The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
- Wakishamtoa rais wa sasa, ni nani anayefaa kushika nchi naona hili swali halijibiwi, vipi?

William.

Wapo wengi wanaofaa, ni vile hawana majina na hawategemewi kugombea ndio maana huwezi kusema ni huyo au ni yule. Si kila anayefaa kuongoza lazima ajulikane na kila mtu. Kumbuka pia kiongozi unayemuona anafaa anaweza asiwe kiongozi bora kwa mwingine kutokana na kuwa na vigezo tofauti!
 
- Kwa maoni yako mkuu ni nani anayefaa ndani ya CCM kuweza kumshinda rais wa sasa na kuweza kuibadilisha nchi?

- Forget ya CCM kugombana maana hawagombani, Waheshimiwa Rostam na Mwakyembe, walitaka kushirikiana kuanzisha kampuni, lakini wakashindwa kuelewana sasa eti unaweza kusema leo wanagombana? Na wakigombana basi CCM inagombana? Hapana.


William.

Kama utatafuta nani anayefaa kati ya hawa waliopo utahangaika sana. Mimi naamini kuwa kizazi hiki kimeharibika chote, ni ubatili mtupu uliopo. Tunahitaji kizazi kipya kutuokoa
 
Urais CCM 2010: JK apewa mtihani mzito

Monday, 06 April 2009 16:49

Kauli za wenyeviti zazua jambo

Na Said Mwishehe

Majira

KUNDI la watu waliojitambulisha kuwa wana-CCM wa Mrengo wa kati au wana-CCM Mseto limedai litampinga Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete kwenye mchakato wa kutafuta mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho mwakani kama atashindwa kuwashughulikia mafisadi waliopo ndani ya chama hicho.

Wanachama hao wamedai endapo chama hicho kitazidi kukumbatia mafisadi na kuwaonea haya kuwatosa kisiasa, watakuwa tayari kuondoka CCM na kujiunga na kambi ya upinzani ili kuendeleza mapambano dhidi ya ufisadi.

Kauli ya wanachama hao imekuja siku moja baada ya wenyeviti wa mikoa wastaafu wa CCM kutoa tamko la kupambana na wenye nia ya kusisima kumpinga Rais Kikwete kwenye uchanguzi mkuu ujao mwakani.

Hata hivyo walisema hawamzuii mtu yeyote kugombea nafasi hiyo, lakini hawaoni sababu ya kuwapo upinzani wakati Rais Kikwete anatarajia kumalizia kipindi chake cha pili.

Wenyeviti hao wakiongonzwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa wenyeviti wa mikoa yote wa CCM, Bw. Pancras Ndejembi, walionya dhidi ya viongozi wa chama hicho wanaotaka kuyatumia mapambano ya rushwa kama mtaji wa kisiasa na kujipatia umaarufu.

Wakizungumza Dar es Salaam jana na Majira kwa masharti ya kutotajwa majina, makada hao walidai dhamira ya kweli ya Rais Kikwete kupambana na mafisadi itaonekana pale tu atakapowaengua haraka ndani ya chama watuhumiwa wote wa ufisadi.

"Uhakika wa kweli kama ameamua (Rais Kikwete) kufa na mafisadi ni pale tu tutakapoona wale waliohusika katika tuhuma za ufisadi wanashughulikiwa kikamilifu ndani ya CCM mbali ya kujiuzulu serikalini," kilisema chanzo hicho.

Wanachama hao walisema wanataka kuona mafisadi wote waliohusika na kashfa za Kagoda, Richmond, Buzwagi, Deep Green, Meremeta, Rada, IPTL na zingine wanatinga kortini au kuvuliwa uanachama kabla ya 2010 vinginevyo watakihama chama hicho.

"Umefika wakati kusema ukweli wa mwenendo mzima wa chama chetu. Haiwezekani chama kishindwe kuwachukulia hatua mafisadi na kuendelea kuwalea. Katika mazingira hayo lazima tumpinge kwa misingi ya kidemokrasia mwaka 2010. Kushindwa kuwashughulikia mafisadi ni kushindwa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya chama," alisema kada huyo.

Kada mwingine kutoka kundi hilo alisisitiza kuwa watakuwa tayari kumuunga mkono Rais Kikwete katika uchaguzi huo endapo atafanya kazi moja tu ya kuhakikisha mafisadi waliopo ndani ya chama, wanachukulia hatua za kichama sasa ikiwa ni pamoja na kuvuliwa uanachama.


Alisema endapo Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho ataongoza mapambano kuwatimua wote wanaoandamwa na kashfa za ufisadi, atapita bila kupingwa.

Kada mwingine wa mrengo wa kati ambaye naye aliomba kutotajwa jina gazetini, aliwalaumu wenyeviti hao na kudai wameshindwa kutofautisha ukweli wa mambo na vita ya ufisadi inayoendelea.

"Hawa wenyeviti wanadhani mkakati wa kumpinga Rais Kikwete 2010 unaendeshwa na mafisadi, hili si kweli bali mafisadi ndio wanamponza Rais mbele ya wanachama safi kwa kushindwa kuwatosa!

"Hatuwataki mafisadi na tunataka chama kiwang'oe, hata wakiomba kura hatuwapi, ndio maana tunataka Rais Kikwete aoneshe njia kwa kuwatosa nje ya chama, vinginevyo na yeye tumpinge kidemokrasia kwenye mchakato mwakani," alisema kada huyo na kufafanua:

"Hawa wenyeviti ni kama wanatubeza sisi tunasema viongozi hususani Mwenyekiti Rais Kikwete aoneshe dhamira ya kweli kupambana na mafisadi, kama anashindwa kuwang'oa mafisadi ndani ya chama kwanini wanachama wengine watakaokuwa na ubavu wa kuwang'oa watu hao wasijitokeze tuwape nafasi?


"Kumtetea mtu aliyeshindwa kuwang'oa mafisadi ndani ya chama ni kama kushabikia ufisadi na kuwabeza waliojitolea kwa nguvu zote kupambana na ufisadi."

Kada huyo alisema baadhi ya viongozi wa ngazi za kati ndani ya chama hicho wakiwemo wabunge wamefanya kazi nzuri ya kupambana na mafisadi zaidi ya viongozi wakuu wa chama hicho, hivyo madai kwamba walio mstari wa mbele katika mapambano hayo wanajitafutia umaarufu hayana msingi.

Alitoa mfano kwa Mbunge wa Kyela (CCM), Dkt. Harrison Mwakyembe na Mbunge wa Nzega (CCM), Bw. Lucas Selelii kuwa wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kazi nzuri waliyoifanya katika kupambana na mafisadi.

"Wanaopambana na ufisadi kama hao niliwataja lazima waungwe mkono, binafsi sioni kama Rais Kikwete anawashughulikia mafisadi waliopo ndani ya CCM. Mambo ya chama na Serikali ni tofauti, ukitimuliwa serikalini mnaanza kutafuta haki mahakamani, lakini chama ni kama dini ukishakuwa na doa ni kuondoka kama hutaki unaondolewa," alisema.

Alimtaka Rais Kikwete kufuata nyayo za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika kukiongoza chama na kusema kwamba hakuvipa nafasi vitu hivyo na wote waliobainika, walitimuliwa bila kujali hali na nafasi zao.

Alikwenda mbali zaidi na kudai ana wasiwasi wenyeviti hao wasije wakawa wanatumiwa bila kujijua na baadhi ya watu ili kuwahadaa wanachama wengine na kupotosha dhana na matokeo ya vita ya ufisadi hadi sasa.

Wenyeviti walioambatana na Bw. Ndejembi ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Hemed Mkali, Bw. Tasir Mgoda (Iringa) na Bw. Jumanne Mangara (Pwani).


Hadi sasa miongoni mwa wana-CCM walioonesha nia ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho ni pamoja na Mbunge wa Maswa, Bw. John Shibuda.

Last Updated ( Monday, 06 April 2009 17:18 )




Watu wa namna hii hawatufai kwani si wagombea bali ni Maruhani (Kama wale wa Pemba)
Ikiwa viongozi wanashindwa kujitambulisha na kukaa mafichoni na kungojea mwaka 2010 ndio waanze Mapambano ya ufisadi. Hivyo Mkuu wangu BUBU tuwaamini watu hao wasiokuwepo? Mbona kina Dr. Slaa wameyaanza zamani mapambano na hawajifichi? Naogopa kuwaaamini watu wanaongojea sijui wakati gani wakati Watanzania tunaendelea kuumia.
 
...nilivyomuelewa Mkandara ni kwamba 'virusi' vya mtandao vimeenea kila pembe ya hicho chama kwa sasa, ugonjwa ushaenea na wala hautibiki kirahisi.

Kumbuka kwenye kura za maoni kupata wabunge na wawakilishi mpaka kiti cha Uraisi 2005, wangapi walitakiwa na wananchi lakini wakaishia kutupwa na kapu?

halafu kama hiyo haitoshi, jina lake (MAGUFULI) inabidi lipitie kwenye hili kapu linalojumuisha pia hawa;

Wajumbe wa Kamati Kuu, waliochaguliwa ni Dk Maua Daftari, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Bw. Muhammed Seif Khatibu, Bw. Omar Yusufu Mzee na Bi. Fatma Said Ali.

Wengine ni Bw. Yusuf Hamad Yusuf, Samia Suluhu Hassan, Bw. Rostam Aziz, Bw. Andrew Chenge, Bi. Pindi Chana, Dk. Abdallah Kigoda, Bw. Abdulrahman Kinana na Bi. Anna Makinda;

swali: MAGUFULI akifanya mkutano na waandishi wa habari na kutangaza kugombea?
Unadhani hawa wajumbe wataweza kumzuia. Hawawezi kutoa jina lake. Soma nyakati.

Hawawezi kuzui democrasia isitokee. wataiba kura wakati wa mkutano mkuu.
Ndio maana hawa viongozi hawapendi vyombo vya habari, na ndio maana wana katisha tamaa mtu yoyote asitangaze kugombea.


INAONEKANA WATU MNATAKA KUJUA BUBU ANAMFIKIRIA NANI, NA SIO KAMA MNATAKA MABADILIKO. NA BUBU KASHAWASOMA NDIO MAANA HATAKI HATA KUTOA JINA.
INGAWA UKITAKA UNAWEZA KUIWEKA WAZI LAKINI KURA NI SIRI.
WALA USIWAPE JINA BUBU KAA KIMYA TU.
 
Nashukuru Mkuu bubu na kwa mujibu wa majibu yako ya kipengele hadi kipengele nafikiri bado hujakataa kuwa kwa CCM hakuna anaeweza kutuongoza na maadam kama ulivyosema hapo awalli kuwa LAZIMA TUONGOZWE na CCM basi ni bora tuendelee na zimwi tulijualo.

Mambo ya Zimwi likujualo yamepitwa na wakati. Yalikuwa ni ya mwaka 47 sasa hivi tuko 2009 hivyo hatuna haja ya kuogopana au kuoneana haya. Mtu kama hawezi kazi basi ni lazima aambiwe kazi imekushinda kaa pembeni.

Bubu nilijaribu kukueleza kuwa ndani ya CCM tunashindwa kumpata alie safi kutokana na kuwa waliingia madarakani kwa jasho letu kupitia ufisadi wa EPA.

Ni lini mmejaribu kumpata liye safi ndani ya CCM na kushindwa kumpata msafi huyo? Je ni watu wangapi katika idadi ya wanachama millioni 4 wa CCM ambao walfanyiwa tathini ili kujua kama ni wasafi au la!?

Nilikueleza pia kuwa hawako tayari kuisaliti ngazi iliyowapeleka huko. NAFIKIRI HILI LIMETHIBITISHWA NAWE KWA KUSEMA KUWA KIKWETE KASHINDWA KUUCHUKULIA HATUA UFISADI. Sasa huyo unayemzungumza ni mwenyekiti wa hao wengine wote na kwa msimamo wao mmoja wamenyamazia ufisadi uliowapeleka huko juu. Wanatafauti gani hawa na Kikwete zaidi ni bora Kikwete ambaye juu ya jitihada zenu mmeshindwa kutueleza anamiliki Kampuni gani la Kibepari wa Kizalendo (kwani huwa mnajidanganya kuwa kuna ubepari tofauti wa mwananchi mweusi na mwananchi wa"uraia wa nchi tatu).

Narudia tena Kikwete kashindwa kazi na hiyo ni sababu tosha ya kutomrudisha madarakani.
 
swali: MAGUFULI akifanya mkutano na waandishi wa habari na kutangaza kugombea?
Unadhani hawa wajumbe wataweza kumzuia. Hawawezi kutoa jina lake. Soma nyakati. Hawawezi kuzui democrasia isitokee. wataiba kura wakati wa mkutano mkuu.
Ndio maana hawa viongozi hawapendi vyombo vya habari, na ndio maana wana katisha tamaa mtu yoyote asitangaze kugombea.

- Mkuu wangu hivi unajua jinsi Kikwete, alivyotishiwa kabla ya kugombea mwaka 2005? Wabongo tuache uoga, mbona Shibuda amesema wazi kwani amefanywa nini so far?

- Kubalini tu kwamba hata nyinyi hamna uhakika nani anafaa, na huku ndani ya CCM kumejaa waoga wengi wanaotegemea msaada kutoka mbinguni, ndio maana mtu anayejiweza na asiye muoga kama Kikwete ndiye atakayeendelea, na mwishoni mwa kumaliza kwake ataamua nani awe mrithi wake maana tumekuwa waoga mno.

Respect.

FMES!
 
- Kwa maoni yako mkuu ni nani anayefaa ndani ya CCM kuweza kumshinda rais wa sasa na kuweza kuibadilisha nchi?
- Forget ya CCM kugombana maana hawagombani, Waheshimiwa Rostam na Mwakyembe, walitaka kushirikiana kuanzisha kampuni, lakini wakashindwa kuelewana sasa eti unaweza kusema leo wanagombana? Na wakigombana basi CCM inagombana? Hapana.
William.

William, Pamoja na mfumo wa chama kimoja nakumbuka Mwalimu Nyerere alipotangaza kuwa angeng'atuka na asingegombea tena nafasi ya Uraisi, hali ya wasi wasi iliikumba nchi na kuna watabiri walioona hali ya machafuko ikiinyemelea Tanzania. Hali hii ilisababishwa zaidi na kujengeka kwa imani na hofu ya Tanzania bila Nyerere !!

Baada ya kuingia kwa mfumo wa vyamam vingi hali ya hofu kama hiyo iliigubika nchi tena na imetumiwa sana kama mtaji mkubwa na chama tawala hadi leo - hofu ya Tanzania bila CCM !!. Sababu zinazotolewa ni zile zile zinazoendeshwa na wasioitakia mema taifa kama vile CCM ina hatimilki ya amani Tanzania na wasiwasi wa wapinzani kusababisha machafuko na vita.

Katika msingi huo huo Raisi JMK pamoja na mapungufu yake yote, kuna wanaojaribu kutumia hoja hiyo hiyo kuwa Tanzania bado inamhitaji na nia yoyote ya kumtoa ni kuchokoza hali ya utulivu na amani. Ndani ya CCM kwa sasa haitarajiwi yeyote ajitokeze kumpinga na atakayethubutu ni adui na mvurugaji kama inavyoanza kuenezwa na mitume bandia.

Naamini kwa dhati kuwa kama JMK, kwa mapenzi yake kwa taifa, ataweza kung'amua mapungufu yake mapema, atajitoa katika kinyang'anyiro cha mwaka 2010. Ambacho sina hakika ni kama ataweza kuwa hata na ujasiri huo na hii inatokana na tabia yake ya kukumbatia ushikaji katika utawala wake na kushindwa kufanya maamuzi mazito.

William, leo hii JMK akitangaza kuwa hatagombea, mtu/watu a/watajitokeza na nakuhakikishia wapo wengi tu na wenye uwezo na ushawishi mkubwa. Kutokujitokeza kwa sasa hivi ni kwa sababu ya woga wa katiba inayotoa nafasi kwa vyombo vya dola kufumbia macho uvunjaji wa sheria kwa kuangalia sura, itikadi, wadhifa na nafasi katika jamii.

Kujitoa kwa JMK kutatoa nafasi kwa taifa kupata wigo mpana na huru wa wagombea. Kujitoa kwa JMK kutaleta neema katika ushindani kwa kutoa nafasi sawa kwa wagombea watakaoingia ulingoni. Kujitoa kwa JMK kutaidhoofisha CCM kwa kiwango fulani lakini hili naamini ni jambo jema kwa taifa - CCM is too fat and it needs to diet. Kujitoa kwa JMK kutamjengea heshima katika jamii kuwa angalau aliweza kuwa na ujasiri wa kufanya hivyo kwa maslahi ya taifa.

JMK, jitoe uinusuru Taifa !!
 
Mtu kama hawezi kazi basi ni lazima aambiwe kazi imekushinda kaa pembeni.Narudia tena Kikwete kashindwa kazi na hiyo ni sababu tosha ya kutomrudisha madarakani.

- Ni kweli kabisa, ila dawa ni kumumbia tizama umeshindwa kazi, tizama flani alivyoweza, ni vyema umpishe na kumuachia huyu flani, au?


william.
 
- Mkuu wangu hivi unajua jinsi Kikwete, alivyotishiwa kabla ya kugombea mwaka 2005? Wabongo tuache uoga, mbona Shibuda amesema wazi kwani amefanywa nini so far?

- Kubalini tu kwamba hata nyinyi hamna uhakika nani anafaa, na huku ndani ya CCM kumejaa waoga wengi wanaotegemea msaada kutoka mbinguni, ndio maana mtu anayejiweza na asiye muoga kama Kikwete ndiye atakayeendelea, na mwishoni mwa kumaliza kwake ataamua nani awe mrithi wake maana tumekuwa waoga mno.

Respect.

FMES!

Mambo ya kisiasa si rahisi kuyatabiri, ndiyo maana hakuna alitabiri kwamba Obama angekuwa mgombea wa Democrats na hatimaye kuwa Rais wa Marekani.

Hivyo hivyo si rahisi kutabiri ni nani anayefaa kumreplace Kikwete maana kutabiri mambo haya si rahisi hata kidogo.

Kikwete ni muoga sana ndiyo maana pamoja na recommendations za kamati ya Mwakyembe ameshindwa kuchukua hatua zozote dhidi ya Hosea na Mwanyika, pamoja na ushahidi wa kutosha kuhusu ufisadi wa Rada ameshindwa kuchukua hatua dhidi ya chenge na Idrissa Rashid, pamoja na ushahidi wa kutosha dhidi ya Richmond/Dowans, Kagoda ameshindwa kuchukua hatua zozote dhidi ya Rostam. Pamoja na ushahidi wa kutosha kuhusu uuzwaji wa kifisadi wa Kiwira ameshindwa kuchukua hatua zozote dhidi ya Mkapa na Yona. Pamoja na ahadi chungu nzima kuhusu kuipitia upya mikataba ya uchimbaji wa madini yetu hadi hii leo ikiwa ni mwaka wa nne tangu aingie madarakani ameshindwa kufanya lolote ili kuibadilisha mikataba hiyo kwa maslahi ya Watanzania. Rais muoga na ambaye haweki mbele maslahi ya nchi na Watanzania HATUFAI na hili siyo siri.
 
- Ni kweli kabisa, ila dawa ni kumumbia tizama umeshindwa kazi, tizama flani alivyoweza, ni vyema umpishe na kumuachia huyu flani, au?


william.

Obama hakuwa na record yoyote ya maana alipoamua kugombea lakini waliweza kumuamini na kumkabidhi aiongoze nchi. Hivyo nasi tunaweza kumpata Mtanzania ambaye anatimiza masharti yote ya kugombea Urais na kumkabidhi nchi na akafanya kazi nzuri na kuweka maslahi ya nchi mbele zaidi ya Kikwete.
 
William, Pamoja na mfumo wa chama kimoja nakumbuka Mwalimu Nyerere alipotangaza kuwa angeng'atuka na asingegombea tena nafasi ya Uraisi, hali ya wasi wasi iliikumba nchi na kuna watabiri walioona hali ya machafuko ikiinyemelea Tanzania. Hali hii ilisababishwa zaidi na kujengeka kwa imani na hofu ya Tanzania bila Nyerere !!

Baada ya kuingia kwa mfumo wa vyamam vingi hali ya hofu kama hiyo iliigubika nchi tena na imetumiwa sana kama mtaji mkubwa na chama tawala hadi leo - hofu ya Tanzania bila CCM !!. Sababu zinazotolewa ni zile zile zinazoendeshwa na wasioitakia mema taifa kama vile CCM ina hatimilki ya amani Tanzania na wasiwasi wa wapinzani kusababisha machafuko na vita.

Katika msingi huo huo Raisi JMK pamoja na mapungufu yake yote, kuna wanaojaribu kutumia hoja hiyo hiyo kuwa Tanzania bado inamhitaji na nia yoyote ya kumtoa ni kuchokoza hali ya utulivu na amani. Ndani ya CCM kwa sasa haitarajiwi yeyote ajitokeze kumpinga na atakayethubutu ni adui na mvurugaji kama inavyoanza kuenezwa na mitume bandia.

Naamini kwa dhati kuwa kama JMK, kwa mapenzi yake kwa taifa, ataweza kung'amua mapungufu yake mapema, atajitoa katika kinyang'anyiro cha mwaka 2010. Ambacho sina hakika ni kama ataweza kuwa hata na ujasiri huo na hii inatokana na tabia yake ya kukumbatia ushikaji katika utawala wake na kushindwa kufanya maamuzi mazito.

William, leo hii JMK akitangaza kuwa hatagombea, mtu/watu a/watajitokeza na nakuhakikishia wapo wengi tu na wenye uwezo na ushawishi mkubwa. Kutokujitokeza kwa sasa hivi ni kwa sababu ya woga wa katiba inayotoa nafasi kwa vyombo vya dola kufumbia macho uvunjaji wa sheria kwa kuangalia sura, itikadi, wadhifa na nafasi katika jamii.

Kujitoa kwa JMK kutatoa nafasi kwa taifa kupata wigo mpana na huru wa wagombea. Kujitoa kwa JMK kutaleta neema katika ushindani kwa kutoa nafasi sawa kwa wagombea watakaoingia ulingoni. Kujitoa kwa JMK kutaidhoofisha CCM kwa kiwango fulani lakini hili naamini ni jambo jema kwa taifa - CCM is too fat and it needs to diet. Kujitoa kwa JMK kutamjengea heshima katika jamii kuwa angalau aliweza kuwa na ujasiri wa kufanya hivyo kwa maslahi ya taifa.

- Mkuu naona hoja tatu muhimu, nazo ni uoga wa baadhi ya wana-CCM, ushikaji, na kujitoa kwa rais mapema.

- Well, kwenye hili la uoga unakuwa sio mstaarabu unaposema kwamba hoja usizozikubali za baadhi ya wajumbe wa CCM, basi zinatolewa na mitume bandia kwa nini usiruhusu hoja yako hata siku moja isimame bila this kind of abusive language? Wao wametoa tamko lao la nani wanamtaka na sababu zao, sasa labda na wewe utoe zako na ushinde hoja zao, maana otherwise, unaonekana kuongelea kutoka kwenye corner ya defeatism na that is scaring kwa sababu ni haki yao kikatiba kuona wanavyosema.

- Umesema pia hoja ya Ushikaji kama moja ya pungufu kubwa la rais wa sasa, sawa lakini tizama mzizi wa ushikaji na uongozi wetu wa taifa, utaona kwamba huyu rais wa sasa, anajaribu kufuata nyayo zilizowekwa kabla yake na ni tabia iliyoko kwenye kila kona ya uongozi katika taifa letu, ukabila, udini, na ushikaji, sasa kweli unaamini hili kuwa ni kosa lake au anaendeleza tu aliyoyakuta?

- Mwisho unaongelea yeye kujiuzulu voluntarily, kwa sababu gani hasa? Kwa sababu ningeelewa kama ungesema kuwa tizama huyu kiongozi X wa CCM anayefaa, katika miaka mitano ya utawala wa awamu ya nne, amefanya one, two three as opposed na rais Kikwete, kwa hiyo ni bora ampishe kiongozi X, au? Otherwise, sioni hoja ya msingi ya rais wa sasa kujiuzulu au kama ipo lakini haikusemwa!

Kwa kumaliza ninasema hivi, wa-Tanzania tuache uoga, tuache ku-assume na tuheshimu mawazo tofauti na yetu.

Ahsante.

William.
 
...mimi naamini kuwashinda CCM lazima kuanzie kwenye viti vya ubunge la sivyo kuwaondoa hawa jamaa itakuwa ndoto na wataendelea kutufisadi na kututia umaskini wa milele,siamini chama chenye wabunge wasiozidi 20 kati ya 400 kinaweza kushinda uraisi,battle zote zipo bungeni na kule ndio kelele zinaweza make sense sio za kina Mrema kule manzese wanaonekana wendawazimu tuu!
 
- mkuu wangu hivi unajua jinsi kikwete, alivyotishiwa kabla ya kugombea mwaka 2005? Wabongo tuache uoga, mbona shibuda amesema wazi kwani amefanywa nini so far?

-
fmes!

shibuda has got nothing to loose, he is not regarded as a threat to kikwete. Its a win win situation for him.
Kikwete is so nervous of standing against anyone.
 
- - Mwisho unaongelea yeye kujiuzulu voluntarily, kwa sababu gani hasa? Kwa sababu ningeelewa kama ungesema kuwa tizama huyu kiongozi X wa CCM anayefaa, katika miaka mitano ya utawala wa awamu ya nne, amefanya one, two three as opposed na rais Kikwete, kwa hiyo ni bora ampishe kiongozi X, au? Otherwise, sioni hoja ya msingi ya rais wa sasa kujiuzulu au kama ipo lakini haikusemwa!
Ahsante.

William.

Hili la kutoa jina la nani anayefaa mimi sikubaliani nalo na mfano wangu tena ni kwa Obama, maana kama Democrats wangeamua watote majina ya wanaofaa kuwa wagombea wa chama hicho jina la Obama lisingekuwemo kwa sababu hakuwa na umaarufu mkubwa ndani ya chama hicho, ni mweusi na tulishasikia mara nyingi kwamba America is not ready for a black president, he has a funny name na his middle name is Hussein and also no big accomplishments in politics or leadership to show off. Ndiyo maana napingana na wenye dhana ya kutaka watu wataje majina. Maana kwa mantiki hiyo leo hii Obama asingekuwa Rais wa Marekani.
 
Kinachouma wengi hapa (pamoja na mimi) ni
1. kushindwa kwa kiongozi uliepo madarakani kuleta maendeleo yoyote ambayo aliahidi kwenye uchaguzi uliopita,
2. kushindwa kutekelezwa kwa ilani ya CCM (chama ambacho hata mimi ni mwanachama),
3. kushindwa kutekelezwa kwa sheria sawia kwa watu wote nchini (wezi wadogo kufungwa hata bila kuwepo ushahidi wa kutosha, na wezi wakubwa kutochukuliwa hatua zozote hata kama ushahidi upo),4. kuanza kwa kampeni zenye nia ya kukemea wanaCCM kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Urais (kikatiba) ndani ya chama chao,
5. kuanza kwa kampeni kabla ya wakati (kumpigia chapuo kiongozi aliepo madarakani).


Siamini kuwa kuna mtu mwenye mamlaka ya kukataa mtu yeyote asiteue mtu ampendae. Kinachosumbua ni kuanza mapema uteuzi usio rasmi wenye nia ya kulazimisha (ku-influence) viongozi wengine wote kuunga mkono azimio lisilo la kikatiba, lenye nia ya kudhoofisha haki ya mtu kuchaguliwa. Viongozi wanaotakiwa kuwa na subira hadi wakati muafaka wa kuchagua/kuteua/kupendekeza wameanza mapema mno na hasa kwa kuwafanya wengine wasitumie haki yao kwa ukamilifu. Viongozi wengine wote wanalazimika sasa kuonyesha msimamo wao katika utetezi wa mgombea Urais (watake, wasitake). Madhara yake ni wao kushiriki kwenye kile wasichokiamini.

Kila mtu anaweza kuwa na chaguo lake la mTanzania anaemuona kuwa anafaa kuwa Rais wa nchi. Ila mapenzi yoyote kwa mtu huyo, hayana maana kama mtu huyo hana nia ya kuomba kuwa Rais kwa kufuata taratibu zilizopo (ambazo zimeanza kukiukwa makusudi). Mimi naweza kusema kuwa, ninaamini kuwa naweza kufanya vizuri zaidi ya yaliyofanywa na Rais wetu kwa miaka mitano (5 years). Ninaamini kuwa ninaweza:
1. kutetea na kuilinda sheria ya nchi kwa kuhakikisha kuwa inatumika ipasavyo kwa wote bila kujali tabaka la mhusika
2. Ninaamini kuwa ninaweza kulinda rasilimali za nchi hii zisitumike kufaidisha watu binafsi na kuliacha Taifa likiangamia katika umasikini
3. Ninaamini kuwa nchi ina watu wenye uwezo, nia, na matamanio ya kuwa na hali bora na wako tayari kushirikiana na serikali kufikia malengo yoyote yanayokubalika. Nina uwezo wa kuwashirikisha kufanya hivyo
4. Ninaamini kuwa ninaweza kudumisha/kuendeleza/kuhakikisha uhuru, amani na utulivu unakuwa wa kweli nchini
5. Ninaamini kuwa kila tatizo lina ufumbuzi wake, na ufumbuzi wake ni nia ya kulitatua tatizo hilo kwa vitendo bila subira.
6. Ninaamini kwa dhati kuwa KATIBA ya nchi hii inatakiwa iundwe upya ili kuweka usawa wa kweli kwa kila mtanzania, kuweka mipaka ya utendaji wa mihimili mikuu ya nchi, kuweka demokrasia zaidi, na kuhakikisha utawala bora.



Huu ni uongo mkubwa na aibu kwa Taifa hili. Haiwezekani kufikiria kuwa nchi hii ni masikini wa upeo/uwezo/ujuzi na akili kiasi cha kutokuwa na watu wenye uwezo wa kufanya mambo makubwa kwa Taifa hili zaidi ya JK. Ni kauli inayosikitisha sana.

Ninaamini kuwa ndani ya CCM kuna watu wengi sana ambao wana uwezo wa kufanya mambo mazuri zaidi ya wote uliowataja hapo juu. Watu hao ambao wamedidimizwa wasionekane au hawana nafasi ya kufanya mambo hayo (either kwa kujali amani, utulivu, na hekima) wanafanya hao unaowataja hapo juu waanze sasa kukemea nia ya yeyote kuomba kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania kupitia chama chake.

Ndio maana tukasema bora huyo JK. Uko serious kweli na unayoyasema?
Unataka maendeleo yalyokosekana miaka 50 uyapate kwa kipindi cha miaka mitano na huku unakaa kwenye Forum na kuanika pumba ukitaka Jk akuletee maendeleo? Maendeleo huletwa na watu sio mtu binafsi.

Unaijua Ilani ya CCM? Ni kujinufaisha na hilo lilihakikishwa kabla Mkapa hajaondoka Kwa Fedha zetu. JK anatekeleza vizuri na ndio maana wanamgangania
Tangu aingie Kikwete angalau mauwaji ya Polisi yanafanyiwa kazi. Hata hivyo si kazi ya Rais kufatilia Kesi na ukichungua hivi sasa ndio wakati ambao haki mara nyingi zinafuatwa.
Na hizi harakati za wanaojipendekeza nazo umbebeshe yeye? Lini katika hotuba zake ukamsikia kama Rais wetu aliepita akisema kila wakati " Nilpoingia madarakani nchi ilikuwa hivi .............,vile.........?
Tumekuwa tukiomba kupatiwa mbadala wa Kikwete na tutaendeleza kudai hivyo, wewe la!
 
Suala si anayefaa, wao tayari wanaye mtu wao wa kushika nafasi. Kwamba anafaa hilo ni suala jingine ambalo Watanzania watalazimika kujifunza kwa kutumia uhalisia.
Lakini pia kwao sasa hivi suala la nani atachukua nafasi si relevanty, vita yao kwa sasa ni kuondoa huyu aliyepo

Akina nani Mkuu? CCM au kina BUBU?
 
Wapo wengi wanaofaa, ni vile hawana majina na hawategemewi kugombea ndio maana huwezi kusema ni huyo au ni yule. Si kila anayefaa kuongoza lazima ajulikane na kila mtu. Kumbuka pia kiongozi unayemuona anafaa anaweza asiwe kiongozi bora kwa mwingine kutokana na kuwa na vigezo tofauti!

Mkuu jina lako liheshimike. Kikwete alijitangaza tukajuwa kuwa anajiona anaweza, basi na hao wengine mpaka watakapojulikana ndio watapata nafasi, sio scientific ilivyo kuwe na substance?
 
kumchagua tena kikwete itamaanisha kwamba watanzania tuko tayari kuchagua uzembe kwa mara nyingine na hao wazee unaowaona wote ni wa pambe na njaa zao.

ukiniuliza nani apewe nakuambia MAGUFULI. hata wizara ya minofu anafanya kazi na kama kawaida inaonekana kuna nguvu zinamsimamisha baada ya kuchukua hatua. hata alivyokuwa wizara za nyuma alikuwa anafanya kazi lakini bosi wake alikuwa anamsimamishwa, kama ilivyo bosi wa sasa hivi. kumpeleka magufuli minofu ni kumnyima media attention ili kuua nguvu yake kisiasa.



putin aliwekwa kwenye urais na oligarchs na alivyokuwa rais akawachukulia wote atua na kuhakikisha utajiri wa rusia unatumika kuinua uchumi wa russia na sio familia chache.

magufuli akichaguliwa atapambana na kina rostam kwa ajili yeye ndio mwenye nguvu zote.
kikwete sio kama hawezi kuwachukulia hatua bali hataki.

na magufuli nae asipofanya kazi miaka 5 tu mwisho.

mkandara unaabisha JF kuona kwamba ushakubali ya ishe, watu regular wa JF kama nyie mnakubali ya ishe inaonekana hamtaki CHANGE.

mabadiliko yanatakiwa kila miaka mitano mpaka viongozi waanze kufanya vizuri.
MKANDARA WEWE HUNA TOFAUTI NA HAO WAZEE SIJUI NA WEWE NI MZEE.
YOU ARE RESISTANCE TO CHANGE, IT IS TIME FOR YOU TO START SUPPORTING THE CHANGE MOVEMENT.
HII INAONYESHA WEWE NI MKAZI WA DAR NA SIO WA TARIME.


Hongera angalau umeonyesha njia. Lakini usiwabebeshe watu wengine failure yake. Hebu tupe ushahidi wa kikwazo cha Mkapa kwa Magufuli na Baadae tupe kikwazo cha JK kwa kushindwa kufanya kazi zake.
Mambo mawili kama umezingatia moja ni kuwa Wizara alizopita Magufuli kazikuta na uozo wa rushwa na huondoka akiziwacha bado katika hali hiyohiyo au zaidi. Sasa wizara mojamoja ni hivyo atakapopewa jinchi lililooza kwa rushwa itakuwaje?
Jambo la pili kwa kigezo cha ushujaa wa humu JF hafai kwani hapambani na Mafisad ndani ya CCM.
Ama kwa data nafikiri akichaguliwa Urais kutakuwa hakuna haja ya Seketeri wa kumwandikia data atakuwa nazo kichwani.
 
Siyo kweli kabisa kusema kwamba Kikwete hakufanya moja tu. Vita dhidi ya mafisadi imemshinda. Mjadala mkubwa dhidi ya ununuzi wa Dowans alinyamaza kimya bila kutia neno na yule Comical Slava akatwambia Watanzania Kikwete hahusiki kabisa na Dowans!!! Lakini katika hotuba yake ya juzi alitaka mjadala wa Dowans ufungwe haraka pamoja na kuwa bado kuna maswali chungu nzima kuhusiana na Dowans. Mjadala wa Vitambulishho vyenye thamani ya shilingi 200 bilioni hakutia neno, alikaa kimya kabisa pamoja na kuwa yeye ndiye Kiongozi Mkuu wa nchi yetu. Aliahidi kuipitia upya mikataba ya uchimbaji madini yetu mbali mbali ikiwemo dhahabu, sidhani kama hili lilihitaji miaka minne kabla ya kulishughulikia, lakini hadi hii leo hajafanya chochote. Pamoja na kuwa kuna ushahidi wa kutosha kwamba Chenge na Idrissa Rashid walinufaika na ufisadi wa ununuzi wa Rada ya $40 million ambao Watanzania wengi tuliukataa lakini hadi hii leo hajachukua hatua zizote dhidi yao na bado wanapeta uraiani. Katika ripoti ya Mwakyembe na timu yao walirecommen kuondolewa madarakani Mkuu wa PCCB Edwards Hosea na Mwanasheria Mkuu Johnson Mwanyika hajafanya hivyo hadi leo na hajatwambia sababu zozote za kutotimiza recommendations za Kamati ya Makyembe. Huu ni ushahidi wa kutosha kwamba utendaji wake ni dhaifu.



Mimi hizi alinacha kwamba hakuna kiongozi anayeweza kuchukua hatua dhidi ya kingozi mwingine sitaki kuzisikia kabisa. Kama wote ni watenda dhambi basi hawafai kutuongoza maana dhambi zao zinaisababisha nchi yetu kutopata maendeleo yoyote yale wakati wao wakiendelea kuaccumulate wealth na kuwa mabilionea. Kama wote ni mafisadi basi ni lazima tuwaambie ukweli kwamba nyie ni mafisadi na Watanzania hatutaki kuongozwa na mafisadi.



Labda wewe ndiyo unaona kwamba Lowassa na mtandao wametemwa, lakini mimi sioni hivyo. Kwa sababu Lowassa bado anahudhuria vikao vya juu kabisa ndani ya CCM na juzi juzi tuliona wanamtandao walivyohakikisha kwamba watu wao wa karibu katika Wakuu wa Wilaya hawatimuliwi madarakani. Hivyo mtandao bado una nguvu za kutosha tu kuweza kufanya lolote lile walitakalo.



Wewe ndio mnafiki usiyetaka mabadiliko kwa ajili ya maslahi ya nchi yetu. CCM kina wanachama million 4, halafu unategemea mimi nikupe jina la mtu anayefaa kati ya hao watu millioni 4!!!!! Ha ha ha ha acha alinacha zako!!!! Nimekupa mfano rahisi kabisa wa Obama kwamba hakuna aliyemdhania kwamba Obama atachaguliwa kuwa mgombea wa Democrats kwa sababu Wazee na wananchama wengi wa Democrats walimtaka Hillary kwa sababu ya jina kubwa, good organization when it comes to big elections, Mumewe ana heshimika sana ndani ya chama chao, lakini pamoja na hayo yote ambayo yalikuwa ni disadvantage kwa Obama hakukata tamaa akaingizana tu na hatimaye kuwashinda akina Clinton na kuweka history ya kuwa Mweusi wa kwanza kuwa rais tangu Marekani ipate uhuru miaka 253 iliyopita. Achana na alinacha za kutaka nikutajie majina makubwa kama unavyotaka wewe, anaweza kabosa akatokea mtu ambaye hajulikani sana lakini akafanya vitu vyake na kumbwaga Kikwete na hatimaye kuwa Rais wa Tanzania.

Acha utetezi wako wa madikteta ndani ya CCM. Katiba ya CCM haisemi popote pale kwamba vitisho na ubabe utatumika ili kuwatisha wale wanaotaka kumpinga Rais aliyemaliza awamu moja madarakani katiba ifuatwe bila vitisho wala ubabe.

Njemba zinazojiita Wazee wa CCM zinajua Kikwete ni mtupu hawezi akasimama katika jukwaa lolote lile ndani ya nchi na kuorodhesha his accomplishments for the past four years, maana hakuna hata moja ndiyo maana wameanza na zengwe zito la kuwatisha wale wote wanaotaka kumpinga Kikwete. IT IS TIME FOR CHANGE!!!!!


Mkuu Bubu hebu kuwa na msimamo unaoeleweka. Namna unavyoelezea mfumo mbaya ulioko CCM na baadae kufikiria kuwa huyo mwanachama alieko Manzese tawini ataweza kupata nafasi ya kuteuliwa nafasi ya urais Duh! nafikiri hii ndio aninacha sio hiyo unayoiona wewe.
Be realistic nani kwenye CCM alitokea tawini tu akawa mjumbe wa halmashauri kuu sembuse kamati kuu na nafasi ya kugombea urais.
Mfano wako wa Obama does nt hold water na hali hii tunayoizungumza. Obama alipitia nafasi zote na ilikuwa stahiki yake kupanda hapo alipo na kwa mfano huohuo wa Obama na sisi tunawapima wana CCM walikokuwa tayari kufikia kiwango hicho cha kugombea urais na tunashindwa kumuona na hasa kwa kigezo chako mwenyewe kuwa wote si safi kwa vile wamebebwa na Chama kilichokuwa si safi.
Kama unakubali kuwa CCM ina mizizi katika ufisadi utawezaje kutegemea mmoja wa wajumbe wa mafisadi kupigana na ufisadi. Ni miaka minne sasa tangu CCM iingie madarakani kwa pesa za EPA ni nani katika CCM,awe mbunge, Waziri,Mwenyekiti wa Mkoa au mjumbe aliekikana Chama kwa ufisadi wake?
Mapambano tunayoyaona si mapambano ya kukisafisha chama bali ni kulipizana kisasi kwa wanachama binafsi. ingekuwa vita hivyo ni dhidi ya shina hasa CCM basi tungesema kuwa anaweza akatokea mtu alietofauti na wenzake ndani ya CCM na kwa hivyo huyo alieko mwache amalize muda wake, kwani si hatuna Chama chengine cha kushika Madaraka.?
 
Vigogo waanza kukorogana

Mwandishi Wetu Aprili 8, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Baadhi wawabeza Ndejembi na wenzake

Wengine: Kuna mbio za kumuwini Kikwete

Wasema hoja ya msingi si urais, ni ufisadi

BAADHI ya wanachama waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamesema uamuzi wa kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete kuwania tena urais mwakani si jambo la msingi bali jambo la msingi ni hatari iliyopo ya dola kuelekea kutekwa na kikundi cha matajiri.

Kwa mujibu wa wana-CCM hao, kuna msukumo mkubwa kwa matajiri nchini na hasa wenye maadili yanayotia shaka, kuwekeza katika siasa kwa kuwania nafasi za uongozi lakini kwa malengo ya kulinda maslahi yao.


Maelezo ya viongozi hao waandamizi wa CCM yanakuja siku chache baaa ya baadhi ya wenyeviti wa mikoa wastaafu wa chama hicho kufanya mkutano na waandishi wa habari na kutangaza pamoja na mambo mengine kumuunga mkono Rais Kikwete katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Katika mkutano wao huo uliofanyika Aprili 5, mwaka huu, wazee hao Pancras Ndejembi ambaye ni mwenyekiti mstaafu mkoa wa Dodoma, Tasil Mgoda (Iringa), Jumanne Mangara (Pwani) na Hemed Mkali (Dar es Salaam), walisema wanamuunga mkono Kikwete na kukemea tabia inayojitokeza ya baadhi ya viongozi kutumia vita ya ufisadi kama mtaji wao wa kisiasa hata kama wameshindwa kutekeleza wajibu wao kwa wananchi.

“Tupigie kelele rushwa lakini turudi kwenye kuitaka Serikali iimarishe taasisi na vyombo vya kupambana na rushwa. Huko ndiko watuhumiwa wa rushwa wanachunguzwa, wanakamatwa na hatimaye wanahukumiwa.

“Baada ya kuhukumiwa na mahakama ndipo tunawaita mafisadi. Kumuita mtu fisadi kwenye gazeti au kwenye mkutano wa waandishi wa habari peke yake hakutoshi kama tunataka kushinda mapambano haya. Ni lazima vyombo vya na taasisi za kupambana na rushwa viwe imara,” alisema mzee Ndejembi kwa niaba ya wenzake.

Alidai pia kwamba kila wanachama wa CCM wanachukia rushwa kwa kiwango sawa na kwamba vita dhidi ya ufisadi ni ya chama hicho na si ya kikundi kidogo cha wana-CCM ambacho kinatumia mwanya huo kama mtaji wa kisiasa.

Kutokana na maelezo hayo ya akina mzee Ndejembi, viongozi wengine waandamizi wa CCM wamezungumza na Rai Mwema wakijaribu kutafuta kiini hasa cha kuibuka kwa wazee kuzungumza mapema kumuunga mkono Kikwete na matatizo ya msingi yanayokizonga chama chao, ambayo hayajafichuliwa.

“Baadhi katika kuhakikisha wanawekeza katika siasa hususan ndani ya CCM wamehakikisha wanakuwa wafadhili wakubwa wa chama na ndiyo maana baadhi ya misaada yao aliyowahi kupokea Rais Jakaya Kikwete imezua maswali mengi,” alisema mmoja wa viongozi wa kitaifa wastaafu.

Ingawa kiongozi huyo hakuwataja kwa majina matajiri hao ambao maadili yao yana utata, mwaka jana Rais Kikwete aliwahi kupokea msaada kutoka kwa tajiri Tamil Somaia, kwa ajili ya kusaidia uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kitendo hicho cha Rais Kikwete kupokea msaada huo kwa ajili ya UVCCM huku ikifahamika wazi kuwa mhusika anahusishwa katika tuhuma za ufisadi wa rada kilizua mjadala mkali miongoni mwa wana-CCM na makundi mengine yasiyofungana na vyama vya siasa nchini, wakiwamo waandishi wa habari.

Kiongozi mwingine ambaye pia hakutaka kuandikwa jina lake gazetini ambaye pia ni mstaafu ngazi ya kitaifa, alisema hatua ya baadhi ya wenyeviti wastaafu wa mikoa wa CCM kutangaza kumuunga mkono Rais Kikwete imedhihirisha makundi yaliyopo ndani ya CCM hadi sasa.


“Unajua kuna siri moja. Mzee Malecela (John) bado ana heshima kubwa ndani ya CCM na kwa sasa wanachama wengi ndani ya chama wanamwona kama kiongozi wa kundi la viongozi wanaopinga ufisadi hadharani bila woga.

“Sasa kitendo cha Malecela kutoka hadharani na kuzungumza kumuunga mkono Kikwete mwaka 2010, maana yake ni kwamba kundi lake la wapambanaji wa ufisadi liko karibu na Rais Kikwete, lakini kwa upande wa Ndejembi (Pancras) huyu ni hasimu mkubwa wa kisiasa wa Malecela,” anasema kiongozi huyo na kuongeza kuwa;

“…pia Ndejembi mbele ya wanachama wengi wa CCM anajulikana kuwa katika kundi moja la akina Peter Kisumo, Kingunge Ngombale-Mwiru na wengine ambao kauli zao zinatafsiriwa na wanachama kama zinawaonea huruma mafisadi na kwamba kundi lao linaendeshwa kwa maelekezo ya waathirika wa ufisadi na rushwa ambao baadhi wamejiuzulu.”

Naye mbunge mmoja ambaye pia alishirikishwa na gazeti hili kutoa mawazo yake kuhusu hatua ya baadhi ya wastaafu kuzidi kujitokeza kumuunga mkono Rais Kikwete, alisema mashindano ya kila mmoja kujitokeza kumuunga mkono Rais mwakani ni kutaka kundi husika kujisogeza jirani naye.

“Haya mashindano si suala la msingi, lakini msingi hapa naamini kwamba ni kuwapo kwa juhudi na wasiwasi wa nchi kufikishwa katika hali tunayoweza kusema state capture…yaani dola kubakwa hasa na matajiri haramu.

“Hii ndiyo hali iliyojitokeza nchini Italy. Italy imejikuta ikiongozwa na kampuni kubwa na matajiri…wananchi hawana nguvu wala sauti. Nikupe siri moja hata hapa kwetu huo mkakati upo ingawa umesitishwa baada ya kulipuka kwa kashfa ya Richmond…lakini watu wachache walijipanga kutawala uchumi na siasa za nchi na hatimaye vyombo vyote vya dola yakiwamo majeshi yetu,” alisema mbunge huyo ambaye amejijengea heshima kubwa mbele ya jamii katika miaka ya hivi karibuni.


Katika kusisitiza maelezo yake alisema; “Walijipanga na kuhakikisha siasa inakuwa kwa ajili ya watu wenye pesa kuanzia ubunge lakini ule mchakato wa kwenda kwenye state capture umetingishwa na suala la Richmond na wanaonekana kukata tamaa na hizi vuruguru za hapa na pale kutoka kwao ni sawa na mateke ya mfumo unaoondoka,” alisema.

Mbunge mwingine aliyezungumzia mwenendo wa sasa katika CCM ambaye pia kama ilivyo kwa wenzake hakutaka kuandikwa jina lake, akihofia kuvuruga uhusiano wake na wazee hao wa CCM, alisema; “Jambo la kutia moyo ni kishindo cha nguvu ya umma kutokuwa upande wao."

Hata hivyo, alishangazwa na baadhi ya wazee wa CCM wanaojitokeza kukemea wanaopinga hadharani ufisadi huku wakishindwa kukemea watuhumiwa wa ufisadi ambao kwa mujibu wa mbunge huyo wanatumia fedha zao kuanzisha magazeti ya kuwachafua wana-CCM wenzao.
 
Back
Top Bottom