share
JF-Expert Member
- Nov 22, 2008
- 6,063
- 10,476
Bokassa umenena, beba tano mzee. Hatutakubaliana hapa nani anafaa kuwa rais wetu ajaye. Tutajaza pages za thread tu. Kumbuka hatuna itikadi moja. Tutaishia kupondana, kukashifiana na hata kuchafua majina ya watu bure.
Ndiyo maana nilisema awali "kwa usalama wao"si vyema kuwataja majina wakati huu. Kipindi cha kampeni hakijafika, na hata kikifika muhusika anayo nafasi ya kukubali au kukataa. Akikubali ndiyo hapo jamii inaweza kumchambua nje na ndani kama anafaa.
Sasa muhusika mtakayempendekeza hajasema wala kukubali kuwa atawania hiyo nafasi, halafu sisi tuanze kumchambua hadharani hatuoni kuwa hatumtendei haki mtu? Obama, Maccain walichambuliwa kila kona kwa sababu wenyewe walikuwa wako katika kinyangányiro kwa hiari yao, hivyo wamarekani walikuwa na haki ya kuweka mambo hadharani ili wawe katika hali nzuri ya kumpata rais wao atakayefaa.
Sisi kipindi hicho hakijafika. Tukianza kubandika majina ya watu bila hata uhiari wao wakati we don't share the same vision, objectives,missions nk kama alivyosema Bokassa tutaishia kukashifiana humu ndani. "usalama" hauna maana ya kuuawa tu bali ni heshima ya majina yao waliyojijengea kwa jamii.
Ndiyo maana nilipendekeza tuijadili kwa kina serikali iliyopo madarakani. Hapo tunayo haki ya kufanya hivyo maana huyu muungwana kwa hiari yake aliomba kazi kwetu na sisi tukamuajiri. Tunayo haki ya kumchambua kama anastahiili au hastahili kupata kazi kwetu tena 2010. Muungwana anajadiliwa sambasamba na serikali yake inayoundwa na mawaziri na watendaji kadhaa wanaoteuliwa na huyu muungwana tuliyempa ajira ya kutuundia serikali hiyo.