The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Zitto, nakupongeza kwa hatua hiyo ila kuna haja ya kujitokeza hadharani lakini isiwe leo ama kesho kwani najua waandishi wa mtandao watataka kulitumia hilo kama njia ya kuwafanya watu wasahau BUZWAGI.

mapambano naamini kuwa bado yatakuwa yanaendelea kwani nchi imeshauzwa hii tena bei poa.
 
Nimefurahishwa na uamuzi huu wa Zitto si kwamba ni mpiganaji mashuhuri ambaye anatakiwa kuwa kule bungeni hasa kipindi hiki cha uamsho!

lakini pia hii imekata kilimilimi cha wazee waspinn walio kwisha zusha kwamba anataka Mpiku Mbowe ili yeye ndo agombee Urais kwa nia ya kuwachonganisha!

Bravo Zitto Kaza buti mpaka kieleweke!
 
Basi ni uamuzi mzuri sana.Hata hivyo tufikie mahali tuwe wakweli.Hivi Zitto hilo suala alivumishiwa? ok,yeye nakumbuka alisema aliongea na yule mwamndishi wa habari ila hakufanya press comference lakini mwandishi akaibeba kama alifanya nae press comference.Hata hivyo zitto atafanya jambo la maana sana kama safari hii atafanya press comference atangaze msimamo ili kuondoa comfussion na saije akashabihiana na CCM.Mzee zitto heshima yako mkuu,jaribu tu kuweka mambo clear mapena kwani kwa uzoefu wangu nadhani mabo kama haya yana madhara sana kisiasa

Kuna mambo mawili hapa, maana Zitto alinukuliwa akisema hivyo, na mojawapo ya magazeti yaliyoandika habari ni Daily News (la serikali). Lipo na jingine la Kiswahili silikumbuki.

Hoja zaweza kuwa mbili.

1. Alikuwa akidokeza kwamba jimbo si mali yake, na kwamba anaweza (hata) asigombee ubunge mwaka 2010 ali ajiendeleza kielimu na kujenga chama chake, jambo aliwahi kulisisitiza. Wao wakachukua hiyo, wakasema: "Asema hatagombea." Sensationalism!

2. Ilikuwa dhamira yake kabisa kwamba hagombei 2010 ili akasome au afanye shughuli nyingine. Kwa hiyo atakuwa amebadili msimamo, jambo ambalo ni la kawaida.

Kwa vyovyote vile, kauli yake hii haiwezi kupuuzwa, lazima iungwe mkono. Hatuwezi kukubali kumpoteza akiwa ndo anahitajika. Agombee tena walau kipindi kimoja tu, baadaye aache aende afanye kazi zake.

Kuhusu Zitto kuja hapa kuthubitisha siyo lazima, ilimradi awe na nia hiyo. Kwani atuthibitishie sisi ndio nani? Kama amesema si amesema? Naona siku hizi Chadema hawaji hapa kujibu hoja, wako kazini. Hapa kijiweni wanakuja kama hobby tu baada ya kazi, na kama kuna kazi wanajua inakopaswa kufanyika. Hivyo, simtarajii aje hapa kuwekwa kiti moto, kwani haitamsaidia kitu.
 
Kuna mambo mawili hapa, maana Zitto alinukuliwa akisema hivyo, na mojawapo ya magazeti yaliyoandika habari ni Daily News (la serikali). Lipo na jingine la Kiswahili silikumbuki.

Hoja zaweza kuwa mbili.

1. Alikuwa akidokeza kwamba jimbo si mali yake, na kwamba anaweza (hata) asigombee ubunge mwaka 2010 ali ajiendeleza kielimu na kujenga chama chake, jambo aliwahi kulisisitiza. Wao wakachukua hiyo, wakasema: "Asema hatagombea." Sensationalism!

2. Ilikuwa dhamira yake kabisa kwamba hagombei 2010 ili akasome au afanye shughuli nyingine. Kwa hiyo atakuwa amebadili msimamo, jambo ambalo ni la kawaida.

Kwa vyovyote vile, kauli yake hii haiwezi kupuuzwa,, lazima iungwe mkono. Hatuwezi kukubali kumpoteza akiwa ndo anahitajika. Agombee tena walau kipindi kimoja tu, aache aende afanye kazi zake.

Kichwamaji,

Unajifanya hujui Zitto alikuwa na maana gani alipotangaza hatagombea tena?

Hivi nyie mnatufanya Watanzania wote ******* sana?

Zitto hana haja ya kuogopa, awaambie Watanzania tu kwamba kabadili msimamo wake. Hivi nani ambaye hajawahi kubadili msimamo wake katika dunia hii?

Ingelikuwa pigo sana kwa ujenzi wa demokrasia kama Zitto angeamua kuachia ubunge mwaka 2010. Hivi sasa yeye ni role model
kwa vijana walioko mashuleni na tunahitaji role models wengi kwa faidi ya nchi yetu.
 
Hii story ina lengo la kuwafanya ccm waanze kuona kuwa kuna uasi ndani ya chama ili waache kuhoji hay6a mambo ya ufisadi ndani ya chama na kuwafanya waanze kuungana kama chama.

Hapa mtu mzima kashikwa ugoni na mkwe sasa sijui nini kitaendelea ila wajue tuu kwamba watanzania wa leo sio wale wa jana na wale wa jana wameamka pia.

Huyu chenge ana kitu gani kinamlinda, mbona anasema yeye hajali , hizi tiuhuma ni ukweli mtupu kwani kwa hawa wanasheria wawili kutokutaka kwenda mahakamani kinamaanisha kuwa wanajua kuwa huku ushahidi utaytolewa na wataumvbuka zaidi na hivyo kumlazimisha hata jk awatimue.

Taifa hili sijui liko njia gani na linakoelekea sipajui kabisa, LOWASSA naye jana mwanza wananchi wa sengetrema wamemtaka aeleze ni lini maisha bora yatapatikana kwani wamechoka na hali ya umasikini wakati wao wakiendelea kutumbua pesa za taifa hili.
 
Huyu chenge ana kitu gani kinamlinda, mbona anasema yeye hajali , hizi tiuhuma ni ukweli mtupu kwani kwa hawa wanasheria wawili kutokutaka kwenda mahakamani kinamaanisha kuwa wanajua kuwa huku ushahidi utaytolewa na wataumvbuka zaidi na hivyo kumlazimisha hata jk awatimue.

ALICHO NACHO CHENGE HIKI HAPA
THISDAY REPORTER
Dodoma

THISDAY have now verified that TANGOLD Limited was registered as an offshore company in Port Louis, Mauritius in April 2005, with at least five top government functionaries listed as directors.

They included the BoT governor, Dr Daudi Ballali, and the Permanent Secretary in the Ministry of Finance, Gray Mgonja, who both still retain the same positions todate despite a government changeover in the interim.

Others were the then attorney-general Andrew Chenge; the then permanent secretary in the Ministry of Energy and Minerals, Patrick Rutabanzibwa; and the then permanent secretary in the Ministry of Livestock Development, Vincent Mrisho.

Furthermore, despite minister Karamagi’s claims that TANGOLD Limited is wholly government -owned, the company’s constitution has provisions that give its directors - Ballali, Chenge, Mgonja, Rutabanzibwa and Mrisho - the right to transfer their shares to family members.

’Any share may be transferred by a shareholder to, or to trustees for, the spouse, father, mother, child, grandchild, son-in-law or daughter-in-law of that shareholder; and any share of a deceased shareholder may be transferred by his executors or administrators to the spouse, father, mother, child, grandchild, son-in-law or daughter-in-law of the deceased shareholder.’’

kwa mwendo huu Anahaki zote za kuona tuhuma zote ni UTUMBO!!

kwani yeye Ana mamlaka ya kurithisha mali za Taifa letu kwa vitukuu na vilembwe zake!!think about it
 
Nimelazimika kumtafuta Zitto na kusema naye . Kama kuna mtu wa forum anataka namba yake aseme hapa wazi nimpe ili tusikie maneno yake kupitia kwa watu wengine .Kaanza Lunyungu , nimesema na Zitto mimi kasema alichosema Lunyungu ni sahihi maana amefanya maongezi naye leo hii asubuhi kwa njia ya simu Lunyungu akiwa Ughaibuni.

Zitto hajawahi kukanusha habari ile maana anasema hawezi kukimbilia maelezo kwa kila jambo lisemwalo. Alikuwa hajaamua ama akasome ama aendelee na Ubunge haya aliyasema na mwandishi mmoja wakiwa safarini kwa shughuli za Afrika mashariki kule kanda ya Ziwa.

Mwandishi alikurupuka na kutaka kuuza story kwa nia gani Zitto hajui. Zitto anasisitiza kwamba atasimama kugombea na anaomba sala zetu na tumuunge mkono kwa kuwapeleka wapinzani wengi Bungeni .

Kasema kusoka PhD can happen later na hakuna haja ya kufanya hilo sasa kwa kuwa Tanzania inahitaji ukombozi na yeye kajitolea kwa hilo.
 
Halafu kuna watu hapa wanataka JK awekwe pembeni kwenye huu ujinga eti yeye ni msasfi ila anakwamishwa na wenzake tena aliowateua yeye binafsi.

Hapa JK kama unataka upate watetezi basi fanya maamuzi mazito uliyowahi kutuahoidi wakati ule ukiwapeleka mawaziri wako kule NGURUDOTO, nami nimeanzisha NGURUKURWA, karibu JK na mafisadi wako. mje kujipatia semina mim8i gharama zangu ni bei poa sana.
 
Nakandamiza Kibara,

Kwa kukuheshimu nitasema ujumbe wako una USANII mwingi badala ya kutumia neno la uwongo.

Lunyungu akiwa Ughaibuni?

Zitto hajawahi kusema hatagombea?

Sawa mimi nitasubiri Zitto aandike kwa maneno yake na kisha tumletee ushahidi.

Mimi naamini unaweza kuwa kwenye siasa na bado ukawa mkweli, nina wasiwasi kwenye thread hii ukweli ni adimu mno.
 
nnakumbuka hapa iko thread ilianzishwa kuzungumzia uamuzi wake wa kutogombea na yeye alichangia kutetea msimamo wake na watu wakampinga sana na akaja na falsafa nyingi.

ndio maana nnaamini kuna watu wanataka aje live wamuwekee maandiko yake.
hapa hapendwi mtu si CCM tu hata Kabwe akileta za uongo tutamgiladio hapa hapa
 
Mtu wa Pwani,

Hiyo thread tunaijua na tunailinda ili mtu asije akaifuta au ku edit.

Njia ya Mwongo fupi, hawa jamaa wanafikiri watu wote hapa wajinga kiasi cha kuja na statements za ajabu ajabu wakidhani wananchi hatuwaangalii.

Mimi naogopa sana watu ambao wanadanganya hata bila sababu ya msingi, huwa najiuliza kwanini? Hivi kusema nimebadili msimamo ni kubaya kuliko kudanganya?
 
Baada ya watu kunivumishia kwamba sitagombea mwaka 2010 kwa sababu ambazo wenyewe walitaka kuzisema natangaza rasmi kwamba nitasimama mwaka 2010.Huu ni uamuzi wangu mwenyewe na pia maombi makubwa toka Jimboni kwangu .Wazee wa Jimbo langu wamenifuta hapa nyumbani kwangu.Haya ni maneno ya Zitto mwenyewe ananieleza haya .Zitto anaendelea kusema kwamba anaamini mwaka 2010 kutakuwa na wabunge wengi zaidi vijana wa Upinzani so nataka kuwapo tuenmdelee kuitetea Tanzania yetu kwa ajili ya watoto wetu na vizazji vijavyo.Zitto anahitimisha kwa kusema mniombee kwa Mungu .

Mimi nasema Homgera Zitto kwa kutoa msimamo wako huo .

Napenda ifahamike kwa uwazi kabisa kuwa maneno ya kutogombea sikusingiziwa. Nilitamka mwenyewe. Ingawa mwandishi alitumia ukaribu wetu na hivyo kupata habari hiyo na akaiona ni scoop, akaandika. Hata hivyo nilisema sitagombea. Sababu za kutogombea nilizitoa.

Ni kweli kuna shinikizo kubwa kutoka katika chama, marafiki na wazee Jimboni kuwa nifute kauli ile. Wazee wa chama chini ya Mzee Mtei wamenikalisha chini na kunisihi kuondoa msimamo huo.

Kama kiongozi ni lazima nisikilize. Ingawa sikuombwa na mtu kugombea Ubunge 2005, lakini ndio hivyo tena ukishakuwa Kiongozi si wewe tena. Maamuzi ni lazima yaangalie matakwa ya jamii.

Nimeshauriwa na nimesikiliza. Hata hivyo sijatoa kauli rasmi juu ya hilo. Ni lazima nijue yale niliyopanga kufanya after 2010 nitayafanyaje nikiwa bado Mbunge. Kwa kuwa bado sijatoa kauli rasmi, msimamo wangu bado upo palepale.

Jambo la msingini kuzingatia kuwa, sikuwekewa maneno mdomoni. Nilisema sitagombea. Ni rahisi sana wanasiasa kukana maneno yao. Mimi najiepusha na hilo. Wakati mwafaka nitasema!
 
Asante sana kijana wetu Zitto.Kila kitu kiko wazi na ni mategemeo yetu kwamba utasimama kugombea maana hapa pekee JF kila mtu anataka uendelee . Afya njema kijana
 
Shukran Mheshimiwa,

Binafsi nimefarijika sana kwa wewe kuja kuweka sawa hili jambo. Na kama kasi hii hii ungeitumia ktk kuweka sawa kuhusu sakata la AC tusengekuwa ktk mess tuliyokuwa nayo.

Anyway uli choose kumsikiliza Mwanakijiji & co na ni haki yako anyway....
 
Mimi naamini unaweza kuwa kwenye siasa na bado ukawa mkweli, nina wasiwasi kwenye thread hii ukweli ni adimu mno.

Mtanzania, hili ndilo tunajaribu kufanya katika opposition, kuwa wakweli na kusimamia maneno na kauli zetu pamoja na kutembea katika maneno yetu. Itakuwa mbaya sana kama tutafanya kama ambavyo wamekuwa wakifanya, lazima tuwe tofauti na ndio njia pekee ya kupata credibility.

Kuna watu walitaka kumlisha Zitto maneno, lakini naona ameshaweka mambo sawa, tena timely. Hiyo ndiyo tunaita responsible politics, kitu ambacho ni adimu sana kukipata kwa wenzetu wa CCM!

JF members, we are a good watch dog, and Im sure the opposition takes our comments and observations seriously. we/you are playing a very important role in taking our struggles for true democracy to the next level.
 
For sure am happy na hiiumeisawazisha. Safi sana kijana kazi nzuri Hapa Tembo lazima alale chali! Ni jiwe juu ya jiwe, na nondo kwa kwenda mbele!
 
Kuna watu walitaka kumlisha Zitto maneno, lakini naona ameshaweka mambo sawa, tena timely. Hiyo ndiyo tunaita responsible politics, kitu ambacho ni adimu sana kukipata kwa wenzetu wa CCM!

Kwenye la response Kitila, you are very right na ninamshukuru Kabwe kwa kutweka swa on hili kuwa hajaamua, ingawa kwa maneno yake mwenyewe kwa ku-read betweeen the lines inaelekea kuwa atagaombea, kwenye hilo ninampa heko maana hata baadhi ya viongozi wa CCM wangependa asiache ubunge!

Bravo mkuu Zitto!
 
Hii ni spin inayofanywa na akina Salva na Kingunge ili kuupotosha umma wa Tanzania. Wanajaribu kuharibu credibility ya hawa warriors wa upinzani ili watu waone juhudi zao hazina ukweli.

CCM itashindwa tu hata wafanye nini!
 
Napenda ifahamike kwa uwazi kabisa kuwa maneno ya kutogombea sikusingiziwa. Nilitamka mwenyewe. Ingawa mwandishi alitumia ukaribu wetu na hivyo kupata habari hiyo na akaiona ni scoop, akaandika. Hata hivyo nilisema sitagombea. Sababu za kutogombea nilizitoa.
Ni kweli kuna shinikizo kubwa kutoka katika chama, marafiki na wazee Jimboni kuwa nifute kauli ile. Wazee wa chama chini ya Mzee Mtei wamenikalisha chini na kunisihi kuondoa msimamo huo. Kama kiongozi ni lazima nisikilize. Ingawa sikuombwa na mtu kugombea Ubunge 2005, lakini ndio hivyo tena ukishakuwa Kiongozi si wewe tena. Maamuzi ni lazima yaangalie matakwa ya jamii. Nimeshauriwa na nimesikiliza. Hata hivyo sijatoa kauli rasmi juu ya hilo. Ni lazima nijue yale niliyopanga kufanya after 2010 nitayafanyaje nikiwa bado Mbunge. Kwa kuwa bado sijatoa kauli rasmi, msimamo wangu bado upo palepale.

Jambo la msingini kuzingatia kuwa, sikuwekewa maneno mdomoni. Nilisema sitagombea. Ni rahisi sana wanasiasa kukana maneno yao. Mimi najiepusha na hilo. Wakati mwafaka nitasema!

Hongera Mheshimiwa Zitto kwa kuja hapa kutolea maelezo Suala lako la Kuwania tena Ubunge 2010.Mara ifikapo wakati mwafaka ,Ita Waandishi wa Habari na hakikisha kuwa News inapatikana kwenye vyombo vya HABARI VYOTE!

Wewe ni mtu wa watu na usiruhusu habari zako muhimu kuwa midomoni mwa watu wachache!,Uwe mwepesi kukubali au kukanusha habari zinazokuhusu.Kukaa kwako kimya kunatufanya tuamini habari ambazo "si za kweli" kuwa ni "kweli".Najua unajua kuwa UONGO usipokanushwa huwa UKWELI.Kwa mara nyingine tunasubiri Tamko lako kuhusu maamuzi yako hayo ya kugombea Ubunge 2010."Bado tuna imani kubwa nawe".

Wewe si Mwakilishi wa kigoma kaskazini tu!Mimi nakuona kwamba ni Mwakilishi wa Watanzania wote bila kujali mipaka ya Majimbo.
 
Napenda ifahamike kwa uwazi kabisa kuwa maneno ya kutogombea sikusingiziwa. Nilitamka mwenyewe. Ingawa mwandishi alitumia ukaribu wetu na hivyo kupata habari hiyo na akaiona ni scoop, akaandika. Hata hivyo nilisema sitagombea. Sababu za kutogombea nilizitoa.
Ni kweli kuna shinikizo kubwa kutoka katika chama, marafiki na wazee Jimboni kuwa nifute kauli ile. Wazee wa chama chini ya Mzee Mtei wamenikalisha chini na kunisihi kuondoa msimamo huo. Kama kiongozi ni lazima nisikilize. Ingawa sikuombwa na mtu kugombea Ubunge 2005, lakini ndio hivyo tena ukishakuwa Kiongozi si wewe tena. Maamuzi ni lazima yaangalie matakwa ya jamii. Nimeshauriwa na nimesikiliza. Hata hivyo sijatoa kauli rasmi juu ya hilo. Ni lazima nijue yale niliyopanga kufanya after 2010 nitayafanyaje nikiwa bado Mbunge. Kwa kuwa bado sijatoa kauli rasmi, msimamo wangu bado upo palepale.

Jambo la msingini kuzingatia kuwa, sikuwekewa maneno mdomoni. Nilisema sitagombea. Ni rahisi sana wanasiasa kukana maneno yao. Mimi najiepusha na hilo. Wakati mwafaka nitasema!

Mheshimiwa Zitto,

Asante sana kwa kuweka mambo sawa tena kwa muda mfupi.

Mimi nilishangaa kweli kuona kauli za baadhi ya watu hapa na
ilibidi kufungua makabrasha kutafuta ukweli. Nilikuwa tayari kuuweka huo ukweli wazi lakini binafsi nikaona si vizuri kumhukumu mwana JF kwa maneno ya wapambe na badala yake nikaona nisubiri kauli yako mwenyewe.

Bahati nzuri umekuja mwenyewe. Binafsi nimefurahi maana ninataka opposition yenye nguvu na kuwepo kwako bungeni kunahitajika sana.

Tunakushukuru kwa kubadili msimamo wako wa kwanza. Ushauri, habari muhimu kama hizi uhakikishe unazitoa mwenyewe na sio kuwaambia watu pembeni kwanza maana walio wengi wanapenda Ku SPIN kwa faida zao binafsi.
 
Back
Top Bottom