Watu wanavyoukwaa Urais:
. kwa uroho na uchu wa cheo
. kwa ajali ya mkuu wake
. kwa kusukumwa na wezi na mafisadi
. kwa kukubalika na watu wakiamini anaweza
. kwa kujititimua mtu mwenyewe akijua ataweza,
. kwa kukosa kazi nyingine ya kufanya maana zote kubwa kamaliza,
. kwa kujiona ana elimu na maarifa tosha kuongoza,
. kwa kuchaguliwa na viongozi wa dini,
. kwa kuchaguliwa na vijana,
. kwa kuchaguliwa na wazee,
. kwa kuchaguliwa na wanawakae,
. kwa kuchaguliwa na wajinga,
. kwa kuchaguliwa na shetani,
. kwa kuchaguliwa na Mungu.
Mwenye kazi ngumu sana ni huyu wa mwisho. Atataka kweli kuongoza watu kwenye njia iliyonyooka lakini siku zote atakuwa akishindana na mashetani wa kweli na mashetani watu. Hawa wengine kazi yao ni rahiiisi, kwani kazi yake inakuwa ni kulipa fadhila au kutoa ahadi tu!
Wa mwisho ni rahisi kukataa kuendelea kuwa Rais. Lakini anayechaguliwa kwa njia hizo zingine ataamini yeye tu ndiye anayefaa Urais.
Wa mwisho anajua Mungu kampa watu kuwatumia. Atawatumia kuongoza vyema nchi. Lakini aliyeupata kwa njia hizo zingine sikuzote atajifanya yeye Mungu na walio chini yake watu. Hushindwa kuongoza vizruri na akaishia kufanya madudu mwanzo mpaka mwisho.
Wa mwisho huamini anayeiongoza nchi ni Mungu naye kapewa kufanya kazi ya Mungu. Yule anayekuja kwa njia nyingine huamini yeye ndiye anayeiongoza nchi.
Wa mwisho hufahamu yeye ni binadamu wa kawaida na hana ubora wowote kwa wacha Mungu. Wa aina nyingine huamini yeye ni bora zaidi na mtakatifu na wengine ni watu wa kawaida. Hujenga pepo ya duniani huku akibomoa pepo ya akhera!
Wa mwisho hadanganyi. Na hasemi uongo. Wa njia nyingine hudhani kazi yake ni kudanganya na uongo. Hatimaye hujidanganya hata yeye mwenyewe.