The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema amekiri, kwamba Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kina utaratibu mzuri wa kuandaa wagombea wake katika nyadhifa za juu ukiwamo urais. Mrema alisema hayo jana kwenye mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania kilichorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) .

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, suala la mtafaruku ndani ya TLP, si la yeye kung’ang’ania madaraka, bali inapokuwa chama hakijaandaa mgombea madhubuti atakayeweza kuwa mtetezi mkubwa wa chama hicho, ndipo suala hilo linapojitokeza.

“Watu wanaandaliwa, kama watu wa CCM, unawasikia kuwa mwaka 2010 ni Kikwete tu, wana utaratibu … wanaandaa, hawaendi kiholela ili mradi tu umechukua fomu sijui nani …na wanajua kazi aliyofanya Kikwete na wameridhika,” alisema Mrema na kuongeza: “Wao wanafikiri kwamba si kazi ya kubughudhi tena kwa sasa … wanatamka hivyo na kwa jambo hilo huwezi kusema hiyo si demokrasia ama huo ni udikteka,” alisema Mrema.

Alishangazwa kuona wakati CCM ikijipanga vizuri namna ya kuachiana madaraka, vyama vya Upinzani hususan chama chake, jambo hilo ni tofauti kiasi cha kufikia kuwapo mtafaruku mkubwa wa kuwania madaraka. Hata hivyo alisema, hang’ang’anii madaraka ya kuwa mwenyekiti wa chama hicho, bali hakuna mwanachama madhubuti kwa sasa aliyeandaliwa kukiongoza vyema chama hicho. “Akiandaliwa mtu sawa … nimewaambia Halmashauri Kuu ya Chama, kwamba sing’ang’anii uenyekiti … watu wanaandaliwa kushika nyadhifa hizi,” alisema Mrema na kuongeza:

“Mnataka Mrema aondoke … haondoki mtu mpaka chama hiki kijengwe na nijue nitamwachia nani, siwezi kukiacha chama changu barabarani, haiwezekani.” Akizungumzia nia yake ya kugombea ubunge mwakani Moshi Vijijini kwa tiketi ya TLP, alisema atafanya hivyo kutokana na kuombwa na wananchi wa jimbo hilo. Hivi sasa Moshi Vijijini inawakilishwa na Dk. Cyril Chami wa CCM ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko.

.......ndiyohiyo
Nafikiri siyo kweli anayosema ndg yangu Mrema mbona ulikiacha NCCR-Mageuzi
hata TLP unaweza kuacha/stepdown uwaachie wengine waongoze kisha nyie wazee wa siku nyingi muwe washauri wa vijana/damu mpya.
 
"Watu wanaandaliwa, kama watu wa CCM, unawasikia kuwa mwaka 2010 ni Kikwete tu, wana utaratibu … wanaandaa, hawaendi kiholela ili mradi tu umechukua fomu sijui nani …na wanajua kazi aliyofanya Kikwete na wameridhika," alisema Mrema na kuongeza: "Wao wanafikiri kwamba si kazi ya kubughudhi tena kwa sasa … wanatamka hivyo na kwa jambo hilo huwezi kusema hiyo si demokrasia ama huo ni udikteka," alisema Mrema.
Duh, ama kweli Mrema kachoka! yaani anaanza siasa za Mugabe?.. hivi ni nani aliyetakiwa kuandaa mgombea TLP kama sii kazi yake yeye.. Kwani yeye aliandaliwa na nani vile, maanake mimi sikumbuki Mrema kupitia mafunzo ama maandalizi ya kuwa rais..
 
'Acheni ukweli uitwe ukweli'

Hongera Mh Mrema kwa kusema yale yaliyo ya kweli.
 
- Ndio maana mara nyingi mimi huwa ninauliza kwamba kiongozi wa Upinzani anakuwaje powerful na kuogopwa ndani ya chama cha upinzani?

- Hana jeshi, hana nguvu ya dola, hana polisi, sasa kwa nini anakuwa na nguvu sana ndani ya chama chake? Sasa kwa maneno haya ya Mrema ndio unapata jawabu la swali langu,

- kumbe huwa wanategemea CCM.

Respect.

FMES!
 
Duh, ama kweli Mrema kachoka! yaani anaanza siasa za Mugabe?.. hivi ni nani aliyetakiwa kuandaa mgombea TLP kama sii kazi yake yeye.. Kwani yeye aliandaliwa na nani vile, maanake mimi sikumbuki Mrema kupitia mafunzo ama maandalizi ya kuwa rais..


Wanagombea ruzuku tu. Vyama vikinyimwa ruzuku itabidi wenye personality waongoze na utitiri wa vyama kupungua/
 
Mrema a "Fallen Hero"; ni fundisho kubwa sana kwa wale wanaokuja; usibishane na system iliyokuweka. Fikiria, alipoiona ile "dhahabu" pale uwanja wa ndege na kujua ni ya nani na kunyamaza yasingemkuta haya! Masikini! Hawaoni wenzie waliochagua kunyamaza wanavyokula pension! Think Mrema was at a level of PM; and now? He thought he was fighting for the people and now things have changed the very people are fighting him! This is vanity and striving after wind!!
 
- Ndio maana mara nyingi mimi huwa ninauliza kwamba kiongozi wa Upinzani anakuwaje powerful na kuogopwa ndani ya chama cha upinzani?

- Hana jeshi, hana nguvu ya dola, hana polisi, sasa kwa nini anakuwa na nguvu sana ndani ya chama chake? Sasa kwa maneno haya ya Mrema ndio unapata jawabu la swali langu,

- kumbe huwa wanategemea CCM.

Respect.

FMES!

Jamani vyama vya siasa vya upinzani haviko sawa. Kuna vyama vya mtu binafsi kama DP, CHAUSTA, TLP nk halafu kuna vyama vya umma kama CHADEMA na CUF. Kwa hiyo muwe mnatofautisha mnapojadili. Kundi la kwanza la vyama na hilo la pili ni kama mbingu na ardhi!

Asha
 
Dalili za mvua ni mawingu mtakuja sikia jamaa karudi kwa baba CCM ndicho kilicho mlea.
 
Jamani vyama vya siasa vya upinzani haviko sawa. Kuna vyama vya mtu binafsi kama DP, CHAUSTA, TLP nk halafu kuna vyama vya umma kama CHADEMA na CUF. Kwa hiyo muwe mnatofautisha mnapojadili. Kundi la kwanza la vyama na hilo la pili ni kama mbingu na ardhi!

Asha

Dada Asha hata CHADEMA ni cha watu binafsi.
Mwenyekiti wa kwanza CHADEMA alikuwa mzee Edwin Mtei kutoka mkoa wa Kilimanjaro unaweza kunipatia maelezo ya kina ni kwanini mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA ni Mheshimiwa Freeman Mbowe naye anatoka mkoa wa Kilimanjaro ambaye atamwita mzee Mtei baba mkwe ?.

Tusitake kudanganyana vyama vyote vya upinzani vina mapungufu makubwa katika suala zima la demokrasia ukivilinganisha na CCM.

CHADEMA imeelemea zaidi kanda ya kaskazini labda kutokana na historia ya mwanzilishi wake mzee Edwin Mtei.
 
Dada Asha hata CHADEMA ni cha watu binafsi.
Mwenyekiti wa kwanza CHADEMA alikuwa mzee Edwin Mtei kutoka mkoa wa Kilimanjaro unaweza kunipatia maelezo ya kina ni kwanini mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA ni Mheshimiwa Freeman Mbowe naye anatoka mkoa wa Kilimanjaro ambaye atamwita mzee Mtei baba mkwe ?.

Tusitake kudanganyana vyama vyote vya upinzani vina mapungufu makubwa katika suala zima la demokrasia ukivilinganisha na CCM.

CHADEMA imeelemea zaidi kanda ya kaskazini labda kutokana na historia ya mwanzilishi wake mzee Edwin Mtei.

Unaanza uchokozi wako Ngogo. Asante, maelezo ni kwamba Mtei yeye aliasisi chama, na Mbowe amechaguliwa na wajumbe miaka karibu kumi baadae, wakati Mtei akiwa hayuko madarakani. Mbona hujasema chama ni cha wasukuma baada ya kutoka Mtei kuwa mwenyekiti wa CHADEMA na akafuatia Makani kuwa Mwenyekiti? Kama kingekuwa chama cha familia si angefuatia mtoto au mke wa Mtei? Hayo ya ukwe mi nitayajuaje, pengine baada ya Mbowe kuwa karibu na Mtei kwenye siasa ndio akapata kumwona mtoto wa Mtei na kumuuoa! Mi siyajui hayo. Mbowe angekuwa mtoto wa Mtei hapo tungepiga kelele kama angeteuliwa na Mtei mwenyewe. Lakini Mbowe si mtoto wa Mtei na Mbowe hakumfuatia Mtei, amemfuata Makani.

Sasa tuje CCM; kwa hiyo tuseme CCM Zanzibar ni chama cha familia? Maana amekufa Karume kule Zanzibar amekuja tena mwanae Karume hivi sasa!

Au tuseme CCM ni chama cha familia kwa sababu Nyerere kafa na sasa mwanae Makongoro ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara wakati baba yake aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa?

Au tuseme basi serikali ya CCM ni ya familia kwa sababu Sitta ni Spika na Mkewe ni Waziri katika serikali hiyo hiyo!

We unasema CCM ina demokrasia kuliko vyama vingine. Hebu kawaulize Malecela na Dr Salim Ahmed Salim!

Huwezi kabisa kufananisha TLP na CHADEMA kuhusu demokrasia. Ni kama kufananisha shubiri na asali

Asha
 
Nadhani Mrema akiri kitu kimoja kuwa, yeye kama mwenyekiti wa chama alitakiwa kuwa mfano wa kukibadili kiwe katika mfumo mzuri zaidi hata ya huo wa CCM.

Hii ni dalili ya kuchemsha kabisa. Unapokuwa na mshindani, ukaona ana mbinu flani ambazo unakiri ni nzuri katika uendeshaji wa chombo husika, basi huna budi (hasa kwa nafasi ya mwenyekiti) kuleta mabadiliko ya kweli na kuonyesha ukomavu wako katika nyanja husika kumzidi mpinzani wako.

Katika hili, napata wasiwasi na uenyekiti wa Mrema. Hata anvyoendesha chama ni kiubabe sana. Anatakiwa kukiri kushindwa, anatakiwa kuachia nafasi aliyo nayo kwa wazalendo (ambao ni wengi) wanaoweza kuleta mabadiliko. Very sad!

Binafsi, sifurahishwi na viongozi aina ya Mrema, pamoja na uwezo wake kiutendaji lakini kiuongozi anaonekana hataki washauri. Vyama vya upinzani (vyote) vinatakiwa kuwa na washauri ambao ni watu wenye hekima na mitizamo (vision) mikubwa kwa maslahi ya taifa. Wengi katika vyama hivi wanaonekana wazi hata wanapoongea wanakuwa hawajawasiliana na washauri wao au hawana washauri kabisa.

Upinzani ni muhimu kwa maendeleo ya taifa letu.
 
Hatimaye yule mwanasiasa machachari wa miaka ya tisini amekosa hata mbunge mmoja ktk bunge la Tanzania.

Ule Msemo,SIASA NI KIINI MACHO umetimia,hainingii akilini mwanasiasa huyu alivokuwa mashuhuri,anapendwa na watu wengi ktk historia hii leo hana mfuasi.

Alipendwa na wengi kiasi kwamba hata mkuu jk&mwl hawakufua dafu.

Ktk thread hii,tuangalie kupanda na kushuka kwake,na nini fundisho ktk wanasiasa wanaochipukia na hasa ktk suala la kuhama hama vyama ovyo.

<<NAWAKILISHA>>
 
Alikuwa hana mikakati na tena hakujengwa kitaasisi zaidi kwani alitegemea umaarufu wake na siasa. Kuna Kizazi Kipya siku hizi na tena anaonekana kuwa ni mbabe mbele za watu wengine na asiye jifunza jipya.
 
Huyo mzee nampa heko kwa kukuza mageuzi nchini, lakini tungemchagua kuwa Rais wa nchi tungejuta kuwa Watanzania. Mzee huyu ni mroho wa madaraka pengine kuliko Mugabe. Mrema angediriki hata kubadilisha katiba ili aendelee kutawala.

Hata huko TLP ilikuwa bora angatuke sasa na kubaki mshauri tu. Sasa hivi hana hoja, hana mvuto wa kisiasa kabisa. Ameweka kambi Biharamuro na kuishia kura chini ya 200. Kumbuka hilo ndo lilikuwa jimbo la chama chake.

Ameshangaza sana kuwatimua wagombea wenzake chama (Mtungirehi & ...) ili apite bila kupingwa. Hiyo ni laana ktk demokrasia. Mzee huyu apumzike sasa.
 
wakati umaarufu wake ukiongezeka yy alihangaika kujitafutia na kujiongezea maadui badala ya marafiki. Watu walioonekana wanaakili waliomzunguka aliwafukuza wote, kabaki peke yake.
 
Namfahamu Augustine Lyatonga Mrema tangu tukiwa wote watoto Marangu. Alihitimu kuwa Mwalimu, lakini baada ya kufundisha kwa muda mfupi,alijiunga na Idara ya Polisi (? Usalama wa Taifa).

Siasa aliingia seriously 1985 alipogombea na kuchaguliwa kuwakilisha Jimbo la Vunjo. Katika kipindi cha pili cha Rais Ali Hassan Mwinyi, Lyatonga aliteuliwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Enthusiasm yake ktk kushughulikia wahalifu, kwa kubuni hata kura za maoni za jamii ilimfanya Rais amteuwe "Naibu Waziri Mkuu", licha ya kwamba wadhifa huo haukuwa katika Katiba. Mrema alikuwa outspoken sana dhidi ya waliokuwa wamepora mashamba ya mkonge (?Chavda?). Ilipodhihirika kwamba alikuwa anataka publicity mno, Rais alimpeleka Wizara ya Kazi na Ustawi wa Jamii ambayo ilikuwa haina haiba kama wizara ya Mambo ya Ndani.

Licha ya kuwa Waziri wa Kazi, Mrema aliendelea na matamshi yake makali. Akiwa Bungeni ktk kipindi ambacho Bunge lilikuwa karibu lifikie kikomo na Uchaguzi Mkuu uandaliwe, alipinga muswada wa Serikali, na Rais Mwinyi akasitisha uteuzi wake kama waziri kwa kukiuka utamaduni wa Cabinet Solidarity.

Bunge lilipovunjwa Agosti 1995, Mrema akatangaza anajiondoa ktk Chama cha Mapinduzi. Vyama kadhaa vya siasa vya upinzani ambavyo ndio mara ya kwanza kuingia ktk kampeni za Uchaguzi Mkuu, vikaanza kumshawishi Mrema ajiunge navyo.

Mrema akaweka masharti kwamba angejiunga na Chama ambacho angekiongoza kama Mwenyekiti Taifa, na ambacho kingemteuwa kuwa Mgombea wa u-Rais ktk Uchaguzi Mkuu wa 1995. Mwishowe akajiunga na NCCR-Mageuzi, akichukua uenyekiti taifa kutoka kwa Mabere Marando, na kuteuliwa Mgombea wa u-Rais kwa tiketi ya NCCR.

Kampeni za Mrema 1995 zlikuwa na vituko vingi: Gari lake likisukumwa na vijana washabiki na Mrema akitandikiwa khanga atembee juu yake na wanawake walioshangilia. Mrema akiwa na uhakika angeshinda alianza kutoa vitisho kwa viongozi wa Serikali aliodai ni wala rushwa. Alitishia k.m. kwamba atamtia mbaroni Mwinyi,na kwamba wiki mbili baada ya kuingia Ikulu, "Mwinyi angekuwa anakunywa maji kwa karai huko Ukonga". Washauri wake walimwomba ku-tone down vitisho walipuuzwa.

Alipotembelea Baba wa Taifa, kijijini Butiama akiwa na timu yake ya kampeni Mkoani Mara, inasemekana Mwalimu alitamka "I shall never allow my country to be thrown to the dogs". Wana NCCR walidai Mwalimu aliwaita mbwa. Lakini baada ya hapo, Mwalimu alijitolea wazi wazi kumfanyia kampeni Benjamin Mkapa. Mrema akashindwa ingawa alipata asilimia 28 ya kura za u-Rais.

Kukosa fadhila kwa Mrema kulianza kujionyesha zaidi pale alipoanza kugombana na Mabere Marando. Mwisho akitaka kumfukuza Mabere toka NCCR, mambo yalimgeukia akatoka NCCR-Mageuzi na kujiunga na Tanzania Labour Party iliyokuwa inaongozwa na Lwekama. Ktk Tanzania Labour Party nako alikaribishwa kuwa Mwenyekiti Taifa. Lakini soon afterwards, mgogoro baina ya Mrema na viongozi wa awali wa T.L.P. ukaanza.

Uchaguzi Mkuu wa 2000, T.L.P. ikamsimamisha Mrema kama mgombea wao, lakini licha ya kukiimarisha chama, Mrema alikuwa mgombea wa tatu, Profesa Lipumba akichukua nafasi ya pili baada ya Mkapa. Hakujifunza kwa vile migogoro ndani ya T.L.P. iliendelea na ktk Uchaguzi Mkuu wa 2005, Mrema aliambulia kura chache sana kama mgombea wa U-Rais, chama chake kikipata kiti kimoja tu cha Ubunge huko Biharamulo Magharibi.

Mrema ameendelea kulumbana na wanachama viongozi ktk T.L.P. na mwaka huu alipokuwa na Mkutano Mkuu wa T.L.P., aliwafukuza wajumbe akabakia na wajumbe 163 tu, waliomchagua Mwenyekiti wa Taifa kwa miaka mitano ijayo. Tumeshuhudia kusambaratika kwa chama chake kule Biharamulo wiki iliyopita, ambako yeye mwenyewe alikwenda kumkampenia mgombea wake aliyeambulia kura 187, zikiwa ni asilimia 0.57 za kura zilizopigwa.

Mrema amechoka na amekwisha kisiasa. Bora arudi Kiraghacha, Marangu kunywa mbege. Tutamkaribisha.
 
Ninamkumbuka Mrema kama mbunge na waziri mwenye meno; alikuwa na uwezo wa kuuma tofauti na viongozi wetu wengi ambao ni wasanii tu majukwaani.

Afadhali kuongozwa na Mrema kuliko hawa waliopo sasa ambao wanashindwa kushughulikia hata mambo ambayo yako wazi mno.

Namshauri Mrema akagombee ubunge Vunjo, akifanya hivyo mimi nitamchangia hata kama ni laki moja tu, haitamsaidia sana lakini ni ishara ya kushukuru kwa kazi zake kubwa alizofanya huko nyuma kama mbunge na waziri.

Bila Mrema kuingia upinzani kabla ya uchaguzi wa 1995 huenda mpaka leo upinzani ungelikuwa hoi mno. Wale watu ambao Mrema aliwaonjesha harufu ya upinzani ndio hao ambao sasa wengi wako na vyama vingine vya upinzani.

Popote ninapomwona Mrema mimi huwa namvulia kofia. Anaweza kuwa hakusoma kama wengine lakini amefanya kazi kubwa kuliko hao wanasiasa maprofesa na madaktari wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom