliwekwa kwenye urais na oligarchs na alivyokuwa rais akawachukulia wote atua na kuhakikisha utajiri wa rusia unatumika kuinua uchumi wa russia na sio familia chache.

magufuli akichaguliwa atapambana na kina rostam kwa ajili yeye ndio mwenye nguvu zote.
kikwete sio kama hawezi kuwachukulia hatua bali hataki.

na magufuli nae asipofanya kazi miaka 5 tu mwisho.

mkandara unaabisha JF kuona kwamba ushakubali ya ishe, watu regular wa JF kama nyie mnakubali ya ishe inaonekana hamtaki CHANGE.

mabadiliko yanatakiwa kila miaka mitano mpaka viongozi waanze kufanya vizuri.
MKANDARA WEWE HUNA TOFAUTI NA HAO WAZEE SIJUI NA WEWE NI MZEE.
YOU ARE RESISTANCE TO CHANGE, IT IS TIME FOR YOU TO START SUPPORTING THE CHANGE MOVEMENT.
HII INAONYESHA WEWE NI MKAZI WA DAR NA SIO WA TARIME.

Well done!!! Thank you Semilong, Wakati wa kukumbatia uzembe na unafiki umepitwa na wakati. Sasa ni lazima tuambiane ukweli bila woga wa kificho kuhusu uongozi wa nchi yetu. Matatizo makubwa ya nchi yetu yanatokana na viongozi mafisadi, waliweka mbele maslahi yao badla ya yale ya Taifa, wasio jasiri kupambana na mambo mbali mbali yanayokwamisha maendeleo yetu yakiwemo ya rushwa na ufisadi. Kikwete na wapiga debe wake waorodhoshe yale aliyoyafanya tangu aingie madarakani 2005 ambayo yameleta maendeleo kwa Watanzania wengi na hatimaye nchi yetu. Kwa maoni yangu hakufanya lolote na hivyo hii ya kushindwa kufanya lolote ni sababu tosha ya kumwambia BASI, MUDA TULIOKUPA UMETOSHA NA HATUJARIDHIKA NA UTENDAJI WAKO HIVYO TUNATAKA RAIS MPYA.
 
Recta,
Mkuu wangu nakusikia sana na kilio cha Watanzania.. sii wewe peke yako ila tupo wengi sana. Tofauti yangu na wewe ni ktk imani.. Wewe unaamini atakayetupeleka peponi ni mtu lakini sii Kikwete..Wakati mimi hapa naamini kinachokupeleka peponi sii mtu ila ni imani nzima ya dini (kile alichotufundisha) na sisi tukafuata.
Ikiwa sera za chama CCM zina mapungufu na toka tupate Uhuru hatujaweza piga hatua wakati kuna marais watatu wamepokezana, then something is very wrong na utawala huu (imani ya dini hiyo) haijalishi nani kiongozi na wala sii swala la uchaguzi wa nani akuongoze kwani sisi sio kundi la kondoo..hakunamtume huko CCM anayefahamu pepo inapatikana vipi..
So the only thing kwangu mimi siwezi kumkataa Yesu kwa sababu tu nina imani zaidi na Mohammad... hapana mkuu wangu, tofauti zetu ni ktk mafundisho na sii watu..

Hata kama Recta ndiye angekuja na ujumbe sawa na Koran ningemfuata yeye na sii Mohammad kwani bado ningekuwa Muislaam. Uislaam unajengwa kwa imani ya dini na sio jina la mwakilishi wa Ujumbe..tofauti zetu zinatokana na kitabu (ujumbe na sii uzawa na makeke ya kiongozi)..

Ikiwa kuna mtu CCM ambaye wewe unafikiria ni mbora mtaje mkuu wangu mbona swali dogo sana!
 
Babu ataka kusema,
Mkuu kitu kimoja tu Kikwete hakufanya kulingana na wanaCCM nacho ni kumwacha Apson, Mahita, Lowassa, Karamagi, Meghji, na baraza zima la mawaziri . Kikwete katengua katiba ya chama kuwaondoa viongozi wote wanaotaka kufanya biashara wakiwa mawaziri. Utawala wa Kikwete umewafikisha Yona na Mpamba mahakamani.

Siyo kweli kabisa kusema kwamba Kikwete hakufanya moja tu. Vita dhidi ya mafisadi imemshinda. Mjadala mkubwa dhidi ya ununuzi wa Dowans alinyamaza kimya bila kutia neno na yule Comical Slava akatwambia Watanzania Kikwete hahusiki kabisa na Dowans!!! Lakini katika hotuba yake ya juzi alitaka mjadala wa Dowans ufungwe haraka pamoja na kuwa bado kuna maswali chungu nzima kuhusiana na Dowans. Mjadala wa Vitambulishho vyenye thamani ya shilingi 200 bilioni hakutia neno, alikaa kimya kabisa pamoja na kuwa yeye ndiye Kiongozi Mkuu wa nchi yetu. Aliahidi kuipitia upya mikataba ya uchimbaji madini yetu mbali mbali ikiwemo dhahabu, sidhani kama hili lilihitaji miaka minne kabla ya kulishughulikia, lakini hadi hii leo hajafanya chochote. Pamoja na kuwa kuna ushahidi wa kutosha kwamba Chenge na Idrissa Rashid walinufaika na ufisadi wa ununuzi wa Rada ya $40 million ambao Watanzania wengi tuliukataa lakini hadi hii leo hajachukua hatua zizote dhidi yao na bado wanapeta uraiani. Katika ripoti ya Mwakyembe na timu yao walirecommen kuondolewa madarakani Mkuu wa PCCB Edwards Hosea na Mwanasheria Mkuu Johnson Mwanyika hajafanya hivyo hadi leo na hajatwambia sababu zozote za kutotimiza recommendations za Kamati ya Makyembe. Huu ni ushahidi wa kutosha kwamba utendaji wake ni dhaifu.

Pungufu moja kubwa kwa wananchi ni mtu mmoja tu Lowassa..jambo ambalo hakuna kiongozi hata mmoja Tanzania ambaye angeweza hata kumsimamisha madaraka kwa sababu madhambi ya Chimwaga na uchaguzi mkuu waliyafanya wote ndani ya chama.

Mimi hizi alinacha kwamba hakuna kiongozi anayeweza kuchukua hatua dhidi ya kingozi mwingine sitaki kuzisikia kabisa. Kama wote ni watenda dhambi basi hawafai kutuongoza maana dhambi zao zinaisababisha nchi yetu kutopata maendeleo yoyote yale wakati wao wakiendelea kuaccumulate wealth na kuwa mabilionea. Kama wote ni mafisadi basi ni lazima tuwaambie ukweli kwamba nyie ni mafisadi na Watanzania hatutaki kuongozwa na mafisadi.

Na nakuhakikihsia Kitendo cha Kikwete kuwatema Lowassa na mtandao ni ushindi kwa wananchi na wana CCM kwa sababu hakuna mtu ndani ya chama hicho angeweza kufanya hivyo..na leo hii hakuna kiongozi yeyote anayeweza kufanya unayoyataka wewe.kwa sababu sifa unazotafuta hazipo ktk uongozi bora wa CCM isipokuwa nje ya chama.

Labda wewe ndiyo unaona kwamba Lowassa na mtandao wametemwa, lakini mimi sioni hivyo. Kwa sababu Lowassa bado anahudhuria vikao vya juu kabisa ndani ya CCM na juzi juzi tuliona wanamtandao walivyohakikisha kwamba watu wao wa karibu katika Wakuu wa Wilaya hawatimuliwi madarakani. Hivyo mtandao bado una nguvu za kutosha tu kuweza kufanya lolote lile walitakalo.

Huo ndio UNAFIKI kupiga kelele nyuma ya pazia..na bado tu mkuu unakazania JK wakati sijakusikia ukitaja mtu anayefaa!.. sasa Unataka JK ongembee na UKUTA.. yaani turudishe zile picha za uchaguzi wa Nyerere na Ukuta mkuu wangu!

Wewe ndio mnafiki usiyetaka mabadiliko kwa ajili ya maslahi ya nchi yetu. CCM kina wanachama million 4, halafu unategemea mimi nikupe jina la mtu anayefaa kati ya hao watu millioni 4!!!!! Ha ha ha ha acha alinacha zako!!!! Nimekupa mfano rahisi kabisa wa Obama kwamba hakuna aliyemdhania kwamba Obama atachaguliwa kuwa mgombea wa Democrats kwa sababu Wazee na wananchama wengi wa Democrats walimtaka Hillary kwa sababu ya jina kubwa, good organization when it comes to big elections, Mumewe ana heshimika sana ndani ya chama chao, lakini pamoja na hayo yote ambayo yalikuwa ni disadvantage kwa Obama hakukata tamaa akaingizana tu na hatimaye kuwashinda akina Clinton na kuweka history ya kuwa Mweusi wa kwanza kuwa rais tangu Marekani ipate uhuru miaka 253 iliyopita. Achana na alinacha za kutaka nikutajie majina makubwa kama unavyotaka wewe, anaweza kabosa akatokea mtu ambaye hajulikani sana lakini akafanya vitu vyake na kumbwaga Kikwete na hatimaye kuwa Rais wa Tanzania.

Acha utetezi wako wa madikteta ndani ya CCM. Katiba ya CCM haisemi popote pale kwamba vitisho na ubabe utatumika ili kuwatisha wale wanaotaka kumpinga Rais aliyemaliza awamu moja madarakani katiba ifuatwe bila vitisho wala ubabe.

Njemba zinazojiita Wazee wa CCM zinajua Kikwete ni mtupu hawezi akasimama katika jukwaa lolote lile ndani ya nchi na kuorodhesha his accomplishments for the past four years, maana hakuna hata moja ndiyo maana wameanza na zengwe zito la kuwatisha wale wote wanaotaka kumpinga Kikwete. IT IS TIME FOR CHANGE!!!!!
 
Recta,
Mkuu wangu nakusikia sana na kilio cha Watanzania.. sii wewe peke yako ila tupo wengi sana. Tofauti yangu na wewe ni ktk imani.. Wewe unaamini atakayetupeleka peponi ni mtu lakini sii Kikwete..Wakati mimi hapa naamini kinachokupeleka peponi sii mtu ila ni imani nzima ya dini (kile alichotufundisha) na sisi tukafuata.
Ikiwa sera za chama CCM zina mapungufu na toka tupate Uhuru hatujaweza piga hatua wakati kuna marais watatu wamepokezana, then something is very wrong na utawala huu (imani ya dini hiyo) haijalishi nani kiongozi na wala sii swala la uchaguzi wa nani akuongoze kwani sisi sio kundi la kondoo..hakunamtume huko CCM anayefahamu pepo inapatikana vipi..
So the only thing kwangu mimi siwezi kumkataa Yesu kwa sababu tu nina imani zaidi na Mohammad... hapana mkuu wangu, tofauti zetu ni ktk mafundisho na sii watu..

Hata kama Recta ndiye angekuja na ujumbe sawa na Koran ningemfuata yeye na sii Mohammad kwani bado ningekuwa Muislaam. Uislaam unajengwa kwa imani ya dini na sio jina la mwakilishi wa Ujumbe..tofauti zetu zinatokana na kitabu (ujumbe na sii uzawa na makeke ya kiongozi)..

Ikiwa kuna mtu CCM ambaye wewe unafikiria ni mbora mtaje mkuu wangu mbona swali dogo sana!

Mkandara Mkuu, mimi nakubaliana na wewe sana hasa kwenye issue ya imani. Naamini kwa ufahamu mzuri ulionao, unaoanisha imani ya sera za chama tawala na mafanikio ama kushindwa kwa malengo ya Taifa letu. Mimi naamini kama wewe, nishichokiamini ni kuwa CCM haina sera nzuri. Hili si la kweli. CCM ina sera nzuri sana tu na pia ina imani na malengo mazuri. Kama umefuatilia kwa makini nilichokisema kwenye post iliyotangulia, niliweka pia kushindwa kutekelezwa sera nzuri za CCM.

Mkuu, mafundisho ya imani ya dini, au itikadi yoyote yanategemea sana na kiongozi/mfundishaji/msimamizi wa mafundisho hayo n.k. CCM imeshaweka sera zake ambazo kwa kweli ndizo zilizotufanya tusisite kukichagua kwa mara nyingine mwaka 2005. Sera hizo nzuri zilisambazwa vizuri, zikaeleweka. Ambacho hakikufanyika ni utekelezaji wa sera zenyewe. Hili ndilo linalotufanya tuamini kuwa tulilaghaiwa na sasa inatosha. Sioni sababu ya kuendelea kuamini kuwa itafika siku mtu yule yule alieshindwa akaweza kutekeleza vyema yote aliyoahidi. Sioni mwelekeo huo.

Kufananisha walioshindwa na kudhani kuwa wote ni watakaoshindwa nalo ni kosa kubwa. Bondia akianguka kwenye pambano, halafu akaanza kufikiria waliowahi kuanguka katika mashindano ya nyuma, ni wazi kuwa ataishia kushindwa kwa knock-out. Tunachotakiwa kama Taifa ni kuangalia tulipoanguka na kuchukua hatua za kutuhakikishia kutoanguka tena siku za mbele. Kwa maneno mengine ni kwamba, inatakiwa kujua kuwa, tulianguka wapi, kivipi na jinsi gani ya kukwepa kufikia kuanguka kama huko.

Mkandara ndugu yangu, mimi naweza kutaja watu wengi tu ndani ya CCM wenye uwezo mkubwa wa kuleta unafuu kiuchumi, kisheria, kijamii, n.k., kuliko tunavyoendelea hivi sasa. Ila nitakuwa siwatendei haki watu hao kama nitawataja na wao wasiwe na nia ya kutaka kuongoza Taifa hili. Ndio maana nikasema (hapo juu), kuwa hata mimi ninaamini kuwa ningeweza vizuri zaidi.

Ninachoweza kukiomba chama changu CCM ni kutoa ruhusa kwa wenye uwezo kugombea nafasi hiyo kwa usawa na haki. Baada ya wote kuchukua form na kuzirudisha, ndipo tutakapoweza kuona options tulizonazo.
 
TZ needs a new direction 2010, they need to mbeki-nize him and choose a new leader

That is the point. Walio ndani wameshaona kuwa kuna hatari ya mtu kuondolewa. Hatari hii ipo ndani ya CCM kwa sababu tathmini zote zinaonysha kuwa mpaka hivi sasa upinzani haujawa hatari kiasi cha kuwafanya wazee watoke kwenye ustaafu wao na kuanza kujiingiza kwenye shughuli.
Humo CCM si shwari na ndio maana unaona watu wanahangaika kuhalalisha kitu ambacho kwa mantiki hakikuhitaji kuhalalishwa
 
- Wakishamtoa rais wa sasa, ni nani anayefaa kushika nchi naona hili swali halijibiwi, vipi?

William.

Katiba iachwe ifuate mkondo wake, siyo lazima atakayemreplace Kikwete awe na jina kubwa, anaweza kabisa kuwa si mtu ambaye anajulikana sana ndani ya CCM au hata Tanzania. Kumbuka Obama hakuna mtu aliyemtabiria kuwa angeibuka kuwa mgombea wa Democrats na hatimaye kuwa Rais wa Marekani. Hovyo basi nasi tunaweza kabisa kumpata Obama wetu, mtu ambaye hana jina kubwa, si maarufu sana ndani ya CCM au Tanzania lakini kutokana na sera zake atakazomwaga basi wengi ndani ya CCM wanaweza kabisa kuamua kumsupport na hatimaye kuibuka kama mgombea wa CCM.

Ni lazima tuachane na dhana kwamba Rais wa Tanzania ni lazima awe na jina kubwa lenye umaarufu kwa siku nyingi katika anga za siasa za nchi yetu.
 
- Wakishamtoa rais wa sasa, ni nani anayefaa kushika nchi naona hili swali halijibiwi, vipi?

William.

Suala si anayefaa, wao tayari wanaye mtu wao wa kushika nafasi. Kwamba anafaa hilo ni suala jingine ambalo Watanzania watalazimika kujifunza kwa kutumia uhalisia.
Lakini pia kwao sasa hivi suala la nani atachukua nafasi si relevanty, vita yao kwa sasa ni kuondoa huyu aliyepo
 
Katiba iachwe ifuate mkondo wake, siyo lazima atakayemreplace Kikwete awe na jina kubwa, anaweza kabisa kuwa si mtu ambaye anajulikana sana ndani ya CCM au hata Tanzania. Kumbuka Obama hakuna mtu aliyemtabiria kuwa angeibuka kuwa mgombea wa Democrats na hatimaye kuwa Rais wa Marekani. Hovyo basi nasi tunaweza kabisa kumpata Obama wetu, mtu ambaye hana jina kubwa, si maarufu sana ndani ya CCM au Tanzania lakini kutokana na sera zake atakazomwaga basi wengi ndani ya CCM wanaweza kabisa kuamua kumsupport na hatimaye kuibuka kama mgombea wa CCM.

Ni lazima tuachane na dhana kwamba Rais wa Tanzania ni lazima awe na jina kubwa lenye umaarufu kwa siku nyingi katika anga za siasa za nchi yetu.

- In your opinion nani anaweza kufaa na kumshinda rais wa sasa?

William.
 
Suala si anayefaa, wao tayari wanaye mtu wao wa kushika nafasi. Kwamba anafaa hilo ni suala jingine ambalo Watanzania watalazimika kujifunza kwa kutumia uhalisia.
Lakini pia kwao sasa hivi suala la nani atachukua nafasi si relevanty, vita yao kwa sasa ni kuondoa huyu aliyepo

- Kwa maoni yako mkuu ni nani anayefaa ndani ya CCM kuweza kumshinda rais wa sasa na kuweza kuibadilisha nchi?

- Forget ya CCM kugombana maana hawagombani, Waheshimiwa Rostam na Mwakyembe, walitaka kushirikiana kuanzisha kampuni, lakini wakashindwa kuelewana sasa eti unaweza kusema leo wanagombana? Na wakigombana basi CCM inagombana? Hapana.

William.
 
- In your opinion nani anaweza kufaa na kumshinda rais wa sasa?

William.

Wengi tu, tusijilimit katika kutafuta jina la nani anayeweza kumshinda Kikwete, maana majina yatakayotolewa yatakuwa ni yale majina yenye umaarufu katika anga za siasa ambayo tunayafahamu kwa miaka chungu nzima.
 
Wote wanaotaka kugombea toka CCM kama ni akima Mwandosya na wengineo wote waruhusiwe kuchukua form na kuwe na mjadala kati yao na atakayeonekana anafaaa kuliko mwingine basi apitishwe. Hili la kutoa jina kwamba fulani anafaa mimi siliafiki maana nakumbuka Mwalimu (RIP) alisema Mkapa ndiye aliyemuona anafaa kuwa Rais 1995 yalitokea baada ya hapo wote tunayajua.

Vigezo gani mlivyotumia kufikia conclusion kwamba ndani ya CCM hakuna mbadala wa Kikwete? Hata wanaotaka kugombea hawajapewa nafasi ya kufanya hivyo, tayari nyie mmeshaona kwamba hakuna mwingine ila Kikwete!!! Je mmeenda kwa Sheikh Yahya au kwa Toboa tobo kuweza kufikia conclusion yenu!?

Kikwete kashindwa kupambana na mafisadi ndiyo maana wahusika wote wa ufisadi akina Chenge, Rostam, Idissa Rashid na wengine wengi bado wanapeta uraiani. Huoni Rais ambaye anashindwa kutetea sheria za nchi na kuweka maslahi ya nchi mbele kwamba hafai kuiongoza nchi hiyo maana sheria za nchi zinazidi kukiukwa kila kukicha bila athari yoyote kwa wale wanaokiuka sheria hizo? Wakati umefika wa kutafuta mtu atakayeisafisha CCM na Tanzania kwa ujumla

Kwako wewe ufisadi si kila kitu katika maendeleo lakini inapotokea watu wanaifisadi nchi karibu shilingi Trilioni ($1 billion approximately)moja katika kipindi kifupi na kama ukaguzi wa EPA ungefanywa kuanzia 1995 mpaka 2006 badala ya 2005/2006 basi si ajabu pesa iliyoibwa ingefika hata shilingi Trilioni 2 ($2 billion approximately) , hili ni tatizo kubwa sana kwa nchi yoyote ile inayotaka kupata maendeleo kwa wananchi wake wote, kama wewe unaliona hili ni dogo hiyo ni juu yako. Inapotokea Rais anashindwa kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha wageni badala ya wananchi wake pamoja na kuwa aliahidi kulishughulikia tatizo hilo hii ni dalili nyingine ya kiongozi dhaifu ambaye hastahili tena kurudi madarakani. Je ni akina nani hao uliowasema hapo juu walioshindwa na Kikwete!? Na wameshindwa katika mambo gani!? Na hiyo tathmini iliyomuonyesha Kikwete kawashinda hao ilifanyika lini na wapi!?[/B]

Narudia tena, ndani ya CCM kuna wengi ambao wanaona wana uwezo wa kuiongoza Tanzania vizuri zaidi ukilinganisha na Kikwete. Katiba ya CCM na ya nchi pia zinawaruhusu kugombea nafasi hiyo bila vitisho wala mizengwe toka kwa Malecela, Chiligati, Msekwa au Wazee wa CCM. Hakuna haja ya mimi kutamka kwamba fulani ndiye anayefaa kuwa Rais 2010. Wote wanaotaka kugombea ndani ya CCM waachwe wafanye hivyo na kama baada ya taratibu zote ndani ya CCM kufuatwa na bado ikaonekana Kikwete ndiye anayefaa kuwa mgombea wa CCM basi hapo taratibu za CCM zitakuwa zimefuatwa bila upendeleo wala vitisho dhidi ya wagombea wengine, lakini huu udikteta wa "watakaompinga Kikwete watakiona" na "Wasitumie ufisadi kutaka umaarufu wa kisiasa' Kamwe hilo mimi silikubali. Mambo ya kulinda viongozi dhaifu na mafisadi ni lazima tuyapige vita kwa nguvu zetu zote maana hawa ndiyo tatizo kubwa la nchi yetu kutokuwa na maendeleo ya kuridhisha pamoja na misaada na mikopo chungu nzima tunayopata toka nchi mbali mbali za wafadhili na mashirika ya kimataifa pamoja na rasilimali nyingi tulizojaaliwa na Mungu.

Nashukuru Mkuu bubu na kwa mujibu wa majibu yako ya kipengele hadi kipengele nafikiri bado hujakataa kuwa kwa CCM hakuna anaeweza kutuongoza na maadam kama ulivyosema hapo awalli kuwa LAZIMA TUONGOZWE na CCM basi ni bora tuendelee na zimwi tulijualo.
Bubu nilijaribu kukueleza kuwa ndani ya CCM tunashindwa kumpata alie safi kutokana na kuwa waliingia madarakani kwa jasho letu kupitia ufisadi wa EPA.
Nilikueleza pia kuwa hawako tayari kuisaliti ngazi iliyowapeleka huko. NAFIKIRI HILI LIMETHIBITISHWA NAWE KWA KUSEMA KUWA KIKWETE KASHINDWA KUUCHUKULIA HATUA UFISADI. Sasa huyo unayemzungumza ni mwenyekiti wa hao wengine wote na kwa msimamo wao mmoja wamenyamazia ufisadi uliowapeleka huko juu. Wanatafauti gani hawa na Kikwete zaidi ni bora Kikwete ambaye juu ya jitihada zenu mmeshindwa kutueleza anamiliki Kampuni gani la Kibepari wa Kizalendo (kwani huwa mnajidanganya kuwa kuna ubepari tofauti wa mwananchi mweusi na mwananchi wa"uraia wa nchi tatu). Si rahisi kunambia bepari awe mgombea urais kwani hao waliokuwa kwenye nafasi nyengine wameshatuchosha.
Kila mtu ana haki kugombea nafasi na wananchi au wanachama ndio watakuwa waamuzi. Nakubaliana nawe kuwa si haki kuwakatalia haki wanachama lakini hili na tuwaachie wenyewe walitatue lakini kwa njia hiyohiyo ya haki tusimzuie Kikwete kuteuliwa kugombea ILA tusimpe kura kama tunaona kuwa hafai kutuongoza tena. Wazee na waseme wanayotaka na wengine watakuja na ya kwao na itakapofika zamu ya BUBU kufanya vitu vyake kwenye kura na afanye atakavyo kwa mujibu wa haki.
 
Back
Top Bottom