Nadhani sio haki kuwaachia wapinzani peke yao kueleza mabaya ya MAFISADI hawa waliotuzunguka. Ni wajibu wetu sisi waTZ kusimama kidete kuikomboa nchi yetu. Saa ya ukumbozi inakaribia kwa TZ na ni sisi watanzania ndio tutakaoifanya saa hiyo itufikie kwa haraka.. jamani ni lazima tujuwe kwamba kila mTZ anahaki ya kuyafikisha haya kwa jamii zetu kwa kiasi cha uwezo wetu.
Tusiishie tu kusoma na kupiga makelele humu lazima tutoke na tuieleweshe jamii. Hubu tufikirie gharama za UFISSDI huu kwa watoto wetu na vizazi vijavyo.....ni jukumu letu watanzania kuwatokomeza mafisadi kwa gharama zote kwani tukikaa kimnya hatuwatendei haki wale ndugu zetu walioko vijijini[/QUOTE
]
...hapa sioni cha kupinga, zaidi ya kukuongezea nguvu!!!
Tusiishie kwenye Forum ya JF tu, kwani huku Kijijini kwetu hizi mada hazitufikii wala hatujui haya yanayoendelea kwa undani.
Kwani mpaka leo tunaletewa zile Cinema za vitambaani na kuonyeshwa mauaji ya Kimbari ya Rwanda mwaka 1994, na zile t-shirt za A to Z zenye maandishi chagua SiSi-eM, ambapo ukiifua mara moja shingo yake inavutika na kufikia kifuani, mpaka siku moja nikamuuliza mama kayaii kwanini alivaa t-shirt yangu wakati ananyonyesha?...amesababisha ivutike shingo: kumbe nilimsingizia kwani hata ya mdogo wangu nayo ilikuwa vivyo hivyo.
Nisitoke kwenye Mada sana; NJOOONI KIJIJINI kwetu mtuelimishe..tusiwahi sana kuitaka nafasi ya Ikulu,kwani tukiwahi sana huko..tutashindwa kung'oa visiki vya Ufisadi, tutakuwa tumekata Matawi kwa Juu baadae mvua zikinyesha yanachipua tena!
Nahisi ni busara tuanze kujipanga chini, TUFANYE MWAKA 2010 NI WAKUPELEKA WABUNGE WENGI BUNGENI...ikiwezekana 50% ama ZAIDI itoke kwetu, asilimia hiyo naamini kabisa itatuwezesha kung'oa Visiki...maana haya majitu yalishaanzisha hadi Bendi na kutuimbia nyimbo za Mafumbo wa Tz...et! Mimi Kisiki cha Mpingo, unakuja na panga, wenye shoka wamenishindwa, unajisumbua.....teh! teh! teh! huku kijijini kuna mengi sana!
Slaa, Zitto, Hamadi Rashid, nguvu zao pekee haziwezi kushinda ile alisimia kubwa ya Mafisadi yaliyojiotea Mizizi!!Huku kwetu mti ukikomaa sana huwa unaota ndevu kila mahali...sijui ninyi uzunguni kama ipo. Halafu sasa hapo 2015..tutakuwa tunaelekea Head Office....et! mtu anajiita Kingung..!!teh..teh
Tuacheni utani, msisahau kuja kijijini kwetu...
Contd.....
UBUNGE
Lakini ukiangalia kwenye ubunge, zaidi ya wagombea 20 wa Chadema walipata zaidi ya 30% ya kura. CUF wao wanao wagombea wengi zaidi waliopata zaidi ya 30%. That means, with additional efforts na mazingira ya sasa ya siasa TZ yaliyo mazuri kwa wapinzani, sehemu kubwa ya hawa wagombea, kama wakipewa resources zaidi wanaweza wakawa wabunge. Ukiongezea majimbo ya mafisadi kama akina Basil Mramba, Chenge n.k., uwezekano wa kuibuka na wabunge wengine say 10-40 kutoka kwenye hii mizoga unaongezeka.
Then kuna kundi la akina Mnyika n.k., ambao walipata between 10% to 20%. Hawa nao wako wengi sana. Chadema peke yake ina kama 17 hivi. Hawa watahitaji mtaji mkubwa zaidi kuwafanya wawe competitive. Lakini kwa vile hawatakuwa wanashindana na JK, bado nguvu ya ushindani watakuwa nayo na wanaweza wakashinda.
Contd.....
UBUNGE
Lakini ukiangalia kwenye ubunge,
Then kuna kundi la akina Mnyika n.k., ambao walipata between 10% to 20%. Hawa nao wako wengi sana. Chadema peke yake ina kama 17 hivi. Hawa watahitaji mtaji mkubwa zaidi kuwafanya wawe competitive. Lakini kwa vile hawatakuwa wanashindana na JK, bado nguvu ya ushindani watakuwa nayo na wanaweza wakashinda.
Contd.....
MUUNGANIKO WA VYAMA
Pia **** maeneo ambayo wapinzani walipigana wenyewe kwa wenyewe ngwara wakawaachia CCM ubunge. Kwa mfano jimbo la Vunjo, Chadema ilipata kura (11.9%), TLP (31.2%), NCCR (11.5%) jumla 54.6%. Halafu CCM wakapata 43.8% tu, kwa hiyo kwa rule ya simple majority wakajichukulia ubunge kiulaini.
Ndio maana nasisitiza kuwa, kama wapinzani wanataka ushindi wa maana, na hata kumtoa mtu ambaye angeshinda ubunge kafara, say Dr.Slaa, ni vema wakafanya hivyo tu baada ya kuungana na wala sio kama walivyo vipande-vipande hivi sasa, maana odds za ushindi as Chadema au CUF hazipo.
To be Contd.....
Contd.....
UMAARUFU WA MGOMBEA
Mbowe alipoacha jimbo lake na kugombea uraisi, jimbo likachukuliwa na CCM, licha ya kuwa yeye, ambaye ni mgombea uraisi wa Chadema, alikuwa maarufu sana hapo awali. Baada ya kushindwa uraisi, umaarufu wake nje ya Chadema nao ukapungua kitu ambacho kinaweza kikawa tatizo kwake kama akiamua kurudi kugombea ubunge Hai.
Hivyo ni wazi kuwa, kama ilivyokuwa kwa Mbowe, wapiga kura wengi wanapopiga kura hutofautisha kura za ubunge na uraisi. Ndio maana vyama vya upinzani vilipata kura nyingi kwenye ubunge kuliko uraisi.
WaTZ wengi wako radhi kumpa ubunge mgombea wa upinzani kama anawavutia, lakini ni wagumu kufanya hivyo kwenye uraisi. Hii ina maana kuwa hata Slaa akigombea, umaarufu wake sio kweli kuwa utasaidia kuleta kura. Hivi ni nani maarufu zaidi, Dr. Slaa wa 2010 au Mrema wa 1995?? Mrema aliingia ulingoni, sio tu baada ya kulipua mabomu na kukamata dhahabu airport, bali nchi nzima ilikuwa inamtambua maana alikuwa kiongozi wa ngazi ya juu na maarufu zaidi ya wengine wote. Lakini bado alipigwa chini kiulaini na Mkapa. Hivi sasa sidhani kama Dr.Slaa ana even 1/2 ya umaarufu alioingia nao Mrema kwenye kinyang'anyiro.
Lakini nina uhakika hii inaweza kubadilika kama major oppostion parties zikiamua kuungana. Faida ziko wazi;
Lakini wakiendelea na huu mchezo wa kila mtu na vyake, au hata kushirikiana tu bila kuvivunja vyama, kama ilivyokuwa Vunjo,
- Watakuwa na Resources nyingi zaidi kwenye ubunge, na kwenye uraisi.
- Wananchi watakuwa wanacompare qualities za watu wawili tu na sio utitiri.
- Hata kama hawatashinda uraisi, lakini bado wanaweza wakawa na majority bungeni, badala ya kupoteza wabunge, maana chaguo la wananchi litakuwa wazi either CCM au upinzani.
- Watashindwa kushindana na CCM sababu ya mgawanyiko
- Overheads zao zitakuwa kubwa na
- Sio ajabu wataishia kutapanya vipesa vichache walivyo navyo kwenye uraisi, maana kila mmoja wao atakuwa na mgombea, badala ya kuzipeleka kwenye ubunge.
Lakini nina uhakika hii inaweza kubadilika kama major oppostion parties zikiamua kuungana. Faida ziko wazi;
Watakuwa na Resources nyingi zaidi kwenye ubunge, na kwenye uraisi.
Wananchi watakuwa wanacompare qualities za watu wawili tu na sio utitiri.
Hata kama hawatashinda uraisi, lakini bado wanaweza wakawa na majority bungeni, badala ya kupoteza wabunge, maana chaguo la wananchi litakuwa wazi either CCM au upinzani.
JINA LAKO NA POST YAKO VINAFANANA SANA.Hayo ya ukabila na udini tunayaonea kwa wanaKilimanjaro ndani ya Chadema na CUF kwenye misikiti.
Tokea Mrema apate almost 30% ya kura mwaka 1995, hakujatokea mgombea mwingine aliyekaribia hata 20%. This is a fact.
.... Sasa Mbowe, Dr Slaa na wengine kama wanataka kugombea uchaguzi 2010 wataanza kuaandaa mazingira mapema kabla ya 2010 ikiwemo kujenga mtandao wa chama nchi nzima.
Asha
Nadhani wengi wetu mnalijua jina la Dr. Wilbroad Slaa Mbunge wa Karatu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA. Mimi ni Mtanzania ambaye sifungamani na chama chochote lakini mwenye kuamini kabisa ya kwamba, miongoni mwetu kuna Watanzania ambao wanaweza kuleta mabadiliko makubwa katika njanja mbalimbali kama za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Nchi yetu iko kwenye wakati mgumu sana hivi sasa na tunahijati kiongozi bora na sio bora kiongozi ambaye ataweza kuleta mabadiliko makubwa na ya kweli katika kuiendeleza nchi yetu kiuchumi.
Kama mjuavyo tatizo la ufisadi na rushwa limekithiri sana na imeshajionyesha wazi ya kwamba, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameshindwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza majukumu yake aliyopewa na watanzania kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naamini huu ni muda thabiti kabisa kumtafuta mtu atakayefaa kukichukua kiti chake itakapofika wakati wa Uchaguzi wa mwaka 2010. Binafsi ningependa Kikwete aondoke hata leo hii na arudi kijijini kwao Bagamoyo akalime Mananasi yake na huku akiendelea kujichekesha mbele ya ndugu zake. Naamini kabisa Dr. Slaa ndio mtu anaefaa kuwa Rais wa nchi yetu na mwenye uwezo mkubwa wa kulianzisha gurudumu la maendeleo nchini. Mimi niko tayari kulipia gharama zote za kutengeneza tovuti ya Dr. Slaa na kulipia hosting charges kutoka hivi sasa mpaka wakati wa uchaguzi mwaka 2010. Kwa hiyo ningeomba watanzania wenzangu tumhamasishe Dr. Slaa agombee hiki kiti cha Urais mwaka 2010. Tumebakisha miaka miwili na nadhani huu ni muda muafaka kuanza kujiandaa ili kuhakikisha Kikwete na CCM hawarudi tena kwenye uongozi.
Ahsanteni.
(Haya ni maoni yangu binafsi hayaingiliani kabisa na maamuzi ya CHADEMA) www.drwilbroadslaa2010.com
I am not sure whether this gentleman has what it takes to be the President. Nadhani kuwa rais ni zaidi ya kulipua mabomu. Mrema alilipua mambomu lakini wengi tuliona hafai kuwa rais.
Tunachoitaji Watanzania sasa sio kumpeleka strong man kama yule ikilu, tutakuwa hatujafanya la maana kama tunataka maendeleo ya kweli na kule haendi peke yake, sisi wananchi tutampeleka kule lakini atakao wateua je watajali masirahi ya wananchi?
We need those strong men in the parliament waweze kusaidia kuchange system iliyopo ambayo sasa hivi ni kifisadi, hata JK anaodoka leo hali itabakia ile ile maan system yote ni ya kifisadi na inaweza kubalidilishwa bungeni tu, watu waogope na kueshimu bunge badala ya sasa linaoneka kana kwamba ni sehemu ya kwenda kuchulia poso tu.
Jamani, jamani. Ni kweli mawazo binafsi umeleta na bila shaka ulitegemea watu kuchangia hoja yako.
Naomba Nikuulize ni kweli Unamaaanisha kwa kuaangalia Alama za Nyakati? Kwanini isiwe Mbowe au Zitto Kabwe.
Elewa kuna Kukubalika kwa Wananchi na Kukubalika Bungeni na wabunge wenzio na wasomi walio wachache wenye kuelewa maana ya siasa na nchi inapoelekea. Ukiniambia aje kuwa WAZIRI MKUU nitakubaliana na wewe ila sio Uraisi(Maoni yangu haya)
Nadhani haujatoa sababu ni kwa nini unadhani Dr. Slaa Slaa hafai kuwa President ukilinganisha na Zitto,Mbowe au mtu mwingine yeyote. Mimi kama wengi wetu hapa naamini kabisa Dr. Slaa ni mtu mwenye judgement nzuri na ambaye ni competent kuwa President wa nchi yetu. Pia ni kiongozi mahiri mpenda nchi yake na mwenye kujitoa mhanga kuhakikisha anatetea maslahi ya nchi kwa njia zote zile. Tunachokiona hivi sasa ni jinsi viongozi wa CCM wanavyoweka mbele maslahi ya matumbo yao kuliko nchi yetu. CCM inanuka na haifai kuiongoza Tanzania. Tumeshavumilia vya kutosha na kilichobaki ni jukumu letu watanzania kuwafukuzia mbali hawa watu wa Chama Cha Mafisadi na Majambazi (CCM). Tusije kujilaumu tukiendelea kuwachagua makanyaboya kutoka CCM.
Kalamu nakubaliana nawe kabisa kuhusiana na hilo na nadhani kutokana na kwamba kuna baadhi ya wanachama na viongozi kutoka vyama vya upinzani ambao wanakuja hapa, ni bora wachukue maoni yetu.Geeque,
Leo ni 25/04/2008. Bado hapaonekani dalili zozote kwamba wapinzani wana(me)jiandaa kuikabili CCM hapo 2010.
Mawazo mengi na mazuri yamekwishachambuliwa hapa JF, katika mjadala huu, na ule wa Rev. Kishoka unaozungumzia kujiandaa kwa 2010.
Mimi ninapendekeza, kama inawezekana, (kwa hisani ya Invisible na wenzake) nakala za mijadala yote hii miwili, au zaidi ipelekwe kwenye ofisi za vyama vya upinzani ili yaliyomo humu yajadiliwe na kuchambuliwa huko na wanachama wao.
Zaidi ya hivyo, tujiandae tu kuendelea na CCM yetu na uozo wote tunaoupigia kelele hapa.
Ni kwasababu kuna watu wanachagua viongozi kama vile wanavyoenda kuchagua malapa dukani!I am not sure whether this gentleman has what it takes to be the President. Nadhani kuwa rais ni zaidi ya kulipua mabomu. Mrema alilipua mambomu lakini wengi tuliona hafai kuwa rais.
THE MAN HAS CREDENTIALS BANA ACHA HIZO!WE HAVE TO LOOK BEYOND THE MABOMU AND WE THEN CAN SEE IF HE QUALIFIES NA SIO VIJEMBE!HOJA BANA!I am not sure whether this gentleman has what it takes to be the President. Nadhani kuwa rais ni zaidi ya kulipua mabomu. Mrema alilipua mambomu lakini wengi tuliona hafai kuwa rais.
Kalamu nakubaliana nawe kabisa kuhusiana na hilo na nadhani kutokana na kwamba kuna baadhi ya wanachama na viongozi kutoka vyama vya upinzani ambao wanakuja hapa, ni bora wachukue maoni yetu. Unajua mwaka 2010 sio mbali kabisa na mikakati ya ushindi inabidi ianze sasa na sio kuongojea hadi inapokaribia muda wa kampeni. Tatizo la vyama vyetu vinakuwaga havina long term plans za mambo yao mbalimbali. Wakati ni huu na wakiamua kufanya ngoja ngoja itawapa nafasi zaidi CCM.