Hapo ndio umuhimu wa katiba kubadilishwa unapokuja, katiba ya nchi bado imekaa kichama kimoja sana (mambo ya kushika hatamu).
nani atabadilisha katiba kama ccm hawataki?
Hapo ndio umuhimu wa katiba kubadilishwa unapokuja, katiba ya nchi bado imekaa kichama kimoja sana (mambo ya kushika hatamu).
LoL,anaijua siasa ya Tz? anatakiwa tu aliyeko bongo ambaye anaiweza misukosuko. Say Mnyika?
nani atabadilisha katiba kama ccm hawataki?
nani atabadilisha katiba kama ccm hawataki?
LoL,
Mnyika hapana mama! Huyu atinge tena kwenye kinyang'anyiro cha Ubungo na sasa tunamhakikishia ushindi kwa udi na uvumba...! Anahitajika Bungeni huyu
Qeeque kaanzisha mjadala mzuri, lakini kama ilvyo kawaida ya JF, tayari umekwishapindishwa.
Pendekezo limetolewa Dr. Slaa agombee 2010. Bado sijasoma hoja nzito inayopinga pendekezo.
Mabadiliko ya katiba yatakuja pale tu tutakapokuwa na Rais ambaye yuko tayari kufanya mabadiliko hayo. Kwa sababu hawa watu wana njia zao za kuchelewesha maamuzi mbambali hata kama yametolewa na mahakama. Kwa hiyo ni muhimu sana kuhakikisha pamoja na kuing'oa CCM kwenye viti vya ubunge ni muhimu pia kuwang'oa kwenye Urais.
Nyani mimi sijamsoma/kumsikia John Mashaka kwa hiyo ndio maana inaniwia vigumu kujua uwezo wake katika utendaji na yapi ana uwezo wa kuyatekeleza akiwa kama kiongozi.
Geeque,
Katiba haiwezi kubadilishwa kwa kuipigia magoti CCM ikubali kuibadili. Kenya walifanikiwa kuanza mchakato wa kuibadili katiba yao kwa kumlazimisha Moi.
Wapinzani, Civic organizations, na wananchi wanahitaji viongozi tu wa ushawishi mkubwa kuwafanya CCM wasalim amri.
Ndo maana nimesema mchango wa NGO katika kuakikisha Tanzania inakuwa nchi yenye good governance bado ni mdogo, hizi ndo zinatakiwa kuwaelimisha wananchi vijijini lakini wamekaa mjini tu.
Nadhani wengi wetu mnalijua jina la Dr. Wilbroad Slaa Mbunge wa Karatu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA. Mimi ni Mtanzania ambaye sifungamani na chama chochote lakini mwenye kuamini kabisa ya kwamba, miongoni mwetu kuna Watanzania ambao wanaweza kuleta mabadiliko makubwa katika njanja mbalimbali kama za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Nchi yetu iko kwenye wakati mgumu sana hivi sasa na tunahijati kiongozi bora na sio bora kiongozi ambaye ataweza kuleta mabadiliko makubwa na ya kweli katika kuiendeleza nchi yetu kiuchumi.
Kama mjuavyo tatizo la ufisadi na rushwa limekithiri sana na imeshajionyesha wazi ya kwamba, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameshindwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza majukumu yake aliyopewa na watanzania kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naamini huu ni muda thabiti kabisa kumtafuta mtu atakayefaa kukichukua kiti chake itakapofika wakati wa Uchaguzi wa mwaka 2010. Binafsi ningependa Kikwete aondoke hata leo hii na arudi kijijini kwao Bagamoyo akalime Mananasi yake na huku akiendelea kujichekesha mbele ya ndugu zake. Naamini kabisa Dr. Slaa ndio mtu anaefaa kuwa Rais wa nchi yetu na mwenye uwezo mkubwa wa kulianzisha gurudumu la maendeleo nchini. Mimi niko tayari kulipia gharama zote za kutengeneza tovuti ya Dr. Slaa na kulipia hosting charges kutoka hivi sasa mpaka wakati wa uchaguzi mwaka 2010. Kwa hiyo ningeomba watanzania wenzangu tumhamasishe Dr. Slaa agombee hiki kiti cha Urais mwaka 2010. Tumebakisha miaka miwili na nadhani huu ni muda muafaka kuanza kujiandaa ili kuhakikisha Kikwete na CCM hawarudi tena kwenye uongozi.
Ahsanteni.
(Haya ni maoni yangu binafsi hayaingiliani kabisa na maamuzi ya CHADEMA) www.drwilbroadslaa2010.com
Nashauri tupitie vizuri members list,humo tutayaona majina halisi,tena ya watu wenye mwelekeo wa siasa,na sera zao walishaandika humu,angalia kama huyu http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=10727Hata mimi nakubaliana nawe katika hili ... Hawa wengine mpaka tuwajue kwa majina yao halisi ili tufanye upembuzi wa kina katika hili
Kama ambavo huwa wanaonesha mshikamano wao kama huo hapo juu, basi wakiungana pamoja na kuunda chama kipya basi muda bado upo wa kujitayarisha na sisi wapambe tupo tayari kusaidia kimawazo.
ingeleta bonge la upinzani na CCM wangetoka jasho viganjani. Bado umuhimu wa kuelimisha wananchi wa vijijini maana halisi ya upinzani na umuhimu wake. Waeleweshwe kuwa hali zao duni kimaisha ni matunda ya serikali ya CCM so itakuwa vema na haki kutowapa kura katika chaguzi zijazo. Wananchi wakipata elimu hii na wakaelimika mambo yatakuwa rahisi, vinginevyo mchezo utakuwa ule ule.
Wanashirikiana sasa hivi uchaguzi ukikalibia kila chama kivyake
Wanashirikiana sasa hivi uchaguzi ukikalibia kila chama kivyake
siku hao viongozi wa upinzani wakipopigwa picha inayoonekana kwenye thread hii,waliahidi kusimamisha mgombea mmoja wa urais ifikapo 2010.