The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

Mag3,
As a politician I believe Mrema is a man who's time has come and gone. Tanzania tunahitaji uongozi unao "inspire" si kupikapika majungu tu. We have so much to learn from the Obama phenomenon.

Umemaliza, asante sana kwa ukweli.
 
Haya mambo ya Mrema niliyaeleza toka mwaka jana, watu humu wanakinishambulia sana!
PM

Mkuu si wewe peke yako, tuko wengi ambao tulijaribu hapo nyuma kutoa tahadhari lakini hayo makombora yaliyoelekezwa kwangu !! Mrema ni mtu atakayekumbukwa kwa kuwapa watu vilema vya maisha akijaribu kuzuia tsunami ya mageuzi mwaka 1992. Alipoona hatari ya kutoswa na CCM, alikubali kuwa pandikizi na mlolongo wa mafanikio yake katika kuua upinzani ni mrefu. Siku Bwana C. Liundi atakapoamua kuongea, tutaweza kujua kwa nini akina mama na heshima zao walikuwa tayari kujivua nguo na kulala barabarani - kisa ? kumtetea Mrema (duniani kuna mambo).

Sasa ngoja nisubiri nitakavyoshambuliwa na waliojaa Mremamania - wako wengi humu, karibuni.
 
Pamoja na yote aliyoyafanya Mrema, Mutungurehi bado ni mwanachama halali wa TLP na ni Katibu Mwenezi, kwa sababu zoezi zima limekiuka Katiba ya TLP, na kama kweli wajumbe waliridhia, basi TLP hakuna Chama.

Kwa kufuata principles of natural justice, 'No one is condemmed unheard', Mrema alipaswa kumuelekeza Katibu Mkuu wake kuitisha Kikao cha dharura cha Secretarieti ya Nec ya TLP na kuwasilisha agenda hiyo ya kumfukuza Mutungurehi, azmio la secretarieti hiyo ndilo lenye mamlaka ya kuitisha kikao cha dharura cha Nec ya TLP na kuijadili hiyo ajenda iliyo mbele yake, halafu Mutungurehi, angepaswa kuitwa na kuhojiwa kabla ya kufukuzwa. Hata kama angekataa, basi mamlaka ya kikao hicho ni kumsimamisha uanachama na kupeleka azimio hilo Mkutano Mkuu ambao ndio wenye mamlaka ya kikatiba ya kufanya hivyo.

Mrema yeye ndiye Mwenyekiti wa TLP, na Katibu ndiye Yeye, Kamati Kuu ni Yeye, Sectarieti ya TLP pia yeye, Halmashauri Kuu ni yeye na amejifanya pia ndiye Mkutano Mkuu kumfukuza Katibu Mwenezi ili awe yeye!. Huu ni udikiteta wa hali wa juu na naamini Msajili wa vyama halalifumbia macho hili, yaani chama chote kiko mfukoni!.

Niliwahi kusema mahali huko nyuma, Mrema is gone case na spent force, hana jipya na siku zake zimekwisha, anasubiri kusukumwa tuu na kuanguka kama unamsukuma mlevi.





Secretarieti
 
Mrema kafanya tathmini na kugundua kuwa akisimama na Mutungirehi hawezi pata upenyo. Juhudi zake za sasa ni kuhakikisha kuwa anakuwa mgombea pekee wa uenyekiti. Kuna chaguzi alizojaribu kuzisimamisha kwenye baadhi ya mikoa bila mafanikio. Tusubiri tuone kama kwa njia hizi za kimafia atafanikiwa.
 
Mrema amefirisika siku nyingi kimwili na kiakili, na kama kweli kuna wajumbe ndani ya TLP hadi leo bado wanamwamini na kubariki maono yake... Sijui hao wako katika hali gani.

Habari ambayo napenda kuieleza hapa ni ya huyu Mutungirehi. Huyu ni kibaraka na mtu asiye na fadhila kwa watu au wananchi wanaomuamini na kumchagua. Nakumbuka katikati ya miaka ya 90 pale chuo kikuu cha DSM, jamaa huyu alikuwa ni Rais wa Daruso. kwa maneno yake matamu na mifano na changamoto hai, aliweza kushinda kwa kishindo uchaguzi wa Daruso na kusimikwa Urais.

Haikupita hata miezi mitatu, jamaa akaanza kubadilika na kuacha kuyasimamia yale yaliyomfanya achaguliwe na kuanza kufifisha kwa makusudi juhudi za wanafunzi kudai haki zao.

Ndipo alipoondolewa na kuvuliwa Urais kwa demokrasia na wanafunzi pale Nkrumah kwa mateke na mangumi. Nadhani wengi wenu humu kama mlikuwepo pale Nkrumah siku ile, mtakuwa bado mnakumbuka kisago kile.

Mutungirehi alinunuliwa kwa vihela vichache na visafari vya nje na kuwasaliti wanazuoni waliomchagua. Mie siwezi kumsahau msaliti huyu, na nasema hafai kuongoza chama chochote cha kijamii!!!
 
Mrema akiondoka TLP utakuwa ndio mwisho wa chama chenyewe, Mrema amegeuzwa tingatinga la kusafishia watu njia....The guy worked harder for his country and the people. Mambo anayolalamikia Dr. Slaa leo Mrema aliyaanza 15 years ago lakini masiki mrema hakupata support, mabomu yake watu waliyabeza na kumuona kichaa mafisadi yakadi kuchimbia...baada ya mafisadi kuiburuza nchi kwa sana na wananchi kusota, ndio sasa wanaanza funua shuka (wakiwa bado kitandani). The man is very strong and practical lakini mtazamo duni wa watu ndio umechangia kumuangusha. Acha awapeleke Kikomunist hao wa TLP, demokisia wakati mwingine is not useful...Bongo watu huwa wanasubiri mtu atangeneze kitu, kikisha kaa sawa na ulaji ukaongezeka mh, ugomvi unanza hapo hapo.....Vyama vyote kila kukicha migogoro, serikalini migogoro, dini na vyuo migogoro, wakulima na wafugaji migogoro, muungano migogoro and u expect maendeleo hapo? forget.
 
Jamani mimi nikifikiri zaidi ya hapo naona hizi ndizo siasa za nchi yetu, hivi kiujumla kunatofauti gani alichofanya Mrema na kauli za wana CCCM "2010 ni Kikwete tu!, Mwacheni JK amalizie miaka yake 10!, Ataempinga Kikwete 2010 kukiona!" na matakataka mengi tu!?
Hamna tofauti, hakuna demokrasia ya kweli kwenye vyama vyetu, na hii ndiyo inatuletea 'watawala wabovu' nchini kwetu.
 
Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema ameitisha kikao cha ghafla cha NEC ya chama hicho na kumtimua kwenye chama hasimu wake na mshindani wake katika nafasi ya uenyekiti ya chama hicho, Benedict Mutungirehi. Awali kikao hicho cha Halmashauri kuu kilipangwa kufanyika tarehe 18 Aprili siku moja kabla ya mkutano mkuu wa chama hicho, lakini Mrema akameitisha jana na leo kikao cha dharura na kuwalipia wajumbe gharama zote yeye mwenyewe kwa fedha za mfukoni. Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wajumbe 60 bila kuwa na ajenda nyingine yoyote Mrema alitumia fursa hiyo pia kutangaza maandalizi ya mkutano mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Aprili katika ukumbi ambao mpaka sasa ni siri. Mrema aliwatangazia wajumbe kuwa msajili wa vyama vya siasa amekubali kwamba chama hicho kinaweza kupunguza wajumbe wa mkutano huo kutoka 1407 wanaopaswa kufkisha akidi kwa mujibu wa katiba ya chama hicho mpaka wajumbe 163 ambayo ilipunguzwa kwa azimio la kikao cha Halmashauri kuu ya chama hicho.

...........ndiyohiyo
Hii inaitwa 'Controlled Democracy'

Lyatonga ni mpiganaji na kazi yake tunaitambua na kuikubali lakini hili la Mutungirehi litampa tabu sana kulimaliza. Huyu jamaa hafukuziki! Wale waliokuwa Mlimani miaka ya '90 watakumbuka jinsi wanafunzi walivyopata taabu kumwondoa kwenye uraisi wa DARUSO hadi kuwatoa kafara baadhi yao katika mgomo ulifuatia sakata hilo.

Hii sinema ndio kwanza inaaza, mpaka watakopomalizana tutaona mengi!
 
Huyu Mzee arudi kwao Moshi akagombee ubunge huu uongozi awaachie vijana
 
Huyu Mzee arudi kwao Moshi akagombee ubunge huu uongozi awaachie vijana

Nakubaliana na wewe Augustino Lyatonga ameshachoka, kila anapoenda yeye ni maugomvi tu,Halafu anataka kuwa Rais! Urais hauvuliwi kama samaki, Huu ni UDIKTETA kabisa. Arudi Kilalacha tu akamalizie muda wake uliobaki.
 
Augustino Amechoka lakini Mutungirehi naye mmmh! nikikumbuka aliyoyafanya kabla ya kuondolewa kwa nguvu pale Nkrumah -UDSM 1994 sidhani kama anaaminika kuchukua jukumu zito la kuongoza jahazi la chama. Ni bora watafute Damu mpya kabisa.
 
Wafuatao ni baadhi tu ya waliowahi kukatiza anga za Augustine Lyatonga Mrema, na bado wengi watafuatia mpaka siku atakapoamua kurudi kundini - kwa mafisadi wenzake.

Chiku Abwao
Prince Bagenda
Harold Jafu
Mohammed Tao
Msafiri Mtemelwa
Juma Kilimba
Abbas Mtemvu
Mustapha Wandwi
Thomas Ngawaiya
Sheik Ali Iddi
Sheikh Mtopea
Dk. Masumbuko Lamwai
Makongoro Nyerere
Steven Wasira
Ndimara Tegambwage
Rev. Kasyupa
Benedict Mutungirehi
Leo Lekamwa
Mabere Marando
Joram Kinanda

Vifuatavyo ni vyama vya Siasa vinavyojaribu navyo:-

NCCR - Mageuzi
CUF
Chadema

Mzee wa Kiraracha si mchezo - na bado !!
 
Huyu mzee nilimsapoti sana kuwa urais mwaka 1995 na ndiye mgombea pekee wa kiti hicho aliyeitetemesha CCM huku Bara hadi sasa. Lakini sasa hivi nikitizama nyuma, naona pengine mimi na mamilioni wengine waliompigia kura tulifanya makosa, kwani inavyoelekea, kama angeupata, hadi sasa angekuwa bado rais -- katiba ingebadilishwa kwa kuondoa ukomo wa vipindi. Angeanza ku-develop na kuwa kama akina Mzee Bob wa zimbabwe, Museveni, Kagame, Bongo, Biya, Bouteflika na wengine.

Kwa hilo Mola alitunusuru.
 
Mrema aahh aahh Mrema...mrema ee
Mrema aahh aahh Mrema
Mrema Sokoine...

Mkuu invisible tuwekee na hii kwenye zilipendwa tafadhali!
 
Jamani mimi nikifikiri zaidi ya hapo naona hizi ndizo siasa za nchi yetu, hivi kiujumla kunatofauti gani alichofanya Mrema na kauli za wana CCCM "2010 ni Kikwete tu!, Mwacheni JK amalizie miaka yake 10!, Ataempinga Kikwete 2010 kukiona!" na matakataka mengi tu!?
Hamna tofauti, hakuna demokrasia ya kweli kwenye vyama vyetu, na hii ndiyo inatuletea 'watawala wabovu' nchini kwetu.


Ndugu yangu mawazo ya wachache waliofirisika kisiasa ccm yasikufanye ukate tamaa,siasa ndivyo ilivyo si hapa tu hata nchi nyingine, kinachotakiwa mimi na wewe na wengine tutambue wajibu wetu wa kuchagua kiongozi bora na si bora kiongozi,mambo mengine yote hayo unayoyasikia kutoka kwa waliofirisika mawazo will die a natural death.
 
Mzee umenikumbusha mbali. Nawaza ndo maana mrema hataki kumuachia japo nafasi ya kujinadi, kwani anaweza kumdondosha iwapo wakisimama wawili kujinadi.
 
Kama demokrasia yenyewe ya vyama vyetu vya siasa ni hii ya Mrema na tulivyoona Lipumba alivyompiga vita prof.Safari tutafika kweli? Mtu umeshagombea Uraisi mara 2 au 3 kaa pembeni waachie wengine labda watafanya vizuri zaidi yako.
 
Huyu ni kuwadi wa ccm kazi yake moja tu. kutibua vyama vya upinzani baasss.
 
Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema amekiri, kwamba Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kina utaratibu mzuri wa kuandaa wagombea wake katika nyadhifa za juu ukiwamo urais. Mrema alisema hayo jana kwenye mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania kilichorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) .

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, suala la mtafaruku ndani ya TLP, si la yeye kung’ang’ania madaraka, bali inapokuwa chama hakijaandaa mgombea madhubuti atakayeweza kuwa mtetezi mkubwa wa chama hicho, ndipo suala hilo linapojitokeza.

“Watu wanaandaliwa, kama watu wa CCM, unawasikia kuwa mwaka 2010 ni Kikwete tu, wana utaratibu … wanaandaa, hawaendi kiholela ili mradi tu umechukua fomu sijui nani …na wanajua kazi aliyofanya Kikwete na wameridhika,” alisema Mrema na kuongeza: “Wao wanafikiri kwamba si kazi ya kubughudhi tena kwa sasa … wanatamka hivyo na kwa jambo hilo huwezi kusema hiyo si demokrasia ama huo ni udikteka,” alisema Mrema.

Alishangazwa kuona wakati CCM ikijipanga vizuri namna ya kuachiana madaraka, vyama vya Upinzani hususan chama chake, jambo hilo ni tofauti kiasi cha kufikia kuwapo mtafaruku mkubwa wa kuwania madaraka. Hata hivyo alisema, hang’ang’anii madaraka ya kuwa mwenyekiti wa chama hicho, bali hakuna mwanachama madhubuti kwa sasa aliyeandaliwa kukiongoza vyema chama hicho. “Akiandaliwa mtu sawa … nimewaambia Halmashauri Kuu ya Chama, kwamba sing’ang’anii uenyekiti … watu wanaandaliwa kushika nyadhifa hizi,” alisema Mrema na kuongeza:

“Mnataka Mrema aondoke … haondoki mtu mpaka chama hiki kijengwe na nijue nitamwachia nani, siwezi kukiacha chama changu barabarani, haiwezekani.” Akizungumzia nia yake ya kugombea ubunge mwakani Moshi Vijijini kwa tiketi ya TLP, alisema atafanya hivyo kutokana na kuombwa na wananchi wa jimbo hilo. Hivi sasa Moshi Vijijini inawakilishwa na Dk. Cyril Chami wa CCM ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko.

.......ndiyohiyo
 
Kilichobaki kurudi tu sasa, na kupewa makombo ya mezani kama wenzako.
 
Back
Top Bottom