Unamwonea KadaMpinzani...! Usimwone kuwatetea ila facts zikija hata kama anazipinga zinamwingia sana akilini. Hawezi kuwa sawa na wao! Trust me, hapa tunafundana na nina imani kishajifunza mengi sana. He's a fast learner I assure you. That's KadaMpinzani
Nyani kwa maana hiyo mimi na wewe hatufai? Basi wengine kina Mtanzania na Mwafrika wa Kike wanafaa!
Ila tuwe waangalifu na watu wanaotumia haya majina ya bandia humu ndani...wengine ni wanafiki tu....Ninayemuona anafaa ni Kitila Mkumbo peke yake...wengine ninaguna kidogo...
Mh!Hata mimi nakubaliana nawe katika hili ... Hawa wengine mpaka tuwajue kwa majina yao halisi ili tufanye upembuzi wa kina katika hili
Mh!
Sasa hapo ndipo pabaya...! Mkuu Lunyungu anatumia jina lake la kweli. Then naye aaminiwe na atakapoomba ridhaa na ushirikiano wetu tumpe kila aina ya mchango aweze kutinga Bungeni mwaka 2010. Itabidi watu waanze kujianika ikikaribia kipindi cha uchaguzi basi.
Back to the hoja,Naamini kabisa Dr. Slaa ndio mtu anaefaa kuwa Rais wa nchi yetu na mwenye uwezo mkubwa wa kulianzisha gurudumu la maendeleo nchini.
Back to the hoja,
Siamini kuwa Dr. Slaa anafaa kuwa rais! Naamini anafaa kuendelea kuwepo Bungeni. Think of it Geeque
Back to the hoja,
Siamini kuwa Dr. Slaa anafaa kuwa rais! Naamini anafaa kuendelea kuwepo Bungeni. Think of it Geeque
Basi huu ni muda muafaka kwetu sote tukitumia nafasi ya kuongea na ndugu na jamaa zetu kule nyumbani kuwafahamisha jinsi gani CCM ilivyoharibu na inavyoendelea kuharibu Uchumi wa nchi yetu kila kukicha. Tutumie nafasi hizo wakati wanataka kutupiga mizinga au hata kabla ya kuwa-western union mambo fulani(joke) Tunahitaji mabadiliko na tusipokaza buti ndugu zangu tutabaki tukijilaumu wenyewe. CCM Has To Go, Kikwete Has To Go.
Dr Slaa anafaa sana kuwa nje kwa ajili ya balance and checks, ukiwa mtendaji unabanwa na majukumu so inabidi udelegate power, na hilo ndio tatizo kwa vile wanaoaminiwa na kupewa power mara nyingi hufanya ndivyo sivyo
CCM si rahisi kung'oka kirahisi kihiiiiivyo. Cha muhimu ni kuhakikisha kunakuwa na wabunge wengi wa upinzani, na ingawa atatoka ccm basi ushindi uwe kwa 51%, then 2015/20 upinzani unaweza kuchukua urais
Kama sio Dr Slaa, je nani agombee?
Kama sio Dr Slaa, je nani agombee?
John Mashaka je?
Mama,
umesahau kuwa ccm wanatumia kila mbinu kushinda hata viti vya ubunge. Sasa hivi wanafanya kampeni ya kumtoa Chacha Wangwe kule Tarime. CCM wanauwezo wa kuchukua viti karibu vyote vya bara na Unguja kama wakipenda.
Katika hili tusidhani utani. CCM lazima inyang'anywe nguvu kubwa ya dola waliyonayo na ndipo wapinzani watapata hata hiyo asilimia 30 ya viti Bungeni. Umesahau alichofanya Mkapa kwa vyama vya upinzani kati ya 1995 na 2005? Alichukua karibu majimbo yao yote na kuvidumaza kabisaaaa
Ataweza kweli misukomisuko? Yeye amesema kuwa hataki siasa kwa sasa labda tusubiri tuone kama atagombea huko musoma awatoe kina Mkono
John Mashaka