WembeMkali
JF-Expert Member
- Jun 16, 2007
- 282
- 3
Jamani tunazungumzia muda wa miaka miwili kufikia 2010.Kwa mtazamo wangu wa chapchap ni kwamba bila ya kujipanga vizuri tutawaachia tena mafisadi warudi tena madarakani.
Sasa kabla ya kuanza kuwalaumu wananchi kwa kuipenda mno CCM huku wao wakifa masikini hebu tuangalie tu kwanza mfumo mzima wa uchaguzi nchini kwetu kama unaweza kutangaza ushindi kwa chama cha upinzani kama kikishinda.Maana katiba bado ni ileile,mwenyekiti wa tume ya uchaguzi huteuliwa na rais,na ippmedia ya mengi nayo huipigia debe CCM.
Sasa wenzangu mnalionaje hili?
-Wembe.
Jamani wenzangu. Watanzania wenye uchungu na nchi hii. Wajasiriamali. Masikini. Wazalendo na watoto wa Tanzania.
Kwenye jambo la kweli na lenye maslahi ya Tanzania na watu wake, lazima lisimamiwe na litetewe kwa kila tone la damu la maji ili watoto wetu, hata kama siye hatutakuwepo li kunusuru ustawi wa nchi.
Nimekutana na watu kibao, wakizungumzia kuhusu uchaguzi ujao, 2010. Yawezekana kuwa mbali, lakini lazima tukubaliane kuwa tunahitaji mtu wmenye uchungu, anayesema No na ikawa hivyo, akaisimamia na kueleza sababu za kusema hivyo. Mtu ambaye hayumbishwi na marafiki mafisadi. Mtu ambaye anaamini katika misingi ya haki kuongoza Tanzania.
Katika vikao ambavyo sivyo rasmi; katika harusi, vijiwe, ofisini, kwenye baa na vituo vya mabasi yetu ya jumla, mazungumzo sasa ni kumpata Mtanzania ambaye ana uchungu na nchi. Huyu wanamtaka awe Rais wa Tanzania 2010.
Wanamtaka warioba, Joseph Sinde achukue fomu mwaka huo utakapofika ili aokoe jahazi, kwani wanasema kuwa nchi imevurugika, haina misingi, haina visheni kwa sasa, licha ya kusifiwa na Bush na wasanii wengine wa ndani na nje.
Hebu changieni hapa wana-JF ili tupate muafaka na tukiweza tuweke msimamo wetu mapema kuwa tunampendekeza nani kwa mwaka huo, utaratibu wa kwamba rais lazima amalize miaka 10 haufai kwa sasa katika Tanzania iliyochanika kiasi hiki.
Nakulilia mama Tanzania kwa machozi ya damu kwa jinsi baadhi ya viongozi wetu wanavyokutafuna wakijitahidi kugawana fito za nyumba yako. Ee Tanzania... Ewe Tanzania.

Warioba aendelee kula pensheni yake ya WM... Inatosha!Warioba Nitamuunga Mkono....mnajua Kuwa Kikwete Ni One Term President??? Ambao Hawaamini Wasubiri..mwaka 2011..inshaalah Tutakumbushana Hapa...lakini Ndo Hivyo...hana Akili Wala Uwezo Wa Kutawala Miaka 10..hili Hata Yeye Analijua ....
Warioba Nitamuunga Mkono....mnajua Kuwa Kikwete Ni One Term President??? Ambao Hawaamini Wasubiri..mwaka 2011..inshaalah Tutakumbushana Hapa...lakini Ndo Hivyo...hana Akili Wala Uwezo Wa Kutawala Miaka 10..hili Hata Yeye Analijua ....
Hivi Mwungwana aliutaka urais ili afanye nini? Ametumia kipindi cha miaka kumi kuwania.
Lakini mbona visheni imempiga chenga? Mimi nadhani hapa swala si personality kwamba nani anaweza kusaidia kuwakomboa Watanzania. Suala linapaswa kuwa nini tunachopaswa kukifanya kuwakomboa Watanzania kutoka hili wimbi la mafisadi? Ni kweli Mwungwana ni mwenzao na si mwenzetu. Tuorodheshe kwanza yale yanayotakiwa kufanyika halafu ndiyo tuanze kutafuta ni nani kati yetu aliye na uchungu wa kutosha kuyafanyia kazi yale tuliyoyaorodhesha. Nakumbuka mwaka 1995 kilio kilikuwa rushwa. Mwalimu alifikiri Mkapa angetusaidia. Alipoingia Ikulu akasema hatafanya "witchhunting." Badala yake akaungana nao mafisadi. Tujifunze kutoka makosa kama haya.
Warioba aendelee kula pensheni yake ya WM... Inatosha!
JK is the right man at the right time in the right place... wenye chuki mjinyonge... Chini ya JK GDP imepanda na kufikia 6.2% katika 2007 na this year itafika 7.3%. Mwendo mdundo hadi 2015
Kwa mtaji huu tuliokuwa nao nasema Mrema would be the best Presidaa kwa Tanzania hii ya Mafisadi.