Namfahamu Augustine Lyatonga Mrema tangu tukiwa wote watoto Marangu. Alihitimu kuwa Mwalimu, lakini baada ya kufundisha kwa muda mfupi,alijiunga na Idara ya Polisi (? Usalama wa Taifa).
Siasa aliingia seriously 1985 alipogombea na kuchaguliwa kuwakilisha Jimbo la Vunjo. Katika kipindi cha pili cha Rais Ali Hassan Mwinyi, Lyatonga aliteuliwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
Enthusiasm yake ktk kushughulikia wahalifu, kwa kubuni hata kura za maoni za jamii ilimfanya Rais amteuwe "Naibu Waziri Mkuu", licha ya kwamba wadhifa huo haukuwa katika Katiba. Mrema alikuwa outspoken sana dhidi ya waliokuwa wamepora mashamba ya mkonge (?Chavda?). Ilipodhihirika kwamba alikuwa anataka publicity mno, Rais alimpeleka Wizara ya Kazi na Ustawi wa Jamii ambayo ilikuwa haina haiba kama wizara ya Mambo ya Ndani.
Licha ya kuwa Waziri wa Kazi, Mrema aliendelea na matamshi yake makali. Akiwa Bungeni ktk kipindi ambacho Bunge lilikuwa karibu lifikie kikomo na Uchaguzi Mkuu uandaliwe, alipinga muswada wa Serikali, na Rais Mwinyi akasitisha uteuzi wake kama waziri kwa kukiuka utamaduni wa Cabinet Solidarity.
Bunge lilipovunjwa Agosti 1995, Mrema akatangaza anajiondoa ktk Chama cha Mapinduzi. Vyama kadhaa vya siasa vya upinzani ambavyo ndio mara ya kwanza kuingia ktk kampeni za Uchaguzi Mkuu, vikaanza kumshawishi Mrema ajiunge navyo.
Mrema akaweka masharti kwamba angejiunga na Chama ambacho angekiongoza kama Mwenyekiti Taifa, na ambacho kingemteuwa kuwa Mgombea wa u-Rais ktk Uchaguzi Mkuu wa 1995. Mwishowe akajiunga na NCCR-Mageuzi, akichukua uenyekiti taifa kutoka kwa Mabere Marando, na kuteuliwa Mgombea wa u-Rais kwa tiketi ya NCCR.
Kampeni za Mrema 1995 zlikuwa na vituko vingi: Gari lake likisukumwa na vijana washabiki na Mrema akitandikiwa khanga atembee juu yake na wanawake walioshangilia. Mrema akiwa na uhakika angeshinda alianza kutoa vitisho kwa viongozi wa Serikali aliodai ni wala rushwa. Alitishia k.m. kwamba atamtia mbaroni Mwinyi,na kwamba wiki mbili baada ya kuingia Ikulu, "Mwinyi angekuwa anakunywa maji kwa karai huko Ukonga". Washauri wake walimwomba ku-tone down vitisho walipuuzwa.
Alipotembelea Baba wa Taifa, kijijini Butiama akiwa na timu yake ya kampeni Mkoani Mara, inasemekana Mwalimu alitamka "I shall never allow my country to be thrown to the dogs". Wana NCCR walidai Mwalimu aliwaita mbwa. Lakini baada ya hapo, Mwalimu alijitolea wazi wazi kumfanyia kampeni Benjamin Mkapa. Mrema akashindwa ingawa alipata asilimia 28 ya kura za u-Rais.
Kukosa fadhila kwa Mrema kulianza kujionyesha zaidi pale alipoanza kugombana na Mabere Marando. Mwisho akitaka kumfukuza Mabere toka NCCR, mambo yalimgeukia akatoka NCCR-Mageuzi na kujiunga na Tanzania Labour Party iliyokuwa inaongozwa na Lwekama. Ktk Tanzania Labour Party nako alikaribishwa kuwa Mwenyekiti Taifa. Lakini soon afterwards, mgogoro baina ya Mrema na viongozi wa awali wa T.L.P. ukaanza.
Uchaguzi Mkuu wa 2000, T.L.P. ikamsimamisha Mrema kama mgombea wao, lakini licha ya kukiimarisha chama, Mrema alikuwa mgombea wa tatu, Profesa Lipumba akichukua nafasi ya pili baada ya Mkapa. Hakujifunza kwa vile migogoro ndani ya T.L.P. iliendelea na ktk Uchaguzi Mkuu wa 2005, Mrema aliambulia kura chache sana kama mgombea wa U-Rais, chama chake kikipata kiti kimoja tu cha Ubunge huko Biharamulo Magharibi.
Mrema ameendelea kulumbana na wanachama viongozi ktk T.L.P. na mwaka huu alipokuwa na Mkutano Mkuu wa T.L.P., aliwafukuza wajumbe akabakia na wajumbe 163 tu, waliomchagua Mwenyekiti wa Taifa kwa miaka mitano ijayo. Tumeshuhudia kusambaratika kwa chama chake kule Biharamulo wiki iliyopita, ambako yeye mwenyewe alikwenda kumkampenia mgombea wake aliyeambulia kura 187, zikiwa ni asilimia 0.57 za kura zilizopigwa.
Mrema amechoka na amekwisha kisiasa. Bora arudi Kiraghacha, Marangu kunywa mbege. Tutamkaribisha.