The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

Mpango Mkakati kamili hauko kwenye website ya chama, huo ni muktasari tu wa maeneo ya juu kwa ajili ya umma wa wanachama. Mpango Mzima ni siri.

Ndio maana nilikwambia kama upo mwingine wengine tunachotarajia kukiona ni matunda au matokeo ya mkakati huo. Kwa tuliyoyashuhudia karibuni ni ngumu sana kujenga imani juu ya mkakati wenu huo kama upo.

Jiunge na CHADEMA utapata hayo kwenye vikao vya ndani.

Bahati nzuri nimekuwa karibu na siasa za vyama tangu vinaanzishwa. Kuna mahala nilitaja kidogo historia ukaniambia napiga propaganda, nikaacha. Naijua vema Chadema.

Labda nikueleza kuwa miongoni mwa watu waliokikwamisha chama hicho ni Kuchaguliwa kwa Kaburu kuwa katibu mkuu kwani huyu jamaa hakufanya juhudi zozote za kukikuza chama bali maslahi yake binafsi. Wakati mzee Makani anashika uenyekiti chaguo lake la Katibu Mkuu alikuwa Eric Mchata, Kaburu alikuwa Chaguo la Mzee Ndesamburo.

Sasa hivi Chadema imepata nguvu ya vijana wadogo wasomi lakini kwa bahati mbaya, pamoja na mapungufu mengine, wana upungufu wa experienced visionary leaders hususan katika Uongozi wa juu. Maoni ya Chacha Wangwe yalikuwa yakufanyiwa kazi. Aliyoyataja Wangwe ndani ya Chadema hayana tofauti na yanayosemwa kichinichini ndani ya CUF.

Haya hebu tupe japo kwa ufupi Strategic Plan ya vyama vingine tulinganishe na CHADEMA.

Kukosa mkakati sikuitaja Chadema peke yake Asha, hebu soma vizuri. Nimeitaja na CUF kwani alau kwa sasa ndio vyama vyenye kukubalika kiasi.

Halafu mbona waliokupongeza wote ni wanaCCM tu waliojitambulisha humu JF? Inaelekea maoni yako yamewakuna sana wenzako eeehhhhh

Tatizo kubwa la vijana wa Chadema waliomo humu JF hawapendi mapungufu ya chama chao yatajwe. Wale wanaojaribu kukikosoa wanaonekana wanakipinga au wametumwa na CCM. No wonder mnapata wanachama from frustrated university graduates/students.

NN.
 
..... Hata sisi kwenye mafunzo ya Zanzibar hatukupewa mpango mzima lakini nyaraka tuliyowepewa ilikuwa na SWOT, Objectives, Stakeholders na Targets za CHADEMA za mwaka 2010. Sasa hizi ni silaha za ushindi haziwezi kumwagwa hadharani wewe. Jiunge na CHADEMA utapata hayo kwenye vikao vya ndani.


Asha
Asha ikiwa wewe uliendani ya Chadema..hujapewa..itakuwa mwanachama Mpya?...au kusubiri makapi ya CCM akina Mwita muyachukue!!!
 
Mrema ndio mnafiki zaidi dhidi ya CHADEMA:

a. Aliahidi kwenda Kiteto kuunga mkono CHADEMA, hakwenda aliishia DSM. Chaguzi za CUF zote huenda mwenyewe

b. Tarime, Mrema aliunga mkono NCCR Mageuzi. Kwanini hakuunga mkono CHADEMA iliyokuwa na nguvu zaidi?

c. Huyu ndiye aliyeshiriki kusema Mbowe alimuua Wangwe, na naibu katibu Mkuu wake akaandika barua kwa IGP kuwa Mbowe alifanya sherehe Afrika Kusini. Mrema akamsifu kwa barua hiyo

Kwa ujumla ni hasira zake kwa Mbowe na CHADEMA kwa kuchukua nafasi ambayo yeye na TLP walikuwa nayo katika siasa za Tanzania.

Hivi kwanini vyama vyote vinaishambulia CHADEMA jamani? Ina nini cha pekee, CCM, CUF,TLP, NCCR nk

Asha


Asha

Nakubaliana na wewe hawa jamaa sipati picha nikitafakari kampeni zao chafu dhidi ya Chadema, lakini kufanya ushirika na watanzania ni jambo jema sana kuliko ushirika wa CUF,TLP ,NCCR na CHADEMA, na Chadema tumeamua kufanya ushirika na watanzania.

Mbinu za kutaka tuache kazi takatifu inayofanyika ya kuwakomboa watanzania hazitafanikiwa sisi ni kanyaga twende tu, mpaka kieleweke.
 
- Kwa Chadema kushindana na Mrema publicly ni kujishusha hadhi, maana the man has nothing to gain zaidi ya kusubiri atoke kwenye siasa, Chadema go easy on this na Mrema maana mtajishusha bure hadhi!
 
FMES,
Mkuu wajishushe mara ngapi?...Chadema tayari wamekwisha bugia sumu ya wale waliotaka kuibomoa... Na trust me, acha watu waseme wanavyotaka lakini ukweli ni kwamba Chadema, CUF na TLP wote hawana tena nguvu iliyojengwa mwanzoni..
Na machoni mwa wananchi huu ugonvi wao unaonyesha wazi kwamba wanagombea ruzuku - Obvious! hata kipofu anaweza kusoma alama hizi. The more unapo win majimbo ndivyo pango linazidi kuwa kubwa..Hivyo kinachowasumbua wote ni NJAA tu.. If kiongozi wa CUF, Chadema au TLP ndiye sababu ya ugonvi huu kwa nini msiwakilishe hoja yenu kwa wananchi!..Ya Mbowe yalishindikana na Uongo ulijitenga iweje leo tuzue mapya mengine kutafuta wachawi!..I't's all about U people nani kafanya hivi ama vile - Pure simple minded leadership!..

Kwa viongozi wote, sSababu kubwa iliwafanya wananchi kuipenda Chadema ni uwezo wa viongozi wake kuwa msitari wa mbele kutetea hoja zote zinazohusu mirengo tofauti..viongozi wa Chadema kama wawakilishi wakubwa wa Upinzani nikiwa na maana machoni mwa wananchi, Chadema walipewa dhamana bila kiapo idhini ya kuwakilisha maoni ya vyama vingi kisiasa, hivyo wananchi bila kujali tofauti zao za kiitikadi walikuwa nyuma ya mawazo mengi ya viongozi wa Chadema.
Wananchi walimuunga mkono Dr. Slaa au Zitto (Ufisadi) kwa sababu hawa viongozi walikuwa viongozi wabunge wetu sote ktk Upinzani huko bungeni na hoja zao zilitoka kama sauti ya Upinzani..Na laukama nafasi hizo wangeshika watu wengine tungewapa sifa vilevile kutokana na ujasiri wao kusimamia maslahi ya Taifa.. The matter of fact is no one cares about Chadema, CUF wala TLP isipokuwa who stand on our side iwe toka CCM, Mfanyabiashara au Pofesa Chevji wa UDSM.
Inaudhi ssana kuona viongozi wa Chadema, TLP, CUF na NCCR badala ya ku reach out kwa wanachama na wananchi kwa ujumla wanazidisha dose ya sumu waliyopewa..Mrema ni kiongozi aliyekwisha pigwa Albadir na katu hawezi kusimama kuwa mtu tena...Amini usiamini, huyu sasa hivi ni Chale Chaplin tu... yaani comedian.

Kilichonichosha zaidi ni pale viongozi wote wa pande hizi na hasa Chadema wanapochukulia maneno ya Comedian kama vile ndio matusi ya nguoni..Leo hii viongozi wetu wanapochukulia maslahi ya chama kuwa it's about them! na ugonvi baina yao unatumika kujenga chuki za chama kizima. Chadema sio Mbowe, Zitto wala Dr. Slaa, TLP sio Mrema na kundi lake wala NCCR-Mageuzi sio Mbatia na wafuasi wake isipokuwa hawa watu wamepewa dhamana na wananchi kuwaongoza..Kama asemavyo Obama - it's not about me it's about YOU - lakini Bongo ugonvi mzima unaonyesha wazi it's about me...
Nimechoka na siasa za Bongo mweee!
 
FMES,
Mkuu wajishushe mara ngapi?...Chadema tayari wamekwisha bugia sumu ya wale waliotaka kuibomoa... Na trust me, acha watu waseme wanavyotaka lakini ukweli ni kwamba Chadema, CUF na TLP wote hawana tena nguvu iliyojengwa mwanzoni..

Mkuu Bob,

- Ninakusikia sana, ila I beg to differ kwenye ishu moja ya nguvu za vyama kua chini, Chadema haijawahi kuwa na nguvu za kisiasa kama sasa, nasema never at anytime huko nyuma, ndio maana siku zote nina heshima sana na Mbowe, kwa kuweza kuipa Chadema haya meno waliyonayo sasa.

- I mean kuishidna CCM Tarime haikuwa kazi rahisi sana, ingawa ilionkeana kama ni kazi rahisi, maana ingekua Makamba, asingekua alipo sasa kisasa ndani ya CCM, yaani empty suit ni kwa sababu ya kiboko cha Tarime.

- Huenda wana some ishus ndogo ndogo wanazohitaji kuzifanyia kazi, lakini kwa mazingara yetu ya kisiasa za bongo, kwa kweli wamejitahidi sana na huwezi waweka level moja na vyama vyote vingine vya upinzani bongo, tatizo ninaloliona sasa ni kushindwa kwao kutanuka kwa kasi kubwa nationally, ingawa pia linaeleweka kuwa you need a lot of money zile siasa za maneno matupu na kujitolea bure tu ziliisha siku hizi,

Otherwise, binafsi bado ninawapa heshima zaidi Chadema kwamba they did all they could, lakini mazingara yetu bongo ni magumu sana maana kumbuka kuna wananchi mpaka leo bado hawaamini kuwa Mwalimu hayupo, na CCM pia inahusika sana na kuwadhoofisha kutokana na umasikini wetu wanachi, wa kuanzia physically mpaka akilini, wananchi tunahitaji sana kuwa-support Chadema maana bila ya wao CCM inaweza hata kuchapa viboko barabarani, ninasema hivyo kwa sababu leo viongozi wengi wa juu wa CCM na serikali linapotaka kutokea jambo la kinyume kisiasa wanaporekebishana neno lao la kwanza unajua huwa ni nini? Chadema wakisikia hili tutapita wapi?

- Kwa mfano mtoto mmoja wa Mramba, alikuwa anajaribu kumuomba kiongozi mmoja mzito wa serikali amsaidie kumtoa baba yake rumande ili ahudhurie harusi tu na kurudi rumande, nakumbuka yule kiongozi akimjibu yule kijana pamoja na mengine kua are you out of your mind? Unafikiri Chadema watatuacha? Wataenda pale kwenye mlango wa rumande na kumpiga picha baba yako akitoka kwenda kwenye harusi, halafu watampiga picha sana tena kwenye harusi, na pia atakapokuwa anarudi rumande baada ya harusi, halafu sisi serikali na CCM tutapita wapi? Sasa unaona mkuu hawasemagi TLP, wala CUF neno la kwanza huwa ni Chadema.

- Kweli katika mazingara ya ushindani wa kisiasa ni lazima kudai more kutoka kwa vyama vyetu, lakini pamoja na mimi kuwa CCM damu, bado ninawapa Chadema heshima zaidi, ingawa sometimes wanazidisha mahesabu ya kisiasa maana huwezi waste your time na Mrema.

Thanxs!
 
FMES,
Mkuu wangu, lini CCM wameshinda Tarime?..kulikuwa na kila sababu Chadema kushinda Tarime hata kama mbinu chafu za CCM zingetumika vipi...Jamani tusizungumzie ngome ya mtu kuwa sababu kwani Tanzania nzima sio Tarime wala mkoa wa Mara..CUF nao kila siku huja na habari za Zazibar kutupa mifano na uwezo wake..Bila shaka CUF watashinda huko Zanzibar na sioni sababu kabisa ushindi wa Zanzibar au nguvu yao Zanzibar itumike kila kona..
Trust me mkulu, Chadema wamekuwa na nguvu kwa sababu kwanza ni Umoja uliokuwepo kisha hoja nzito za Ufisadi zilikuwa changamoto kubwa kwa wananchi kutoweza kuziona tofauti zao kichama kama vile tumesimamisha Taifa Stars.. Sasa ikija swala la Simba na Yanga wakati sote hapa tunajua wazi kwamba wanachama wa vyama hivi Tanzania ni manazi kama ushabiki wa mpira tukaanza kuliunga mkono na kushangilia tutakuwa tumepotea sisi..
Leo hii CUF wote, TLP Na NCCR wanaamini kabisa mkosa ni Chadema bila hata kufikiria mbali na nina hakika wanachama wa Chadema wanaona vile vile hakuna story zaidi..I personally naamini makosa ni ya wengine sio Chadema kwa sababu nawaamini viongozi wangu kwanza..
The all point ni kwamba maswala ya Ukabila, Udini na kadhalika yatatumika dakika za mwisho za 2010 na hakuna chama hata kimoja cha Upinzani kitaweza kushika hata wabunge 10 wa kuchaguliwa toka bara..narudia tena WATU na MAZINGIRA ndilo somo la kwanza ktk ujenzi wa kitu chochote..nguvu ya Chadema sii muda itakuwa nguvu ya soda na inaniuma sana kwani tulifika mahala nikaanza kujenga matumaini..
Believe me, kama hali ndio hii nimeandika leo na matokeo turudi hapa 2010!..
 
Msajili wa vyama vya siasa nchini, Bw. John Tendwa, amewashushua watu wanaojitambulisha kuwa ni wanachama wa Chama cha TLP na kueneza taarifa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Augustino Mrema na viongozi wenzie wanaongoza isivyo halali kuwa hawajui walisemalo kwani Mrema yuko madarakani kihalali.

Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu akiwa Dodoma, Bw. Tendwa amesema kuwa Mrema na viongozi wenzie hawajavunja katiba ya chama chao na hivyo wanaongoza kihalali.

Aidha, Bw. Tendwa amesema wanachama hao wanaodai Mrema na viongozi wake hawaongozi kihalali, hawana mawasiliano na uongozi wa chama chao na kwamba amebaini kuwa wao ndio wanaozua migogoro ndani ya chama hicho.

``Hawana mawasiliano na chama chao na hawa ndio ambao wanazua migogoro ndani ya vyama vya saisa,`` akasema Bw. Tendwa.

Pamoja na hayo, akaongeza kuwa hadi sasa hajawahi kupokea barua kutoka kwa wanachama hao kama wanavyodai, ya kumalizika kwa muda wa uongozi wa chama hicho.

Akasema kuwa uongozi wa chama hicho ulishaomba muda ili uweze kujiandaa na uchaguzi mkuu, jambo ambalo wamelikubali na kuwapa miezi miwili zaidi.

``Hawa wameomba muda ili waweze kukamilisha maandalizi ya uchaguzi na sisi tumewakubaliana nao na kuwapa miezi miwili... tatizo liko wapi?`` akasema Bw. Tendwa.

Kwa mujibu wa maelezo ya msajili huyo, ni kwamba muda wa Mrema na wenzie kuongoza chama hicho unaisha mwezi Machi mwaka huu.

Akaongeza kuwa mbali na TLP, vyama vingine vingi viliomba kuongezewa muda na kutoa sababu za msingi kama vile kushiriki katika chaguzi ndogo za Mbeya Vijijini na Tarime.

Akasema wanachama hao wanapoteza muda kwa kuzungumzia mambo hayo ambayo tayari yameshapatiwa ufumbuzi.

SOURCE: Alasiri
 
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema ambaye ameombwa kugombea ubunge Jimbo la Vunjo lililopo mkoani Kilimanjaro mwaka 2010 amekubali kugombea nafasi hiyo ikiwa atatakiwa hivyo na Mkutano Mkuu wa Chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya kumwandikia barua Mrema ya kumtaka kugombea jimbo hilo, aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo hilo kati ya mwaka 2000 na 2005, Jesse Makundi alisema kuwa ameandika barua hiyo Februari 8 mwaka huu na kuikabidhi jana kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, John Komba ili amkabidhi Mrema.

Alisema lengo la kumwomba kugombea nafasi hiyo, ni kutokana na mgawanyiko wa vyama vya upinzani ambao wameshajipanga kugombea jimbo hilo hali inayoonekana itaifanya CCM kupata ushindi jimboni humo.

Tayari Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia ameshatangaza kugombea jimbo hilo na kwa mujibu wa Makundi, Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, Susan Lyimo atagombea jimbo hilo mwaka 2010.

Kwa upande wake, Mrema aliliambia gazeti hili jana kwa njia ya simu akiwa mkoani Kilimanjaro kuwa yupo tayari kugombea nafasi hiyo ikiwa atapitishwa na Mkutano Mkuu wa Chama chake.

"Hilo jambo kubwa inabidi Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu waangalie hali ya siasa nchini na baadaye Mkutano Mkuu utatoa uamuzi kama nigombee au nisigombee nafasi hiyo, mimi nitatekeleza maamuzi ya Mkutano Mkuu" alisema Mrema.

Akitoa sababu za kumtaka Mrema agombee nafasi hiyo, Makundi alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuona katika jimbo hilo anahitajika mtu mwenye nguvu kisiasa ambaye ni tishio kwa CCM na mpambanaji asiyekata tamaa.

Mrema atakuwa Mwenyekiti wa nne kugombea nafasi ya ubunge. Tayari Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameshatangaza kugombea Jimbo la Hai, Mbatia atagombea Vunjo na kwa sasa Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo ni Mbunge wa Bariadi Mashariki.

Source:Habari leo
 
Ni wazo zuri, wapinzani wakifanikiwa kuongeza wabunge na madiwani ni mwanzo mzuri wa kujitangaza. Na kwa kuwa bunge ndio linalotunga sheria, itakuwa rahisi kwao kupigania yaliyo muhimu kwa demokrasia, kama katiba ambayo itatupeleka kwa tume ya uchaguzi iliyo huru.
 
Mi naona Mrema atakuba kwa sababu naona umarufu wake unayoyoma taratibu rabda akiwa bungeni anaweza kusikika kidogo.
 
Wazo zuri ili kuongeza nguvu Bungeni. Lipumba na Mbowe nao wakagombee ubunge majimboni kwao maana wote sio watu wa kushinda uraisi.
 
Naunga mkono Bwana Mrema kugombea kiti cha ubunge Vunjo.Kuna uwezekano mkubwa Bwana Mrema kushinda kiti cha ubunge Vunjo na hivyo kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni.Natoa mwito kwa viongozi wengine wa upinzani kugombea ubunge kwenye majimbo yao ya uchaguzi kuliko kupoteza muda na rasilimali ndogo kugombea urais.Nafasi ya urais inahitaji mtandao mkubwa wa chama ulioenea kila sehemu kitu ambacho wapinzani hawana.
 
Niliwahi sema kuwa hawa wenyekiti kukaa na kupinga kampeni kwenye majukwa...na kugombea urais ambao tumeona wakishidwa kwa nguvu zote...sasa ni wakati wa wao kwenda bungeni kwenda kuchangia hoja bungeni ona wenzao wakina zito,slaa,mdee na wengine wanavyo toa mchango vyema kwenye nchi hii....

Mfano huu uigwe na UF pia..mtu kama Lipumba,Sherif Hamad....waje kwenye bunge watoe michango yao si kuhubiri uko...wakati wa matatizo wanakimbilia UK.

Buswelu
 
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema ambaye ameombwa kugombea ubunge Jimbo la Vunjo lililopo mkoani Kilimanjaro mwaka 2010 amekubali kugombea nafasi hiyo ikiwa atatakiwa hivyo na Mkutano Mkuu wa Chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya kumwandikia barua Mrema ya kumtaka kugombea jimbo hilo, aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo hilo kati ya mwaka 2000 na 2005, Jesse Makundi alisema kuwa ameandika barua hiyo Februari 8 mwaka huu na kuikabidhi jana kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, John Komba ili amkabidhi Mrema.

Alisema lengo la kumwomba kugombea nafasi hiyo, ni kutokana na mgawanyiko wa vyama vya upinzani ambao wameshajipanga kugombea jimbo hilo hali inayoonekana itaifanya CCM kupata ushindi jimboni humo.

Tayari Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia ameshatangaza kugombea jimbo hilo na kwa mujibu wa Makundi, Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, Susan Lyimo atagombea jimbo hilo mwaka 2010.

Kwa upande wake, Mrema aliliambia gazeti hili jana kwa njia ya simu akiwa mkoani Kilimanjaro kuwa yupo tayari kugombea nafasi hiyo ikiwa atapitishwa na Mkutano Mkuu wa Chama chake.

"Hilo jambo kubwa inabidi Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu waangalie hali ya siasa nchini na baadaye Mkutano Mkuu utatoa uamuzi kama nigombee au nisigombee nafasi hiyo, mimi nitatekeleza maamuzi ya Mkutano Mkuu" alisema Mrema.

Akitoa sababu za kumtaka Mrema agombee nafasi hiyo, Makundi alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuona katika jimbo hilo anahitajika mtu mwenye nguvu kisiasa ambaye ni tishio kwa CCM na mpambanaji asiyekata tamaa.

Mrema atakuwa Mwenyekiti wa nne kugombea nafasi ya ubunge. Tayari Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameshatangaza kugombea Jimbo la Hai, Mbatia atagombea Vunjo na kwa sasa Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo ni Mbunge wa Bariadi Mashariki.

Source:Habari leo
huo sasa uwe ndo mwendo wa kukuza demokrasia kwa wapinzani wetu.
tumegundua kuna umuhimu wa kuwaongeza wapinzani bungeni kwani mchango wao umekuwa chachu sana katika kuboresha michango na maendeleo ya wananchi kupitia taasisi ile.

mrema ana nafasi nzuri tuu kisiasa jimboni kwake vunjo kwani mchango wake bado upo na unakubalika mnooooooooooooooooooooooo.

mzee wa kiraracha naona hata kwa maelezo yake AMERIDHIA TAYARI.
 
Ni wazo zuri, wapinzani wakifanikiwa kuongeza wabunge na madiwani ni mwanzo mzuri wa kujitangaza. Na kwa kuwa bunge ndio linalotunga sheria, itakuwa rahisi kwao kupigania yaliyo muhimu kwa demokrasia, kama katiba ambayo itatupeleka kwa tume ya uchaguzi iliyo huru.

Kuna uzuri gani katika hili? Mrema, Suzan na Mbatia wagombee alongside mgombea wa CCM! Si kuipa ushidni CCM bila jasho jingi! Inachotakiwa waelewane kabla kuwa wanamwachia mmoja wao na hakuna kuhujumiana
 
Hii mikakati mingine ya kisiasa jamani? haya 2010 Jk ndo anapata kabisa 95%
 
mzee wetu naona apumzike sasa ameshachoka! atafute kitu kingine cha kufanya sidhani kama ni lazima kwake kufanya siasa tu.
 
Ndiyo maana nikasema Mrema anatakiwa agombee sehemu neutral kama Dr au Arusha hata Mbatia pia kwa sababu siasa zao ni za juu ya majimbo.Huko wangemuacha Suzan Lyimo na mgombea wa CCM. Wakigombea Dar au Arusha wanaongeza chance za kuwa na viti vingi zaidi Bungeni na pia majimbo ya Dar hayana watu kutoka upinzani.So very powerful politicians ndiyo wanahitajika frm opposition.
 
Back
Top Bottom