The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Mimi nashusha mavitus tu. Hayo ya chuki na ukabila unayaleta wewe na nitawaachia wasomaji wengine wenye fikira nzuri wa-tu-judge. Wakishasoma na ku-comment then nitajibu hoja including za bibie Asha. Naipost tena hoja yangu kwa manufaa ya wasomaji.

Kama hivi ndio mnaita mavitus basi kuna haja ya kutafuta tafsiri mpya ya neno mavitus
 
Asha Abdala said:
Mimi napingana na hilo wazo la kumpendekeza Dr. Slaa kuwa mgombea uraisi. Ku-focus kwenye uraisi pekee ni moja ya sababu kubwa ya wapinzani kushindwa kwenye kila uchaguzi. Ufumbuzi wa matatizo ya mtanzania hautatokana na upinzani kuingia ikulu, bali kwa kubadilisha mfumo mzima wa kiutawala. Ni vema tukaelewa yafuatayo;

Contradiction!

Huwezi kubadili mfumo mzima wa utawala kama hutabadili institution ya urais ambayo inateua mawaziri, wakurugenzi, mabalozi, wakuu wa wilaya nk. Hivyo wapinzani lazima walenge pia kumwondoa Kikwete 2010 na CCM.


Yes We Can. Kenya just did by being the majority in the parliament. Zimbabwe is on her way of doing the same. Uraisi is not the only way to democracy.

Wapinzani have to be smart on how to achieve their objectives. They should stop inhibiting themselves by overspending on unachievable projects.
 
Yes We Can. Kenya just did by being the majority in the parliament. Zimbabwe is on her way of doing the same. Uraisi is not the only way to democracy. Wapinzani have to be smart on how to achieve their objectives. They should stop inhibiting themselves by overspending on unachievable projects.

Kama huna taarifa, Kenya na Zimbwabwe wapinzani walishinda vyote pamoja - bunge na uraisi. Tafuta mfano mwingine.
 
Asha Abdala said:
  1. Nchi haijengwi na mtu mmoja na ndio maana Nyerere yalimshinda. Kwa hiyo kama mfumo wa kiutawala hautabadilishwa na kuondoa madaraka makubwa aliyonayo raisi na serikali yake hivi sasa, na kuyahamishia bungeni, mahakamani na kwa wananchi, yeyote yule atakayeingia anaweza akaifuja nchi bila kipingamizi.


Tofauti ya kuwa na mtu mmoja mzuri inaonekana bayana ukimlinganisha Nyerere na Kikwete. Rais ana mamlaka makubwa ya utuezi na utendaji. Ukiwa na Rais msanii kama Kikwete utakuwa na Mawaziri kama Chenge, Mramba, Lowassa na wenzake lakini ukichagua Rais bora utapata safu nzuri ya uongozi

Soma tena comments zangu utanielewa. Napinga kutegemea mtu mmoja kuwa ndio mkombozi. Haya ndio yaliyomshinda Nyerere. Tunahitaji muundo wenye nguvu sawia kati ya executive, legislature na judiciary. System ikiwa nzuri uteuzi pia hutegemeana na hizo balance of powers.

Sasa hivi haziko balanced, na ndio maana kikwete anamteua Cheyo na wabunge wanakua hawana la kusema. By the way Kikwete will never be Nyerere.
 
1. Nadhani wengi wetu mnalijua jina la Dr. Wilbroad Slaa Mbunge wa Karatu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

2. miongoni mwetu kuna Watanzania ambao wanaweza kuleta mabadiliko makubwa katika njanja mbalimbali kama za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

3. Nchi yetu iko kwenye wakati mgumu sana hivi sasa na tunahijati kiongozi bora na sio bora kiongozi ambaye ataweza kuleta mabadiliko makubwa na ya kweli katika kuiendeleza nchi yetu kiuchumi.

Mazee Geeque!,

Heshima mbele bro, hii ilikuwa imenipita lakini sijachelewa, kwanza Mkulu wangu, naomba umwage CV lake, Dr. Slaa tuichambue.

Ahsante Bro!
 
Kama huna taarifa, Kenya na Zimbwabwe wapinzani walishinda vyote pamoja - bunge na uraisi. Tafuta mfano mwingine.

Labda and wish so. Lakini tunajua Kenya raisi bado ni Kibaki.

Lakini mafanikio ya Odinga na wenzake ni kuwa hivi sasa hawana uraisi lakini bado wataongoza mijadala yote bungeni no matter what? This is what should be upinzanis target.
 
Asha Abdala said:
3.Hadi hivi sasa hakuna dalili zozote zinazoonyesha uwezekano wa CCM kushindwa kwenye kinyang'anyiro cha uraisi 2010, hata baada ya kulipuliwa kwa mafisadi wote wakiwa wanaCCM. Uchaguzi wa hivi karibuni Kiteto inatoa picha ya ugumu uliopo.


Unajichanganya!

Kama unasema wapinzani hawatashinda urais 2010 kwa kuwa wameshindwa Ubunge Kiteto kwanini unawashauri tena kwamba ni vyema wakagombea Ubunge? Kwanini ushiwashauri wajenge mazingira ya kushinda vyote ama kutoshiriki uchaguzi kabisa? Au unataka kuhamamisha attention yao kwa Kikwete?

Mgawanyo wa upinzani umeouna wapi wakati sasa wana ushirikiano na wamekuwa wakisimamisha mgombea mmoja katika hizi chaguzi za hivi karibuni? Kipimo chako cha mgawanyiko huo ni kipi wakati wapinzani wanashirikaina katika mambo mbalimbali?

Asha

Nawashauri wote wenye uwezo wa kushinda kugombea ubunge na sio uraisi, Kama JKN alivyowashauri hapo awali. Mrema, Lipumba, Freeman, Dr. Slaa n.k. wote wana nafasi nzuri sana ya kushinda ubunge.

Lakini probability ya wao kushinda uraisi hivi sasa na utitiri wa vyama ni ndoto. Mgombea uraisi anaweza akawepo, kama vile Asha, MwK nk., watu abao hawana nafasi za kuwa wabunge na nguvu nyingi zisielekezwe huko kwenye uraisi.
 
Asha Abdala said:
4.Mgawanyiko na tamaa katika kambi ya upinzani ni kikwazo kikubwa sana kwao kupata ushindi. Hata kama Nyerere angefufuka na kuwa mgombea wa chama kimojawapo cha upinzani, bado ingekuwa vigumu kwao kuunganisha nguvu zao kuing'oa CCM.
5.Uongozi mbovu ndani ya vyama vya upinzani nao ni kikwazo kikubwa katika kuwavutia wasomi na wafanyabiashara wengi ambao wanakerwa na CCM. Ni muhimu kutatua masuala kama ya udini, ukabila na umungu-mtu ndani ya vyama ili kuondoa hali ya hivi vyama kuwa na ushabiki wa kimajimbo na wenye upeo mwembamba.


Acha generalization wewe?

Uongozi mbovu upi? Wa Katibu Mkuu Dr Slaa wa CHADEMA au Mwenyekiti Lipumba wa CUF?. Wasomi na wafanyabiashara hawaachi kujiunga na upinzani kwa kuwa kuna uongozi mbovu bali ni hofu tu ya kulinda maslahi yao. Mbona Msomi Prof Baregu amejiunga CHADEMA? Au mfanyabiashara Ndesamburo mbona anafanya vizuri tu katika siasa za upinzani.

Ushabiki wa kimajimbo gani huo ulioko kwenye vyama?

Mi naona wewe kazi yako ni kupandikiza hofu tu kwa wananchi ili waogope kujiunga na upinzani.

Asha
Haya ni mawazo yangu kulingana na malalamiko tunayoyaona. Mfano mzuri ni haya malalamiko yasiyoisha ya ukabila na udini ndani ya Chadema na CUF.

If you think everything is Ok, leave aside my comments as bogus. Lakini kama yana kaukweli kadogo ndaniyake, basi read my lips, uraisi 2010 kwa Chadema, CUF ni ndoto za mchana.
 
Asha Abdala said:
6.Nyerere alisema upinzani wa kiukweli TZ utatoka ndani ya CCM, na mimi nakubaliana naye kabisaa hata baada ya kufariki. Hili litawezekana kwa CCM wenyewe kupingana au kwa wapinzani kuwa na vyama ambavyo vitawavutia walioCCM kuhamia kwao. Hivi sasa la awali la CCM kupingana linakaribia linalohitajika ni kwa wapinzani kuunda mazingira yatakayoweza kuwavutia wanaCCM kuhamia kwao.

Dr Slaa alitoka CCM; kama assumpition yako juu ya kauli ya Nyerere ni sahihi kwanini bado unampinga Dr Slaa kuwa hafai? Mbona wanaCCM wanahamia tu? umewaona wakina Pesha, Balozi Ngaiza etc


Karibu kila mtu aliyeenda JKT miaka ya 90s na kurudi nyuma, ilibidi awe CCM au TANU by default.

Elewa kuwa sipingi Dr. Slaa au mwingineo yeyote kugombea uraisi, ninachosema ni kuwa ni vema kwa yule mwenye nafasi ya kushinda ubunge agombee ubunge maana kushinda uraisi probabilities zake ni ndogo.

Wapo wengi ambao hawana uwezekano wa kushinda ubunge lakini wana-qualify kugombea uraisi, na hao ndio ningependekeza wapewe hiyo nafasi lakini resources nyingi zipelekwe kwa wagombea ubunge.
 
Karibu kila mtu aliyeenda JKT miaka ya 90s na kurudi nyuma, ilibidi awe CCM au TANU by default.

Elewa kuwa sipingi Dr. Slaa au mwingineo yeyote kugombea uraisi, ninachosema ni kuwa ni vema kwa yule mwenye nafasi ya kushinda ubunge agombee ubunge maana kushinda uraisi probabilities zake ni ndogo. Wapo wengi ambao hawana uwezekano wa kushinda ubunge lakini wana-qualify kugombea uraisi, na hao ndio ningependekeza wapewe hiyo nafasi lakini resources nyingi zipelekwe kwa wagombea ubunge.

Unapendekeza mambo mengi sana mkuu, wakati at the same time ukisema kuwa wengine hawafai kugombea uraisi, au kuwa ni ndoto kwa wapinzani kushinda uraisi! unajichanganya sana, hebu soma ulichoandika kwa sauti ili uone vile unavyoweka commedy hapa ukumbini.
 
6. Msisitizo kwa upinzani uwe katika kuandaa wabunge wengi iwezekanavyo. Na hii ndio sababu kubwa ya kupinga kumuingiza Dr. Slaa kwenye kinyang'anyiro cha uraisi. Uwezekano wa yeye kushinda ubunge ni mkubwa kuliko uraisi na isingekuwa vema akakosekana kwenye ulingo wa kisiasa kwa miaka 5, kama ilivyokuwa kwa Mrema, na kushindwa kufanya yale tuliyoona anaweza kuyafanya akiwa bungeni. Kila mpinzani aliye na uwezo wa kushinda ubunge, aanze kujengwa hivi sasa kwenye majimbo yao ili agombee ubunge na kuimarisha upinzani bungeni.
7. Upinzani wapunguze hili la ku-focus zaidi kwenye uraisi, na kutumia rasilimali zao kwenye ubunge. Kwa mfano CHADEMA walitumia zaidi ya TShs 220millioni (30% ya pesa waliyokuwa nayo) kwenye kukodisha helicopter tu. Lakini jumla ya pesa yote walizowapa wagombea wa ubunge wao ilikuwa ni TShs. 59 millioni tu (8% tu). Kama wangewekeza zaidi kwenye wabunge labda watu kama Bob Makani wangekuwa wabunge hivi sasa.
[/list]Changamoto langu kwa vyama vya upinzani ni kuungana na kuwekeza zaidi kwenye ubunge maana kwa hali ilivyo hivi sasa, hakuna atakayemng'oa CCM in 2010.


We kweli kubwa jinga!

1. Kwani hiyo helikopta ilikuwa inafanya kampeni Kenya? Si ilikuwa inapita maeneo ya wagombea ubunge na udiwani ikiwa imembeba mgombea Urais na Mgombea ubunge wa eneo husika kupiga kampeni? Sasa maanake ni kwamba hizo milioni 200 za helikopta zimetumika pia na wagombea ubunge kwa kuwa walipanda helikopta kwenda kwa wapiga kura wao. Zitto na Mnyika si waliwahi kusema kuwa walitumia helikopta ilipokwenda kwenye majimbo yao?

2. Hebu tumia akili, hizo milioni 59 walizopewa wagombea ubunge ni zile walizopewa fedha taslimu. Hizo milioni 500 zingine hazikutumiwa na mgombea urais binafsi. Utaona humu kulikuwa na fedha za mafunzo ya wagombea ubunge, kutengeneza vifaa vya kampeni na kufanya kampeni za vyombo vya habari nk. Vyote hivi vingine vilikuwa vinatumiwa na wagombea ubunge wenyewe moja kwa moja na vingine vililenga kujenga taswira ya CHADEMA. Na ukijenga taswira ya CHADEMA unawasaidia pia wagombea ubunge katika maeneo yao.

Sasa nieleze, kati ya hizo milioni 700 CHADEMA ilizotumia kwenye kampeni zake, ni zipi ambazo Freeman Mbowe kama mgombea urais alitumia mwenyewe; ni zipi hazikutumika katika majimbo. Kwani mgombea urais alifanya kampeni zake katika sayari ya Mars? Kazi yake si ilikuwa kuzunguka nchi nzima kuwanadi wagombea wake? Hebu acha kuwakatisha tamaa watanzania kuunga mkono upinzani.

Ni kweli ni muhimu kuweka mkazo kwenye ubunge, lakini si kwa unavyoonyesha wewe. Wewe hukosoi kwa kujenga, unabwabwaja kwa lengo la kuchafua.

Au ndio maana ya kubwa jinga? Hivi kwani nini umechagua jina hilo?

Asha

Asha,

Usipandishe munkari. Pole sana naona damu yako ina chembe chembe za CHADEMA. KJ ni jina muhimu sana kwenye ukoo wangu kwa hiyo usilichezee. Ndio maana nikampa Avantar yangu jina hilo.

Hapa tunajadili future ya chama tunachokipenda. Lakini ukijaribu kutetea upupu hutakisaidia Chadema, bali utakisaidia CCM kushinda kwa vile Chadema watakua wanarudia makosa ya 2005. Kwenye uchaguzi wa 2005 pesa nyingi ilitumika kwenye uraisi ijapokua ilikuwa wazi kuwa wapinzani hawatashinda.

Sasa sijui tuuiteje huo uamuzi wa kupeleka pesa zisikozaa. Kama angalau 50% tu ya millioni 700 zingetumika strategically kwenye maeneo ambayo Chadema walikuwa na nafasi ya kushinda, sio ajabu wangekuwa na wabunge wengi hivi sasa. Kuna wagombea wa Chadema zaidi ya 15 ambao walipata zaidi ya 30% ya kura, jambo linaloonyesha kuwa kama wangeongezewa nguvu labda wangeshinda. Hili pia ni tatizo kwa vyama vingine.

Kwa hiyo, kama wapinzani wanataka kuibuka kidedea, lazima waachane na ubinafsi na mambo mengine madogo madogo yaliyomo kwenye vyama vyao. Ningefurahi kesho tukaamka na kusikia kuwa Chadema, TLP, NCCR, na CUF vimevunjwa na kimeundwa chama kimoja chini ya jemadari mmoja. Hapo ndio kutakuwa na uwezekano wa kuipiga bao CCM. Lakini kama kila mtu atataka kuwa mwenyekiti na ndugu zake wabunge and then wanawaambia wananchi kuwa eti nyie ndio wanademokrasia na mnashirikiana, ni wajinga tu na day dreamers ambao watawasikiliza.

Kenya walilitambua hili na sasa wamefanikiwa kushinda. Kama Asha unataka uwe shujaa, pigania hili na uache kufukia kichwa mchngani.
 
Labda and wish so. Lakini tunajua Kenya raisi bado ni Kibaki. Lakini mafanikio ya Odinga na wenzake ni kuwa hivi sasa hawana uraisi lakini bado wataongoza mijadala yote bungeni no matter what? This is what should be upinzanis target.

Mhhh,

wewe unachotaka ni Kikwete kubaki madarakani hata kama akishindwa kama vile ilivyotokea Kenya?
 
Kubwajinga:

Una hoja sana kwenye posts zako. Lakini ambacho sijakupata ni kwa nini hasa wapinzani wasi-focus kwenye utais wakati uchaguzi unahusu urais, ubunge na madiwani?

CHADEMA tuna uzoefu mzuri sana; chama chetu kimepata jina kubwa baada ya kusimamisha mgombea wa urais serious. Chama chetu pia kilipata idadi kubwa zaidi ya wabunge baada ya kuwekeza nguvu kubwa kwenye urais. Kwetu sisi, ushahidi tunao unaoonyesha a statistically significant correlation kati ya kusimamisha mgombea imara wa utais na kupata viti vingi vya ubunge.

Sasa pamoja na maelezo yako mengi na mazuri hujatuonyesha ushahidi wowote wa kimantiki au kisayansi wa kuonyesha uhusiano uliopo kati ya kugombea urais na kutopata idadi kubwa ya wabunge.

Jambo jingine ambalo unajichanganya mno ni pale unapotoa mifano ya Kenya na Zimabwe. Ambacho hutaki kukiri katika mifano yako hii ni ukweli kwamba huko kote ulikokutaja hivyo vyama vya upinzani vilipata wabunge wengi wa upinzani baada ya kusimamisha mgombea wa urais serious. Again, ushahidi unaonyesha kwamba hakuna chama cha siasa kinachoweza kupata wabunge wengi bila kuwa na mgombea urais anayekubalika.

Hili ni kweli kwa upinzani na CCM pia. Kuna wabunge wengi sana ambao walipata ubunge through CCM kupitia mgongo wa JK na isingekuwa mvuto wa JK 2005 wangeula wa chuya. Na hili si Tanzania au Africa tu. Hapa nilipo UK mara zote chama cha siasa kimepanda au kushuka umaarufu kutokana na kiongizi wake ambaye pia ndiye mgombea wa kiti cha uwaziri mkuu. Kila mara chama kilipokuwa na mgombea uwaziri mkuu goigoi kilijikuta kinapata wabunge wachache.

Kuna propaganda ambayo imetumiwa muda mrefu kwamba wapinzani wakazania ubunge na waachane na urais. Lakini hebu tuambie basi kuna ubaya gani hasa kuwa na mgombea urais mzuri na wagombea ubunge wazuri? Tupeni mifano ambapo chama cha siasa kiliweza kupata wabunge wengi bila kuwa na mgombea urais wa maana?

Ambacho pia hamtuelezi ni kwa nini hasa mnafikiri upinzani wanafaa sana bungeni lakini hawafai katika kiti cha urais. Na muhimu zaidi hiyo CCM ya leo ni kitu gani hasa cha maana wanachokifanya huko serikalini ambacho wapinzani wasingeweza kufanya?

Hatuwezi kupumbazika tena kuacha kuweka mgombea imara kwenye kiti cha urais maana madhara yake tunayajua. Tutaweka mgombea imara moja kwa kambi nzima ya upinzani katika uchaguzi wa 2010.
 
Mimi hawa watu wanaosema eti wapinzani bado hawawezi kushikilia uraisi wananiudhi sana. Kama uraisi wenyewe unashikiliwa na watu kama Mwinyi, Mkapa, na Kikwete,...how worse can it get?
 
Mimi hawa watu wanaosema eti wapinzani bado hawawezi kushikilia uraisi wananiudhi sana. Kama uraisi wenyewe unashikiliwa na watu kama Mwinyi, Mkapa, na Kikwete,...how worse can it get?

Nilimuuliza hili swali hapa akakimbia kwenye mambo ya kipuuzi kama ukabila na udini. Wao wanataka tu kuwa na wabunge wengi bila kukumbuka kuwa Presidaa wa nchi ana nguvu yote ya dola na akifanya kama kile Mkapa alifanya dhidi ya wapinzani, kuna uwezekano miaka michache ijayo kukawa hakuna mbunge wa upinzani hata mmoja Tanzania bara!
 
KJ said:
Karibu kila mtu aliyeenda JKT miaka ya 90s na kurudi nyuma, ilibidi awe CCM au TANU by default.

Elewa kuwa sipingi Dr. Slaa au mwingineo yeyote kugombea uraisi, ninachosema ni kuwa ni vema kwa yule mwenye nafasi ya kushinda ubunge agombee ubunge maana kushinda uraisi probabilities zake ni ndogo. Wapo wengi ambao hawana uwezekano wa kushinda ubunge lakini wana-qualify kugombea uraisi, na hao ndio ningependekeza wapewe hiyo nafasi lakini resources nyingi zipelekwe kwa wagombea ubunge.



Unapendekeza mambo mengi sana mkuu, wakati at the same time ukisema kuwa wengine hawafai kugombea uraisi, au kuwa ni ndoto kwa wapinzani kushinda uraisi! unajichanganya sana, hebu soma ulichoandika kwa sauti ili uone vile unavyoweka commedy hapa ukumbini.

Mwafrika wa Kike,
Isome tena article yangu, yooooteee bila ushabiki na hapo ndio utakapoelewa vema ninachoongelea. Asha angalau anakubaliana na mimi kuwa pesa nyingi itumike kwenye ubunge na sio kurusha watu na helicopter. Shida yake ni moja tu kuwa, article yangu pia inaipiga vijembe CHADEMA, na kusahau kuwa ukilea mtoto lazima umchape na kumfokea.

Dr. Slaa ni vema akabaki kwenye ubunge ambapo ana uhakika wa kupata, kuliko kuingia kwenye uraisi na kutumia over 60% ya mtaji halafu unapata kura 10%.

Huu unaitwa ukichaa au u-bishoo. Ugombea uraisi apewe mtu asiye na jimbo analoweza kushinda. Wengine wote wakazanie ubunge au hata udiwani.
 
Mwafrika wa Kike,
Isome tena article yangu yooooteeee bila ushabiki na hapo ndio utakapoelewa vema ninachoongelea. Asha angalau anakubaliana na mimi kuwa pesa nyingi itumike kwenye ubunge na sio kurusha watu na helicopter. Shida yake ni moja tu kuwa, article yangu pia inaipiga vijembe CHADEMA, na kusahau kuwa ukilea mtoto lazima umchape na kumfokea.

Dr. Slaa ni vema akabaki kwenye ubunge ambapo ana uhakika wa kupata, kuliko kuingia kwenye uraisi na kutumia over 60% ya mtaji halafu unapata kura 10%. Huu unaitwa ukichaa au u-bishoo. Ugombea uraisi apewe mtu asiye na jimbo analoweza kushinda. Wengine wote wakazanie ubunge au hata udiwani.

Bado hujatoa sababu za kwanini Dr Slaa asigombee uraisi na kwa nini wapinzani wawaachie ccm kwenye uraisi. Katika hili bado unacheza makida na pumba zako unazoziita 'mavituz'
 
Kubwa jinga nafikiri zile zidumu fikra zilikuingia vizuri sana.

Tanzania mpaka sasa hivi chini ya chama cha... imekwama inaelekea kuzimu pamoja na raslimali zote, unasikia wenzako miaccount mpaka hawajui wameweka wapi, wanafanya kusomba tu. Hao hao unataka waendelee kuchukua nchi.

Kwa taarifa bila watanzania kuamua kuwa sasa wanahitaji maendeleo, kamwe hayatakuja kwa kutembea. Hata mlo mmoja kwa siku utakosa wakati waliopewa nchi wananunua visiwa.
 
Back
Top Bottom