The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Mtanzania, hili ndilo tunajaribu kufanya katika opposition, kuwa wakweli na kusimamia maneno na kauli zetu pamoja na kutembea katika maneno yetu. Itakuwa mbaya sana kama tutafanya kama ambavyo wamekuwa wakifanya, lazima tuwe tofauti na ndio njia pekee ya kupata credibility.

Kuna watu walitaka kumlisha Zitto maneno, lakini naona ameshaweka mambo sawa, tena timely. Hiyo ndiyo tunaita responsible politics, kitu ambacho ni adimu sana kukipata kwa wenzetu wa CCM!

JF members, we are a good watch dog, and Im sure the opposition takes our comments and observations seriously. we/you are playing a very important role in taking our struggles for true democracy to the next level.

Kitila,

Nakubaliana na wewe kwamba ukweli ndio itakuwa silaha ya kuishinda CCM.

Washaurini viongozi wenu kwamba wahakikishe habari muhimu kama
hii ya Zitto lazima wawe na mahali maalumu pa kuitolea na sio kuruhusu wapambe waanze ku spin.

Nilikuwa nakusubiri mkuu uandike lakini nilipoona kimya nikajua hapa mkuu kashutuka kuna jambo sio sawa.

Tumeelewana na tuendelee mbele kwa faida ya nchi na kijiwe chetu JF.
 
Asante sana kwa kuweka mambo sawa tena kwa muda mfupi.

Mimi nilishangaa kweli kuona kauli za baadhi ya watu hapa na
ilibidi kufungua makabrasha kutafuta ukweli. Nilikuwa tayari kuuweka huo ukweli wazi lakini binafsi nikaona si vizuri kumhukumu mwana JF kwa maneno ya wapambe na badala yake nikaona nisubiri kauli yako mwenyewe.

Unajua hii forum ni vigumu sana kudanganya wananchi, ahsante mkuu Zitto, kwa kutuweka sawa kuwa hujabadili kauli yako ya kutogombea ubunge tena!
 
NA MIMI HAPA NNALAZIMIKA KUKUPONGEZA SANA TU, MH ZITTO.
NA NNAKUPA ZA WADI QUATATIONS HIZI TATU:

1. is the breath of life to human society. It is the food of the immortal spirit. Yet a single word of it may kill a man as suddenly as a drop of prussic acid. ~Oliver Wendell Holmes


2 Every truth passes through three stages before it is recognized. In the first, it is ridiculed, in the second it is opposed, in the third it is regarded as self-evident. ~Arthur Schopenhauer

3Truth, like gold, is to be obtained not by its growth, but by washing away from it all that is not gold. ~Leo Tolstoy

NA WASWAHILI TUMEMALIZIA KWA KUSEMA MUUNGWANA NI VITENDO
 
Leave our MP Shibuda alone, Maswa constituents tell Makamba

2007-09-29 09:06:27
By Anceth Nyahore, PST, Shinyanga
.

Voters in Maswa constituency, Shinyanga Region, have advised Chama Cha Mapinduzi secretary general Yusuph Makamba to stop picking on their legislator, John Shibuda but instead direct his attention to the problem of corruption in party ranks.

Talking to PST recently, they said claims by Makamba that Shibuda had engineered disunity and formation of factions in party ranks were baseless, saying the best he (Makamba) could do was to enhance discipline in his party and nab party functionaries who indulged in corruption and made it impossible for poor aspirants to be elected irrespective of their leadership abilities.

Deo Mwenda, a resident of Nyalikungu in the district, said voters were best placed to decide Shibuda`s fate in his constituency.

Another resident, Silvester Kasulumbai, said there had been a long-standing tendency for leaders to pick on Shibuda, but when investigations were carried out on the issue, it always showed that everything amounted to nothing but political mongering.

`Some party executives in the district have always held Shibuda in disdain, and they are probably the very people who misinformed Makamba,` said Kasulumbai, a CUF counsellor for Ipililo ward.

Commenting on Makamba`s claims, Shibuda said the party leadership in the region had been blaming him for dividing the party.

He proposed formation of a party committee to probe his general behaviour in and out of the party instead of baselessly blaming him.

Meanwhile Chama Cha Mapinduzi secretary general Yusuf Makamba has castigated disunity among party members in Shinyanga Region.

Makamba made the remarks here on Wednesday when referring to disputes that cropped up after party elections at district and regional levels.

He called for immediate rectification of the situation to make sure that factions created were dissolved to bring about unity of the party in the region.

Addressing district party executive committee members from Shinyanga Rural and Urban districts, Makamba said after completing party elections in the region it was obvious that there was disunity among party cadres, adding that this had to be rectified immediately for the well-being of the party.

`The kind of solidarity I had known among party members in Shinyanga is no longer there. It is absolutely necessary that party members and their leaders take up the challenge and work out a common strategy to rebuild unity,` Makamba said.

It was reported that during district and regional elections of delegates to the party national congress and membership to the National Executive Committee (NEC) some opposing camps had emerged in support of different vying candidates.

He said now that the elections had been completed the opposing camps had to be dissolved with immediate effect.

SOURCE: Guardian
 
huyu makamba nae nini, aache wananchi wachague viongozi wanaowafaa wao na sio viongozi wa kupachikwa !
 
Makamba amezidi kuwa mropokaji ... nadhani katika watu ambao ni wakurupukaji ndani ya CCM basi nadhani Makamba anaongoza. Sijui ilikuwaje JK akamuweka kwenye hiyo post ambayo inatakiwa ipate mtu makini.

Sasa matokeo yake naona ameamua kuwachukua wapayukaji wengine akina Msabah, Akwilombe na Hiza akidhani kwamba wataweza kumsaidia na kumbe wanazidi kuongeza liability kwenye chama chake!
 
Makamba ,hana uwezo wa kujua nini akizungumze wapi na wakati gani unafaa kukizungumza hicho,

Huwezi ukawa na katibu mkuu wa aina hiyo halafu ufikiri kuwa chama na serikali viinaweza kufanya kazi ya kuleta maisha bora ,ilani itatekel;ezwa vipi wakati katibu mkuu hayupo ofisini kuangalia program za kiserikali kama zinakidhi matakwa ya ilani,

Hapa kuna tatizo kubwa kuliko tunavyoweza kufikiri kwani kama kila mmoja yupo mkoani ki8la kukicha ni nani sasa wa kuangalia utekelezaji wa hayo maamuzi.

Wakina hizza na akwilombe wanawezaje kujua ilani ambayo wakati wote wa kuitengeneza hawakuwepo na pia waliipinga wawezeje leo kuwa watetezi bila hata kufundishwa kilichomo humo kwenye ilani.
 
Hawa wazee wanaplay old politics, the bad thing ni kwamba upinzani nao hawana AK 47 mpya. This is the time to shut CCM down kama upinzani wangejipanga.
 
CCM Maswa sasa yawatisha madiwani wake

na Samwel Mwanga


MADIWANI 14 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Maswa mkoani Shinyanga, wametishiwa kuvuliwa uanachama baada ya kukataa kukanusha taarifa zilizotolewa na gazeti hili, kuwa hawakushawishiwa na Mbunge wa Maswa, John Shibuda, kutohudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wilayani humu, kilichokuwa kimeitishwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuph Makamba.
Akiongea na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu, mmoja wa madiwani hao, alisema kwa niaba ya wenzake kuwa, jana waliitwa katika ofisi ya katibu wa CCM wilayani humu na kuhojiwa kwa takribani saa tisa.

Alisema kuwa kila diwani alihojiwa kwa takriban dakika 20 na kutakiwa kukanusha taarifa hizo mara moja, vinginevyo watafukuzwa uanachama na hivyo kupoteza sifa za kuwa madiwani.

Walisema kuwa kutohudhuria kwao katika kikao kilichoitishwa na Makamba si kosa lao, bali lawama zote atupiwe Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Mberito Magova, ambaye alishindwa kutoa mialiko na kutoa mialiko mingine ambayo haikuonyesha kwa usahihi ukumbi ambako mkutano huo ungefanyika.

"Tuliitwa na Katibu wa Wilaya na kila mtu alipewa fomu ya kujieleza ni kwa nini hakuhudhuria kikao cha Katibu Mkuu… anasema kuwa ameagizwa hivyo kwa njia ya simu na Makamba, akitutaka tukanushe habari hizo vinginevyo watatufukuza ndani ya chama," alisema diwani mmoja ambaye hakuopenda jina lake liandikwe gazetini.

Walisema wao walionyesha msimamo wa kutokubaliana na mawazo ya katibu huyo wa wilaya, kwani watakuwa wanaingiliwa uhuru wao binafsi wa kujieleza kwa sababu ya maslahi ya mtu mmoja.

"Sisi lazima tuseme ukweli, mbunge wetu hajatuzuia kuhudhuria kikao cha Katibu Mkuu ila wao viongozi wa CCM wilaya walifanya hivyo kwa lengo la kutaka kumpaka matope Shibuda, jambo ambalo hatuwezi kulikubali… sisi hatukuchaguliwa kuwa madiwani na wanachama wa CCM bali na wananchi wa kata zetu," alisisitiza diwani mwingine.

Madiwani hao, ambao tisa ni wa kata na watano wa viti maalumu, wanaulaumu uongozi wa CCM wilayani humo na kudai kuwa wao ndiyo wanaowagawa madiwani katika makundi kwa kigezo kuwa wamekuwa hawawaungi mkono katika mambo yao ambayo hayana maslahi na chama.

Walisema kuwa hawawezi kukanusha habari yoyote na iwapo Katibu wa CCM wilaya ana ushahidi wa madai yake, basi yeye binafsi akalalamike katika vyombo husika.

"Habari tulizozitoa ni za uhakika, hivyo basi hatuwezi kuzikanusha, ni lazima umma ujulishwe mambo yote yanayojiri, hiyo ni kazi ya vyombo vya habari na tunavishukuru sana kwa kuweka mambo haya hadharani," alsiema diwani mwingine.

Alipoulizwa kwa njia ya simu jana, Magova alikiri kuwaita madiwani hao katika kikao hicho, lakini alikataa kuthibitisha kuwa aliwatishia kuwafukuza uanachama.

Alisema anashangazwa na habari hizo kulifikia gazeti hili, kwani walielezana katika kikao hicho kuwa yaliyojadiliwa yasifikishwe kwenye vyombo vya habari.

"Ni kweli tulikuwa na kikao ambacho niliwataka watoe maelezo ni kwa nini hawakuhudhuria kikao cha Katibu Mkuu wa CCM, na pia niliwataka wakanushe habari iliyotoka katika gazeti la Tanzania Daima Septemba 29, mwaka huu, mimi niliagizwa na bwana mkubwa, hivyo sina budi kutekeleza ili nisije nikaharibikiwa," alisema Magova.
 
Makamba yeye ni mbunge wa viti maalumu na ni kuwa hajawahi kugombea ma kuchaguliwa na wananchi kwenye historia ya maisha yake, siku zote amekuwa akipewa vyeo vya kuteuliwa tuu ,hajui uchungu wa kwenda jimboni na kushinda anafikiri wananchi waliomchagua huyu bwana ni machizi eeh,
 
Naona itabidi tuanze kuzungumzia harusi ya mwanae na Manji alitoa shs ngapi kuchangia...
 
I'm just suspicious if Upinzani will be able to take as many sit as posible in the Bunge. Will it happen like 1995?

Kama upinzani wanataka kumake changes what is their strategy?
What they will offer? How about their experience in piblic services? Will they be better than Nazi's CCM? au it will be worse?

I have alot of question, but few answers. It is assymetric situation. I know we're going somewhere, but i don't trust the driver.
 
Ni Chama Cha Mapinduzi.

Looh!! kama CCM ni chama cha Manazi, basi wananchama wa CCM ni Manazi, na wananchi kwa mamilioni waliowapigia kura ni mashabiki wa manazi.

Tanzania tuna manazi wengi kweli kweli!!!

Labda kuna mtu haelewi maana ya manazi. Labda ni wale wapanda minazi kule pwani, Kigoma, na sehemu zingine.
 
Lowassa: Tusipotekeleza ahadi zetu mtunyonge 2010

Shedrack Sagati

WAZIRI Mkuu Edward Lowassa amesema iwapo serikali haitatekeleza ahadi walizoainisha ndani ya Ilani ya CCM, basi wananchi wawanyonge katika uchaguzi wa mwaka 2010.

Akihutubia mkutano wa hadhara mjini Tunduma, Lowassa alisema kwa vile serikali iliyopo madarakani imechaguliwa kwa kura nyingi, ndiyo maana hawalali usiku na mchana kuhakikisha wanatimiza ahadi zote wazozitoa wakati wakiomba kura.

Lowassa alitoa ahadi hiyo baada ya kuulizwa kero mbalimbali za maji pamoja na ahadi za ujenzi wa barabara ya Tunduma kwenda Sumbawanga.

Alisema barabara hiyo itawekewa lami ndani ya kipindi cha miaka mitano, kauli ambayo wananchi hawakuridhika nayo, lakini akawahakikishia kwa kueleza, “jamani yaani mnataka sisi tukisema tu leo na kesho ianze kuwekwa lami, haiwezekani ndugu zangu, lakini mtuamini kuwa tutaijenga barabara hii kwa kiwango cha lami.”

Waziri Mkuu alisema serikali iko makini kutekeleza ahadi zake na ikifika mwaka 2010 watakuwa wametekeleza kile walichoahidi. “Ikifika 2010 bila maji msiichague CCM; lakini nawahakikishia kuwa tutatekeleza ahadi zote,” alisema Waziri Mkuu.

Kuhusu maji ambayo ni moja ya kero kubwa zinazowasumbua wananchi wa eneo hilo, aliwahakikishia wananchi hao kutohofu kwani kuna miradi kadhaa ambayo imetengewa fedha ambayo itatekelezwa katika Wilaya ya Mbozi.

Awali Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge aliwaambia wananchi hao kuwa moja ya ahadi za serikali ni kuijenga barabara hiyo ambayo kwa muda mrefu imekuwa inalalamikiwa na wananchi.

“Hili tutalifanya kwani limo kwenye ilani yetu, alisema Chenge ambaye amefuatana na waziri mkuu na amekuwa anajibu maswali yote yanayoulizwa na wananchi juu ya kero za barabara.

Source: HabariLeo
 
mwaka 2010 watakuja na hadithi nyingine ya 2015 na wananchi wa hayo maeneo wataendelea kuteseka.

SIasa za tanzania usanii umezidi. hawa mabwana wamekaa madarakani kwa miaka 2 sasa toka wachaguliwe ambayayo ni karibu ya 50% ya muda wa miaka mitano kama inavyojulikana kikatiba. Sasa swali la kujiuliza je, hawa jamaa wameshatimiza hata walau 25% ya ahadi zao? maana tunaweza kufanya asesment na tukajua kuwa huko wanako elekea watatimiza yote waliyo ahidi. Inamaana hawa wananchi hawaoni kuwa hata 5% ya ahadi hazijatekelezwa?

Ahadi kibao kama vile sijui tutatengeneza ajira milioni ngapi, sijui tutasafiri na taxi kutoka Mtwara hadi Mwanza, Sijui tutakuwa na maisha bora kwa kila mtanzania.
Sijui tume ya kurekebisha mishahara ya umma. Je kuna lolote lilotekelezwa?


Matokeo yake ni tofauti.

1. Mfumoko wa bei kutoka 4.5% hadi 10%
2. Unemploment imeongezeka vijana wamachinga hawana kazi.
3. Matatizo ya umme ndio usiseme.
4. Serikali haijajenga hata Km moja ya bara bara mpya.
5. Budget yetu inazidi kuwa tegemezi kutoka 35% hadi 43%
6. Hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kila kukicha
7. Rasili mali za taifa ndio zinaibiwa kwa kweda mbele.
8. wananchi wanazidi kupoteza imani ha vyombo vya sheria hadi wanavamia Polisi.
9. Ukuwaji wa uchumi ndio unazidi kuporomoka
10. Pengo kati ya masikini na tajiri linazidi kuongezeka kwa kasi ya ajabu.
10 etc.

Kweli hawa jamaa wametimiza hata 5% ya hadi zao kwa miaka hii waliyokaa madarakani?
 
Barabara ya Tunduma - Sumbawanga itajengwa ndani ya kipindi cha miaka 5 from now! Hivyo itakamilika baada ya 2010, kwa hiyo imeondolewa kwenye Ilani kimtindo, itawekwa tena kwenye Ilani ya 2010.

Watakachofanya before 2010 ili kupunguza maswali ni kurundika kifusi na kuweka ma-greda kwenye site halafu wakati wa kampeni ukifika wanasema vifaa viko kwenye site na kazi imeishaanza ahadi yenu inatekelezwa! Hapo naona wadanganyika wenzangu wa Tunduma wamepigwa bao la kisigino na msanii EL. Kilichonifurahisha ni kwamba wananchi wameonyesha ku-doubt hiyo ahadi na hivyo kama aliitoa kisiasa kazi kwake asubiri 2010 watakapomkumbushia JK ahadi ya Kaimu Rais.

Wakati huo huo Chenge anasema iko ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya 2005, mpaka leo haijaanza kujengwa, wakati barabara za Singida - Nzega bado zinawaumiza vichwa mpaka leo hii. Kwenye hiyo contradiction ya statement ndipo utaona jinsi wadanganyika tunavyoridhika kirahisi na majibu mepesi ya watawala wetu. Kweli hawa watawala ni reflection yetu, maana maswali yetu ni mepesi sana na majibu nayo ni mepesi vile vile, wakija tena tunatia kura kwa chama tawala ili waendelee kutupatia majibu mepesi.
 
Kutokana na ongezeko kubwa la bei ya mfuta duniani, mfumo wa biashara duni ambao unazipendelea nchi tajiri, mvua haba ambazo zilisababisha ukame katika baadi ya mikoa yetu hivyo kusababisha upungufu mkubwa wa mavuno ya mazao ya biashara na chakula YADA YADA YADA YADA YADA tumeshindwa kutimiza ahadi zetu tulizozitoa katika kampeni ya 2010.

Maskini Wadanganyika! Watawachagua tena kwa matumaini ya mambo kuwa mazuri ifikapo 2015. Swali kwa mheshimiwa mmeshakaa madarakani zaidi ya miaka miwili na nusu sasa, je katika muda huo ni kipi mlichofanikisha katika ahadi zenu mlizozitoa?

Jibu, HAKUNA WALICHOFANIKISHA!
 
Back
Top Bottom