The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

Mrema ni spent force, kwisha habari yake. Uwezo wake umefikia ukomo na hana jingine lolote awezalo, amebaki kuwa king'ang'anizi ili kupigania tumbo lake. Na hata akiukwaa tena huo uenyekiti wa TLP, kwa muonekano wake, its only a matter of time.
 
Ni vigumu Mrema kuacha siasa kwani yeye ni pandikizi la chama tawala,Mie nawaeleza leo CCM ikipigwa mwereka mtaona kama Mrema atangangania tena siasa.
Payroll ya Mrema bado iko serikalini panga pangua Mzee huyu anataka ale pensheni yake kiulaini.Ni mpinzani gani kila mara anazua mitafaruku ndani ya upinzani pamoja na kuhakikisha kuwa Muungano wa upinzani haufanikiwi kwa jinsi yoyote ile.Ni hukumu gani kati ya kesi zote alizonazo Mrema mahakamani aliwahi kushindwa?Hivi watanzania hatuelewi nini katika hili la Augostine Lyatonga Mrema?
Leo anarudi jimboni kwake akawachanganye wananchi wamchague.Hakika kuna somo twapaswa kujifunza kuliko kudhani kuwa huyu Bwana ajipumzikie!!!
Kama kuna kazi kubwa aliyowahi kuifanya katika historia ya chama chake ni pale alipohakikisha kuwa Bwana Benjamen William Mkapa anaingia Ikulu akisaidiana na Marehemu Mwalimu Nyerere.Mkapa alikuwa hafaahamiki vizuri kwa wananchi pia uwezo wake haukujulikana kuwa angeweza kuingoza nchi hii .Mwalimu ndiye alijua siri hiyo.Mrema alitumika kama chombo cha kuhakikisha Mkapa anaingia Ikulu.JAMBO LILOWEZEKANA!
Sasa Mrema katulia tuli baada ya kuona Kikwete anakubalika kiurahisi hasa wakati wa kampeni.Leo hii Mrema anajitokeza kutaka kurudi actively kwenye sias a baada ya kuona mwelekeo wa CCM unaenda mrama.Anataka tena kututosa tumchague JK ili CCM iendelee kupeta tena.MREMA ACHA MAMBO HAYA!!!!

Kimatire hapo umenigusa.
Ndugu yangu huyu jamaa alipelekwa upinzani kwa makusudi mazima.
Alitakiwa aibue vipaji na wale wote ambao ni wapinzani wa kweli.
Kati ya aliowaibua ni akina Masumbuko Lamwai na baadhi ya maafisa wa polisi na marehemu Kombe akiwemo. Kombe akiwa usalama wa taifa kama alivyo Lyatonga alikuwa akivujisha siri na kuwafanya wapinzani wapate updated issues toka serikalini, walimfanya nini? Wote tunajua,,,,, kamwe huwezi kumlinganisha Kombe na White Sambuo, Hilo haliingii akilini.
Masumbuko, kijana msomi wa pale chuo kikuu akajitosa kwenye ukombozi wa nchi hii bila kujijua kuwa anajiangamiza. Alikuwa na potential ya upinzani wa kweli. Akawachemsha kweli,,, ni nani asiyejua yaliyompata. Aliachishwa kazi pale mlimani, akajichimbia kwenye uwakili,,,, wakamfutia leseni akakimbilia Zanzibar,,, wakamwambia kuwa nako ni Tanzania,,, akarudi Kimara kufuga. Baadhi ya wazee wakamshauri arudi CCM na alipofanya hivyo mambo yakamnyookea,,,, nani anabisha.
Hali kadhalika yule bwana Nyaucho, kijana wa usalama wa Taifa hili baada ya kuubomoa upinzani yuko wapi? Anakula kuku baada ya kuteuliwa na CCM kuwa mbunge wa Africa Mashariki,,,,, Uongo?
Tunakula nao humuhumu ndugu zangu,,,,,
Mrema keshasema hana mpango wa kugombea Uraisi wa Tanzania anarudi kugombea ubunge huko Kiraracha kwake,,,, kuna akina Aloyce Kimaro huko wanagusa mambo ya wazee ni lazima waondoke!
Mrema ni msanii mzuri sana anaweza kuwafanya ndugu zangu Wachaga wakacheza mbasa (ngoma ya kichagga)na kumchagua tena kuwa mbunge wao.
Tusubiri anakuja na episode gani tena.
Aika Mangi
 
Now:
1445038.jpg


Augustine Lyatonga Mrema (born 1945) is a Tanzanian politician and chairman of the Tanzania Labour Party (TLP) party. Mrema is a member of the chaga tribe from Kiraracha Village in Kilimanjaro. He is the second born in a family of five children.

289202.jpg
 
Picha ya kwanza ndivyo alivyo sasa mzee wetu huyu na ya chini ni ya zamani kidogo enzi zake zikiishiaishia
 
MWENYEKITI wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Agustino Mrema amesema baadhi ya wagombea ambao wamedai kugombea nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho hawana historia yoyote ya chama hicho hivyo kushinda nafasi hiyo ni ndoto.

Mrema aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa Nifahamishe ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Alisema amekuwa akisikia kupitia vyombo vya habari kuwa wapo watu ambao wametangaza nia ya kugombea nafasi hiyo ya Uenyekiti lakini ukweli utabakia pale pale kuwa hamna zaidi ya Mrema.

Mwenyekiti huyo wa TLP alisema watu kujitokeza kugombea nafasi yoyote ni haki yao ya msingi na ndiyo demokrasi ya kweli lakini wagombea hao watakuwa wasindikizaji.

Mrema alisema pamoja na kuwa suala la wao kugombea nafasi ni haki yao ya msingi wajumbe wa mkutano huo ndio wataweza kutoa maamuzi juu ya nani anafaa kuwaongoza hivyo anawaachia wao waamue.

Alisema katika uchaguzi huo ambao unatarajiwa kufanyika Aprili 19 jijini Dar es Salaam anaamini kuwa wajumbe wa chama hicho watakuwa makini ili kukiendelezea chama na sio kukiweka rehani.

"Ni kesho kutwa Aprili 19 jibu litapatikana na hao wote ambao wanadai kuwa wana uwezo wa kushindana na mimi wataona matokeo," alisema.

Source: Nifahamishe.com
angelulizwa G.Liundi huyu mzee ni nani katika upinzani na kajakutafuta nini?
 
Hapana siyo mkorogo Mrema ni mgojwa ansumbuliwa na kisukari muda mrefu nadhani ndo inamsababishia ngozi kubabuka, atumie mkorogo wa nini?
 
Mimi naona Mrema anataka kufia kwenye kutafuta kura 2010,mtu kesha chakaa hivyo anatafuta nini kwenye siasa badala ya kutulia kulea wajukuu,mimi naona anatumiwa tuu kutokana na njaa zake sasa ya kutokuwa na ruzuku.Mrema hafai hata kuwa kiongozi wa TLP tena kama kweli TLP ina nia ya kujijenga.Pia asitarajie ubunge kwa Alois Kimaro mzalendo anayepambana na ufisadi.Anayemtumia Mrema ndio huyo huyo anamtumia Makalla wanafaziliwa na mafisadi ili wawaweke vibaraka wao kwenye nafasi mbalimbali ili wawe nyuma yao kufanya ufisadi wao.JK anawajua lakini anaogopa kwani aliingizwa madarakani kwa utapeli pia.Wana JF chondechonde tuwaelimishe watanzania kuhusu njama hii ya kuiteka nchi yetu kwa kutumia fedha walizotuibia.
 
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Kilimanjaro, Philemon Ndesamburo, amesema Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, amepoteza sifa za kujenga chama na kumtaka apumzike katika masuala ya kiuongozi na abaki kuwa mshauri tu.

Akizungumza katika mikutano ya hadhara ya Operesheni Sangara katika Jimbo la Vunjo, Ndesamburo alisema Mrema amekuwa akihamahama vyama kwa lengo la kuvidhoofisha kisiasa ili CCM iendelee kuongoza nchi.

“Mrema si kiongozi makini na ni myumbishaji mkubwa wa upinzani…yuko kwenye upinzani kwa maslahi ya CCM,” alisema Ndesamburo.

Alitolea mfano mwaka 1995 wakati Mrema anahamia NCCR-Mageuzi wakati huo ikiongozwa na Mabere Marando, chama hicho kilipata wabunge 16 ambao baadaye katika uchaguzi wa mwaka 2000 NCCR ilipoteza viti vyote.

Alisema baada ya Mrema kudaiwa kutaka kukiuka chama cha NCCR, alijiondoa na kuhamia TLP ambacho kilikuwa na viti vinne katika uchaguzi wa mwaka 2000, kikashuka na kupata kiti kimoja cha ubunge katika Jimbo la Biharamulo ambapo Mbunge wake, Fares Kabuye, alifunguliwa kesi ya kupinga kuchaguliwa kwake.

Ndesamburo alisema awali Mrema alifanya jitihada za kuwarubuni wananchi wakahama CHADEMA, wakiamini ni kiongozi mzuri ambaye anaweza kuongoza.

Alisema Mrema hawezi kusema anajenga chama wakati ndiye anachangia kwa kiasi kikubwa kumaliza nguvu ya vyama vya upinzani nchini. Hivi sasa CHADEMA ni chama chenye nguvu nchini ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa, na kwamba kimejiongezea idadi ya wabunge katika Bunge la Tanzania wanaowatetea wananchi hivi sasa.

Alisema umefika wakati kwa wananchi kukiunga mkono CHADEMA kutokana na mchango wake katika jitihada za kutaka kubadili maisha ya Watanzania, ambao rasilimali zao za nchi haziwasaidii na wanabaki kuwa watumwa katika nchi yao.
 
Huyo ndesamburo ndiye anayewafanya wakazi wa moshi kuishi kwa shida na wengi kuhama mkoa kutokana na mkandamizo wa chama tawala. akitaka awashawishi wananchi wa tz kuiondoa ccm madarakani!
 
Huyo ndesamburo ndiye anayewafanya wakazi wa moshi kuishi kwa shida na wengi kuhama mkoa kutokana na mkandamizo wa chama tawala. akitaka awashawishi wananchi wa tz kuiondoa ccm madarakani!

Ndesamburo si vyepesi kumtoa Moshi.
Huyu anawajali sana wapiga kura wake. Shida kama sipo zinaletwa na SISI Mijizi aka SISI Mafisadi . Wakizile chama cha mapinduzi na wachague moja kwa moja Chadema. Wasipokubali maumivu yatakuwa kwa wote. Wenye viherehere na SISI M na vyama vya siasa vingine pia.
 
Ndesamburo si vyepesi kumtoa Moshi.
Huyu anawajali sana wapiga kura wake. Shida kama sipo zinaletwa na SISI Mijizi aka SISI Mafisadi . Wakizile chama cha mapinduzi na wachague moja kwa moja Chadema. Wasipokubali maumivu yatakuwa kwa wote. Wenye viherehere na SISI M na vyama vya siasa vingine pia.

Your absolutely right.
 
Mrema ni mwanasiasa mkongwe nchini ambeye amechangia kwa namna moja au nyingine kuukomaza upinzani.Lakini kwa yeyote anayesoma vizuri alama za nyakati atagundua kuwa siasa za Tanzania zimebadilika hivyo zinahitaji wanasiasa wenye nguvu za kueneza siasa za sera ya vyama vyao.Mrema ameanza kubadilika kwenye uchaguzi wa Tarime na hadi leo msimamo wake haueleweki.Hata kwenye chama chake ni vurugu tupu,yeye ni Mzee aliyetakiwa awaachie chama vijana kama walivyofanya akina Mtei,Makani na wengineo.Sasa kwa namna anavyoendesha siasa zake si ni kama anatumiwa ili kuwavuruga wapinzani na hatimaye kuwapa mwanya mafisadi na kuinyima nchi yetu uongozi makini?Ngoja kwanza niishie hapa,wana JF mnaonaje?
 
Nadhani ni haki yake kama mwanachama wa TLP kugombea kwa muda wowote kama katiba ya TLP ilivyo haina kikomo cha uongozi. Kuhusu wanasiasa wenye nguvu za kueneza sera, nadhani wako katika mchakato wa uchaguzi sasa, kama watamuona amechoka na ni muda wa kupumzika watampumzisha kidemokrasia, kama watamuona anafaa ni juu yao kumchagua. Hili la kuvuruga upinzani siwezi kubali ama kataa, lakini na vyama vya upinzani lazima vijue palipo ushindani kuna mapandikizi.
 
Mrema, Mabere Marando, Lwamwai na wengine wanaofanana na hao walipandikizwa katika vyama vya upinzani ili wavimalize... Wale wengine walichoka kutukanwa na kudhalilishwa wameamua kurudi walikotoka.

Huyu jamaa sijui bado anatafuta nini? Hata anachosema siku hizi hakieleweki! Labda TLP wanamwelewa... tusubiri tuone
 
Mrema, Mabere Marando, Lwamwai na wengine wanaofanana na hao walipandikizwa katika vyama vya upinzani ili wavimalize... Wale wengine walichoka kutukanwa na kudhalilishwa wameamua kurudi walikotoka.

Huyu jamaa sijui bado anatafuta nini? Hata anachosema siku hizi hakieleweki! Labda TLP wanamwelewa... tusubiri tuone

Mundu,
Ni kweli kabisa ulichosema. Mrema na Marando wote ni watumishi wa usalama wa taifa na nasikia hiyo kazi huwa haiachwi hivihivi vinginevyo wanakuua maana ubebea siri nzito za nchi. Kama mtakumbuka kulikuwa na kipindi cha "wako wapi" kilichokuwa kikirushwa na TVT (now TBC1) huko nyuma walimtembelea bibi mmoja ambaye yuko kwenye nembo ya taifa aliyeshikilia pembe upande wake alieza mambo mazito sana ikiwemo jinsi yeye alivyopandikizwa kwenye vyama vya upizani miaka ya 50s/60s na kuanza kuwatukana akina Nyerere na TANU na wapinzani wakaona wamepata mtu mpaka alipowavuruga na kuvimaliza nguvu vyama vya upinzani. Hiki ndo anachofanya Mrema kwa sasa. Huyu ni CCM damu damu yuko kuharibu wapinzani tu na hana la maana lolote analolifanya.
 
Ili kumfahamu Mrema anamtumikia nani, nadhani ni vyema tufahamu vyanzo vyake vya mapato ya kujikimu kimaisha vinatoka wapi? maana hakuna biashara ya wazi tunayoifahamu inayoendeshwa na Mrema na sidhani kama katiba ya TLP inakipengele cha kumlipa mshahara mwenyekiti.
Tunafahamu kuwa wapo watu wanalipwa katika payroll za siri, Jee Mzee wa Kiraracha ni miongoni mwao?
 
Back
Top Bottom