The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Kwa kuliaokowa taifa lisitumbukie katika janga la matatizo kuna umuhimu kumuachia kikwete aendelee na uongozi kwa kipindi kingine cha miaka mitano kwani kumuondowa kikweteni kuleta kizaza ndani ya taifa hilo kutokana na makundi ya watu wanaotaka kuchukuwa mdaraka kwa manufaa yao binafsi kwa hilo kuna ulazimu wa kuwazuwia na kumwachia kikwete aendelee
 


Mkandara Mkuu, mimi nakubaliana na wewe sana hasa kwenye issue ya imani. Naamini kwa ufahamu mzuri ulionao, unaoanisha imani ya sera za chama tawala na mafanikio ama kushindwa kwa malengo ya Taifa letu. Mimi naamini kama wewe, nishichokiamini ni kuwa CCM haina sera nzuri. Hili si la kweli. CCM ina sera nzuri sana tu na pia ina imani na malengo mazuri. Kama umefuatilia kwa makini nilichokisema kwenye post iliyotangulia, niliweka pia kushindwa kutekelezwa sera nzuri za CCM.

Mkuu, mafundisho ya imani ya dini, au itikadi yoyote yanategemea sana na kiongozi/mfundishaji/msimamizi wa mafundisho hayo n.k. CCM imeshaweka sera zake ambazo kwa kweli ndizo zilizotufanya tusisite kukichagua kwa mara nyingine mwaka 2005. Sera hizo nzuri zilisambazwa vizuri, zikaeleweka. Ambacho hakikufanyika ni utekelezaji wa sera zenyewe. Hili ndilo linalotufanya tuamini kuwa tulilaghaiwa na sasa inatosha. Sioni sababu ya kuendelea kuamini kuwa itafika siku mtu yule yule alieshindwa akaweza kutekeleza vyema yote aliyoahidi. Sioni mwelekeo huo.

Kufananisha walioshindwa na kudhani kuwa wote ni watakaoshindwa nalo ni kosa kubwa. Bondia akianguka kwenye pambano, halafu akaanza kufikiria waliowahi kuanguka katika mashindano ya nyuma, ni wazi kuwa ataishia kushindwa kwa knock-out. Tunachotakiwa kama Taifa ni kuangalia tulipoanguka na kuchukua hatua za kutuhakikishia kutoanguka tena siku za mbele. Kwa maneno mengine ni kwamba, inatakiwa kujua kuwa, tulianguka wapi, kivipi na jinsi gani ya kukwepa kufikia kuanguka kama huko.

Mkandara ndugu yangu, mimi naweza kutaja watu wengi tu ndani ya CCM wenye uwezo mkubwa wa kuleta unafuu kiuchumi, kisheria, kijamii, n.k., kuliko tunavyoendelea hivi sasa. Ila nitakuwa siwatendei haki watu hao kama nitawataja na wao wasiwe na nia ya kutaka kuongoza Taifa hili. Ndio maana nikasema (hapo juu), kuwa hata mimi ninaamini kuwa ningeweza vizuri zaidi.

Ninachoweza kukiomba chama changu CCM ni kutoa ruhusa kwa wenye uwezo kugombea nafasi hiyo kwa usawa na haki. Baada ya wote kuchukua form na kuzirudisha, ndipo tutakapoweza kuona options tulizonazo.

Tunapata nafuu kusikia kada akitowa maelezo ya kukitetea chama chake kwa sera nzuri. Suwala langu lipo hapa, Jee umejiunga na CCM lini?
Nauliza hivyo kwa kuwa CCM ipo madarakani tangu mwaka 1977 na kama hivi sas hapana maendeleo basi hivyo vipindi vya nyuma kulikuwa na hali mbaya zaidi. Sasa kwanini huko nyuma mlituachie viongozi wenu waliofanya mabaya mengi na hata kuwa maadui wa demokrasia tunayoipata sasa?
Huu unausema wewe ni undumila kuwili, hebu fikiria maovu yalioyotendwa wakati wa Mkapa, jee ile ilikuwa sera yenu mliyompa aitekeleze? Hebu taja lolote baya la JK kama hutokuta kayika utawala uliopita ni zaidi. Nanyi CCM mlikuwepo wapi hata mkatupa Mkapa miaka yote kumi.
Halafu jambo linalonifanya kuona kuw kwa CCM hamna mtu safi ni kuwa hakuna aliekuwa tayari kuzungumzia ufisadi wa jumla wa CCM kwa fedha zetu za EPA. Ufisadi eti ni ule wa Richmond pekeyake kwa vile mlikuwa mnamaliziana visasi vyenu lakini lile la jumla lililokupelekeni kwenye utawala hamko radhi kutaja.
Huo msururu wa watu ulionao kwanza itabidi tuwapeleke mahakamani kwa kuficha wizi na kunufaika nao na baadae ndio tuzungumzie uchaguzi.
 
Mkuu Bubu hebu kuwa na msimamo unaoeleweka. Namna unavyoelezea mfumo mbaya ulioko CCM na baadae kufikiria kuwa huyo mwanachama alieko Manzese tawini ataweza kupata nafasi ya kuteuliwa nafasi ya urais Duh! nafikiri hii ndio aninacha sio hiyo unayoiona wewe.

Msimamo wangu unaeleweka kamwe usitake kupindisha hilo. Wapi nimefikiria kwani mwanachama wa tawi la Manzese kama anatimiza taratibu zote zilizowekwa ndani ya CCM kwanini asistahili kuteuliwa kama Rais wa Tanzania!!!? Au kuna matawi maalum yanayoruhusiwa kutoa wagombea wa Urais na mengine ni marufuku kutoa wagombea wa Urais!!? 😕

Be realistic nani kwenye CCM alitokea tawini tu akawa mjumbe wa halmashauri kuu sembuse kamati kuu na nafasi ya kugombea urais.
Mfano wako wa Obama does nt hold water na hali hii tunayoizungumza.

Wewe ndiye unahitaji kuwa realistic na mfano wa Obama unalingana kabisa na yanayoendelea nchini maana wakongwe ndani ya chama chake asilimia kubwa sana walimuunga mkono Hillary, hivyo wangejkuja na vitisho kama Wazee njaa wa CCM kwamba atakayempinga Hillary atakiona basi, Obama asingekuwa Rais wa Marekani lakini wakaacha katiba ya chama chao ichukue mkondo wake na yaliyotokea wote tunajua.

Obama alipitia nafasi zote na ilikuwa stahiki yake kupanda hapo alipo na kwa mfano huohuo wa Obama na sisi tunawapima wana CCM walikokuwa tayari kufikia kiwango hicho cha kugombea urais na tunashindwa kumuona na hasa kwa kigezo chako mwenyewe kuwa wote si safi kwa vile wamebebwa na Chama kilichokuwa si safi.

Obama katika wale waliokuwa wanampinga walidai kwamba hakuwa na experience yoyote katika mambo mbali mbali na alikuwa senator kwa kipindi kifupi mno cha miaka minne na pia walidai kama Senator hakuiniate policies zozote nzito hivyo kutokuwa na uzoefu ilitumika dhidi yake. Wacha katiba ya chama ifanye kazi yake!!!!! Na hapo ndiyo mtajua kama kuna mtu mwingine zaidi ya Kikwete anayestahili kuwa Rais au la, na siyo kutaka kuikana na kuikimbia katiba iliyotungwa na kupitishwa na wanaCCM wenyewe.

Kama unakubali kuwa CCM ina mizizi katika ufisadi utawezaje kutegemea mmoja wa wajumbe wa mafisadi kupigana na ufisadi. Ni miaka minne sasa tangu CCM iingie madarakani kwa pesa za EPA ni nani katika CCM,awe mbunge, Waziri,Mwenyekiti wa Mkoa au mjumbe aliekikana Chama kwa ufisadi wake?

Wako wengi tu ndani ya CCM waliojaribu kupambana na ufisadi na juhudi zao wakapigiwa simu za kutukanwa matusi ya nguoni au hata kutishiwa maisha yao. Hili siyo siri.

Mapambano tunayoyaona si mapambano ya kukisafisha chama bali ni kulipizana kisasi kwa wanachama binafsi. ingekuwa vita hivyo ni dhidi ya shina hasa CCM basi tungesema kuwa anaweza akatokea mtu alietofauti na wenzake ndani ya CCM na kwa hivyo huyo alieko mwache amalize muda wake, kwani si hatuna Chama chengine cha kushika Madaraka.?

Kwanini kiongozi dhaifu aendelee kumaliza muda wake wakati kazi imemshinda!? Miaka mitano kuwa na kiongozi dhaifu ambaye maslahi ya Taifa hayana umuhimu wowote kwake ni muda mrefu sana kwa nchi yoyote ile duniani. Kwa hiyo wakati umefika wa kumwambia ukweli mpishe mwingine maana wewe kazi imekushinda
 
Msimamo wangu unaeleweka kamwe usitake kupindisha hilo. Wapi nimefikiria kwani mwanachama wa tawi la Manzese kama anatimiza taratibu zote zilizowekwa ndani ya CCM kwanini asistahili kuteuliwa kama Rais wa Tanzania!!!? Au kuna matawi maalum yanayoruhusiwa kutoa wagombea wa Urais na mengine ni marufuku kutoa wagombea wa Urais!!? 😕

Kama CCM ingekuwa inaenda hivyo unavyofikiri wewe tusingekuwa na viongozi walewale. Nasema huna msimamo kwa kukisema kuwa chama kimeoza na huku ukitegemea mkubwa mmoja atakuwa safi. Basi waliosafi na wajitokeze na kujikosha na tuhuma za kuingia madarakani kwa fedha za EPA na hilo lifanyike sasa ingawa wameshachelewa kwani wamekuwa wakila fedha zetu kipindi cha miaka minne.



Wewe ndiye unahitaji kuwa realistic na mfano wa Obama unalingana kabisa na yanayoendelea nchini maana wakongwe ndani ya chama chake asilimia kubwa sana walimuunga mkono Hillary, hivyo wangejkuja na vitisho kama Wazee njaa wa CCM kwamba atakayempinga Hillary atakiona basi, Obama asingekuwa Rais wa Marekani lakini wakaacha katiba ya chama chao ichukue mkondo wake na yaliyotokea wote tunajua.

Obama alijitokeza kwasababu alikuwa msafi na ili uwe mfano umekamilika jee tayari huyo mtu kutoka CCM ameshajitokeza?



Obama katika wale waliokuwa wanampinga walidai kwamba hakuwa na experience yoyote katika mambo mbali mbali na alikuwa senator kwa kipindi kifupi mno cha miaka minne na pia walidai kama Senator hakuiniate policies zozote nzito hivyo kutokuwa na uzoefu ilitumika dhidi yake. Wacha katiba ya chama ifanye kazi yake!!!!! Na hapo ndiyo mtajua kama kuna mtu mwingine zaidi ya Kikwete anayestahili kuwa Rais au la, na siyo kutaka kuikana na kuikimbia katiba iliyotungwa na kupitishwa na wanaCCM wenyewe.

Sisi hatupingi experience ya mtu. Sisi tunapinga usafi wa watu wa CCM. Na wala hatukatazi kuwa katiba isifuatwe. Tatizo letu ni kuwa katiba ifuatwe kwa wote ikiwa pamoja na Kikwete kupewa nafasi ya kugombea tena URAIS NA KWA MUJIBU WA KATIBA HIYOHIYO SI VIBAYA KUSEMA KUWA NITAMTETEA MTU FULANI.Wazee hawajasema kuwa mtu asigombee lakini ajuwe tu kuwa wao watamtetea Kiwete. Mimi na wewe tunashindania uwezo wa kugombea urais na tuna haki ya kutofautiana. Hoja ndizo zitakazoamuwa.



Wako wengi tu ndani ya CCM waliojaribu kupambana na ufisadi na juhudi zao wakapigiwa simu za kutukanwa matusi ya nguoni au hata kutishiwa maisha yao. Hili siyo siri.

Mkuu bubu hili la kusema kuwa kitu kipo bila ushahidi si jambo muafaka. Hata mimi nitakwambia kuwa JK amefanikiwa kwa kila jambo lakini utaniouliza mambo gani? Nawe nakuuliza kina nani waliofichuwa siri ya CCM kuingia madarakani ambao tutasema kuwa wanastahiki kuwa Marais?



Kwanini kiongozi dhaifu aendelee kumaliza muda wake wakati kazi imemshinda!? Miaka mitano kuwa na kiongozi dhaifu ambaye maslahi ya Taifa hayana umuhimu wowote kwake ni muda mrefu sana kwa nchi yoyote ile duniani. Kwa hiyo wakati umefika wa kumwambia ukweli mpishe mwingine maana wewe kazi imekushinda

Sijaona udhaifu wa kiasi cha kuwa tusimuamini tena kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Unajuwa kwanini? Sioni tofauti kubwa kati ya utawala huu na tawala zilizopita. Iwapo utawala wa mwanzo tuliuwa njia kuu zote za uchumi na kufa kwa njaa, utawala wa pili ulikuwa utawala wa kutafuta maisha, mitumba,vitega uchumi vya uongo na kusafirishwa nje kwa mali asili zetu, utawala wa tatu kutengeneza viongozi mabepari na kuuza njia kuu za uchumi.
Utawala huu angalau unatowa uhuru kwa akina sie kuwakejeli na kuwaumbua viongozi wetu whether ni mafisadi kweli au shutuma tu huku dola kuwa si tishio kwa mwananchi. Yaliobakia ni yale yale kama tawala nyengine, manufaa kwa wakubwa na kutembeza bakuli. Kwa mtaji huo kama walivyomaliza wengine bado akiletwa na CCM naaendelee.
 
Huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote

Godfrey Dilunga Aprili 8, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

APRILI 5, mwaka huu, baadhi ya wenyeviti wastaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walizungumza mambo yanayokihusu chama chao lakini pia yanayowagusa Watanzania karibu wote.

Wenyeviti hao, mzee Pancras Ndejembi (Dodoma), Tasil Mgoda (Iringa), Jumanne Mangara (Pwani) na Hemed Mkali (Dar es Salaam), walizungumzia mambo mengi lakini makubwa zaidi ni mawili.

Mosi ni kuhusu vita dhidi ya ufisadi nchini. Pili ni kuhusu kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete kuwania tena urais mwakani.

La Rais Kikwete kuungwa mkono kugombea tena mwakani sitalijadili kwa kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko wazi, na hakuna aliye juu ya Katiba au sheria za nchi.

Nitajielekeza katika suala la ufisadi na nikirejea katika mazungumzo ya mzee Ndejembi na wenzake, nitatofautiana nao kuhusu mtazamo wao katika vita dhidi ya ufisadi.

Kwa kuwa nimeshindwa kukubaliana na wazee hawa katika mtazamo wao kuhusu ufisadi, imenilazimu kutafuta mtazamo au mitazamo ya wazee wa zamani zaidi.

Lengo la kufanya hivyo ni kujipima kama nina hoja za msingi katika kutofautiana na akina mzee Ndejembi.

Nitanukuu yale aliyosema mzee Ndejembi kwa niaba ya wenzake. Hata hivyo, kabla ya kufanya hivyo, ninukuu kauli iliyowahi kutolewa na aliyewahi kuwa Rais wa Marekani, Abraham Lincoln (mzee wa zamani zaidi ya akina Ndejembi).

Lincoln aliwahi kusema; "Unaweza kuwadanganya watu wachache wakati wote, lakini huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote."

Sasa wakati unaposoma nukuu ya akina mzee Ndejembi ningependa ukumbuke nukuu hiyo ya 'mzee' Lincoln.

Ndejembi na wenzake wanasema; "Mapambano dhidi ya ufisadi nchini ni mapambano yanayoongozwa na CCM katika kutekeleza Ilani yake ya uchaguzi. Si shughuli ya kikundi cha wanachama wachache."

Anasisitiza zaidi akisema; "Kila mwanachama wa CCM anakula kiapo cha kupambana na rushwa. Sote tunaichukia rushwa kwa kiwango sawa."

"Lakini pia wapo wana-CCM wenzetu wanaotaka kuyatumia mapambano dhidi ya rushwa kama mtaji wa kisiasa. Tusingependa kuona mapambano haya yanatumiwa kama njia ya kujipatia umaarufu binafsi."

Nijadili mtazamo huo wa wazee hao nikiamini kuwa wanayo haki ya kuzungumza kile wanachoamini ni sahihi.

Ni ruksa kwao kuzungumza wanachoamini kuwa sahihi na chenye manufaa kwa taifa.

Hata hivyo, daima tukumbuke kuwa kila mmoja wetu anaweza kuwa sahihi wakati fulani na katika baadhi ya mambo, lakini hawezi kuwa sahihi wakati wote na katika kila jambo.

Tuanze na kauli ya mzee Ndejembi kwamba CCM inaongoza vita dhidi ya ufisadi na wana-CCM wote wanaichukia rushwa kwa kiwango sawa.

Kwanza tukubaliane kimsingi kwamba, lengo kuu la CCM ni kupambana na ufisadi, lengo ambalo pia linaweza kubaki kama nadharia tu au likatekelezwa kwa misingi ya unafiki au hata kuhadaa wananchi.

Lengo hili limetamkwa ndani ya Ilani ya chama hicho ya mwaka 2005, katika ukurasa wake wa 135, kifungu cha 110, kifungu kidogo cha A na B.

Lakini pamoja na CCM kuwa na lengo hilo tujiulize kwa utulivu na umakini mkubwa kwamba je, ni kweli wana-CCM wote wanachukia rushwa tena kwa kiwango sawa kama wanavyotueleza akina mzee Ndejembi na wenzake?

Wazee, vijana na viongozi wa CCM wajiulize swali hili, tena wakikumbuka nukuu nyingine muhimu ya Abraham Lincoln, kuhusu umma.

Katika nukuu hiyo aliyotamka Agosti 21, mwaka 1858 katika mji wa Ottawa, Lincoln anasema; "Public sentiment is everything. With public sentiment, nothing can fail; without it nothing can succeed."

Maudhui ya kauli hii ya Lincoln ni kwamba mtazamo wa umma, ndiyo kila kitu na kinyume chake hakuna kitakachofanikiwa. Kwamba kila jambo ni lazima lifanyike kwa kufikiria umma.

Katika kujiuliza au kutafakari kama kweli kila mwana-CCM anachukia rushwa kwa kiwango sawa, unaweza kubaini makundi mawili yenye mtazamo tofauti katika CCM kuhusu vita dhidi ya ufisadi.

Kundi la kwanza ni la wana-CCM wanaoonekana kupiga kelele hadharani dhidi ya ufisadi, hili linajumuisha baadhi ya wabunge wa chama hicho.

Ukichunguza zaidi utabaini kuwa kundi hili linaungwa mkono na wanachama wengi masikini-wakulima na wafanyakazi, ndani ya chama hicho.

Wanachama ambao wanakosa dawa hospitalini na hata kukosa huduma nyingine za msingi wakiamini kuwa chanzo cha matatizo hayo ni ufisadi.

Kwa hiyo utabaini kuwapo kwa wana-CCM wenye kuchukia ufisadi bila aibu. Wana-CCM katika kundi hili wanaishi katika falsafa ya Lincoln kuhusu umma.

Kundi la pili ni la wana-CCM wanaomini kuwa wanachukia ufisadi huku matendo yao yakiwa tofauti.

Hata hivyo, wakati kundi hili likitaka jamii iamini kuwa wanachukia ufisadi, sehemu kubwa ya jamii hiyo na wana-CCM wengine hususan masikini, wanaamini wenzao hao ni wasanii wanaoigiza kuchukia ufisadi tu.

Watanzania wengi wanawaona kama wasanii wanaovaa sare za CCM na ambao uigizaji wao ni kejeli dhidi ya Taifa.

Kundi hili linajumuisha baadhi ya wabunge, watendaji wa taasisi nyeti nchini. Hata hivyo, wana-CCM wengi wakiwamo wale masikini wanaouza chapati, maandazi na nyanya sokoni ili kupata ada ya shule ya watoto wao, hawafaidiki chochote na waigizaji hawa wenye kupeperusha bendere za CCM, na ndiyo maana wanalazimika kushangilia kundi la kwanza.

Kundi hili la pili unaweza kulitambua kwa njia moja kuu, na hiyo ni njia ya kauli za vitisho vya ëkuumbuana.í

Kwa mfano, utasikia kauli kama tukianza kuumbuana nani atakayebaki? Sasa utajiuliza kama mwanasiasa fulani ni mchafu ni kwa nini usimuumbue kwa manufaa ya umma, na badala yake uishie kutoa tahadhari?

Nini maana na faida ya tahadhari hiyo kwa umma? Ni wazi kuwa tahadhari hiyo itakuwa na lengo la kulinda uchafu wako binafsi kwa njia ya vitisho vya namna hiyo.

Na katika hali kama hiyo ya kutoa vitisho visivyo na matokeo yenye manufaa kwa umma, bado utaendelea kubaki katika kundi la pili, lisilo na msaada kwa wananchi wengi.

Lakini kubwa zaidi, unaweza kutambua waliomo katika orodha ya kundi hili la pili kupitia kauli za wahusia hao. Mwelekeo wa kauli zao ni kujaribu kuonyesha kuwa kelele za hadharani dhidi ya ufisadi ni kukibomoa CCM.

Na katika imani yao hiyo ya kukibomoa chama ndiyo inapojitokeza kauli ya Lincoln kwamba; unaweza kuwadanganya watu wachache wakati wote lakini huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote.

Inashangaza leo hii mzee Ndejembi anayeamini kuwa chama chake ndicho kinaongoza vita dhidi ya ufisadi anatamka kuwa wapo wana-CCM wanaopinga ufisadi kama mtaji wao wa kisiasa.

Tujiulize, hizo kelele za hadharani dhidi ya ufisadi zinakibomoa vipi CCM? je, ni kweli CCM inabomolewa.

Je, wana-CCM wanaweza kupigana vita dhidi ya ufisadi bila milio ya ëmizingaí makombora na hata risasi kusikika? Je, wanaweza kupigana vita dhidi ya ufisadi bila kuathiri maadui.

Tujiulize katika vita hii, hao wana-CCM wasiotaka kelele za hadharani wapo kweli vitani? Kama wapo vitani ni kwa nini wanajitahidi kutibu majeraha wanayopata maadui kutokana na mashambulizi dhidi yao?

Lakini kwa nini CCM ibomolewe wakati imeahidi waziwazi katika Ilani yake ya uchaguzi kuwa itapambana na ufisadi? Kubwa zaidi la kutafakari, kama kweli kila mwana-CCM anachukia ufisadi kwa kiwango sawa kama wanavyotueleza akina Ndejembi kwa nini chama hicho kiogope kelele za hadharani?

Kwa nini chama hicho kilichoko vitani kiogope kelele za mizinga, makombora na risasi zinazofyatuliwa na askari wake hodari na imara kwenda kwa maadui? Kwa nini askari hao hodari na imara vitani waanze kuonekana wanajitafutia umaarufu binafsi, badala ya kupongezwa kama askari wanaopambana kuliletea sifa jeshi lote.

Tafakari ya kina inatuelekeza kuamini kuwa anayeogopa kelele za hadharani dhidi ya ufisadi si chama, bali ni wana-CCM wachache wanaoguswa au kunufaika na ufisadi huo.


Tuseme tu kwamba mzee Ndejembi na wenzake katika hili la ufisadi wanawakilisha hofu ya wanaoguswa na ufisadi kwamba kelele hizo zinawabomoa wao kisiasa na kamwe si CCM kama taasisi iliyoahidi kupambana.

Lakini pia ukichunguza sana utabaini kuna kukiri kuwa ndani ya CCM wapo mafisadi. Kwa maana nyingine, bridegi ya mapambano tayari inao maadui ndani yake.


Hili utalibaini kutokana na kauli za viongozi wa CCM, ambao mara kwa mara wamekuwa wakisikika wakisema ufisadi wa mtu mmoja mmoja usihusishwe na chama.

Tumuulize mzee Ndejembi na wenzake maswali haya ili tujiridhishe kama ni kweli ufisadi unachukiwa na kila mwana-CCM au la.

Tumuulize kilichojiri katika kikao cha wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), na wabunge wa chama hicho mjini Dodoma, Novemba, mwaka jana.

Katika mkutano huo uliibuka mjadala kuhusu ufisadi. Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zilieleza kuwa mjumbe mmoja wa NEC (jina linahifadhiwa) kutoka Zanzibar alisimama na kumshambulia mbunge mmoja aliyemstari wa mbele kupiga kelele hadharani dhidi ya ufisadi.

Mjumbe huyo alidai kuwa mbunge huyo anakibomoa chama hicho, kauli ambazo zinaimbwa na viongozi kadhaa wa CCM kwa malengo maalumu kama nilivyoeleza awali.

Lakini pia tumuulize mzee Ndejembi na wenzake kama kila mwana-CCM anachukia ufisadi ni kwa nini Mbunge mmoja kutoka Kigoma katika kikao hicho cha Dodoma, alipaza sauti akitaka wabunge wanaopiga kelele za ufisadi hadharani waadhibiwe na chama hicho?

Hakika, wana-CCM wanaochukia kelele za hadharani dhidi ya ufisadi zinakibomoa chama hicho wanajaribu kuwadanganya Watanzania, lakini hawatafanikiwa katika hilo wakati wote na kwa watu wote.

Wanaoogopa kelele hizo kwa madai kuwa zinakibomoa chama ni waongo, ukweli ni kwamba kelele hizo zinawabomoa wao kisiasa na mbele ya umma.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
 
Sijaona udhaifu wa kiasi cha kuwa tusimuamini tena kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Nadhani umewasikia mapadri na masheikh wakisema nchi inaelekea pabaya na kuyumba hali kadhalika Watanzania mbali mbali, nadhani umeona migomo mbali mbali ya Wafanyakazi na wanafunzi wetu mbali mbali, nadhani umesikia vilio vya Watanzania ndani na nje ya nchi kwamba mafisadi hawashughulikiwi na pia rasilimali zetu hazituletei faida yoyote bali zinawapa faida wageni. Vilio hivi nina hakika kabisa kwamba vimemfikia Kikwete na angweza kufanya mengi ili kupunguza vilio hivyo lakini hadi hii leo anaendeleza usanii wake tu. Huu ndiyo udhaifu tunaousema na ambao unawafanya Wazee njaa wa CCM watumie vitishi ili kuwakatisha tamaa wale wanaotaka kugombea Urais kupitia nafasi ya CCM


Unajuwa kwanini? Sioni tofauti kubwa kati ya utawala huu na tawala zilizopita.

Wewe kama huoni tofauti hiyo ni juu yako, maana enzi za Mwalimu ufisadi kama huu haukuwepo hii ni tofauti kubwa sana.

Utawala huu angalau unatowa uhuru kwa akina sie kuwakejeli na kuwaumbua viongozi wetu whether ni mafisadi kweli au shutuma tu huku dola kuwa si tishio kwa mwananchi. Yaliobakia ni yale yale kama tawala nyengine, manufaa kwa wakubwa na kutembeza bakuli. Kwa mtaji huo kama walivyomaliza wengine bado akiletwa na CCM naaendelee.

Ndiyo demokrasia hiyo na ukiangalia yanayosemwa yote ni yakweli ndiyo maana wahusika hawayapingi!!! Si unakumbuka Dr Slaa alipotoa list ya mafisadi wengi wao walidai watafungua mashtaka dhidi yake ili awalipe fidia kwa kuwaharibia reputations zao. Hakuna hata mmoja aliyefungua kesi dhidi yake, hii inaonyesha wazi kwamba hizo hazikuwa shutuma ambazo hazikuwa na ukweli
 
...mimi naamini kuwashinda CCM lazima kuanzie kwenye viti vya ubunge la sivyo kuwaondoa hawa jamaa itakuwa ndoto na wataendelea kutufisadi na kututia umaskini wa milele,siamini chama chenye wabunge wasiozidi 20 kati ya 400 kinaweza kushinda uraisi,battle zote zipo bungeni na kule ndio kelele zinaweza make sense sio za kina Mrema kule manzese wanaonekana wendawazimu tuu!

Mkuu Koba, upinzani kushinda viti vya kutosha vya uBunge si rahisi sana kwa sasa. Si rahisi kwakuwa:

1. Wameongeza idadi ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuongeza idadi yao
2. Upinzani inahitaji kuwa na presence katik asehemu kubwa ya nchi ili kuweza kutoa challenge za kutosha kupata viti vinavyoweza kuizidi CCM.

Kwa maoni yangu, upinzani unatakiwa tena kuwa na wagombea uRais kwatika uchaguzi mkuu. Ila wanatakiwa pia kuwa na umoja na hivyo kumpendekeza mgombea mmoja wa uRais ili kuweza kuwa na nafasi ya kupata ushindi. Vinginevyo, itaendelea kuwa ndoto kwao kushinda.
 
Ndio maana tukasema bora huyo JK. Uko serious kweli na unayoyasema?
Unataka maendeleo yalyokosekana miaka 50 uyapate kwa kipindi cha miaka mitano na huku unakaa kwenye Forum na kuanika pumba ukitaka Jk akuletee maendeleo? Maendeleo huletwa na watu sio mtu binafsi.

Gozigumu, sisi wote ni watu wazima na huna haja ya kutumia kauli kali kuelezea jambo. Tumia busara na hekima tutakuelewa.

Mimi sishawishiki na wala siamini kuwa JK pekee anatakiwa kuifikisha nchi hii kwenye neema kwa miaka 5 ya kipindi chake cha kwanza. Siamini pia kuwa yupo mtu mmoja anaeweza kufanya hivyo bila kubadili system nzima ya utendaji wa serikali. JK ni kiongozi wa serikali ambayo ina kila linalohitajika kuleta maendeleo. Ni kiongozi mwenye mamlaka makubwa, nguvu na uwezo wote (kiakili, kiafya n.k.) unaohitajika kufanikisha kila linalotakiwa kufanikiwa kwa kutumia rasilimali zilizopo. Kama hilo haliwezekani, basi tumekwisha.

Ila ninaamini kuwa katika jitihada zozote kuna ishara. Ishara za mafanikio na hata za kushindwa ni bayana sana. Mimi nathubutu kusema kuwa kuna ishara za kutosha kuonyesha kuwa JK na serikali yake wameshindwa. Samahani kama hupendi kusikia hivyo. Hakuna dalili zozote za neema kwa Tanzania kwa uongozi unaokwenda hivi. I AM SORRY.

Mkuu wangu Gozigumu, mimi sio mmoja wa wanaokaa hapa na kuanika pumba wakitegemea serikali iwasaidie. Ila ni mmoja wa waTanzania wanaoamini kuwa umasikini wa ndugu zetu (mamilioni) waliopo sehemu mbalimbali nchini unatokana na jitihada hafifu za kimaendeleo nchini. Ukweli ni kuwa sitegemei serikali inaweza kunisaidia kwa lolote mkuu wangu. Imeshindwa kusaidia wenye kuhitaji msaada, sidhani kuwa inaweza kunisaidi mimi.


Unaijua Ilani ya CCM? Ni kujinufaisha na hilo lilihakikishwa kabla Mkapa hajaondoka Kwa Fedha zetu. JK anatekeleza vizuri na ndio maana wanamgangania
Tangu aingie Kikwete angalau mauwaji ya Polisi yanafanyiwa kazi. Hata hivyo si kazi ya Rais kufatilia Kesi na ukichungua hivi sasa ndio wakati ambao haki mara nyingi zinafuatwa.

Siwezi kujibu hili, wala kulisemea. Kwa maana si jukumu pekee la Rais wa nchi kuhakikisha haya yanafanyika ipasavyo. Ni pure unsupported argument contradictory na haitoshi kwenye kiganja.

Na hizi harakati za wanaojipendekeza nazo umbebeshe yeye? Lini katika hotuba zake ukamsikia kama Rais wetu aliepita akisema kila wakati " Nilpoingia madarakani nchi ilikuwa hivi .............,vile.........?
Tumekuwa tukiomba kupatiwa mbadala wa Kikwete na tutaendeleza kudai hivyo, wewe la!

Sasa akishasema hivyo ndio inakuwaje?

Umemuomba nani akupatie mbadala wa JK? Acha porojo.
 
Gembe,
Mkuu kwani Uongo?
Nani CCM anaweza kuwa bora kuliko Kikwete naomba sababu au vigezo vya mtu huyo ktk Uongozi bora..
Six
Ameonyesha mabadiliko makubwa katika utendaji wa BUNGE.
Ameonyesha uwazi na kuweka maslahi ya taifa before him.
Mambo yaliyofanyika BUNGENI chini ya uongozi wake ,yameandika historia mpya ya taifa hili.
 
Six
Ameonyesha mabadiliko makubwa katika utendaji wa BUNGE.
Ameonyesha uwazi na kuweka maslahi ya taifa before him.
Mambo yaliyofanyika BUNGENI chini ya uongozi wake ,yameandika historia mpya ya taifa hili.

Mkuu umesahau Six alichemka alitumia ubabe na busara ndogo kumtupa nje Zitto Kabwe bungeni?
 
Mkuu umesahau Six alichemka alitumia ubabe na busara ndogo kumtupa nje Zitto Kabwe bungeni?

Pia amezuia mijadala wa Vitambulisho vya shilingi bilioni 200 na ununuzi wa Kiwira ambao una kila dalili ya ufisadi kwa sababu ambazo haziingii akilini. Pia alisimamisha mjadala kufanyika kwa sababu alikuwa amalikwa dinner Marekani. Mimi sikubaliani kwamba ameleta mabadiliko yoyote bungeni.
 
Pia amezuia mijadala wa Vitambulisho vya shilingi bilioni 200 na ununuzi wa Kiwira ambao una kila dalili ya ufisadi kwa sababu ambazo haziingii akilini. Pia alisimamisha mjadala kufanyika kwa sababu alikuwa amalikwa dinner Marekani. Mimi sikubaliani kwamba ameleta mabadiliko yoyote bungeni.

- Mkuu wangu tema mate pembeni, kama sio Six ungeona maaajbu kuliko haya ya sasa, tizama mazingara mkuu, muulize Lowassa, nani aliyemtoa kule juu.

FMES
 
- Mkuu wangu tema mate pembeni, kama sio Six ungeona maaajbu kuliko haya ya sasa, tizama mazingara mkuu, muulize Lowassa, nani aliyemtoa kule juu.

FMES

Sitemei mate popote, maana sioni matinki yoyote ya yeye kuzuia mjadala wa kumuhusu Masha kuhusiana na mradi wa Vitambulisho ambao una maslahi makubwa sana kwa Taifa. Wanataka kutumia shilingi billioni 200 kutengeneza vitambulisho wakati Dar inafurika baada ya mvua ya saa moja tu na shughuli zote katika jiji kusimama, kwa nchi ambayo priorities hazijakaa kichwa chini miguu juu basi kuna umuhimu mkubwa wa kutumia shilingi 200 billioni kuboresha drainage system ya Dar badala ya kutengeneza vitambulisho. Pia alizuia mjadala kuhusu Kiwira hizi kwangu mimi zilikuwa ni juhudi za Sitta kuweka mbele maslahi ya Masha, Mkapa na CCM badala ya yale ya Taifa, hivyo huyu naye ni Kikwazo kikubwa cha kuwa na bunge huru ambalo linafanya kazi ili kulinda maslahi ya Taifa.
 
Pia amezuia mijadala wa Vitambulisho vya shilingi bilioni 200 na ununuzi wa Kiwira ambao una kila dalili ya ufisadi kwa sababu ambazo haziingii akilini. Pia alisimamisha mjadala kufanyika kwa sababu alikuwa amalikwa dinner Marekani. Mimi sikubaliani kwamba ameleta mabadiliko yoyote bungeni.

Mkuu kweli ilitakiwa moto uwake pale pale bungeni wajadili hili swala si unaona limeisha kimya kimya na watu watakula vyao.
 
Kikwete asipoangalia atajutaaaaa kuwafahamu Lowassa na Rostam..it seems they are demons now possessing and controlling him..
 
Umefika wakati kwa jamii yetu kuacha kauli na siasa za kulindana. Wengi wa viongozi wetu na hata jamii wamezoea kutoa kauli za zinazodhihirisha kutumikia matumbo yao, hakuna kingine wanachofikiria!
Unaposema asiwepo wakumpinga Kikwete unamaanisha nini? Nini maana ya kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano? Kwanini kupoteza mamilioni ya kodi za walalahoi kumchagua mtu ambaye hatakiwi kupingwa???! Acheni ujinga jamani, tubadilike..., tujifunze kutoka kwa wenzetu (nchi nyingine) turuhusu mabadiliko.
Mwenye uwezo wa kuongoza ndio aende Ikulu, na hii itafikiwa kwa kuwahamasisha na kuwatia moyo watu wenye sifa kugombea ili kupata the most competent leader kwa maendeleo yetu. kama kikwete bado wamo itambidi kusimama jukwaani ashindane fairly(kwa usawa).., na hii ni lazima ianze kwenye ngazi ya chama...,
Mungu ibariki Tanzania....,
Siku moja.... tutafika!
The fighter
 
Mwakyembe amkomalia Chiligati

Mkuchika kuvaana na Makamba

Na Saed Kubenea

MwanaHALISI~Maslahi ya Taifa Mbele

VITA vya makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake, sasa siyo siri tena. Sasa vinaelekezwa moja kwa moja kwa Rais Jakaya Kikwete, MwanaHALISI limeelezwa.

Taarifa kutoka serikalini na CCM zinasema sasa hakuna uwezekano tena wa makundi yanayopingana kukaa meza moja bila kuparurana.

Katika hali ambayo haikutarajiwa, mwishoni mwa wiki iliyopita, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati “alimwaga ugali hadharani.”

Chiligati, akizungumza katika mkutano wa Kamati ya Kanuni za Bunge, uliofanyika ofisi za Bunge mjini Dar es Salaam na kushirikisha wenyeviti na makamu wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge, alisema hafurahishwi na “malumbano yanayofanyika baina ya viongozi waandamizi wa CCM na wabunge.”

Akizungumza kwa ukali, Chiligati alisema hatua hiyo ya wabunge wa chama chake kutoleana macho inaleta sifa mbaya kwa Bunge na kwa jamii.

Alitishia kutumia vikao vya kamati za wabunge (party caucus) kudhibiti wale “wanaojifanya kimbelembele.”

“Tutalazimika kutumia vikao vya chama bungeni kuulizana kuhusu haya,” alisema Chiligati na kuamsha mguno miongoni mwa wabunge waliokuwepo.

Kauli ya Chiligati ilijibiwa papohapo na mbunge wa Kyela na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Dk. Harrison Mwakyembe, kwamba Chiligati ameibuka kutokana na kile alichoita, “Gwiji limeguswa.”

Dk. Mwakyembe alisema, “Viongozi wetu wanashtuka pale gwiji moja ndani ya CCM linapoguswa. Lakini viongozi haohao wanakuwa kimya wakati gwiji hilo linaendesha mtandao wa magazeti yanayomsulubu Spika (Samwel Sitta) kila siku.”

Alisema viongozi wanakaa kimya pia wakati gwiji hilo linamwandama Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge kuhusu mkataba wa Richmond, wajumbe wa Kamati na baadhi ya wabunge wengine waliosimama kidete kupambana na ufisadi.”

Wajumbe wa kikao, huku wakitazamana, walinong’onezana na minong’ono kusikika kuwa gwiji lililokuwa likitajwa lilikuwa Rostam Aziz mwenye msululu wa magazeti na ambaye ameyatumia hivi karibuni kupambana na akina Mwakyembe.

Mwakyembe alisema anasubiri kwa hamu vikao hivyo ndani ya chama. “Tutakutana huko. Tuko tayari kujibu mapigo na kusema kila tulichonacho,” alinukuliwa akisema.

Hata hivyo, Dk. Mwakyembe hakutaja gwiji hilo kwa jina.


Mkutano wa Kamati ya Kanuni ulishirikisha wenyeviti wote wa Kamati za Bunge wakiwamo wale wanaotoka upinzani, jambo ambalo limedhihirisha kuwa Chiligati alikosa uvumilivu kwa kuyasema hayo mbele ya wapinzani wa chama chake.

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo, ni Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Hamad Rashid Mohammed (Wawi-CUF), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Bunge, Philip Marmo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Mary Nagu, Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Emmanuel Nchimbi na Profesa Mark Mwandosya.

Mkutano huo ulifanyika chini ya uenyekiti wa Naibu Spika, Anna Makinda.

Katika siku za hivi karibuni, Dk. Mwakyembe amenukuliwa akimtuhumu mfanyabiashara na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz kwa kusema ameanzisha magazeti kushambulia viongozi wenzake katika chama na serikali.

Msuguano kati ya Rostam na Dk. Mwakyembe na wenzake unadaiwa kuchochewa na hatua ya Kamati ya Nishati na Madini kushinikiza serikali kutonunua mitambo ya Dowans inayotajwa kumilikiwa na Rostam na kampuni zao kugombea eneo la kuwekeza mradi wa umeme wa upepo mkoani Singida.

Huku makundi hayo yakiendelea kutafunana, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amemfuta kazi Katibu Msaidizi Wilaya ya Hanang, Daniel ole Porokwa, siku 40 baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo.

Porokwa, ambaye kabla ya uteuzi huo aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UV-CCM) Wilaya ya Hanang, alijulishwa kuteuliwa kuwa katibu msaidizi wa CCM wilaya kwa barua rasmi ya 30 Januari 2009 yenye Kumb. Na. CMM/PF. 36236/2, aliyoandika Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, George Mkuchika.

Kwa uteuzi huo, Porokwa alikuwa moja kwa moja ndiye mhasibu wa CCM wilaya, kwa mujibu wa barua hiyo iliyotumwa pia kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha.

Taarifa zinasema katibu wa CCM mkoani Manyara, Katherine Ndahani, alipokea ujumbe wa simu ya mkononi (sms) kutoka kwa Makamba ukielekeza kufutwa kazi kwa Parokwa.

Ndahami alithibitisha Parokwa kuajiliwa, lakini aligoma kuzungumzia kuondolewa kwake kazini, akidai kuwa msemaji katika hilo ni Makamba. “Muulize katibu mkuu wetu (Makamba) yeye ndiyo msemaji wa chama,” alisema.

Lakini katika hatua iliyoshangaza wengi, Mkuchika alifuta uteuzi wa Porokwa bila kueleza sababu yoyote. Taarifa za ndani ya CCM mkoani Arusha na Ofisi ndogo Dar es Salaam, zimesema hilo siyo tukio la kawaida.


Uteuzi wa Porokwa ulifutwa kwa barua ya 11 Machi 2009, yenye Kumb. Na. CMM/PF. 36236/3 iliyosainiwa na A.S. Eriyo kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Bara, ambayo imenakiliwa kwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar na Katibu wa NEC, Idara ya Uchumi na Fedha, Makao Makuu, Dodoma.

“Nimeelekezwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi nikujulishe kwamba uteuzi huo sasa umefutwa mpaka hapo utakapojulishwa vinginevyo,” imesema barua hiyo.

Taarifa zilizofikia MwanaHALISI kuhusu hatua ya kufutwa ghafla kwa uteuzi wa Porokwa, zinasema maelekezo yalitokana na ushawishi wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, ambaye amedaiwa kuwasiliana na Mkuchika na kumwambia kama angemshirikisha, basi (Mkuchika) asingemteua Porokwa.

“Baada ya Mkuchika kugoma kushawishika, inaonekana juhudi zilifanywa kumtumia Katibu Mkuu (Makamba) ambako yalitoka maelekezo ya kufutwa kwa uteuzi wa Porokwa,” kimesema chanzo cha habari.

Hatua ya kumruka Mkuchika, taarifa zimeeleza, imezaa kutoelewana kati yake na Makamba na kwamba huenda ikasababisha mazingira magumu ya kazi kwa viongozi hao wawili.

Porokwa na Lowassa walipata kuwa katika mvutano. Kada huyo kijana alitaka kugombea ubunge wa Monduli lakini akishinikizwa na Lowassa kumuachia kwa maelezo kwamba wangempatia nafasi nyingine. Hata hivyo, ahadi hiyo haikutekelezwa.


Kutokana na hali hiyo, taarifa zinasema Porokwa amejiandaa kukabiliana na Lowassa katika uchaguzi ujao jimboni Monduli.
 
Bubu ataka Kusema,
Mkuu una kila haki ya kusema Kikwete hakuleta maendeleo yoyote.. Wala hauko peke yako.. Ni imani ambayo hata huko Marekani unakozungumzia wapo watu kibao walichukia Bush aliporudia kipindi cha Pili, Clinton aliporudia kipindi cha Pili inategemea na mtazamo wa kila mtu ktk ujenzi wa Taifa..
Sasa ajabu unatuletea mfano wa Obama, kama vile baadhi ya wanachama wa Domokratik walimpendekeza Kelly arudie kusimama na McCain..Licha ya yote hayo Obama kama situation ingekuwa sawa na yetu nina hakika watu wangependekeza majina ikiwa ni pamoja na Obama kusimama against Kelly..hawa watu wote kina Obama, Clinton, Joe wangesimama na kupinga mfumo huo wakisema wao watapenda kugombea Urais na sifa zao watazitaja..
Hii inakwenda vyama vyote, Chadema wanaweza kumsimamisha tena Mbowe, CUF wakamsimamisha Lipumba, TLP na Mrema bila upinzani inategemea na vyama hivyo vimejipanga vipi..Siwezi kutumia sababu za Mbowe kushindwa uchaguzi ama kukiendeleza chama wakati sina mfano mzuri kama vile Dr. Slaa, Zitto na wengineo..
Unapinga kitu ukiwa na mtu mwenye uwezo zaidi ktk matakwa yako, hupingi kwa sababu unapinga wakati gari halina dereva zaidi yake ukisema tu kila mtu anaweza kuendesha.. Cheo ni dhamana ya chama na wananchi.. sasa chama kimechagua nani dereva wao wewe hutaki, tupe jina la dereva mwingine.. hutaki unatumia mfano wa Obama ambaye tunajua kwanza ilikuwa lazima demokratik wawe na ushindani ndani ya chama kumpata mgombea tofauti naa wakati Bush auClinton walipopendekezwa kugombea awamu ya pili...
Mkuu wangu mjadala huu ni mfano mzuri sana wa fikra zetu sisi wenyewe, dhahiri inaonyesha wazi jinsi tulivyojipanga nyuma ya CCM hata kama tunapinga uongozi wa chama hicho na madudu yake yote..

Moja ya miiko ya chama hicho ni KUTUPANA.. nikiwa na maana KULINDANA ni moja ya maadili ya chama nje ya maandishi..na Kikwete anafanya kama chama kinavyotaka KUKILINDAchama na KULINDA viongozi wake waliobarikiwa kama tulivyomuomba Mungu ktk wimbo wa Taifa..
Sasa mimi nitapenda sana kujua mtu huyo ambaye yuko tayari kukiuka haya maadili ya chama ya kulindana ambaye yuko tayari kuwafikisha Mafisadi wote mahakamani kama atapewa nafasi ya Urais mwaka 2010..navyofahamu mimi viongozi wote wa CCM wamekubaliana swala la kumfikisha Mkapa, Lowassa, au Rostam mahakamani ni kuliweka taifa ktk hatari ya kudhoofisha usalama wa taifa... sasa wewe nambie nani ambaye anaamini tofauti na wazo hilo kwani kinacvhogomba hapa ni sisi wote kuamini kwamba JK ameshindwa kuwafikisha mahakamani Mafisadi kwa sababu anakilinda chama badala ya maslahi ya Taifa..

Mkuu there is a thin line between LOVE and HATE, unapoona wewe na kuchukia kwamba JK ameshindwa, hafai na kadhalika, wanachama wanaona JK ameweza kukilinda na kuinusuru nchi toka machafuko ya kisiasa..tena kuna baadhi wanamwona amekuwa soft kuwafikisha mahakamani baadhi ya viongozi au kuachia magazeti kuwazungumzia viongozi waliobarikiwa..Kwa mtazamo wao watu kama wewe are Hater!...na Kikwete hakutakiwa kuwasikiliza, wakati wewe unafikiria kufanya hivyo na zaidi ni kutokana na mapenzi ya nchi yako..

Kwa nini nguvu zako usiziweke kwa Wapinzani!.. hata kamaKikwete atasimama against watu kama Mwakyembe au Lau Masha..nadhani muhimu pia utazame uwezekano wa watu hawa kutuongoza vizuri kwa sababu sio swala la katiba ya chama kutazama maslahi ya Taifa isipokuwa chaguo lako ndilo litatazama maslahi ya taifa. Huyo Mwakyembe , Masha na wengine wote wamesimama upande wa Mafisadi,sasa wanapoweka ushindani ndani ya chama itakusaidia nini wewe zaidi ya kuona utaratibu unaopendekeza wewe umefanyika..Utaratibu ambao won't change maisha ya mwananchi..
 
Mzee Ndejembi, kila zama na mji wake

Na Mbasha Asenga

MwanaHALISI

TUNAJUA kwamba ya kale ni dhahabu, na kwa maana hiyo hiyo uzee ni dawa. Yote haya yakipimwa na kulinganishwa na mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa na wenyeviti wastaafu wa CCM wa mikoa minne, akili inaanza kucheza, kwa wingi wa maswali yasiyojibiwa.

Pancras Ndejembi (Dodoma); Hemed Mkali (Dar es Salaam); Jumanne Mangara (Pwani) na Tasil Mgoda (Iringa) walijitosa kueleza msimamo wao na pengine ushawishi kwa wanachama wenzao juu ya kutaka Rais Jakaya Kikwete, agombee kipindi cha pili cha urais.

Sina ugomvi na msimamo wao. Ni haki yao kumfikiria yeyote kuwa mgombea urais kwani mwisho wa yote kura ndizo huamua. Wana haki kumuunga mkono Kikwete.

Ni utamaduni wa CCM – si sheria – kupenda kila rais anayetokana nao apewe fursa ya kuwania vipindi viwili. Hawavunji sheria yoyote katika mapenzi yao hayo.

Pamoja na kutambua haki hiyo, wazee hawa wamekwaza wananchi pale waliposema – kama alivyonukuliwa msemaji wao, Mzee Ndejembi, akisema:

"Kila mwanachama wa CCM anakula kiapo cha kupambana na rushwa. Sote tunaichukia rushwa kwa kiwango sawa na kazi ya kupambana na rushwa si ya kikundi cha watu fulani ndani ya chama ila kila mwanachama."

Wazee hao walisema jingine linaloelekea kutia doa kubwa juhudi za taifa za kupambana na ufisadi: "Vilevile katika kipindi hiki tunachoelekea uchaguzi mkuu, tusitumie neno mafisadi kutisha au kuzuia wanaotaka kugombea nafasi tunazozishikilia."


Kauli hizi mbili zikiwekwa kwanye mizani moja ni dhahiri zitawaonesha wazee hawa hawana nia ya kupambana na rushwa.

Waliyonayo ni nia iliyojificha nyuma ya pazia kuhusu kupinga ufisadi nchini. Kwanza wanataka wananchi waamini kila mwana-CCM ni askari wa kupambana na rushwa; lakini wakati huohuo wanataka walarushwa wavumiliwe, wasitajwe, wasisakamwe!

Msimamo huu naona ni wa hatari sana. Hebu tujikumbushe hadi sasa nani anatuhumiwa kwa rushwa na ufisadi nchini.


Tuanze na kesi za wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Wanaotuhumiwa ni watu wenye mafungamano – iwe ya moja kwa moja au vinginevyo – na CCM. Kati ya walioko mahakamani, ni Rajabu Maranda, Mweka Hazina wa CCM Mkoa wa Kigoma.

Lakini katika EPA hiyo ipo kampuni ya Kagoda Agriculture Limited iliyochota Sh. 40 bilioni. Ni kampuni imekuwa mfano wa jinni; wamiliki wake wanaogopwa kama ukoma. Hawatajwi hadharani na inaaminika mwenyewe ni kada wa CCM na swahiba wa viongozi wa juu.

Nani inamhusu kashfa ya Richmond? Wazee hawa wanajua kwa yakini Edward Lowassa, alifukuzwa uwaziri mkuu kutokana nayo. Wanajua mawaziri wawili waliotumikia Wizara ya Nishati na Madini, Nazir Karamagi (Mbunge wa Bukoba Vijijini CCM) na Dk. Ibrahim Msabaha (Kibaha Vijijini CCM) nao walijiuzulu.

Twende kashfa ya mlungula katika ununuzi wa rada. Amehusishwa Andrew Chenge, Mbunge wa Bariadi Magharibi CCM aliyepata kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa miaka 10 mfululizo.

Kuna kashfa ya mkataba wa ukaguzi wa thamani ya madini yanayochimbwa nchini uliofanywa na kampuni ya Alex Stewart. Wanaokabili mashitaka mahakamani ya matumizi mabaya ya madaraka ni Basil Mramba, Mbunge wa Rombo CCM aliyekuwa waziri mzoefu na Daniel Yona, aliyewahi kuwa mbunge wa Same na Waziri wa Fedha. Wote ni makada wa CCM.


Silumbani na wazee Ndejembi, Mangara, Mkali na Mgoda, isipokuwa waseme kweli kama vigogo wote ambao ni sehemu ya ufisadi mkubwa unaofanywa chini ya kivuli cha CCM kama na wao ni wanachama wa CCM waliokula kiapo cha kupinga rushwa? Je, wanapiga vita rushwa au wanaipalilia?

Naomba nizidi kuwaomba radhi wazee wangu hawa na kuwataka wawe wakweli ndani ya nafasi zao, hivi chanzo cha rushwa nchini ni nini hasa? Je, si viongozi walioko madarakani wanaotumia madaraka yao vibaya kupindisha sheria, kanuni na taratibu?

Hivi Benjamin Mkapa alikuwa nani hasa kwa kipindi cha miaka 10 – Desemba 1995 hadi Desemba 2005? Kumbukumbu zinaonyesha alikuwa Rais wa Tanzania awamu ya tatu. Mwaka 1997 alivikwa uenyekiti wa CCM.

Je, huyu si anatuhumiwa kwa mengi yakihusu matumizi mabaya ya ofisi? Si amekuwa bubu Dar es Salaam ila hujibu vijiji kusiko waandishi watambuzi wa tuhuma zake?


Ni kashfa ipi utataja nchini petu isiguse CCM kama chama au wanachama wake mmoja mmoja? Ipi? Nani kafikisha nchi kwenye umasikini wa kujitakia kwa sababu ya kuzembea matumizi ya raslimali za taifa? Nani? Si ni CCM na viongozi wake kuanzia kwenye uwindaji wa kitalii, uchimbaji madini, ubinafsishaji mashirika ya umma na uzibuaji bomba la maji machafu?

Kuna kila dalili akina mzee Ndejembi walitaka tu kutumia jina la Rais Kikwete ili kuwasilisha kampeni yao ya kutetea mafisadi. Najua kauli hii si nzuri kwao, ila bora kusema ili umma utambue na kuepuka kutumbukia kwenye mtego mbaya wa kubariki mafisadi.

Kupambana na mafisadi kuna njia nyingi; moja ni kukamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani kama wazee wetu wanavyotaka, lakini njia nyingine ni ya kuwazomea wasikie aibu. Kwa lugha ya watu tunasema "name and shame." Hizi ni mbinu katika vita, hakuna moja inayotibu maradhi yote.

Kwa mfano, katika jamii kama yetu, ambayo wezi walikuwa wanapongezwa na kuonekana majasiri kwa kuiba mali ya umma, ili kuleta mabadiliko, ni lazima mbinu ya "kutaja jina ili kuaibisha" itumike sawasawa maana ndiyo njia pekee ya kubadili mwelekeo wa mambo, kuvunja utamaduni mbaya wa kusifu matajiri wezi wa mali ya umma na kukejeli watumishi wa umma masikini lakini waadilifu.

Na rushwa na kila aina ya uovu ulioumiza nchi vimetokea wakati akina mzee Ndejembi, Mangara, Mkali na Mgoda wakiwapo. Historia ingewatambua iwapo wangehoji, lakini pia sasa inawatambua kuwa hawakuhoji. Aibu kwao ni huku kujitokeza leo na kubabaisha. Tatizo wamesahau kwamba kila zama na mji wake.
 
Bubu ataka Kusema,
Mkuu una kila haki ya kusema Kikwete hakuleta maendeleo yoyote.. Wala hauko peke yako.. Ni imani ambayo hata huko Marekani unakozungumzia wapo watu kibao walichukia Bush aliporudia kipindi cha Pili, Clinton aliporudia kipindi cha Pili inategemea na mtazamo wa kila mtu ktk ujenzi wa Taifa..
Sasa ajabu unatuletea mfano wa Obama, kama vile baadhi ya wanachama wa Domokratik walimpendekeza Kelly arudie kusimama na McCain..Licha ya yote hayo Obama kama situation ingekuwa sawa na yetu nina hakika watu wangependekeza majina ikiwa ni pamoja na Obama kusimama against Kelly..hawa watu wote kina Obama, Clinton, Joe wangesimama na kupinga mfumo huo wakisema wao watapenda kugombea Urais na sifa zao watazitaja..
Hii inakwenda vyama vyote, Chadema wanaweza kumsimamisha tena Mbowe, CUF wakamsimamisha Lipumba, TLP na Mrema bila upinzani inategemea na vyama hivyo vimejipanga vipi..Siwezi kutumia sababu za Mbowe kushindwa uchaguzi ama kukiendeleza chama wakati sina mfano mzuri kama vile Dr. Slaa, Zitto na wengineo..
Unapinga kitu ukiwa na mtu mwenye uwezo zaidi ktk matakwa yako, hupingi kwa sababu unapinga wakati gari halina dereva zaidi yake ukisema tu kila mtu anaweza kuendesha.. Cheo ni dhamana ya chama na wananchi.. sasa chama kimechagua nani dereva wao wewe hutaki, tupe jina la dereva mwingine.. hutaki unatumia mfano wa Obama ambaye tunajua kwanza ilikuwa lazima demokratik wawe na ushindani ndani ya chama kumpata mgombea tofauti naa wakati Bush auClinton walipopendekezwa kugombea awamu ya pili...
Mkuu wangu mjadala huu ni mfano mzuri sana wa fikra zetu sisi wenyewe, dhahiri inaonyesha wazi jinsi tulivyojipanga nyuma ya CCM hata kama tunapinga uongozi wa chama hicho na madudu yake yote..

Moja ya miiko ya chama hicho ni KUTUPANA.. nikiwa na maana KULINDANA ni moja ya maadili ya chama nje ya maandishi..na Kikwete anafanya kama chama kinavyotaka KUKILINDAchama na KULINDA viongozi wake waliobarikiwa kama tulivyomuomba Mungu ktk wimbo wa Taifa..
Sasa mimi nitapenda sana kujua mtu huyo ambaye yuko tayari kukiuka haya maadili ya chama ya kulindana ambaye yuko tayari kuwafikisha Mafisadi wote mahakamani kama atapewa nafasi ya Urais mwaka 2010..navyofahamu mimi viongozi wote wa CCM wamekubaliana swala la kumfikisha Mkapa, Lowassa, au Rostam mahakamani ni kuliweka taifa ktk hatari ya kudhoofisha usalama wa taifa... sasa wewe nambie nani ambaye anaamini tofauti na wazo hilo kwani kinacvhogomba hapa ni sisi wote kuamini kwamba JK ameshindwa kuwafikisha mahakamani Mafisadi kwa sababu anakilinda chama badala ya maslahi ya Taifa..

Mkuu there is a thin line between LOVE and HATE, unapoona wewe na kuchukia kwamba JK ameshindwa, hafai na kadhalika, wanachama wanaona JK ameweza kukilinda na kuinusuru nchi toka machafuko ya kisiasa..tena kuna baadhi wanamwona amekuwa soft kuwafikisha mahakamani baadhi ya viongozi au kuachia magazeti kuwazungumzia viongozi waliobarikiwa..Kwa mtazamo wao watu kama wewe are Hater!...na Kikwete hakutakiwa kuwasikiliza, wakati wewe unafikiria kufanya hivyo na zaidi ni kutokana na mapenzi ya nchi yako..

Kwa nini nguvu zako usiziweke kwa Wapinzani!.. hata kamaKikwete atasimama against watu kama Mwakyembe au Lau Masha..nadhani muhimu pia utazame uwezekano wa watu hawa kutuongoza vizuri kwa sababu sio swala la katiba ya chama kutazama maslahi ya Taifa isipokuwa chaguo lako ndilo litatazama maslahi ya taifa. Huyo Mwakyembe , Masha na wengine wote wamesimama upande wa Mafisadi,sasa wanapoweka ushindani ndani ya chama itakusaidia nini wewe zaidi ya kuona utaratibu unaopendekeza wewe umefanyika..Utaratibu ambao won't change maisha ya mwananchi..

Ha ha ha sasa namchukia Kikwete eti kwa kusema kweli kwamba hakuweka mbele maslahi ya Taifa. Huu ni UNAFIKI WA HALI YA JUU. SITAPOTEZA MUDA WANGU KUJIBU MTU ASIYETAKA KUELEWA HALI HALISI YA NCHI YETU NA SASA UMEANZA KUNIZUSHIA KWAMBA NAMCHUKIA KIKWETE!!!! NIMCHUKIE KIKWETE KWA LIPI ALILONIKOSEA!!!!! KUSEMA KIONGOZI KASHINDWA KAZI NA USHAHIDI WA KUTOSHA KUTHIBITISHA HILI UPO NI KUMCHUKIA!!!! HA HA HA

Happy Good Friday
 
Back
Top Bottom