...Mkapa, aliwataka wana-CCM kuzingatia mambo matano muhimu katika kumchagua mgombea anayefaa ambayo ni pamoja na kujiuliza kama mgombea anakubalika na pande zote za muungano na katika ushindani wa vyama vingi, kuzingatia kuwa wapiga kura wengi ni vijana na wanataka nini toka kwa viongozi wao, kama mgombea amechipuka na kukulia kwenye chama na wachague mtu anayefahamu vizuri chama cha CCM.
Alisema chini ya uongozi wa kiongozi huyo ni lazima mapinduzi na muungano uimarike na Tanzania hiindele kuwa nchi yenye umoja. Aidha, kiongozi huyo asiwe na chuki, hasira
Aliwakumbusha wanachama wasichague mtu kwa kumpenda bali achaguliwe kwa sifa na kutoa mfano wa bangili kwamba hata ikiwa nzuri, lakini inapobana kwenye mkono haifai.
Rais Mkapa alisema kamwe mataifa ya nje hayawezi kuwachagulia Watanzania Rais na kuwataka wananchi wazingatie maslahi ya nchi.
Tujitahidi kutafuta mgombea mwadilifu kadri iwezekanavyo, mwenye dosari chache na asiyetumia madaraka yake vibaya, alisisitiza.
Aidha, aliwataka wanachama hao kukumbuka kuwa kabla ya kupiga kura wapunguze kujifikiria wao binafsi na kundi lao katika chama.
Aliwakumbusha kuwa Rais atakayechaguliwa atakuwa ni Amiri Jeshi Mkuu hivyo anahitaji kuheshimiwa na mtu mwenye msimamo thabiti asiyeyumbishwa.
Aliongeza kuwa hatutaki rais anayeyumbishwa, anayeanza kwa kuchechemea na anayefaa kwa wakati huu tu bali na ujao.