The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Wakati tunaelekeza macho yetu kwenye 2010 naona tusisahau zile kelele za kufanyia mabadiliko Katiba ya Nchi.

Kuna mambo mengi yanatakiwa kuangaliwa na kufanyiwa marekebisho kwenye hii Katiba. Kwa mawazo yangu naona Suala la Rais wa Jamhuri ya Muungano kuwa voted kwenye Jimbo la Uchaguzi na hivyo kuwa kwanza member of National Assembly ndipo awe confirmed kama Rais, liwe mojawapo ya masharti.

Nafikiri hii itasaidia kupata vichwa vizuri kwenye Bunge hususani wale wanaopoteza nafasi kwenye kinyang'anyiro cha Urais.
 
Tuna watu hawa kwanini wasiingie walau Bungeni?
GAME THEORY,
Mwanakijiji,
Mswahili,
Phillemon Mikael,
Field Marshall ES,
.....................,
Mkandara,
Brutus,
Kitila,
Mwendapole,
Ogah,
Rev. Kishoka
Mnyika,
Kasheshe,
KadaMpinzani,
na wengine kibao!

Sasa ndio maana napendekeza wale wanachama ambao mna dhamira ya kufanya vile hima fanyeni hivyo! We can make a big difference
C'mon Invisible,H'w could you forget Mwafrika wa Kike on that X-mas card list of your?? Got2B politicaly correct sometimes-Uknow!!!
**It worked4 JK, why not Us?!
 
Naamini kuwa huu sio muda m-baya (sio mapema wala late) kuanza ku-speculate nani anafaa kukabidhiwa nchi. Ila ieleweke kuwa mtu anaweza kuwa mzuri sana katika upande mmoja na kuwa bomu upande mwingine!

Nani asiyekumbuka manyanga ya Mzindakaya bungeni ktk miaka ileeee? Nafikiri angeweza kuwekwa kwenye list ya watarajiwa ktk kipindi hicho lakini tunajua hivi leo ana profile gani!

Kabla hatujaweka nguvu zetu kwa Dk. Silaa au mtu mwingine yeyote tupate profiles za wengi na tupime.

Oyee 2010!
 
Tuna watu hawa kwanini wasiingie walau Bungeni?

GAME THEORY,

Mwanakijiji,

Mswahili,

Phillemon Mikael,

Field Marshall ES,

Mkandara,

Brutus,

Kitila,

Mwendapole,

Ogah,

Rev. Kishoka

Mnyika,

Kasheshe,

KadaMpinzani,

na wengine kibao!

Sasa ndio maana napendekeza wale wanachama ambao mna dhamira ya kufanya vile hima fanyeni hivyo! We can make a big difference

Mkuu usiyeonekana.
Nadhani hapa ulikuwa unatania,kuna baadhi ya majina yanaleta matumaini, lakini baadhi hayastahili, Mkuu. Watakwenda bubgeni na kuleta ushabiki wa vyama na undugu na si maslahi ya nchi.
 
DUH! KWELI HUYU MZEE HUWA APENDI UPUUZI NA NINAHAKIKA AKIWARAIS PESA ZOTE ZITARUDISHWA NA FAIDA YAKE.
 
C'mon Invisible,H'w could you forget Mwafrika wa Kike on that X-mas card list of your?? Got2B politicaly correct sometimes-Uknow!!!
**It worked4 JK, why not Us?!

Kwi kwi kwi kwi,

Wewe hauxtable, yaani umesahau kuwa waafrika wa kike bado hawatakiwi kuongoza hapo Tanzania ......lol? Invisible amefanya kusudi hapo na wala sio kuwa amesahau....lol

On a serious note though, kuna watu ambao hawafai kuwa magogoni au dodoma kwa vile wako too emotional kutawala. Mmoja kati ya hao watu ni mimi. Mimi nikiwa huko nitajenga magereza zaidi na kuhakikisha kuwa mafisadi ndani ya ccm kuanzia Mkapa hadi yule mzee mwizi wa pesa ya wakulima wa ndizi kuleta Kishozi amefungwa au kuchapwa risasi hadharani.

Kitakachofuatia ni maandamano ya nguvu toka nchi za kinafiki za magharibi na ..... unajua tena kitakachofuatia nikifuta mikataba yote ya sinclair na wenzake .... majeshi ya marekani yatakuja nchini kwa visingizio vya kulinda "human rights"
 
mi bwana nakubaliana na Slaa kuwa presidaa, na shilingi yangu ya turufu siwezi kuitoa katika hilo.
 
Dont dare to think about Presidential post inhal hujafikiri kuhusu posts kama udiwani na ubunge, rejea falsafa ya Mao Ze Dong then tuijaribu hapa kwetu huenda ikawa fruitfull, ila so far FORGET ABOUT URAIS POST KWANZA.
 
Wewe hauxtable, yaani umesahau kuwa waafrika wa kike bado hawatakiwi kuongoza hapo Tanzania ...

Wakati huu wa mapinduzi ni vyema pia kupindua mitazamo yetu juu ya uwezo dhidi ya jinsia! Mimi mwenyewe Dume la Mbegu naanza kuwa na wasiwasi juu ya ubora wa hizi mbegu na mstakabali wa taifa!

Unaweza na unahitajika, Mwafrica wa kike!
 
Kwi kwi kwi kwi,
....... kuna watu ambao hawafai kuwa magogoni au dodoma kwa vile wako too emotional kutawala. Mmoja kati ya hao watu ni mimi.
Usiwe na shaka Bi-Mkubwa,kama nilivyo gusia hapo awali,tuko tayari hata kuazima 'Pattern' ya JK anayoitumia haswa ktk upande huu wa pili wa Kijinsia;Kuna Bond Street(London),DC au hata UN(HQ),vijiwe vya kuwakilisha vipo vingi tu its just a Que.of time.
 
Wakati huu wa mapinduzi ni vyema pia kupindua mitazamo yetu juu ya uwezo dhidi ya jinsia! Mimi mwenyewe Dume la Mbegu naanza kuwa na wasiwasi juu ya ubora wa hizi mbegu na mstakabali wa taifa!

Unaweza na unahitajika, Mwafrica wa kike!

kwi kwi kwi,

wewe na hizo mbegu zako naona zitakupoteza kabisa hadi usahau kuwa hii thread imeanzishwa na mazee GQ kumpigia debe Dr Slaa!
 
Usiwe na shaka Bi-Mkubwa,kama nilivyo gusia hapo awali,tuko tayari hata kuazima 'Pattern' ya JK anayoitumia haswa ktk upande huu wa pili wa Kijinsia;Kuna Bond Street(London),DC au hata UN(HQ),vijiwe vya kuwakilisha vipo vingi tu its just a Que.of time.

Asante kwa hilo ila naona kama hiyo itakuwa ni nafasi ya kunitoa JF na kuwapa breki mafisadi ambao huwa wanapasuka viroho every minute nikiwa hapa online.

Kama nitachagua wana JF, mimi naona kina Kitila Mkumbo na wengi hapa wanafaa kabisaaaa. Otherwise, nitampigia kura dada Asha if I had to na kama akipenda!
 
Nadhani inaonekana kabisa wengi wetu mnakubaliana na suala la Dr. Slaa kuwa mgombea wa kiti cha U-rais. Unajua katika nchi nyingi duniani wagombea u-rais inabidi waonyeshe accomplishments zao katika mambo mbalimbali ya kuitumikia jamii.

Katika suala hili tumeona jinsi Dr. Slaa alivyopigana kufa na kupona katika kuhakikisha MAFISADI wanajulikana kwa wananchi wote na hakuishia hapo tu bali alihakikisha vyombo husika vinafanyia kazi tuhuma zake ili Mafisadi washitakiwe. Kama tujuavyo CCM na viongozi wake karibu wote walipuuzia madai ya Dr. Slaa na kuyaita ni ya uchochezi na ya uongo, lakini leo hii wengi wenu mnaona jinsi mafisadi mmoja baada ya mwingine wanavyoanguka au kujulikana na jamii.

Tunahitaji mpiganaji kama Dr. Slaa katika U-rais, tunahitaji Mzalendo kama Dr. Slaa kwenye kutetea maslahi ya nchi yetu, Tunahitaji kiongozi kama Dr. Slaa katika kutetea haki sawa kwa wote na pia tunahitaji Jasiri kama Dr. Slaa katika kuhakikisha serikali inawajibika kwa wananchi wake na viongozi mafisadi wote hawana nafasi katika jamii yetu na ni jela pekee ambako kunawafaa.

Naamini Dr. Wilbroad Slaa will make a good President.
Dr. Slaa for President 2010.
 
Mi Bado Sijaridhika, Why Not Zitto Kwani Mwaka 2010 Atakuwa Na Miaka Mingapi?
 
Mi Bado Sijaridhika, Why Not Zitto Kwani Mwaka 2010 Atakuwa Na Miaka Mingapi?

Sina uhakika atakuwa na miaka mingapi lakini nae ni kiongozi mzuri sana ingawa naamini Dr. Slaa will make a better President.
 
kwa mtindo huu uliopo jamani hata mimi naweza kabisa kuongoza hii nchi wa vichwa maji! hilo ni neno kubwa, lakini ndio hao waliowapa chchm kura sasa eti wanalalama.

Mtu yeyote sasa anaweza kuongoza, maana tuliowafikiria walichotufanyia hata mimi nisingedhubutu.

Lazima tujiamini, mbona hata Kabila anaongoza, tena limtaifa likubwa tu lenye mpaka vita, sembuse watz, mnisamehe bure tu maana hapa ninamijazba hivyo nitaropoka sasa hivi...!

Slaa akipewa atafanya sehemu yake labda tena bora kuliko hicho cha chchm.
 
Sina uhakika atakuwa na miaka mingapi lakini nae ni kiongozi mzuri sana ingawa naamini Dr. Slaa will make a better President.

Mheshimiwa Kuongoza ni tofauti na Kukosoa. Kukosoa ni rahisi kuliko kuongoza. Unaweza kuwa bingwa wa kukosoa, lakini tabaan ukawa tobwe katika mkuongoza. Jee una hakika na Waheshimiwa (ma-champion wako) hao ambao umebaini kuwa ni mabingwa wa Kukosoa?
 
Kweli Dr. Slaa anafaa lakini ni kwa jinsi gani tunaweza kuwatoa ccm madarakani? itakuwa vipi huku jeshi lao, polisi yao , mahakama yao!!! iko njia moja tuu nanyi mwaijua,tukiitumia hiyo kweli Tanzania twaweza kupata mabadiliko kisiasa na hata kiuchumi
 
Mheshimiwa Kuongoza ni tofauti na Kukosoa. Kukosoa ni rahisi kuliko kuongoza. Unaweza kuwa bingwa wa kukosoa, lakini tabaan ukawa tobwe katika mkuongoza. Jee una hakika na Waheshimiwa (ma-champion wako) hao ambao umebaini kuwa ni mabingwa wa Kukosoa?

Ni kweli kukosoa ni totauti na kuongoza, tulimchagua Kikwete kwa matumaini kuwa ataweza kuongoza lakini mpaka hii leo Rais Kikwete ameshindwa si tu kuongoza bali hata kukosoa.

Inawezekana kabisa mkosoaji akawa mzuri maana zile kosoa kosoa zake zinaweza kuleta mwanga kwa wale wote wataokuwa wanafanya vibaya katika serikali na walio chini yake. CCM na viongozi wake wameshindwa kabisa kuongoza na hata kukosoa na wamebakia kusheherekea na kufurahia jinsi wanavyoiba pesa za Watanzania.

CCM ni chama kinachonuka rushwa, viongozi wakubwa wa CCM ni wala rushwa wakubwa, kwa hiyo tunahitaji kiongozi mpya ambaye ataweza kusafisha uozo na uchafu huu wa CCM. Tunahitaji kiongozi imara, shupavu na asiyetetereka kama Dr. Wilbroad Slaa.

Tunahitaji kiongozi mzalendo na mwenye nia thabiti ya kulitetea taifa letu na rasilimali zake. CCM kumejaa MAFISADI ambao wana uchu mkubwa wa kuiba rasilimali kama FISI aliyeona mzoga. Naamini na nina uhakika wengi mnakubaliana nami Dr. Slaa For President 2010.
 
Back
Top Bottom